Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,989
Kupitia taarifa yao waliyoiwasilisha ‘public’ wameeleza kuwa wamechukua hatua hiyo kwa niaba ya Watanzania 700,000.
Barua yao kwenda kwa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani, wamemtaarifu Balozi kuwa madhumuni yao ni kutaka kwenda katika Vyombo vya Kisheria kwa makosa uliyoyatenda wakati wa ukoloni, hivyo wanataka kufungua mashtaka ya kudai fidia.
Wameeleza kuwa Barua hiyo ni Notisi ya kutaka kufungua mashtaka ya kudai fidia kwa makosa ya mauaji ya halaiki ya watu wenye asili ya Kabila la Wamatumbi, Wapogoro, Wazaramo, Wangindo, Wanguni, Wangarambe na Makabila mengine katika Vita ya Majimaji (1905- 1907).
Soma barua kamili chini...
RAIS WA UJERUMANI ALICHOSEMA OKTOBA 2023
Oktoba 2023, Rais wa Shirikisho la Ujerumani, Dkt. Frank Walter Steinmeier alifanya ziara Nchini ikiwemo kukutana na mwenyeji wake, Rais Samia Sululu Hassan katika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuzungumzia kuhusu kumbukumbu ya Vita ya Majimaji iliyotokea Mwaka 1905 – 1907.
Kiongozi huyo alisema, “Ziara hii nimeiweka katika kuangalia yale yaliyotokea wakati wa Ukoloni na pia kuonana na waathiriwa wa Vita ya Majimaji, kuzungumza na wahanga wa vita hiyo, najua walipitia kipindi kigumu ambacho si cha kupendeza, nitakayozungumza nayo nitayafikisha Ujerumani na ikiwezekana kuangalia namna ya kurusisha mabaki ya watu waliopigana vita.”
Tafsiri ya Barua hiyo upande wa Lugha ya Kingereza