duh.. tatizo ni watu hawajaangalia the issue at hand na badala yake wajanja wachache wakawa "lets get Mwanakijiji".. they missed the whole severity of the tragedy. Hili ni kubwa kweli. Mara karibu nne mwaka huu mabweni kadhaa ya watoto wa kike yamenusurika kuchomwa moto; hatukujifunza kwenye vifo vya Shauritanga, na nawahakikishia hatutajifunza kutoka hili kwani baada ya muda si mrefu (within hours) ule wimbo usio na kibwagizo wa "mapenzi ya Mungu" utaanza kuimbwa na wananchi wataitikia kama maroboti "yatimilike".
Tukianza kuchambua tukio hili tutaambiwa waacheni marehemu wapumzike jamani, kifo ni kifo. Tutaambiwa na watetezi wa uzembe na waamini wa kutokuwajibika kuwa tusimlaumu mtu, taasisi, au chombo chochote kwani "Bwana ametoa, na bwana ametwaa".
Nakataa rasmi wimbo huo, na waimbe wao waliolaaniwa wao na uzao wao na malipo yao yawe humu humu duniani!