Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,848
- 12,082
Siku chache baada ya The United Kingdoms of Afrika (UKOA) kupitia kwa Dr. Moses Katega “Prince Katega II” Na Dr. Fadhili Emily Kabujanja “Mfalme Dr. Fadhili” kuandika barua na kuiwasilisha Ubalozi wa Ujerumani Nchini Tanzania wakidai kulipwa fidia kwa kilichotokea wakati wa Ukoloni, Esther Mkemanzi kutoka Ngome ya Falme ya Kyamutwara, Bukoba Mkoani Kagera ametoa ushauri juu ya mchakato huo.
Katika maelezo yao, UKOA walieleza kuwa Barua hiyo ni Notisi ya kutaka kufungua mashtaka ya kudai fidia kwa makosa ya mauaji ya halaiki ya watu wenye asili ya Kabila la Wamatumbi, Wapogoro, Wazaramo, Wangindo, Wanguni, Wangarambe na Makabila mengine katika Vita ya Majimaji (1905- 1907).
Esther Mkemanzi amesema kuwa tayari Serikali inafanya mchakato huo wa mazungumzo na Serikali ya Ujerumani ambao nao tayari wameonesha mwitikio mzuri wa kushiriki katika mazingumzo ya fidia.
“Wanatakiwa kufuata taratibu, mazungumzo yanaendelea, ndio maana Rais wa Ujerumani alifika hadi kwenye makaburi ya baadhi ya mashujaa wetu, akaomba radhi, pia itambulike Serikali ya Ujerumani haidili na mtu mmoja mmoja, inazungumza na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya suala hilo,” amesema Mkemanzi.
kutoka familia ya ngome ya Kyamutwara Bukoba, Ameshauri waliopeleka barua ya kulipwa fidia na serikali ya Ujerumani kufata taratibu za wizara husika kwani jambo hilo serikali imekwisha anza mchakato mda mrefu .
Pia soma - Wawasilisha Barua Ubalozi wa Ujerumani wakitaka walipwe fidia kutokana na Babu na Bibi zao kuteswa wakati wa Ukoloni.