fogoh2
JF-Expert Member
- Apr 13, 2017
- 5,023
- 5,000
#HABARI Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amemuelekeza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Juma Mkomi kusimamisha mishahara ya viongozi walioshindwa kuwasimamia watumishi wao kujisajili na kujaza mipango kazi yao katika Mfumo wa Usimamizi wa Utendaji Kazi kwa Watumishi wa Umma na Taasisi za Umma (PEPMIS/PIPMIS) na kukwamisha utekelezaji wa zoezi hilo lenye masilahi mapana katika utumishi wa umma na taifa kwa ujumla.
Mhe. Simbachawene ametoa maelekezo hayo leo mkoani Iringa alipokuwa akizungumza na Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma Tanzania Bara wakati akifungua Baraza hilo.
Amesema ujenzi wa mfumo wa PEPMIS/PIPMIS pamoja na mifumo mingine ya TEHAMA ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amedhamiria kwa dhati kuwa na Serikali ya kidijitali itakayorahisisha utendaji kazi wa watumishi wa umma kwa lengo la kutoa huduma bora kwa wananchi.
Vilevile, amekemea tabia ya baadhi ya Waajiri kukataa kuwapokea watumishi wanaohamishiwa kwenye taasisi wanazoziongoza na baadhi kutoruhusu watumishi kuhama hata pale inapoelekezwa na Mamlaka kwani kwa kufanya hivyo ni ukosefu wa maadili na ni jambo ambalo halikubaliki.
Katibu Mkuu-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza hilo amesema elimu ya utekelezaji wa Mifumo ya TEHAMA ikiwemo Mfumo wa PEPMIS/PIPMIS na Mfumo wa Kubaini Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma (HR Assessment) imetolewa nchi nzima lakini kumekuwa na kutowajibika kwa baadhi ya viongozi katika kuwasimamia watumishi wao kutekeleza zoezi hilo.