Rais amekiri kuwa kuna wizi wa fedha za Serikali

koryo1952

JF-Expert Member
Mar 7, 2023
380
763
Rais amekiri kuwa kuna wizi wa fedha za Serikali. Fedha zote zinatunzwa Wizara ya Fedha. Zinatolewa Wizara ya Fedha kwa utaratibu uliokubaliki Waziri wa fedha akiwa na taarifa. Fedha zinaenda TAMISEMI Waziri wa TAMISEMI lazima awe na taarifa.

Kwanini Mamlaka ya uteuzi isiwaajibishe Waziri wa Fedha na Waziri wa TAMISEMI kwa wizi wa fedha za Serikali?.
 
Una hoja ila shida ipo kwa mteuzi wa waziri wa fedha na huko tamisemi hao wote sio rahisi awatengue na ujue mama ana tabia ya kusahau au kujikausha ila ukweli ni kuwa kwa nafasi ya mama ni jikoni, kibarazani kwenye umbea na kusutana.
MWAKAMKE HAFAI UONGOZI KWENYE JAMII.
(Nipigeni niueni sifitu hayo maneno) yule mchaga
 
Rais hakusema kwamba fedha zinaibiwa Hazina, bali ni kabla hazijafika huko

Alijikita zaidi kwenye mtandao unaoiba fedha kabla hazijafika hazina.

Ndiyo maana akataja mfano wa Mbeya ambapo palikuwa na mtandao wa watu binafsi unaokusanya fedha na kutoa risiti sambamba na ule halali wa serikali.

Pia aligusia makusano hafifu kwenye halmashauri, na ndipo akahoji, iwapo fedha zinapotea kwa wizi na uzembe, halmashauri zikiomba fedha, zinategemea zitoke wapi?
 
Mhe. Rais amekiri kuwa kuna wizi wa fedha za Serikali. Fedha zote zinatunzwa Wizara ya Fedha. Zinatolewa Wizara ya Fedha kwa utaratibu uliokubaliki Mhe. Waziri wa fedha akiwa na taarifa. Fedha zinaenda TAMISEMI Mhe. Waziri wa TAMISEMI lazima awe na taarifa. Kwa nini Mamlaka ya uteuzi isiwaajibishe Mhe. Waziri wa Fedha na Mhe. Waziri wa TAMISEMI kwa wizi wa fedha za Serikali?.
Huyo mwanamke hajui hata anataka nini kwani hakuwahi waza atakuwa Rais . Aondolewe Haraka
 
Bwana Kaka, wizi wa fedha za serikali si wa mtu mmoja mmoja bali ni mfumo. Ni ngumu sana mtu mmoja kuiba fedha za serikali, labda aibe vifaa. Sasa mfumo mzima wa serikali kuanzia Waziri hadi muhudumu unaweza kuhamisha mabilioni ya pesa, kila mmoja napata mgao wake na mradi haufanyiki na fedha zinaonekana kimaandishi zimetoka. Tukubali ukweli kwamba malezi yetu kuanzia ngazi ya familia, mashuleni, nk...yanazalisha tabia za watu walafi na wabinafsi. Hivi unakumbuka shule za boarding, chakula kizuri eti wanakula viongozi, au mchuzi wenye mafuta mengi (top layer) unachotwa na kugawia viongozi tu. Sasa hao wakija kuwa viongozi serikalini wataachaje kujipendelea? Rais akitaka kuonesha mfano, siku moja ang'oe mfumo mzima, haijalishi watakuwa watu wangapi. Mwaka 1982 kuna mahabusu wahaini walitoroka Gereza Keko, na katika kuwajibika aliondoka Waziri (Mambo ya Ndani), Kamishna Mkuu wa Magereza, Mkuu wa Magereza Dsm, Mkuu wa Gereza Keko, Afisa wa zamu wa wiki, Afisa wa zamu wa siku hiyo na askari walinzi wote waliokuwa zamu. Utaratibu huu wa uwajibikaji ukifanyika, naamini nidhamu itarudi serikalini..!
 
Mhe. Rais amekiri kuwa kuna wizi wa fedha za Serikali. Fedha zote zinatunzwa Wizara ya Fedha. Zinatolewa Wizara ya Fedha kwa utaratibu uliokubaliki Mhe. Waziri wa fedha akiwa na taarifa. Fedha zinaenda TAMISEMI Mhe. Waziri wa TAMISEMI lazima awe na taarifa. Kwa nini Mamlaka ya uteuzi isiwaajibishe Mhe. Waziri wa Fedha na Mhe. Waziri wa TAMISEMI kwa wizi wa fedha za Serikali?.
rudia kumsikza vizuri Rais alichosema itakusaidia,
unless una issue binafsi na mawaziri ulowataja 🐒
 
Back
Top Bottom