Watoto 19 wafa kwenye disco la Idi Tabora

I am sory, i wish wangekuwa wameokoka, sasa unajua kwa imani yangu, mtu akifa wakati hajampokea Bwana, ndo moja kwa moja motoni, sasa, sisi tuliobaki, tupate fundisho kuwa, sikikuu za kimungu kama hizi sio sikukuu za kufanya maovu. poleni wafiwa.ila hata tukiomba Mungu azilaze mahali pema roho zao, hatafanya hivyo, ni kujilisha upepo tu.
 
Kwa hiyo unaomba vifo viongezeke? Huyu jamaa kweli kadata...

Mliofiwa poleni sana.

Achaneni na maneno maneno ya Masatu Wassira Kada Mpinzani. Mwanakijiji, endelea kufuatilia utujulishe hali za wagonjwa watoto waliolazwa hospitalini

Asha
 
Nashangaa kwanini mwenye ukumbi huo bado hajakamatwa na polisi mpaka sasa hivi. Yaani anathibitisha tu kutokea kwa tukio hilo halafu basi! Eti watoto waliwazidi nguvu walinzi!!!! Tangu lini watoto wakawa na nguvu kuliko baunsa? Hapo ni tamaa ya pesa tu ilitawala mpaka akajaza watoto wengi kuliko uwezo wa ukumbi.

Yale yale ya kusema dala dala halijai kwa kuwa sio ndoo ya maji...!!! Poor Tanzanians!!!
 
I am sory, i wish wangekuwa wameokoka, sasa unajua kwa imani yangu, mtu akifa wakati hajampokea Bwana, ndo moja kwa moja motoni, sasa, sisi tuliobaki, tupate fundisho kuwa, sikikuu za kimungu kama hizi sio sikukuu za kufanya maovu. poleni wafiwa.ila hata tukiomba Mungu azilaze mahali pema roho zao, hatafanya hivyo, ni kujilisha upepo tu.

Haya mambo ya baada ya kufa na kumpokea bwana we umeyatoa wapi... nadhani sii mahala pake...
 
Nashangaa kwanini mwenye ukumbi huo bado hajakamatwa na polisi mpaka sasa hivi. Yaani anathibitisha tu kutokea kwa tukio hilo halafu basi! Eti watoto waliwazidi nguvu walinzi!!!! Tangu lini watoto wakawa na nguvu kuliko baunsa? Hapo ni tamaa ya pesa tu ilitawala mpaka akajaza watoto wengi kuliko uwezo wa ukumbi.

Yale yale ya kusema dala dala halijai kwa kuwa sio ndoo ya maji...!!! Poor Tanzanians!!!

nakwambia ingekuwa ni wajumbe wa sisiem wamekufa ukumbini hapo, watu wote shinyanga wangetafutana wallah...
 
Wakurugenzi wa ukumbi wamekamatwa bado wanahojiana na tume itatoa taarifa leo kabla ya saa 9 mchana
 
Nashangaa kwanini mwenye ukumbi huo bado hajakamatwa na polisi mpaka sasa hivi. Yaani anathibitisha tu kutokea kwa tukio hilo halafu basi! Eti watoto waliwazidi nguvu walinzi!!!! Tangu lini watoto wakawa na nguvu kuliko baunsa? Hapo ni tamaa ya pesa tu ilitawala mpaka akajaza watoto wengi kuliko uwezo wa ukumbi.Yale yale ya kusema dala dala halijai kwa kuwa sio ndoo ya maji...!!! Poor Tanzanians!!!


...Na mimi ndio picha ninayopata hapo! Tamaa!
 
Habari hii inasikitisha. Mola awalaze marehemu pema peponi. Awape afya njema waliojeruhiwa.
Poleni wote mliofiwa.
 
katika hali isiyo ya kawaida ilikuwa majonzi makubwa katika mji wa tabora na vitongoji vyake jana baada ya vijana zaidi ya 19 kufariki dunia, mauti haya yaliwakuta watoto hawa baada ya kula chakula cha mchana na hivyo kwenda katika kile kinachoitwa Disco toto katika kumbi mbili maarufu hap mjini moja ikiitwa Bubbles na nyingine club Royal.

