kichongeochuma
JF-Expert Member
- Jan 21, 2024
- 315
- 567
Nashindwa kuelewa hawa viongozi huwa wana tumia akili gani katika maamuzi yao.
Msidhani kila mtu anaishi mtumba hapo dodoma muwe mnafanya tafiti za kina kabla ya kuleta hiyo mifumo yenu kwanza.
Mfumo wenu unahitaji angalau 3G au H+ Internet speed ili angalau ufanye vizuri wakati huo kuna watumishi wapo vijijini huko ambako hadi leo wanapata internet yenye kasi ya GPRS na EDGE (hilo nina uhakika nalo na ushahidi ninao).
Msitumie ubabe kwenye hili mtatesa watumishi sana, mfumo bado una shida na si rafiki kwa mazingira yetu mnalazimisha nchi kuingia kwenye teknolojia ambazo ki msingi si rafiki kwa kwa aina ya watu na miundo mbinu kifupi hamjawaandaa watumiaji wala miundo mbinu.
Mtumishi ataesimamishiwa mshahara wake alio utumikia mwezi mzima kutokana na majukumu yake kwa mujibu wa makataba wake wa kazi kwa kisa hajajiunga na PEPMIS anione PM kwa masaada wa kisheria.