This is...
JF-Expert Member
- Dec 28, 2014
- 4,903
- 4,979
Sote tunajua kwamba matokeo ya darasa la Saba mwaka 2023 yametoka.
Matokeo haya yanajumuisha ya wanafunzi waliosoma shule za serikali na wale wa sekta binafsi.
Ukiyaangalia matokeo haya utagundua kwamba shule zenye ufaulu mzuri zaidi Ni zile za binafsi ukilinganisha na zile za serikali.
Kimsingi watoto wanaosoma ktk shule za binafsi wanatoka angalao ktk zile familia za vipato vya kati na juu tofauti na hawa wa shule za serikali ambao hawana chaguo lolote zaidi ya kusoma ktk shule za serikali ambazo Zina changamoto lukuki zikiwepo uhaba wa madawati, msongamano madarasani wakati mwingine hata kufikia wanafunzi 60 ktk chumba kimoja,uhaba wa vitabu achilia mbali tatizo sugu la uhaba wa walimu hasa kwa shule za vijijini.
Katika mazingira haya ya shule za serikali kumkuta mwanafunzi ameweza kupata daraja/wastani wa alama 'A' Basi mwanafunzi huyu anahitaji pongezi na motisha chanya.Anahitaji kuangalia kwa jicho la tatu sababu Ni wachache sana.Kwa shule za serikali Ni mmoja ,wawili ,watano na pengine hamna kabisa.Ila kwa shule za binafsi kwao Ni kawaida.
USHAURI/OMBI
Serikali ihakikishe wanafunzi wote wa shule za serikali waliopata wastani wa daraja 'A' wanapewa kipaumbele kujiunga na kidato Cha kwanza ktk shule za serikali zile maalumu mfano Mzumbe,Ilboru, Tabora,Moshi,Ashira na nyinginezo.
Sioni sababu ya watoto kutoka shule binafsi za Watakatifu/Saints kupewa hizi nafasi,waendelee na utaratibu wao wa sekta binafsi sababu wanajiweza. Walishazikimbia shule za serikali tangu shule za vidudu/awali/ chekechea.
Hii ndiyo njia ya kuzisaidia familia duni kuendeleza watoto wale wenye uwezo/ vipanga wanaoachwa ktk shule za kata ambazo hazijaimarika.
Huu uwe Ni mkakati wa kuokoa hivi vipaji kutoka ktk familia maskini kule vijijini.
Kwa kufanya hivi tutaokoa watoto wote wenye vipaji kutoka ktk sekta zote binafsi na umma.Hawa binafsi wazazi wanajimudu.
NB: Unaweza kutafsiri km ubinafsi na ubaguzi lkn km tangu awali wewe km mzazi/mlezi uliona shule za umma hazimfai mwanao kwanini leo unaona kidato Cha kwanza zinamfaa? Kwanini leo unaona mzumbe Ni shule nzuri?(
Ni ukweli kwamba Hali za maisha Kuna kupanda na kushuka lkn watoto wa maskini wapewe kipaumbele kwanza. Hao wengine elimu bora wanaweza kuipata mahali popote.
Mtazamo:
1.Kila wilaya ichaguliwe shule moja ya serikali iimarishwe kwa vifaa vya kufundisha na kujifunza,mabweni na walimu wa kutosha halafu ifanywe shule ya vipaji maaalumu kimkoa na hata kikanda tuokoe vipaji.
2.Tanzania haina uhaba wa walimu bali mgawanyo mbovu/hovyo wa mgawanyo na uhamishaji wa walimu.
Unakuta shule ya mjini/manispaa Ina wanafunzi 1000 Ina walimu 30-40 lkn kule kijijini shule idadi hiyo ya wanafunzi Ina walimu 10 au 12. Na serikali iko kimya.
3.Katika mwaka wa fedha Walimu 10 wanapangwa kazi ktk halmashauri ya Wilaya lkn ndani ya halmashauri hiyo hiyo Kuna walimu 5au 7 wanapewa uhamisho kwenda shule za manispaa au nje ya mkoa kwa mwaka huo huo .Hivyo tatizo linabaki Kama lilivyo. Mwalimu anakuja na barua ya uhamisho direct toka TAMISEMI,inabaki afisa elimu kusaini tu.Japo Sasa hivi kidogo hali hii imepungua.
4.Serikali ibadilishe mtazamo wake kwamba lazima mwalimu mkuu awe na shahada/digrii moja.Uongozi Ni talanta.Wako walimu wenye shahada za uzamili lkn hata kuongoza drasa la kwanza hawawezi.Sembuse hata zamu shuleni hawawezi.Uongozi uangalie uwezo pia.Wale wenye elimu ndogo na Wana uwezo mzuri waachwe.Waandaliwe programu za kuwaimarisha ili waweze kudeliver vitu positive ktk elimu.Tunashughudia vijana waliotoka vyuoni wakipewa Ualimu mkuu na hakuna wanachojua.Hii Ni hatari Sana.
Nb:Mimi naamini ktk kuwekeza kwanza kwa WALIMU,Mwalimu anayeliowa vizuri hata km miundo mbinu siyo rafiki lkn utaona matokeo chanya.
Serikali inakazania uwekezaji ktk vitu badala ya rasilimali watu/walimu bora wanaolipwa vizuri.NA HAPA NDIPO ILIPO SIRI YASHULE BINAFSI ZINAZOFANYA VIZURI.Wekeza kwa walimu kwanza!
Sasa serikali hailipi vizuri walimu ,haina learning facilities bora ,matokeo bora yatatokea wapi.
Huwezi kushinda mechi kwa hamasa bila uwekezaji.
Wasalaamu,mwalimu kijana niliyejistaafisha baada ya miaka 12 ya kushika chaki.
Karibu!