Tamisemi hamisheni taarifa za mishahara ya walimu waliopata uhamisho mwaka Jana mwezi wa kumi wanakwama kuingia katika mfumo wa PEPMIS

SAMFA

Member
Mar 5, 2023
10
18
Habari wadau. Watumishi tuliohama mwaka Jana mwezi wa kumi na kupata vibali hatujahamishiwa taarifa zetu za mshahara mpaka Leo, Hali ambayo imepelekea kushindwa kuingia katika mfumo wa upimaji wa utendaji kazi wq PEPMIS.

Tamisemi waliondoa access ya halmashauri kuhamisha mshahara jukumu wamejipa wao la kuhamisha mshahara ila mpaka Leo hawajahamisha mshahara hata wa mtumishi mmoja. Wahusika tunaomba mutusaidie
 
Poleni sana natumai ombi lenu litashughulikiwa sababu huu mfumo wa PEPMIS hata wao wanaohusika na kuwahamisha utawapima utendaji wao wa kazi, hivyo kuchelewa kuwahamisha ni kutoshughulikia wajibu wao wa kazi
 
Kama mshahara wako unapata bila kashikashi yoyote basi kuwa mvumilivu tu hilo swala lako litafanyiwa kazi ninaamini hilo, umepata uhamisho shukuru japo ni haki yako

Shida walimu kitu kidogo tu mnapenda kulalamika huwa hamuwez kujisimamia mpaka msimamiwe kama wale waliokaa sakafuni wanafunzi wakapewa Viti na Meza

Mpwayungu Village njoo huku Kuna dogo analeta ujuaji
 
Ofisi ya raisi utumishi imetoa barua kwenda kwa wakuregenzi wote na maafisa utumishi wote kuwa mtumishi ambaye hayupo kwenye mfumo wa PEPMIS mpaka tarehe 31/1/2024 hatapokea mshahara wa mwezi wa pili. Wakati wanatoa tangazo Hilo wanajua kabisa Kuna watumishi ambao wamehama wanapitia changamoto katika huo mfumo. Tamisemi ipo kimya haijatoka tamko lolote kwa watumishi wenye shida hii na hata wao utumishi hawajatoa muongozo wowote kwa maafisa wao. Hili jambo limekuwq dilemma wanataka watengeneze tatizo wao wenyewe ili baade wake kulitatua kwa kuchelewa
 
Back
Top Bottom