Mkakati wa Kuongeza Vyanzo vya Fedha kwa Asasi za Kiraia (AZAKI)

Feb 5, 2022
31
48
1689949099587.png
Asasi za Kiraia (AZAKI) katika nchi nyingi zinazoendelea, ikiwemo Tanzania, zinategemea ufadhili wa ndani na nje ili kutekeleza miradi na mipango. Vipaumbele vya wafadhili vimekuwa vikibadilika mara kawa mara, hali iliyopelekea upungufu wa ufadhili kwenye baadhi ya sekta. Ushindani miongoni mwa AZAKI pia umechangia kwa kiasi kikubwa. Kujitegemea kifedha (Financial sustainability) limekuwa ni hitaji la msingi kwa AZAKI ili ziendeleze uwepo wao. Tafiti zinaonyesha kwamba; uwezo wa AZAKI kujitegemea kifedha unakwamishwa na sababu mbalimbali kama vile; miundo mibovu ya uongozi, ukosefu wa rasilimali watu na ukosefu wa mikakati ya muda mrefu ya kutafuta fedha (Long-term fundraising Strategy)

Ili kujitegemea kifedha AZAKi zinahitaji kuwa na muundo wenye kujumuisha vyanzo tofauti vya upatikanaji wa fedha mbali na kutegeme wafadhili pekee. Muundo huu unaweza kujumuisha huduma za Ushauri wa Kitaalamu (Consultancy Service), Uwekezaji kwenye Miradi ya Kibiashara (Social Enterprises), Uwekezaji kwenye mikopo midogo midogo (Microfinance) n.k
Mafanikio katika utekeleaji wa muundo huu, kwa kiasi kikubwa unategemeana na sifa za Taasisi husika pia mazingira (context) ambayo Taasisi inaendesha shughuli zake. Kwa kirefu, miundo ambayo huweza kutumiwa na AZAKI ili kujitegemea kifedha huweza kujumuisha;

  • Huduma za Ushauri wa Kitaalamu (Consultancy Service) Ushauri ni utaratibu wa kutoa utaalamu kwa kipindi cha muda mfupi kwa Taasisi/mtu binafsi juu ya masuala ambayo mlengwa ana ujuzi kidogo au hana kabisa. Hapa AZAKI zinaweza kutoa huduma ya ushauri katika maeneo ya usimamiaji wa rasilimali watu, Teknolojia ya Mawasiliano, Usimamizi wa Fedha, Sheria, Utumiaji na Usimamizi wa Mitandao ya Kijamii n.k, Huduma hii itatolewa kwa kutoza gharama. Pia AZAKI zinaweza kutoa huduma ya mafunzo kwenye maeneo kama vile Uongozi, Uwajibikaji n.k . Mafanikio katika muundo huu yanahitaji uwekezaji katika masoko na matangazo (marketing & advertisement)
  • Ukodishaji wa mali za Taasisi (Assets Building) Hapa AZAKI zinaweza kukodisha mali zinazomiliki kwa muda maalum na kwa gharama kwa mujibu wa makubaliano. Ukodishaji unawea kufanyika kwa vitu kama viti, projekta, ukumbi kwa ajili ya mikutano, sehemu kwa ajili ya matumizi ya ofisi n.k
  • Utayarishaji wa mikutano/makongamano (Event Organization). Katika muundo huu, AZAKI zinaweza kuandaa mikutano au makongamano kwa ajili ya kujenga ufahamu juu ya jambo fulani, au kuzua mjadala kwa wadau maalum. Ili kushiriki katika tukio hili, mhusika atapaswa kuchangia kiasi cha fedha. Utaratibu wa kuandaa tukio kama hili, huanza na kuandaa andiko fupi (concept note), kutambua wahusika/washiriki (target audience), kufanya makisio ya mapato na matumizi (budgeting), uandaaji wa mahitaji (logistical arrangement), usimamiaji (management), utekelezaji (execution) na tathmini (evaluation)
  • Ada za Uanachama (membership fees) Kupitia wanachama waanzilishi, wanachama wa kawaida, na wanachama wa heshima, AZAKI zinapaswa kuwa na utaratibu wa kukusanya michango. Pia AZAKI zinapaswa kuanzisha utaratibu wa kusajili mfadhili mmoja mmoja (individual supporter) na kuwagawa katika makundi kutokana na kiasi cha uchangiaji wao.
  • Miundo mingine, inaweza kuwa; Uleaji wa AZAKI Changa kwa kuzipatia huduma za uendeshaji katika maeneo ya usimamiaji wa fedha, utawala (Incubation), Miradi ya Ukopeshaji wa Fedha (Microfinance) Ufadhili wa Sekta Binafsi (Private Sector Funding) n.k.
................................................................................................................................................................................................................................................
Are you a local nonprofit or an Individual and have done fundraising efforts without satisfactory results? Let us take your organization/endeavor to the next level through the following service;
  • Fundraising Campaigns and Strategy
  • Annual Report and Collateral Materials
  • Case Support Development
  • Donor Cultivation
  • Strategic Planning
  • Grant Writing
  • Prospect Research
  • Training Service
Contact Us Today
Omar Msonga
Mobile: +255 719 518 367
Email: omarmsonga8@gmail.com
Dar es Salaam
 
Back
Top Bottom