Kama inavyoeleweka haswa katika sherehe kubwa kama hii watoto hawa waliingia katika kumbi hizi hili kuanza kusakata mziki, lakini kibaya zaidi ni kuwa ukumbi ambao watoto hawa wamekutwa na mauti unaitwa Bubbles unaomilikiwa na mfanyabiashara mmoja mjini Tabora maarufu kwa jina la Manu Nshashi mwenye asili ya kiasia na mwingine unamilikiwa na bwana mmoja anaitwa POROJO na JAFARI amabao woote wanaishi kitongoji cha National mjini Tabora, kumbi hizi zoote zipo katika jengo la NSSF flat no 1,kama kumbi za mziki zilivyo kumbi hizi hazina AC badala yake wanatumia feni za panga na zile domestic small feni, katika tukio hilo watoto walijaa kumbi zoote jana na ndipo watoto walipokoswa hewa ya kutosha na matokeo yake wakaanza kuvuta hewa ya carbonmonoxide, hivyo watoto walipata Hypoxia na hivyo kufa kama kuku.

Kitu cha kusikitisha kumbi hizi zilijengwa kwa ajili ya mikutano na pation za ofisi lakini hata hivyo mabwana hawa walipoamua kufanya biashara ya kuwa kumbi za mziki wao waliweka sound proof tu kwani kumbi zipo katikati ya mji wa Tabora na chini yake kuna bank ya CRDB.kipindi chote hiki kwa tamaa na urafi wa kupata pesa za haraka haraka kumbi hizi zikichukua watu wengi si zaidi ya watu 100 lakini kwa siku ya jana kumbi hizi zilijaa watoto zaidi ya 500 kitu ambacho ilikuwa ni shida. katika kumbi kulikuwa na joto kubwa na kali sana kiasi kwamba watoto walianza kujinyea hovyo hovyo mbali na makelele ya watoto kuwa tunakufa DJ wa hizi kumbi walienderea kuweka miziki ya Bongo flavour ya kidato kimoja hadi mwisho watoto zaidi ya 100 walipoanguka chini ndo wakastuka na kuwasomba nje na baada ya hapo kukimbia bira hata kutoa tahalifa police.hadi jana walikufa watoto 19 na leo kuna mtoto mmoja kaongezeka na kufanya kuwa watoto 20 waliokutwa na mauti haya.

Ntawawapeni upfdate baadae kwani bado wengine wapo hosp ya mkoa maarufu kwa jina la Kitete Regional hosp.
 
Mwenye ukumbi na walinzi wake wanapaswa kushtakiwa kwa mauaji. Wenyewe wanajua uwezo waukumbi, ilikuwaje wawaachie watoto wengi waingie ndani? Kwamba watoto waliwazidi nguvu walinzi ni utetezi wa kitoto ambao unaweza kumfanya mtu acheke katikati ya majonsi haya. Ni matumaini yanghu kuwa taasisi husika zitachukua hatua zote stahili kwa wanaohusika wote
 
maskini, nilikuwa tabora wiki yote hii na leo niko njiani from tabora nilikotoka juzi, hali ya hewa ni joto kali mjini, mpaka nikawa najiuliza kulikoni tabora joto kuliko dsm? haingii akilini kuwa wamiliki hawa kama wapo tabora hawahisi joto hili hivyo kuwarundika watoto 500 kwenye chumba chenye feni tatu! haingii akilini kuwa jumba linalomilikiwa na wataalamu kama NSSF miaka yote hii wamefumbia macho jengo lao lilikusudiwa kama chumba cha mkutano wa watu wasiozidi 100, kubadilishwa na kuwa ukumbi wa disco kwa watoto 500!
haingilii akilini kuwa, wamiliki hawa hata baada ya watoto wetu kuanza ku-suffocate walilala mbele na kuacha mizoga ya watoto nyuma na wengine wakizirai

tumepoteza watoto wetu, kwa tamaa ya pesa, kwa uzembe, kwa ajali zinazoweza kuepukika, watoto wameteseka sana. najiuliza kwa nini haikuwa mimi na wenzangu, juzi usiku tulipokuwa tunatafuta mahali pa kwenda disco? baada yake tukaenda orion tabora hotel? kwa nini haikuwa wewe au yule? lakini ikatokea kwa watoto hawa, bila shaka ni wale niliwaona wakiwa kwenye madrsa au wakitembea kwenye mitaa ya tabora wiki hiyo nilikuwa pale.

