Waziri Mkuu Ufaransa amteua aliyekuwa mume wake kuwa Waziri wa Mambo ya Nje

LINGWAMBA

JF-Expert Member
Sep 30, 2023
421
951

Screenshot_20240207-120412.jpg

Waziri Mkuu mpya wa Ufaransa Gabriel Attal ambaye ni shoga amemteua mume wake Stephane Sejourne kuwa waziri wa mambo ya nje, siku chache tu baada ya yeye kuwa shoga wa kwanza aliyejinadi hadharani kushikilia wadhifa wa uwaziri mkuu wa nchi hiyo.

Sejourne, ambaye pia anaongoza chama cha siasa cha Rais Emmanuel Macron cha Renaissance na kundi la Renew katika Bunge la Ulaya, anachukua nafasi ya Catherine Colonna katika mabadiliko ya baraza la mawaziri yaliyofuatia kujiuzulu kwa waziri mkuu wa zamani Elisabeth Borne siku ya Jumatatu.

Waziri huyo mpya wa mambo ya nje mwenye umri wa miaka 38 alikuwa mshauri wa Macron tangu akiwa Waziri wa Uchumi na Fedha, kisha akajiunga na timu yake mwaka 2014 na kubaki naye katika katika kampeni za uchaguzi wa Rais mwaka 2017.

Macron alimteua Attal kuchukua nafasi ya Borne siku ya Jumanne, na kumfanya kuwa waziri mkuu mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kutokea nchini Ufaransa na aliyejitangaza hadharani pia kuwa anajihusisha na maingiliano ya kimwili ya watu wa jinsia moja. Kabla ya kuteuliwa kuwa waziri mkuu, Attal aliwahi kuwa Waziri wa Elimu.

Itakumbukwa kuwa baada tu ya kuteuliwa kushika wadhifa huo, alichukua hatua ya kupiga marufuku wanafunzi wasichana Waislamu kuvaa vazi la Abaya maskulini.

Attal na Sejourne walianzisha rasmi mahusiano yao ya kingono mwaka 2017 kupitia 'ufungishaji ndoa' wa kiraia na kuyatangaza hadharani mwaka uliofuata, wakati Attal alipojitokeza hadharani na kujitangaza kuwa ni 'shoga'.

Hata hivyo, mnamo mwezi Oktoba, Attal alidai katika tamko rasmi juu ya migongano ya masilahi kwa Mamlaka ya Juu ya Uwazi katika Maisha ya Umma kwamba hakuwa na mshirika rasmi katika mahusiano ya kingono, ingawa yeye na Sejourne hawajawahi kutangaza hadharani kuwa wametengana kisheria.

Huko nyuma mnamo mwaka 2018, Attal aliwahi kuwa msemaji wa chama cha Macron kwa muda wa miezi 10, wakati huo kikiitwa La Republique en Marche baada ya kukihama Chama cha Kisoshalisti miaka miwili mapema ili kumuunga mkono Macron katika kinyang'anyiro cha kuwania urais.

Mabadiliko ya baraza la mawaziri aliyofanya Emmanul macron siku ya Alhamisi ya wiki iliyopita, yameelezewa kama juhudi za rais huyo wa Ufaransa za kuokoa umashuhuri unaodidimia wa serikali yake.
 
Back
Top Bottom