Waziri wa Elimu: Shule zinazoongoza kwa ufaulu za binafsi haziruhusu mikutano ya wazazi

Revolution

JF-Expert Member
Feb 28, 2008
791
551
Habari ndugu zangu kuna tatizo kubwa katika hili suala nililowasilisha hapo juu. Shule nyingi kuanzia chekechea hadi kidato cha sita zina matatizo makubwa haswa zile zinazotoa ufaulu wa kiwango cha juu. Wanafunzi wanaamka saa nane na wanalala saa saba usiku ili wakeshe madarasani wakariri. Mwisho wa siku tukienda kwenye majadiliano ya kimikataba tunashindwa kujenga hoja. Mzazi una hela na bado unalipa na mtoto anateseka kwa kuamka saa nane usiku ili shule ipate A zote. Tunawaumiza vijana wetu.
 
Uvivu na umwinyi ndio umezalisha huu ujinga tunaouona wa watoto. Enzi zetu za viboko, kutembea kilometa 10 hadi 20 kwenda shule huku unakanyaga umande, unapishana na fisi na hakuna cha breakfast tulikuwa tunafaulu vizuri ila nafasi zilikuwa chache za kuendelea na masomo. Sasa unataka kuleta maneno ya haki za kuiga kutoka ulaya kwenye nywele ngumu unadhani utafaulisha watoto?. Acha wakaze msuli. Mimi shule ambayo haina stick na kibano sipeleki mtoto
 
jana nimepanda gari na watoto wa Olympio wa std 7. Wanadai full week wanaenda shule yani Jumatatu hadi Jumapili wako shule. Masomo huanza saa 1 asubuhi hadi saa 1 jioni except jumamosi na jumapili ndio wanatoka saa 11 jioni😁!

Kiukweli ilibidi nicheke tu maana sidhani kama mtoto wangu atasoma shule kwa style hio. Nataka jumamosi apumzike na jumapili apumzike.
 
halafu lenyewe linajiona limeandika pointi kumbe zezeta
Jambo rahisi saana

Mchukue mwanao mhamishe mpeleke wanapo amka SAA 1 asubuhi. Kwan umelazimishwa kumsomesha hapo??

Kabla ya kuanza shule uliulizia utaratibu wao WA masomo?? Ukaridhika then unataka wabadilike...
sasa unakuta na huyu n mzazi, yaani mwanae ana hasara sana, bora angezaliwa na baba punguani tu
 
Habari ndugu zangu kuna tatizo kubwa katika hili suala nililowasilisha hapo juu. Shule nyingi kuanzia chekechea hadi kidato cha sita zina matatizo makubwa haswa zile zinazotoa ufaulu wa kiwango cha juu. Wanafunzi wanaamka saa nane na wanalala saa saba usiku ili wakeshe madarasani wakariri. Mwisho wa siku tukienda kwenye majadiliano ya kimikataba tunashindwa kujenga hoja. Mzazi una hela na bado unalipa na mtoto anateseka kwa kuamka saa nane usiku ili shule ipate A zote. Tunawaumiza vijana wetu.

Nilienda mwaka jana kutembelea shule yangu Ilboru nikakuta jumapili wanatakiwa waingie kusoma kuanzia saa 9 mpaka saa 12. Wewe mtoto wako anadeki nyumbani hawataweza kuwa sawa maana juma mosi na juma pili wanasoma masaa 6 au zaidi!
 
Huyo mwanao amefungwa kamba hapo, si ukamchukue? Sisi wakati tunaenda shule km 30 ukitakiwa kuwahi namba saa 11 unadhani tulikuwa kutukiamka saa ngapi. Pumbavu huyu mzazi
 
Watanzania wengi tuna akili lakini tuna elimu mbovu. Siamini kwenye tuition wala masomo nje ya muda uliopangwa. Watu wanadhani ni sifa kusoma muda mrefu chini ya walimu wenye uelewa mdogo.
 