hakika, Mungu amechagua ua lilo bora bustanini mwake, nalo ni hawa watoto wetu.LITUKUZWE JINA LA BWANA, JINA KUU KUPITA YOTE-AMINA
 
Wahindi tena,
Kwa Tabora kujaza watu kama Karanga nilishasema. Niliandika jinsi tulivyojazwa ndani ya basi na tukapangwa na kusindiliwa. Hiyo ni kitu cha kawaida kwa Tabora. Ule mkoa ulivyo nyuma ni kuwa uko nyuma kwa kila kitu. Hawa jamaa watapata matatizo tu kwa sababu eneo la National ndiko wanakaa Vigogo wa Tabora. Sintashangaa kusikia watoto wa Vigogo wengi tu walikuwemo. Jii ingelikuwa imetokea sijui Isevya au huko vichochoroni au ndani ya Basi sijui Shakira au Sabena, hakuna kitu kingelitokea na nafikiri hata wasingeliandika. Na kwa sababu mkoa uko nyuma kwa kila kitu, sintashangaa hata SHERIA kuchukua mkondo wake ikashindikana maana hata kwa hilo TUKO NYUMA. Vilafi hawa wameuwa Wadogo zangu. It's good for them.
Mungu awape mapumziko mema na kuwafariji wafiwa.
 
Yes nilihahidi kuja na update za msiba za watoto hawa 20 waliopoteza maisha yao jana, hadi mchana huu wazazi na walezi ikiwa ni pamoja na ndugu na jamaa wa watoto hawa wamekubaliana kuchukua maiti za watoto hawa nakwenda kuwazika kila mmjoja kwani kuna matabaka ya udini.

Likin nirudi katika issue yenyewe ingawa jana watoto hawa walifikishwa katika hospital ya mkoa wa Tabora Kitete lakini bado hosp hii haina madakatari wala Nurses wa kutosha, hata hivyo bado vitu kama oxygen concentrator na oxygen sylinder kwa ajili ya emergency preparedness bado ni shida katika taasisi muhimu kama hii amabayo ni lifesaving kuna haja ya kuweka nakufanya jitihada za kutafuta staff wa kutosha hosp hii. najua wana JF hamuwezi kuamini hosp hii inao madaktari qualified kwa maana ya MD sio zaidi ya 2, na sasa inatumia madaktari wa kichini amabao wamekuja kwa muda je hawa mabwana wakiondoka itakuwaje. kwa siku ya jana ilikuwa ni mshikemshike kwani watoto baada ya kufikishwa Kitete tulitegemea wale majeruhi wangewekwa katika oxygen kwani ndo ilikuwa shida kwa watoto hawa lakini ilifanyika huduma kama ile ya huduma ya kwanza kwa kupetapeta watoto hawa kwa nguo, sidhani kuwa hii ni sahihi kwa chombo kama hiki kutumia nguo na kanga kuanza kupungia watoto au mtu aliyekoswa hewa.

Kwa ujumla hosp ya mkoa wa Tabora bado inahitaji mabadiriko mengi kwa nyanja zoote kwani bado huduma pale zinalegalega sana.

Ndugu zangu wana JF najua serikari ya mkoa itaunda tume lakini pia tungeoomba tume hii iwe huru na itoe haki na si kama tume ambazo tumezoea miaka yooote kutoa tahalifa isiyo nzuli.
 
Ukifunga shuruti unapofungua usifungulie kila kitu unamchukiza mwenyezi Mungu.
 
