Waziri Mwigulu: Sijasema fedha za AZAKI ipewe Serikali

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,434
7,055
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amemaliza mkanganyiko wa taarifa kuhusu fedha za USAID na AZAKI ambayo ilionekana kutoeleweka vizuri na baadhi ya vyombo vya habari, wanaharakati na wadau mbalimbali.

Itakumbukwa kuwa juzi akiwa Dodoma alifanya kikao kwa njia ya mtandao na Mkurugenzi wa USAID kuhusu ushirikiano wa Shirika hilo la Marekani la Maendeleo na Serikali ya Tanzania, ambapo alitoa wito au pendekezo kwamba msaada wa fedha takribani Trilioni 3 ambazo USAID imepanga kuipatia Tanzania kupitia Asasi za Kiraia (AZAKI), zielekezwe kwenye miradi ya kipaumbele ya Serikali.

Kwa maneno mengine, Waziri wa Fedha hakumaanisha USAID ichukue fedha inazotaka Kuzipa AZAKI na kuipatia serikali bali AZAKI zitakazopokea fedha hizo izielekeze katika mipango na vipaumbele vya serikali.

Alitolea mfano kwamba katika sekta ya Afya, Serikali inajenga vituo vya afya na zahanati, AZAKI zinaweza kununua vifaa tiba. Kwenye Elimu, wakati serikali inajenga shule na madarasa, AZAKI zinaweza kununua vifaa vya kufundishia kama vile vitabu na mahitaji mengineyo. Hivyo hivyo kwenye sekta za Kilimo, Uvuvi, Mazingira n.k.

Akiambatanisha kipande cha video akiwa anazungumza kwenye mkutano huo na USAID, Waziri Nchemba amemaliza mkanganyiko kwa kuandika:

"Sio Usaid wachukue Fedha walizotaka kuwapa AZAKI na kuipatia Serikali; bali USAID wanaotoa fedha na AZAKI zinazopokea fedha, waelekeze nguvu zao katika miradi inayoendana sanjari na Dira ya Taifa, Mipango na Vipaumbele vya Serikali." Dkt. Mwigulu Nchemba.
---

UFAFANUZI ZAIDI

"Kama Waziri mwenye dhamana ya Fedha nina Wajibu wa kuwaeleza washirika wa Maendeleo kuhusu mifumo yetu ya Bajeti. Ndicho nilifanya katika mazungumzo na USAID. HATUNA NIA YA KUZICHUKUA FEDHA ZINAZOKWENDA KWA AZAKI isipokuwa ufadhili uendane na malengo yetu.

Naziomba AZAKI kuwianisha shughuli zao na malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 na Mpango wa Maendeleo wa Miaka 5 ili sote kwa Pamoja, Serikali, Sekta Binafsi na Jamii kupitia CSOs tuvute pamoja katika kuleta Maendeleo ya Nchi yetu. Nawasihi DPs kuongeza Fedha kwa CSOs zetu.

Fedha ambazo washirika wa Maendeleo wanazipeleka moja kwa moja kwa Azaki zinasimamiwa na menejimenti/Bodi za Azaki kwa mujibu wa Sheria ya NGO. Fedha zinazotumiwa na Serikali zinapaswa kufuata Sheria ya Bajeti na Sheria za Fedha za umma. HATUJATAKA FEDHA ZA AZAKI ZIJE HAZINA."

Mwisho wa kunukuu.

Pia, soma=> Waziri Nchemba, ameiomba USAID, kuelekeza msaada wa dola bilioni 1.3, kwenye miradi ya kipaumbele ya Serikali ya Awamu ya Sita
 
Tr 13 Tshs ni kama usd 5.5 million. Ni hela nyingi.. kama serikali haiwezi kudhibiti zinatolewa kwa nani na kufanya nini hiyo hela inaweza kua na athari kwa nchi.

Kazi yake inaweza kulemaza taifa kuendelea kisaikolojia kua tegemezi.

Pia hizo azaki zinaweza kugeuza hela hizo mradi wao wa kula hela inayokuja kama rushwa ili kuipenda na kuendeleza maslahi ya Marekani nchini.
 
Na wewe Waziri usikubali hizo fedha wapewe hao Azaki, watazila hakuna kitu cha maana zitafanya.

