Vijana wa Tanzania tunajifunza nini kuteuliwa kwa Waziri Mkuu wa Ufaransa mwenye miaka 34?

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,262
9,715
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wa Ufaransa Mheshimiwa Emmanueli Macron amemteua Gabriel Attal kuwa waziri mkuu wake, kijana mdogo kabisa katika Historia ya Ufaransa mwenye umri wa miaka 34 aliyezaliwa tarehe 16 march 1989.

Je vijana wa kitanzania tunajifunza nini katika uteuzi huo wa kijana mdogo kabisa aliyeaminiwa kuwa waziri mkuu katika Taifa kubwa kabisa na lenye historia kubwa kabisa barani ulaya na Duniani kwote? Ikumbukwe hata Rais Macron alitwaa madaraka ya Urais akiwa na umri wa miaka 39.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wa Ufaransa Mheshimiwa Emmanueli Macron amemteua Gabriel Attal kuwa waziri mkuu wake, kijana mdogo kabisa katika Historia ya Ufaransa mwenye umri wa miaka 34 aliyezaliwa tarehe 16 march 1989...
Mjitambue nyinyi kuwa ni WAPUMBAVU kwa kuwa nyinyi Oktoba mwaka jana mumemchagua Raphael Lulandala mwenye umri huo huo kuwa Katibu wa UVCCM
 
Mjitambue nyinyi kuwa ni WAPUMBAVU kwa kuwa nyinyi Oktoba mwaka jana mumemchagua Raphael Lulandala mwenye umri huo huo kuwa Katibu wa UVCCM
Katibu mkuu wa UVccm hachaguliwi bali anateuliwa. Anayechaguliwa ni Mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa UVCCM Taifa. Hata mikoani na wilayani wanaochaguliwa ni wenyeviti lakini makatibu wote ni waajiriwa wa chama na wanateuliwa na kupelekwa maeneo husika.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wa Ufaransa Mheshimiwa Emmanueli Macron amemteua Gabriel Attal kuwa waziri mkuu wake, kijana mdogo kabisa katika Historia ya Ufaransa mwenye umri wa miaka 34 aliyezaliwa tarehe 16 march 1989...
Luca usijifananishe na watu Ntu yenyewe Mchele Ntekeee🤪
 
We unaewazaga uteuzi tuu!! Miaka 34 ni late adulthood Sasa kijana mdogo kabisa ndonini? maana ujana mwisho miaka 35!!!
Kumbuka huku kwetu mtu mwenye miaka hata 40 anaitwa kijana japo amevuka miaka 35.lakini huyu hata bado kuifikia hiyo 35 kaaminiwa na kupewa uwaziri mkuu wa ufaransa.je umejifunza nini kama kijana au mtanzania?
 
Sasa kwa mfano wewe bwana luka wakupe hicho cheo? Kuna maajabu gan utafanya? Humu mooote tunakujua kwa kitu kimoja tu, uchawa,! Ukipewa mamlaka hayo ndo utazidisha uchawa kwa boss.

Wewe ndo mfano wa vijana hao, na wewe tayari n bomu. Wacha vijana wa umri huo waendelee kubeti. Hata wewe najua unabeti kisirisiri
 
Back
Top Bottom