Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 29,483
- 40,500
Kuna mzee mmoja nilikutana naye eneo moja la kazi miaka 12 iliyopita, na katika mazingira ya kazi tulikuwa tukiheshimiana sana, na tulikuwa tukiishi kama familia; leo tukale wapi au kunywa wapi, mara moja moja ilikuwa ni kitu cha kawaida.
Baada ya muda kupita aliamua kung’atuka na kwenda kujikita kwenye biashara zake katika mkoa mwingine.
Miezi miwili iliyopita, nilipata kasafari katika mkoa aliopo; nikaamua kumtafuta huyo mzee kwa njia ya simu, ili angalau niweze kuonana naye na tuweze kuzungumza mawili matatu; kama binadamu wanavyotakiwa kuishi.
Bahati nzuri, ilikuwa ni siku ya jumapili.
Mzee alifurahi sana, kupokea simu yangu na tukakumbushana mengi, na pia nikamwambia nipo hapa mkoani, naomba kama inawezekana angalau nije nikujulie hali.
Mzee akanijibu, samahani sana mambo yameingiliana, ndio najiandaa hapa kuelekea kwenye biashara yangu, kukagua mapato.
Alivyoniambia hivyo nikajiongeza na kumuambia, ‘’basi siku nyingine kama nafasi itapatikana, tutaonana tuombe uzima’’
Baada ya hapo nikasoma kitabu cha maandiko kama aya mbili hivi, ndipo nikahitimisha kwa kusema, maisha ya sasa hayahitaji kutembeleana kwa ajili ya kupiga stori; bali ni kutembeleana kwa malengo ya kwenda kupeana fursa za ‘win/win situation’
We una mtazamo gani?