Hizo pesa ziwe kwenye account maalumu ya serikali kuzimonitor.

Mwendazake hakuwa mjinga kuzuia hizo pesa kuja kinyemela.

Azaki waainishe miradi ya kutumia hizo pesa sio tuu kuja kununua condom na ped eti ndio matumizi ya maendeleo.

Mwisho hao Azaki wawe wanapanga mipango yao Kwa kuzingatia dira ya maendeleo ya Nchi sio kila mtu anafanya lwake.
 
Nafikiri waziri amefafanua vyema, na kwa mantiki hiyo AZAKI nazo ni vyema zikatoa tamko kuhusu kumuunga mkono ama pia hata kutomuunga mkono.

Lakini ukweli ni kwamba nyuma ya misaada na matumizi ya fedha zinatolewa kwa AZAKI, kuna mambo mengi sana ambayo yamejificha. Kuna usiri mkubwa kuhusu matumizi yake, na hata pia kiasi halisi kinachotolewa ili kiweze kuja kuzifikia AZAKI hizi.
 
Hapana, yuko sahihi. Tazama hata video akiwa anazungumza kwenye kikao, utaona akishauri AZAKI ziende sanjari na Dira ya Taifa, Mipango na Vipaumbele vya Serikali ili kuwe na ushirikiano katika kuleta maendeleo. Hakusema hizo fedha ipewe Serikali.
Tatizo AZAKI huwa hazishirikishwi kwenye upangaji wa Dira za taifa

Wanakaa maofisa wa Serikali peke yao kutengeneza dira na mpango ya maendeleo

Pili AZAKI aziache wafadhili huwa hawapendi AZAKI kuingiliwa na Serikali ni kama Serikali ikiingilia mambo ya mashirikisho ya vyama vya michezo tumeona Kenya ikipigwa marufuku kushiriki michuano ya kimataifa baada ya Serikali ya Kenya kuingilia mambo ya uongozi wa chama cha mpira kenya

TATU ,AZAKI hupeleka write ups zao kwa wafadhili ikiwemo USAID kwenye maeneo ambayo wanaona kuna ombwe ambalo Serikali huwa Haija li cover.
 
Na wewe Waziri usikubali hizo fedha wapewe hao Azaki, watazila hakuna kitu cha maana zitafanya.

Hizo pesa ziwe kwenye account maalumu ya serikali kuzimonitor.

Mwendazake hakuwa mjinga kuzuia hizo pesa kuja kinyemela.

Azaki waainishe miradi ya kutumia hizo pesa sio tuu kuja kununua condom na ped eti ndio matumizi ya maendeleo.

Mwisho hao Azaki wawe wanapanga mipango yao Kwa kuzingatia dira ya maendeleo ya Nchi sio kila mtu anafanya lwake.
Wewe unadhani wanaotoa fedha huwa wanamwaga tu bila kuelezwa hiyo pesa inaenda kufanya nini?

Hiyo ni fedha iliyotengwa, siyo lazima itolewe yote kama vigezo vya mtoaji havijafikika.
 
Tr 13 Tshs ni kama usd 5.5 million. Ni hela nyingi.. kama serikali haiwezi kudhibiti zinatolewa kwa nani na kufanya nini hiyo hela inaweza kua na athari kwa nchi.

Kazi yake inaweza kulemaza taifa kua tegemezi pia hizo azaki zinaweza kugeuza hela hizo mradi wao wa kula hela inayokuja kama rushwa ili kuipenda Marekani.
Mtu akiipenda Marekani anakuwa ametenda kosa gani kisheria?
 
Na wewe Waziri usikubali hizo fedha wapewe hao Azaki, watazila hakuna kitu cha maana zitafanya.

Hizo pesa ziwe kwenye account maalumu ya serikali kuzimonitor.

Mwendazake hakuwa mjinga kuzuia hizo pesa kuja kinyemela.

Azaki waainishe miradi ya kutumia hizo pesa sio tuu kuja kununua condom na ped eti ndio matumizi ya maendeleo.

Mwisho hao Azaki wawe wanapanga mipango yao Kwa kuzingatia dira ya maendeleo ya Nchi sio kila mtu anafanya lwake.
Ni za kwenu?
 
Back
Top Bottom