BWANA PHILEMONI
Unajua baada ya kusom majibu yako kwa kirefu nimeweza kuuunganisha mambo ambayo ni kiini cha mjadala huuu na naweza kusema haya mambo ni naTANO nayo ni; la kwanza ni MUUNGANO la pili ni ZANZIBAR tatu ni OIC nne ni NYERERE na tano ni UDINI
Unajua hatuwezi kuenda mbele bila kuangalia huko nyuma kulitokea mazingira gani yaliyopelekea kutokea kwa conspiracy hizi 2006
Huwezi kuzungumzia ya Zanzibar kujiunga na OIC bila kuangalia huyo Nyerer ambaye japo ni mfu lakini ana IMPACT ndani ya chama tawala...in otherwords wanaogopa kufanya maamuzi kwa sababu mwalimu asingelipenda hilo na naweza kusema kuwa they are right
Halikadhalika hata kama ungekuja na hoja ya namna gani on how innocent NYERERE alikuwa kuhusu huu muungano huwezi kuwaconvnce watu wa visiswani ambao ni 99% waislam MWALIMU na serikali zilizofuata zilikuwa na nia nzuri nao mfano ni pale punde tu baada ya uhuru Kilichofuata kilikuwa ni kukamatwa, kuwekwa kizuizini na kuhamishwa kwa masheikh na Waislamu wengine waliodhaniwa kuwa wanapinga utawala wa Nyerere.
Mashuhuri miongoni mwao walikuwa: Abdillah Schneider Plantan, Sheikh Abdulkarim Abdulwahid, Maalim Popo Saleh, Suleiman Masudi Mnonji, Ali Migeyo, Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Sharff Hussein Badawiy, Shariff Mwinyibaba na Shariff Adnan ,Rajab Kiguu cha Mbuzi na wengine wengi.
sasa unajua sitotaka kuipeleka hii topiki katika mabaya ya Mwalimu na Mchango wake katika hili ila nitaangalia zaidi upande wa KATIBA YA ZANZIBAR ambako ndiko tunaangalia hoja zinaendaje
Bwana PHILEMONI,Ukweli uko wazi, kiini cha tatizo hili la sasa kuhusu Zanzibar na katiba yao ni ukiukwaji uliofanywa makusudi, wa kutokutekeleza vizuri vifungu vitatu muhimu vya mkataba wa muungano wa mwaka 1964.
1. Kutokutekelezwa kwa kifungu namba (m)(b) kilichotaka kuwepo na taasisi za makamu wawili wa Rais ambapo mmoja kati yao aliye mkazi wa Zanzibar ndio anakuwa kiongozi wa Serikali ya Zanzibar na msaidizi mkuu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika utekelezaji wa kazi za kiserikali kwa upande wa Zanzibar.
2. Kutokutekelezwa kwa kifungu namba (vii)(b) kilichomtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa kukubaliana na Makamu wa Rais ambaye ni kiongozi wa Serikali ya Zanzibar, kuitisha baraza la kutunga katiba likiwa na wawakilishi kutoka Tanganyika na Zanzibar katika kipindi cha mwaka mmoja tokea kuanza kwa muungano kwa madhumuni ya kutafakari mapendekezo ya tume ya katiba na kupitisha katiba ya Jamhuri ya Muungano
3. Kutokutekelezwa kwa kifungu namba (viii) kilichotaka mkataba wa muungano kuthibitishwa kwa kutungiwa sheria na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi la Jamhuri la Jamhuri ya watu wa Zanzibar kwa kushirikiana na Baraza lake la Mawaziri na mkataba kupitishwa na kuundwa kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano na ya Zanzibar kwa kufuata masharti yaliyokubaliwa.
Bunge la Tanganyika lilitunga sheria ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Namba 22 ya 1964, Baraza la Mapinduzi la Jamuhuri ya watu wa Zanzibar kwa kushirikiana na baraza lake la mawazi halikutunga sheria iliyotakiwa.
Hii ndio hali halisi ya muungano wetu, japokuwa tulizotaja hapo juu ni baadhi ya dosari nyingi zilizopo.
