Serikali kutolipa mishahara watumishi kwa kisingizio cha kutojaza majukumu yao kwenye mfumo wa ESS ni unyang'anyi usiotumia Silaha

Course Coordinator

JF-Expert Member
Jul 27, 2019
1,682
3,065
Serikali ya awamu ya Sita iliachana na mfumo wa kujaza OPRASS kwenye makaratasi (nakala ngumu) badala yake ikatambulisha PEPMIS kupitia mfumo Employee Self Service kwa kifupi ESS.

Ikiwa na maana kwamba taarifa muhimu na za Msingi kuhusu Mtumishi zitakua kwenye mfumo huu.
Ikiwemo
  • Kujaza majukumu na utekelezaji wa majukumu yao.
  • Kupata salary slip kupitia mfumo huu
  • Uhamisho na kupata mkopo kupitia mabenki husika.
Kwa mwezi Februari baadhi ya Wakurugenzi na Maafisa Utumishi Wilaya walilia kukosa mshahara kwa kisingizio hiki kwamba watumishi walio chini ya taasisi zao hasa Halmashauri hawajajisajili kupitia mfumo huu. Huu ni unyang'anyi usiotumia Silaha.

Ikumbukwe mfumo huu ni Mpya na Elimu haijafikia watumishi hasa waliopo vituoni nikimaanisha kwenye Kata na Vijiji na wengi wao ni wale wazee wengine hata matumizi ya smartphone ni shida, mfano Watendaji wa Vijiji wale wa darasa la 7 , hata baadhi ya walimu hawajajua mfumo huu unavyofanya kazi.

Pamoja na changamoto lukuki kuhusu mfumo huu Serikali bado inachukua jukumu la kufungia mshahara wa Mtumishi wake aliyefanya kazi ofisini kwa siku 28 kisa TU hakujaza Sub Activity au Task na Sub Task kwenye mfumo kama kigezo cha upimaji , wakati kazini amehudhuria na amefanya kazi saa kiutumishi na muda mwingine amefanya kwa kupitiliza

Baadhi ya watumishi wanaangukia kwenye changamoto hii kutokana na Wakuu wao wa taasisi, mfano ikiwa Mkuu wa Idara/ Kitengo hakuwahi kukupa Role ama kwa kujisahau au kutokujua jinsi mfumo unavyofanya kazi maana yake mwezi husika hujafanya kazi kwa mwezi husika. Ikiwa hujaingia kwenye mfumo na huja submit sub task kwa Mkuu wako wa kazi unahesabika kuwa hujafanya kazi yoyote.

Pamoja kuwa Serikali ina nia nzuri kuleta huu mfumo isiwe kigezo cha kunyima watumishi mshahara kisa TU hawajapewa role na kujaza majukumu yao au kufanya tathimini kupitia mfumo huu.

Huu ni unyang'anyi usiotumia Silaha.

Baadhi ya Watumishi hao hao wamepanga wengine wanadaiwa kodi za nyumba.

Baadhi Watumishi hao wamefunga Kwaresima na Ramadhani wanahitaji kununua au kuwanunulia wazazi na ndugu zao chakula kwa ajili ya futari. Baadhi ya Watumishi maisha yao ni magumu hakuna mfano wanategemea huo mshahara kununua mahitaji muhimu Baadhi ya Watumishi wamekopa marejesho yanawasuburi.

Hii inaweza kuleta changamoto kwa baadhi ya Watumishi kuanza kuiba hasa kwa wakusanyaji wa mapato ya Serikali ikiwa ni kufidia mshahara wake aliozuiliwa na Serikali hivo kukosesha Serikali mapato.

Rai yangu
Serikali lipeni watumishi mshahara wa mwezi Machi, watumishi wengi watakaoumia sana sana ni wenye Mishahara ya chini.
 
Ukiachana na hayo yote uliyoaandika,kimsingi watumishi wengi tu wazembe sana,tuvitu vidogovidogo tu hadi tusukumwe sukumwe kama gari bovu hadi wananchi wanatudharau.

Huo mfumo ni mrahisi mnoo lakini nashindwa kuelewa hao laki100 kama ni kweli haiingii akilini wote wawe hawajapewa role na wakuu wao,hawawezi kuwa wengi hivyo.

Acha kila mmoja awajibike ktk eneo lake
 
Mkuu kuna ambao wanakimbilia kustaafu, hata kufungua smartphone hawajui, wengine wako chaka huko mtandao haupo tu akitaka kujaza lazima aende mjini.
 
We jamaa Acha kutetea uzembe.

Unataka miezi mingapi kujaza hizi forms, kitu cha madakika tu mnataka mbembelezweeeee.

Watumishi wa serekali ni wavivu fullstop. Mnafanya kazi kwa mazoea.

Eti ujambazi, yaani unaambiwa jaza majukumu yako hutaki na unaita ujambazi. Badilikeni nyie watu, dunia inaenda kasi sana hii. Acheni kulea ujinga na uzembe
 
Hizo bando za kila siku unatoa wapi ?
 
Naungana na wote wanaosema ni uzembe wa hao watumishi, kama kitu kidogo hvy unashindwa kutimiza utawezaje kutimiza majukumu yako ya kawaida.? Kama huwezi kuingia kwenye mfumo unashindwa vp kuomba msaada kwa wenzako.?
 
Kuna wazembe halaf kuna wale ambao wako porini huko kusiko na mtandao kabisa, shida ya huu mfumo ume assume kila mtu anaishi mjini. Hii ni moja ya weakness ya huu mfumo
 
Kuna wazembe halaf kuna wale ambao wako porini huko kusiko na mtandao kabisa, shida ya huu mfumo ume assume kila mtu anaishi mjini. Hii ni moja ya weakness ya huu mfumo
Kwahy watumishi wa shirika zima hamjaingia kwenye mfumo kisa mtandao hakuna.?
 
Kwahy watumishi wa shirika zima hamjaingia kwenye mfumo kisa mtandao hakuna.?
Not shure ninshirika gani unazungumzia coz sipo kwa gov, but kuna mashirika baadhi ya kada wako so remote, some itabid watolewe huko walipo waje kujazq, now sitaki kuyataja majina. But yes wamepews muda mrefu walitakiwa wawe wameshawafikia hata wale ambao wako interior
 
Umesema Kuna watumishi wapo porini ukimaanisha shirika lipo porini, ndo nauliza kwahy watumishi wote hawajatimiza wajibu wao kwenye huo mfumo.?
 
Back
Top Bottom