Shule zafungwa Ufaransa kwasababu ya Kunguni

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Waziri wa Elimu wa Ufaransa Gabriel Attal ametangaza kuwa nchi hiyo imelazimika kufunga shule saba zinazowapokea wanafunzi wapatao 1,500 baada ya kuvamiwa na kunguni.

Mapema wiki hii, mamlaka ya Paris ilitangaza kufungwa kwa shule mbili kwa sababu ya kunguni, moja huko Marseille na nyingine Villefranche-sur-Saone nje kidogo ya mji wa kusini mashariki wa Lyon.

Serikali ya Ufaransa imefanya msururu wa mikutano wiki hii kuchunguza idadi inayoongezeka ya visa vya kunguni, wakati nchi hiyo ikiandaa Kombe la Dunia la Rugby na ambayo itakuwa mwenyeji ya Michezo ya Olimpiki hapo mwakani.

Serikali mjini Paris imelazimika sasa kuingilia kati kupambana na kunguni hao. Ijumaa iliyopita, Waziri Mkuu wa Ufaransa Elisabeth Borne aliitisha kikao cha baraza la mawaziri kujadili namna ya kupambana na kunguni.

Takwimu za Shirika la Afya na Usalama wa Chakula nchini Ufaransa zinaonesha kuwa angalau nyumba moja kati ya kumi nchini humo ilikuwa na kunguni katika miaka michache iliyopita. Kuwatokomeza kunguni inagharimu pesa nyingi na wakati mwingine zoezi hilo hurudiwa mara kadhaa.

Kunguni wameripotiwa sehemu mbalimbali nchini Ufaransa kama kwenye treni za mwendo kasi katika mji mkuu Paris, na hata katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Charles De Gaulle.

Kunguni ni mdudu mdogo asiyeweza kuruka bali anayeweza kutembea haraka kutoka sehemu moja hadi nyingine au hata nchi hadi nchi, na imekuwa vigumu kumtokomeza kwa kutumia dawa za kuulia wadudu. Lakini pia, kunguni anaweza kuishi hata mwaka mzima bila kula.

DW Swahili
 
Ajabu na kweli,halafu wanaenda kumhonga my Ukraine pesa,kwa kuwa wanachuki na Mrusi badala yakutatua changamoto ndogo za ndani kama hizo,kwa ujinga wao watashindwa hata kuandaa olimpico ijayo.😂
 
Wazungu wanajua kudeka na kijidekeza, sina kumbukumbu km kuna shule ya bweni hizi za serikali hapa nchini kwetu ambayo haina kunguni. Kunguni wanauzi na niwasumbufu ila wanatoka kiwepesi mno ukiamua kupambana nao kiume. Haizidi cku mbili kuwaondosha ndani ya nyumba
 
D
Waziri wa Elimu wa Ufaransa Gabriel Attal ametangaza kuwa nchi hiyo imelazimika kufunga shule saba zinazowapokea wanafunzi wapatao 1,500 baada ya kuvamiwa na kunguni.

Mapema wiki hii, mamlaka ya Paris ilitangaza kufungwa kwa shule mbili kwa sababu ya kunguni, moja huko Marseille na nyingine Villefranche-sur-Saone nje kidogo ya mji wa kusini mashariki wa Lyon.

Serikali ya Ufaransa imefanya msururu wa mikutano wiki hii kuchunguza idadi inayoongezeka ya visa vya kunguni, wakati nchi hiyo ikiandaa Kombe la Dunia la Rugby na ambayo itakuwa mwenyeji ya Michezo ya Olimpiki hapo mwakani.

Serikali mjini Paris imelazimika sasa kuingilia kati kupambana na kunguni hao. Ijumaa iliyopita, Waziri Mkuu wa Ufaransa Elisabeth Borne aliitisha kikao cha baraza la mawaziri kujadili namna ya kupambana na kunguni.

Takwimu za Shirika la Afya na Usalama wa Chakula nchini Ufaransa zinaonesha kuwa angalau nyumba moja kati ya kumi nchini humo ilikuwa na kunguni katika miaka michache iliyopita. Kuwatokomeza kunguni inagharimu pesa nyingi na wakati mwingine zoezi hilo hurudiwa mara kadhaa.

Kunguni wameripotiwa sehemu mbalimbali nchini Ufaransa kama kwenye treni za mwendo kasi katika mji mkuu Paris, na hata katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Charles De Gaulle.

Kunguni ni mdudu mdogo asiyeweza kuruka bali anayeweza kutembea haraka kutoka sehemu moja hadi nyingine au hata nchi hadi nchi, na imekuwa vigumu kumtokomeza kwa kutumia dawa za kuulia wadudu. Lakini pia, kunguni anaweza kuishi hata mwaka mzima bila kula.

DW Swahili
Hawaogi? Hawafui nguo?
Dunia ya leo watu wameshindwa vita na kuelemewa na kunguni...kuna kitu kinafikirisha sana hapo.
 
Wazungu wanajua kudeka na kijidekeza, sina kumbukumbu km kuna shule ya bweni hizi za serikali hapa nchini kwetu ambayo haina kunguni. Kunguni wanauzi na niwasumbufu ila wanatoka kiwepesi mno ukiamua kupambana nao kiume. Haizidi cku mbili kuwaondosha ndani ya nyumba
Labda makundi ya kulinda haki za wadudu itakua yamekuwa yakiingilia kati madawa yasitumike kuua wadudu sababu na wao wana haki sawa ya kuishi.
 
Shida nyingine ya wazungu iko hapo hawachelewi kupinga mahakamani kwamba kunguni nao wanahaki yakuishi kama binadamu na kitendo cha kuwaua hakikubaliki ni ukatili binadamu kwa wadudu wasio jiweza
 
Wana ufala mwingi sana.
 
Wafaransa ni mdebwedo sana kunguni tu wanafunga shule. Sisi waha wa Kigoma kuna kunguni wa kutosha kwenye treni na mabasi yetu ila tunapanda na kulala fofofo hadi hadi Dar.
 
Nimesoma tu kichwa cha habari ila hao wanafunzi wa france ebu wafike Pugu secondary pale wakapate darasa la kuishi na kunguni.
 
Kunguni mdudu mjinga sana,ukifika kwa watu anajianika kweupe.nakumbuka kipindi nipo shule aise kunguni walinikamua damu hadi nikawa nakesha class
 
Kweli inakera sana kuona Binadamu anaua wadudu tena madawa kwa vifo vya kikatili .wadudu waishi duniani tena kabla Binadamu, tena ni Viumbe Mungu. Na tena imeandikwa usiue, ni muda Africa tutazame haki wadudu
 
Miss Zomboko!!! Unamaanisha anaweza kutoka boda ya Tarakea Tanzania kwenda Tarakea ya Kenya??
Anatoka boda Tarakea Kenya mpaka Tunduma Tanzania.
Anasafirishwa kirahisi sana na wasafiri.
Wanaotokea Paris hivi sasa ni rahisi sana kuwapeleka kunguni majumbani mwao.

Kunguni siyo jambo dogo, anakera sana.
 
Back
Top Bottom