Watanzania tuelezwe ni wapi alipo Rais wetu Mpendwa John Magufuli, ni haki yetu kujua

Status
Not open for further replies.

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
UPDATE:

Fuatilia LIVE coverage hapa:

Ikulu: Rais Magufuli awaapisha viongozi walioteuliwa. Mathias Kabunduguru, Godfrey Mweli na Ali Sakila

==========

Heshima kwenu wakuu,
Heshima kwenu wakuu,

Kuna habari zinasambaa kwamba Rais wa Tanzania John Magufuli anaumwa wengine wanasema amekatiza Ziara huko Kusini ili kushughulikia Masuala mengine ya Kitaifa. Hili sina tatizo nalo.

Kinachoniumiza na kunitatiza ni kuona Taasisi ya Rais akiwemo Msemaji Mkuu wa Ikulu na Msemaji wa Serikali kutokanusha au kuweka sawa habari hizi zinazosambaa na kuacha watu waendelee kumsema vibaya Rais wetu. Ukiacha uongo ukaendelea kuongelewa unageuka kuwa kweli.

President_Magufuli.jpg


Rais sio mali ya Ikulu bali ni mali ya Watanzania wote wa vyama vyote, dini zote, rangi zote na Makabila yote.

Msemaji wa Ikulu, Gerson Msigwa huwa ni mwepesi kukanusha na kutupa update za Rais. Ajitafakari kwa hili kama vipi ajiuzulu tu. Kazi imemshinda ya kuwatumikia Watanzania.

Tunapata wakati mgumu kuelewa.

Kama anaumwa sio jambo la kushtua pia kwani maradhi kwa binadamu ni kawaida, kama anaumwa ni haki wananchi wake wakajulishwa na maendeleo yake yakaelezwa kwa uwazi.

Tumefanya hivyo kwa Baba wa Taifa Nyerere, Askofu Mkuu Mwandamizi Yuda Thadeus Ruwa'ichi, Benjamin Mkapa, Kikwete alipoumwa Tezi dume akiwa Rais na wengine wengi.


Rais Kikwete afanyiwa upasuaji wa tezi dume Marekani, hali yake inaendelea vyema


Kama yu mzima wa afya tujulishwe ili roho zetu zitulie.

Ni haki yetu kujua Rais alipo na maendeleo yake sababu anaishi kwa kodi zetu na tulimchagua wenyewe ndio maana Televisheni ya Yaifa inamuonesha popote aendapo bure ili wananchi wajue anachofanya Rais wao.

Hata kama kapumzika Ikulu, hakuna sababu ya kuzua taharuki.

Tunajua Rais wetu anapenda mpira hasa timu ya Taifa, Jana timu yetu imeshinda na kufuzu Michuano ya CHAN, hatujaona anapongeza na kushangilia kama kawaida yake.

Hata Msemaji wa Ikulu hajatuma picha akiangalia mpira wa watoto wake kama kawaida yao.

Tunamtaka Rais wetu.

Asanteni sana

TUJIKUMBUSHE;

"Taifa Stars wameipa heshima nchi yetu. Leo nimeona mpira, sio ule wa siku za nyuma."- Rais Dkt Magufuli akifurahia Tanzania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika #AFCON2019

 
Anamaanisha nini huyu ndugu na haya mafumbo yake, hata Zitto nae simwelewi leo kapost picha ya mama Samia, sijui hata
Screenshot_20191018-145408~2.jpeg

Mamaaaa mamaaaa mamaaaaa ! Mamaaaa huyo mamaaaaa mamaaa huyooo mamaaa huyooo! Nyambafuuuu - haya isiraeli maliza kazi tujimwage majiani sasa kushangilia kama Diatta kafuga goli yaani

Yaani katika topic nilimuelewaga sana mwalimu wangu wa biology mama Matimbwa pale Mkwawa ni jinsi hii kitu inafanya kazi. Basi tu sikuwa dokta

Najisikia raha sana kusoma ibara ya 37(5) ya katibu yetu tukufu ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Najimwambafai sanaaaa yaani kuisoma - eeeh Mungu wa Isaka na Yakobo na iwe kama mapenzi yako yatakavyo..

tapatalk_1571453901191.jpeg
 
Vyovyote itakavyokuwa lazima mama anahusika. Ni samia? Wote hatujui hebu fuatana nami kufuatilia 'senema' hii hadi mwisho. Tafadhali usihame kitini kwako na ikiwezekana usihamishe chaneli kutoka kwenye kuibiwa kompyuta hadi kwingine. Tumalizie igizo hili hadi mwisho.

Nakutakia uangalizi mwema kabisa.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom