Watumishi zaidi ya 200 Wasimamishiwa mshahara kisa ESS (PEPMIS)

Je, ni kweli tetesi za watumishi Halmashauri ya wilaya ya rorya kukosa mshahara sababu hawajajiunga kwenye mfumo wa ESS (Employee Self Service Portal)?
 
Yaani kumbe ni serious... Kitu chenyewe ni kama usanii sanii tu... Yaani mnahangaika weee tija hakuna! Kilichojiwa kinaandikwa kwenye Opras kimehamishiwa kwenye mfumo... Maendeleo!
 
Labda ungetuambia kuna changamoto gani wao kujaza mfumo kama inavyotakiwa?

Maana watumishi wengi hawapendi technolojia wanaona kero...

So hapo kuna shida gani na nini kinapaswa kifanyike?
 
Halafu ni vijana tu. Ila dharau zimewaponza. Eti serikali inajua niko masomoni. Kumbe alitakiwa kuplan halafu aweke barua ya ruhusa, amemaliza.
Walioko masomoni hawakutakiwa kupandisha mpango zaidi tuu ya kujiunga na mfumo. Au huko kwenu walifundisha tofauti?
 
Walioko masomoni hawakutakiwa kupandisha mpango zaidi tuu ya kujiunga na mfumo. Au huko kwenu walifundisha tofauti?
Kuna baadhi ya Halmashauri wanawalazimisha kupandisha mpango kazi. Hasa Rorya jambo linalotia shaka maana unampimaje mtu ambaye hayupo kituoni
 
Back
Top Bottom