Tahadhari kwa watumiaji wa mfumo wa ESS (PEPMIS)

RAINEL LIHAWA

Member
Apr 14, 2015
33
30
Habari za majukumu viongozi?

Naomba tupeane angalizo hususan kuhusu huu mfumo wa PEPMIS.

Kumezuka utapeli mkubwa sana. Watumishi wanapigiwa simu wakitishiwa kuwa mfumo umewatema na hivyo mshahara wa mwezi Januari hawatapata na ili kulitatua hilo wanaombwa fedha.

Mwalimu mmojawapo ndani ya Halmashauri X amepigiwa. Tuchukue tahadhari kubwa.

PIA KITU KINGINE
Hii mifumo uwe nayo makini
Unashauliwa kutumia kwenye device zako tuu kwani mifumo hii ina taarifa zako nyeti.

Usikubali Kwa Kila mtu kumpa au kufanyia kazi kwenye device ya mtu mwingine.

Anaweza ona taarifa zako zote na asije akavuruga mambo huko.

Kama unahitaji msaada usijaribu kutoa check namba yako Kwa mtu usiemjua.

Baadae atakwambia umtumie na password yako. Usije fanya hivyo.

Nawatakia sherehe njema za kuuaga mwaka 2023 na kuupokea mwaka mwaka mpya wa 2024.

Mwenyezi Mungu akatujalie uwe ni mwaka wa kheri na mafanikio tele..
IMG-20231230-WA0007.jpg
 
Kwani ukishajisajili si kutakuwa na kuingia kwa User name na Password au?

Nafikiri muhimu ni kuset strong password na kuzikariri vizuri

Pia wasisahau "ku log out" baada ya kuingia kwny mfumo, hii ni kwa usalama wao pia
 
Back
Top Bottom