Habari ndugu zangu kuna tatizo kubwa katika hili suala nililowasilisha hapo juu. Shule nyingi kuanzia chekechea hadi kidato cha sita zina matatizo makubwa haswa zile zinazotoa ufaulu wa kiwango cha juu. Wanafunzi wanaamka saa nane na wanalala saa saba usiku ili wakeshe madarasani wakariri. Mwisho wa siku tukienda kwenye majadiliano ya kimikataba tunashindwa kujenga hoja. Mzazi una hela na bado unalipa na mtoto anateseka kwa kuamka saa nane usiku ili shule ipate A zote. Tunawaumiza vijana wetu.
Hakuna aliyefanikiwa kwa kuamka saa 1 asubuhi na kulala kama kuku saa 1 jioni.

Hata marais wenyewe hukesha wakifanya hili na lile ama ya kiofiai ama ya binafsi. Wanafanyakazi weekends na hata nyakati ngumu za maisha kama kuumwa na misiba.

Hii ndiyo maana ya muda ni mali. Hizo A si za shule. Ni za mwanao. Kama hupendi mpeleke wanakolala saa 2 na kuamka sa 12 asubuhi.
 
Migodini chai wanakunywa saa 10:30 asubuhi shift inaanza saa 11:00 asubuhi unadhani huyo mwanao ataweza..?
Kitu ambacho mtoa mada hajui ni kuwa mfumo wa maisha unabadilika kwa kasi sana. Wenzetu huko mbelembele wana ajira zaidi ya moja. Asubuhi anafanya kazi taasisi moja halafu jioni anakuwa na part time sehemu nyingine.

Hizi shule zinawaandaa watoto kwa mfumo wa maisha ujao.

Nimejifunza kwa wanangu. Waliosoma kayumba sekondari wana ratiba tofauti na waliosoma private. Hawa wa kayumba ni wavivu hata kuamka tu.

Ukija kujitegemea kusimamia ratiba zao, hawa wa private wako makini sana. Wa kayumba hawajali matumizi ya muda.

Utunzaji wa mali zao nao wanatofautiana. Wa private wako makini kuliko wale wa kayumba.

Kwenye ufaulu ndo kabisa.
 
Hoja nyingine za kipuuzi kweli, wewe kama unaona anateseka si umuhamishe?
 
Habari ndugu zangu kuna tatizo kubwa katika hili suala nililowasilisha hapo juu. Shule nyingi kuanzia chekechea hadi kidato cha sita zina matatizo makubwa haswa zile zinazotoa ufaulu wa kiwango cha juu. Wanafunzi wanaamka saa nane na wanalala saa saba usiku ili wakeshe madarasani wakariri. Mwisho wa siku tukienda kwenye majadiliano ya kimikataba tunashindwa kujenga hoja. Mzazi una hela na bado unalipa na mtoto anateseka kwa kuamka saa nane usiku ili shule ipate A zote. Tunawaumiza vijana wetu.

1. Watoto wanakufa?
2. Wanapata A zote?
3. Mifumo ya nchi inajtaji nini? A?
4. Ajira zinaitaji nini A?

Hawa walimu wanachofanya ni kutoa kile kitu ambacho ajira, na mifumo ya nchi inataka, nacho ni A tu, sio ujuzi wala nini, Kanyaga twende.

Nchi ya hovyo hii...
 
Jambo rahisi saana

Mchukue mwanao mhamishe mpeleke wanapo amka SAA 1 asubuhi. Kwan umelazimishwa kumsomesha hapo??

Kabla ya kuanza shule uliulizia utaratibu wao WA masomo?? Ukaridhika then unataka wabadilike...
Ushauri mwanana kwa Revolution ! Ukiona vyaelea……. Kuku huchokola sawa na mdomo wake. Ndo maana hujawahi kusaidia kuku kisa kakwamwa kooni.
 
Back
Top Bottom