Huu si wakati wa kuendelea kukwepa ukweli, watu wa kulaumiwa katika hali hii ya kisiasa tuliyonayo sasa ni wale waliochangia au kusababisha kuwepo kwa hali hii ya utata kati ya katiba ya nchi na sera za chama, hali inayoonyesha jinsi dhamira zinazodaiwa kuwa ndizo zilizozaa muungano zilivyokuwa za bandia.
Nidhahiri sasa kuwa waasisi wa muungano tunaotakiwa kuulinda kwa gharama zozote kama ulivyo, kila mmoja alikuwa na sababu nyingine za ziada zilizomfanya aukubali muungano tofuati na ile iliyotajwa ya kudumisha udugu wa asili uliopo kati ya Tanganyika na Zanzibar.
Hali tuliyokuwa nayo ya mfumo wa chama kimoja cha siasa wakati wa utawala wa Awamu ya Kwanza, haikuruhusu wala haikutoa fursa kwa wananchi kuweza kufahamu ukweli au jambo lolote kuhusu muungano, ilikuwa ni mwiko wa kisiasa kuutaja muungano kwa kuudodosa.
Mambo yaliyowapata wananchi wenzetu waliokuwa viongozi wa juu kabisa katika serikali ya Zanzibar, Alhaj Aboud Jumbe na Maalim Seif Shariff Hamad kwa kuonyesha dalili tu za kutaka dosari zilizojitokeza katika muungano wetu ziondoshwe, sote tunazijua. WatanzAnia wote tukalazimishwa kukumbatia bomu lililokwisha washwa utambi huku hatufahamu ni lini litalipuka kisa Kumuenzi Mwalimu ambaye alikuwa hana nia nzuri nawaislamna zanzibar kujiunga na OIC.
Vile vile mwaka 1992 Mheshimiwa Jaji, sasa ni Mstaafu Francis Nyalali alieleza wazi katika ripoti yake kuwa muundo wa Serikali mbili una matatizo mwengi, muundo muafaka ni wa serikali tatu. Vigogo walipokutana Chimwaga wakasema hapana, Jaji Kisanga nae kama utakumbuka alirudia yale yale katika ripoti yake, nae pia aliameambiwa hapana sera za Chama Cha Mapinduzi hazibadiliki
Inashangaza leo kusikia mtu akisema kuwa upo uwezekano wa usultani kurudishwa Zanzibar wanataka kurekebisha katiba yao ili kumuwezesha rais wa Zanzibar, wanaemchagua kwa kura zao, kuwa na vipindi zaidi ya viwili atamshi ya aina hii ni ya watu waliofilisika kifikra ambao wanadhani wananchi wote ni wajinga.
Katika mkutano, Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi uliofanyika Dodoma, chama kilipitsha azimio kwamba suala la Urais wa Zanzibar na katiba likajadiliwe katika vikao vya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar. Je unajua kuwa wananchi walihoji ni lini Kadinali na wanasheria wa Chuo Kikuu na Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi wa Tanganyika walipewa mamlaka ya kutengua maamuzi ya mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
Na kama si hivyo, hizi chuki za wazi zinazoonyeshwa dhidi ya wananchi wa Zanzibar na Rais wao sababu yake nini? Haya mayowe tunayoyasikia kila kukicha ni kwa niaba na maslahi ya nani? Na kama watadai kuwa wanatumia haki yao ya msingi kama raia katika kutoa maoni kuhusu mambo ya nchi, ni lini wananchi wa Zanzibar - walinyang'anywa haki hiyo ili wasiwe na uwezo wa kufanyia marekebisho katiba ya nchi yao, pale wanapoona inafaa.
Ni kawaida ya wakati kuwa ndio muamuzi wa kweli na huu ni wakati wa ukweli na uwazi, kwa hivyo ni wakati muafaka kuachana na tabia mbaya tunayotaka kurithi ya kuendesha nchi kwa ngonjera, Propaganda za magazeti na vitisho.
Viongozi waache hofu. Kinachotakiwa kufanywa ni kuilea demokrasia inayoanza kukua kwa faida na maendeleo ya nchi yetu na mojawapo kuaruhusu waZanzibari kujiunga na jumuia ambazo wanaona zitakuwa na mafufaa wao kama OIC