Watanzania wanaotaka Ujerumani walipe fidia ya Ukoloni waambiwa wafuate utaratibu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,988

Siku chache baada ya The United Kingdoms of Afrika (UKOA) kupitia kwa Dr. Moses Katega “Prince Katega II” Na Dr. Fadhili Emily Kabujanja “Mfalme Dr. Fadhili” kuandika barua na kuiwasilisha Ubalozi wa Ujerumani Nchini Tanzania wakidai kulipwa fidia kwa kilichotokea wakati wa Ukoloni, Esther Mkemanzi kutoka Ngome ya Falme ya Kyamutwara, Bukoba Mkoani Kagera ametoa ushauri juu ya mchakato huo.

Katika maelezo yao, UKOA walieleza kuwa Barua hiyo ni Notisi ya kutaka kufungua mashtaka ya kudai fidia kwa makosa ya mauaji ya halaiki ya watu wenye asili ya Kabila la Wamatumbi, Wapogoro, Wazaramo, Wangindo, Wanguni, Wangarambe na Makabila mengine katika Vita ya Majimaji (1905- 1907).

Esther Mkemanzi amesema kuwa tayari Serikali inafanya mchakato huo wa mazungumzo na Serikali ya Ujerumani ambao nao tayari wameonesha mwitikio mzuri wa kushiriki katika mazingumzo ya fidia.

“Wanatakiwa kufuata taratibu, mazungumzo yanaendelea, ndio maana Rais wa Ujerumani alifika hadi kwenye makaburi ya baadhi ya mashujaa wetu, akaomba radhi, pia itambulike Serikali ya Ujerumani haidili na mtu mmoja mmoja, inazungumza na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya suala hilo,” amesema Mkemanzi.

kutoka familia ya ngome ya Kyamutwara Bukoba, Ameshauri waliopeleka barua ya kulipwa fidia na serikali ya Ujerumani kufata taratibu za wizara husika kwani jambo hilo serikali imekwisha anza mchakato mda mrefu .

Pia soma - Wawasilisha Barua Ubalozi wa Ujerumani wakitaka walipwe fidia kutokana na Babu na Bibi zao kuteswa wakati wa Ukoloni.
 
binafsi sijaelewa Wajerumani walipe fidia kwa lipi? kwa kujenga reli ambayo tunaitumia mpaka leo? kwa kujenga bandari ya dar na tanga ambazo tunazitumia mpaka leo hii? kwa kuufanya mlima kilimanjaro hata uweze kupandika na mpaka leo hii tunautumia kwa utalii ? kwa kuchora ramani za mipango miji nchi nzima? walipe fidia kwa kuleta mazao kama mahindi, viazi, mchele au matunda kama machungwa na mapeas? walipe fidia kwa kuleta meli kama liemba ambayo ndiyo meli pekee inayohudumia ziwa tanganyika?

mimi nafikiri sisi ndiyo tulipe fidia kwani hakuna kitu mjerumani alipata isipokuwa aliwekeza sana tu bila ya return yoyote kwani alikuta pori …
 
Back
Top Bottom