Inaitwa "Colonal crime", msamaha hautoshi, Ujerumani ilipe fidia

Bashir Yakub

Member
May 27, 2013
84
1,562
Bashir Yakub, WAKILI
+255 714 047 241.

Hakutembelea Makumbusho ya Vita ya Majamaji bali alitembelea makumbusho ya Uhalifu wa Kikoloni.

Hivi ndivyo inavyoitwa duniani, ni uhalifu wa Kikoloni "Colonial Crimes'. Na hivihivi tumwambie mgeni wetu Rais wa Shirikisho la Ujerumani kuwa hayo ni Makumbusho ya Uhalifu wa Kikoloni.

KUHUSU FIDIA.

KENYA, waathirika 5,228 wa MauMau wamelipwa kiasi cha Euro Milioni 19.9 kwa uhalifu waliofanyiwa na serikali ya Uingereza kipindi cha ukoloni ikiwemo mauaji miaka ya 1950's..

Familia za waathirika zilipokea kiasi hicho baada ya mvutano mkubwa kupitia Waziri wa Mambo ya Nje iliyoongozwa na William Hague.

ALGERIA, mwaka 2022 serikali ya Ufaransa ilikubali kuwalipa askari wenye asili ya Algeria 21,273 maarufu kama "Harkis" ambao iliwatumia kupigana vita kipindi cha ukoloni 1954 - 1962.

NEW ZEALAND, serikali ya uingereza ililazimika kulilipa kabila la Ngati Haua kiasi cha Dola 13.5Milioni ambao ndio wenye wa asili New Zealand kwa kuharibu tu utamaduni wao na kuwaletea utamaduni mpya 1850's walipokuja kama wakoloni.

CANADA, serikali ya Canada ililazimika kulipa kiasi cha Dola za Marekani 31.5Bilioni kutokana na unyanyasaji na ubaguzi uliofanywa kwa wenyeji wa ardhi hiyo kutoka wageni waliongia humo kama wakoloni .

NAMIBIA, serikali hii hii ya Ujerumani imekubali kulipa kiasi cha Euro 1.1Bilioni kwa watu wa jamii ya Waherero na Wanama wa Namibia kwa mauaji waliyofanya kwa watu wa jamiii hizo 1904 - 1908.

Kipindi hicho Namibia ilikuwa ikiitwa German South West Africa. Ndugu wa waathirika wamelipwa na hii hii serikali ya Ujerumani inayoongozwa na mgeni wetu.

Mifano ya waliolipwa kwa matukio ya kikoloni ni mingi.

MAJIMAJI TANZANIA
Inakadiriwa watu 75,000 - 300,000 walifariki katika vita hiyo 1905 - 1907 wakati huo Tanzania ikiwa katika mataifa yaliyojulikana kama German East Africa.

Walioua idadi hii ya watu si wengine bali ni Wajerumani, yakiwemo hayo makaburi mawili ya watu 67 walionyongwa ambayo rais wa Ujerumani ametembelea.

MBALI NA MAUAJI.

Mbali mauaji hayo ya halaiki Wajerumani walitesa watu, walibaka, waliiba mali ikiwemo madini vito nk., walifanya udhalilishaji mfano kuchapa watu viboko wakiwa uchi, walitumikisha bila ujira, waliharibu tamaduni, na mwisho walipora vitu muhimu(ill gotten artefacts) na kuondoka navyo kwenda kuviweka kwenye makumbusho yao Berlin na kwingine ambavyo vinatumika katika utalii huku vikiendelea kuwaingizia mamilioni ya dola hadi hivi leo tunapopata ugeni wa Rais wa Ujerumani.

Ilikuwa ni machungu na mateso ni basi tu haikugusa miili yetu tukajua ni namna gani wazee hawa walipitia madhila.

HII INAWEZA KUISHIA KWENYE MSAMAHA ?.

Hapana haiwezekani. Hata kama sio leo au kesho lakini haiwezi kuishia kwenye msamaha.

Na ni kwanini isiwe leo. Kwanini huu usiwe mda wa kujadiliana na mgeni wetu kuhisu hili.

Kuna tofauri gani waliofanyiwa hawa waliolipwa fidia na yaliyofanywa kwa hawa wa kwetu. Hakika madhila ni yaleyale.

Ujerumani ilipe fidia. Iilipe Tanzania au izilipe familia za wahanga. Familia hizi zipo ni suala la kuamua kuzitafuta.

Kadhalika irejeshe haraka mali zote ilizopora ambazo zinatumika kwenye makumbusho yao kujipatia fedha kwa njia isiyo halali.

Lakini kwani haya yanaweza kufanyika bila sisi kuyasukuma ?. Hapana haiwezekani. Lazima tuanze sisi kuyasukima.

Hao wote waliolipwa fidia walianza wao kusukuma hii ajenda. Mkoloni hawezi kujikumbusha kukulipa fidia. Wewe uliyeumia ndo unatakiwa uanze.

TUNAWEZA KUANZA VIPI.

Tuunde tume. Wote ambao wamelipwa walikuwa na tume. Na sio lazima iundwe na serikali bali hata familia au koo za wahanga wanaweza kufanya hivyo.
Lakini ni bora zaidi tume ikiwa ya serikali.

Tume itafanya tathmini ya uharibifu maalum na wa jumla kuhusu tukio zima. Itatupa takwimu ya hasara ya mali, utu, na maisha(lives).

Baada ya hapo utaratibu wa kawaida wa kisheria wa madai utaanza kwa njia ya kuwaandikia barua/taarifa ya madai(demand notes) kama njia kuanzisha hii safari ya madai.

Taarifa itapewa serikali ya Ujerimani kupitia balozi zake ambapo watapewa siku za kutekeleza madai.

Wakishindwa ama wasipoonesha mwelekeo hatua nyingine za kisheria zaweza kufuatwa.

Mashirika ya haki za binadamu yaalikwe na yawe bega kwa bega katika hii safari Hili ni lazima lifanyike na hata hivyo tumechelewa.

KUOMBA MSAMAHA HAKUTOSHI.

Rais wa Ujerumani ameomba msamaha lakini haitoshi. Msamaha ni uwajibikaji wa kimaadili( moral responsibility) na sasa anatakiwa afanye uwajibikaji wa kisheria( legal responsibility).Uwajibikaji kisheria ni kulipa fidia.

Ukoloni wa Ujerumani ulikuwa ni Uhalifu wa Kimataifa(international colonial.crime).
 
Mi naona ule msamaa wa mamaa kwa mboe kupitia kichaka Cha maridhiano hautoshi

Chama na serikali ilipaswa ilipe fidia zote za waliouwawa,kupotezana na kulemazwa kwa Kisingizio Cha kubaqia madarakani
 
CCM imewafanya Watanzania kuwa wanyongewanyonge hata kwenye mambo ya msingi yanayoweza kuwafuta machunga.
 
crime ipi? mbona watawala wa kiafrika hata samia, magufuli to mention but a few wanafanya hayo hayo aliyokuwa akiyafanya mjerumani. Sheria, muundo wa serikali ni huo huo wa kikoloni, sasa crime inatoka wapi? Makonda amefanya hayo hayo na wakampandisha cheo, Kingai? Niliweka thread kuongelea jambo hilo hapa imefutwa Maxence Melo
 
Kama naviona vile vitukuu vya kinje kitile ngwale vitakavyojitokeza kwa wingi. 😂
 
Serekali ikiweza ianzishe majadiliano hayo na ilipwe fedha ambazo zitasaidia miradi muhimu, tukianzisha suala la waathirika walipwe, maana yake tumekaribisha upigaji na 98% ya hizo fedha zitakwenda kwenye mikono isiyo sahihi, hii ndiyo Tanzania bana!
 
"Yaliyopita si ndwele,tugange yajayo"
Mwisho wa kunukuu......
 
Back
Top Bottom