Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,813
- 11,991
Mratibu wa Miradi ya Ushirikiano kati ya Benki ya Dunia na TARURA, Eng. Humphrey Kanyenye amezungumzia kinachoendelea kuhusu mchakato wa mradi wa Uendelezaji wa Bonde la Mto Msimbazi Jijini Dar es Salaam.
Anasema “Tulianza zoezi la maandalizi ya Mradi huo muda kidogo na ili mchakato ukamilike kulihitajika kuhamisha watu kwenye eneo la bonde, tumefanya zoezi hilo kwa ufanisi tangu Mwaka 2022, tulipata watu takribani 2,592 ambao ndio walikuwa waathirika.
“Kati ya hao tuliofanikiwa kuwapata na kuingiza taarifa zao kwenye Daftari la Fidia na kupata ruhusa ya Serikali walikuwa ni watu 2,329, kati ya hao waliolipwa mpaka sasa ni 2,102.
“Sababu ya waliosalia 227 kutolipwa zipo kadhaa ikiwemo migogoro ya Kifamilia wameshindwa kukamilisha taratibu za ndani za miradhi na wapo ambao hawakujitokeza tena.
“Pia kuna watu 184 ambao waligoma kulipwa kutokana na kiwango ambacho tulikionesha kwao wakidai fidia ni ndogo, hivyo hawakusaini, wengine 186 hatukuwafikia kutokana na mazingira, kuna sehemu watoa tathimini hawakufika maeneo husika na wengine walifika kwenye nyumba lakini hawakukuta wahusika.
“Kuanzia Jumatatu ya wiki hii (Februari 5, 2024) mchakato umeanza kwa wale wengine ambao hawakupatikana kulipwa fidia, tunategemea hadi mwisho wa Februari Daftari litakuwa limemfikia Mthamini Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kuendelea na malipo.”
Waliogomea
Timu inafanya kazi kwa ajili ya kukamilisha Daftari ili limfikie Mtathimini Mkuu wa Serikali.
Ikumbukwe kuwa kwenye Mradi huo hatujalipa ardhi kwa kuwa hiyo seheu Wananchi hawakupaswa kujenga, Rais aliamua kwa wale waathirika (wenye nyumba) walipwe Shilingi Milioni 4 kila mmoja kama kifuta jasho na waweze kupata sehemu nyingine.”
Amesema malipo hayo yanatarajiwa kuanza kuingia leo Februari 7, 2024 na kuwa wahusika wametakiwa kubomoa wenyewe nyumba zao ili kuokoa baadhi ya vitu na mali zao.
Amesema "Watakaoshindwa kubomoa wenyewe sisi tutanza kulitekeleza zoezi hili ndani ya wiki mbili zijazo."
Pia, soma: TAMISEMI mbona mnachelewa kufidia watu wa bonde la mto Msimbazi?
View: https://youtu.be/fl0VTMZPULo?si=-0Rrmdj4B3yUS8OI