Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,989
Akizungumza Oktoba 10, 2023 jijini Dodoma, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema mkutano huo ni wa Kihistoria kwani kwa mara ya kwanza unafanyika ikiwa ni ushirikishwaji wa Sekta Binafsi na unalenga kusikiliza changamoto katika uwekezaji, uendeshaji wa shule na kuona namna ya kusaidia kuzitatua na kuweka mikakati ya pamoja.
Prof. Mkenda ameongeza kuwa kusaidia kutatua changamoto zilizopo katika sekta binafsi na taasisi zisizo kuwa za serikali ambazo zinatoa huduma katika sekta ya elimu ni kutasaidia kuchangia utoaji elimu bora kwa watoto wa kitanzania.
Naye Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omari Kipanga amesema kuwa majukumu ya serikali katika elimu ni kuhakikisha inatoa elimu kwa wote hivyo sekta binafsi na taasisi nyingine zinaisaidia serikali katika jukumu hilo.
Mkutano huo pia umehusisha Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi ajira Vijana na Watu wenye ulemavu ambapo Patrobas Katambi alishiriki. Wengi ni kutoka Wizara ya Ardhi na Makazi, NECTA na TET.