Kufunga si kuahirisha mambo ya kidunia bali mwezi wa toba. Basi kuna haja gani ya kufanya toba ikiwa unajua fika utarudia kosa? Jamani hebu tufike mahala na kugundua kuwa mabaya yote ni ya shetani kwani ni wake. Hapa shetwani aliona mwezi mzima amewakosa na sasa mmerudi kwa kasi ya ajabu ili awapate moja kwa moja akawaua miili ili wafe dhambini na kuwa wake katika moto wa milele pamoja. Ni fundisho they say whenever there is a a change of power few heads must go! Scrutinise JFs
 
Kikwete mourns Tabora disco victims
Daily News; Thursday,October 02, 2008 @15:21


PRESIDENT Jakaya Kikwete has sent his condolences to the families of 19 children who died in a discotheque when celebrating Idd el Fitr in Tabora on Wednesday.

The President has also called for a thorough investigation into the matter and stern measures taken against all those involved.

Police in the region said today that six other children are hospitalized, two of them in critical condition, following the incident.

The owner of the club, Mr Shashi Patel, has been arrested as police continue with investigations.

The Minister for Labour, Employment and Youth Development, Prof Juma Kapuya, said that the president has given 500,000/- to each one of the families of victims of tragedy, the worst in the country’s history.

Prof Kapuya said that President Kikwete has received with profound shock the children’s death that occurred at around 6:30 pm at Bubbles Night Club.

Tabora acting Regional Police Commander, Mr Daudi Siasi, said that the children suffocated after the club was overheated due to poor ventilation.

Temperatures in tabora has been recorded at over 33 degrees Centigrade. The children who perished were aged between 7 and 15 years.

Among others, the Uyui District medical Officer, Dr Makelele lost two children in the tragedy. His wife passed away three weeks ago.

The National Social Security Fund (NSSF), owners of the building that housed the club, have also promised to give 500,000/- to the families of each of the children that died in the tragedy, and 100,000/- to the families of the injured children.

Tabora regional authorities have given each family of the deceased children 50,000/- and the go ahead for the families to bury their dead.

Mr Siasi named those who died in the incident as Veronica Manigu (7), Beatrice Makelele (14), Jacob Gerald (12), Salma Hamis (12), Khadija Waziri (13), Rehema Moto (14), Selemani Iddi (11), Mrisho Seklemani (10), Abdallah Rehani (14) and Agatha manigu (12).

Others are Paulina Emmanuel (11), Mohammed Kapaya (15), Ramla Yenga (15), Habiba Shabani (15), Donald Kasera (12), Mwanahamisi Waziri (11), Philipo Haule (11), Ashura Jacob (12) and Yasini Rashidi (11).

The injured are Msimu Rehani (14), Tatu Amani (15), Kulwa Iddi (12), Sakina Alli (10) who was discharged and later returned to hospital, Jumanne Abdulla whose age was not established and Naomi Joseph (13) who are in critical condition.
My Take:
This is big, this is huge, this is absolutely insane. I'm so maad. Huu sasa ni uhuni. Hii ni mamilioni ya fedha za adhabu. NSSF na mabilioni waliiyonayo wanatoa Shs. 500,000 Really (yaani dola 500 hivi). Hivi watanzania wanajua kiasi kilichotumika kwenye utalii wao juzi New York? Kweli ndio thamani ya watoto wetu hii na ndiyo dalili ya uchungu?

You know what this reminds me of? Kesi ya Ditopile na jinsi wakuu walivyoanza kujitokea na kutoa pole na rambirambi.. tegemea the same Tabora.
 
My Take:
This is big, this is huge, this is absolutely insane. I'm so maad. Huu sasa ni uhuni. Hii ni mamilioni ya fedha za adhabu. NSSF na mabilioni waliiyonayo wanatoa Shs. 500,000 Really (yaani dola 500 hivi). Hivi watanzania wanajua kiasi kilichotumika kwenye utalii wao juzi New York? Kweli ndio thamani ya watoto wetu hii na ndiyo dalili ya uchungu?

You know what this reminds me of? Kesi ya Ditopile na jinsi wakuu walivyoanza kujitokea na kutoa pole na rambirambi.. tegemea the same Tabora.

JF counsels must open up case against the owner and NSSF for the families of the deceased to be compensated handsomely.

But though, money can not replace the lost life. Some of these kids would have been the Sittas and the Lipumba!

Asha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom