hii hoja imekuja wakati muafaka kwa sababu juzi rais karume akiongea kwenye maadhimisho ya mwaka mmoja tangu aanze second term alichokoza hoja mbili
moja alisema kuwa zanzibar kujiunga na OIC kama sehemu ya muungano ni priority.
mbili alisema kuna wazee waliofurahishwa na uongozi wake wameenda kumuomba abadili katiba aendelee kutawala[yaleyale ya salmin] ila yeye anasema amewakatalia.
turudi kwenye OIC sioni faida ya maana ya kiuchumi waliyopata mosambique [ambao pia wamedandia commongwealthy] na uganda.hatukubali kuvunja katiba kwa ajili ya vimisaada mbuzi,afterall nchi yetu ni tajiri so hatuwezi kuuza uhuru wetu wa imani ,utajiri wetu ukisimamiwa vema hata hiyo world bank itatusikia tu,hata hivyo mashirika ambayo tu wanachama kwa sasa yanatosha na wala hayakwazi sehemu ya wananchi wetu.
kuhusu VATICAN ni nchi na ni mwanachama wa UN kama iran ,kenya,china ets n wanawakilishwa sehemu kubwa duniani kama nchi,chini ya papa ambaye ndio head of state ,so waislamu pia wakitaka wanaweza kuungana kidunia wakaamua nchi ya kiislamu ambayo wataamua kiongozi wake atambulike kama kiongozi wa waislamu duniani,kama nchi haiwezekani wachague kiongozi wa waislamu duniani ,apewe heshima,mbona waanglikana .budha,dalai lama,ismailia ets wana viongozi wao wanaotambulika kidunia ,,sasa kama wameshindwa kukubaliana whos in charge ,ndio vatican isiwepo
so hoja ya vatican ni hoja ya upofu,na kwa kifupi OIC sio muarubaini wa matatizo yetu sanasana tutalemaa kama watu wazima wenye mikono wanaouza uhuru wao kwa kujipanga mbele ya maduka ya watu wapewe pesa za bure kila ijumaa,wengine na nguvu zao ,sasa mnataka kutupanga mbele ya OIC Tungojee kutwa kugawiwa bure,tutaendelea kulemaa kwa uvivu,,,
tuchape kazi na kama kukopa tukope world bank na nchi rafiki na tulipe na riba ,,tatizo liko wapi kama kweli tunataka maendeleo,,mbona na mikopo mingine tumesamehewa baada ya kuonyesha juhudi kulipa,,inawezekana tufanye kazi!!!!!!!!!