Wasi Wasi wa Udini

Status
Not open for further replies.
Mzee ES
Well said kuhusu Mkandara kule maoni. Now I have a home, TEF.
 
Sam,
Mzee ES hakujibu kitu isipokuwa katumia hasira kwa kujibiwa vibaya na baadhi ya wachangiaji. Kweli navyojua Mzee ES hawezi kusimama pale watu wanatoa matusi, sio uungwana lakini nae awe msikivu kama wengine tunavyo msikiliza yeye.
Hii mada imekwisha na imekwisha kwa sababu ukweli umetoka na namshukuru sana Mzee mwanakijiji kwani hapakuwepo sababu ya kufika huku.
Hata hivyo imekwisha kwa sababu nyote mmegundua kwamba wakristu ndio wengi ngazi za juu. Kama kweli nyie hamkuwa wadini nadhani mungeweka swali hili mbele.. Kwa nini wakristu ni wengi ktk ngazi za juu serikalini?.... kwa nini kusiwepo uwiano kama mlivyodai.
Hivyo basi, mimi nasema niliyajua haya longtime isipokuwa naamini kwamba UWEZO wa mtu ndio kigezo cha ajira na sio dini ya mtu...
Ubaguzi wa South Afrika ulichosha kwa sababu ajira zilitazamwa kwa rangi zake. Na hata leo hii wanazidi kufanikiwa kuondoa tofauti hizi sio kwa kuhakikisha weusi wanapata kazi isipokuwa weusi wanapata nafasi za kusoma na uwezo wa kushindana ktk kupata nafasi za kazi. Advantage moja anayokuwa nayo mweusi South ni Uzawa kwa hiyo ktk Elimu utawakuta weusi wengi vyuoni kuliko wenye rangi nyinginezo!.
 
Rufiji,

Kosa linalojitokeza ni kusema serikali ni watu. Kuna watu serikalini, lakini sio sahihi kusema serikali ni watu. Serikali ni jumuisho la taasisi zinazoundwa kwa ajili ya utawala wa jamii. Kuna watu kwenye hizo taasisi. Taasisi zenyewe ni za utendaji, utungaji sheria na mahakama.

Sio raia wote wako serikalini. Unaposikia mtu akisema serikali ni wewe ujue anatumia lugha ya kuhamasisha watoto. Sio kweli kwamba wewe ni serikali. Kuna watu wako serikalini, na wana dini zao, lakini serikali haina dini. Hakimu ana dini, mahakama haina dini. Wabunge wana dini, bunge halina dini. Mawaziri wana dini, cabinet hana dini.

Mwishowe naomba niwakumbushe wote kwamba nafasi ambazo sio za kisiasa hazipashwi kujazwa kwa kutumia siasa. Ukitaka kuchagua Injinia Mkuu wa Wizara ya Maji, unatangaza hiyo nafasi, na kila anayependa anatuma ombi lake. Kamati inakaa na kuchukua mwenye sifa kuliko wote, bila kuangalia dini, kabila au jinsia.

Tusipoteze lengo kwa kuanza kubishana kwamba nafasi zote zijazwe kwa uwiano. Hapana, ni nafasi za kisiasa tu.

Augustine Moshi
 
Rufiji
Let assume Watu = 0
Calculate Serikali.
Hint.
Serikali = Watu X Tasisi
Simple math.


Moshi
Pamoja na tasisi mbali mbali pia raia pia wanaunda serikali. Anyway, maana ya maneno huwa yanatolewa na binadamu. Nakuomba tu ukae na definition zako na mimi nikae na zangu.
Kama nikipewa mamlaka ya kubalisha ule upuuzi kwenye katiba unaolezea maana ya serikali, nitaweka maneno matatu tu. SERIKALI NI WATU. Hii ndiyo inawafanya watanzania wawe na hofu kuiondoa CCM madarakani kwani wanajua ukiiondoa CCM madarakani basi unaondoa serikali. For GOD sake, unakuwa umewaondoa viongozi na sera zao tu. That's all. Serikali inabaki pale pale.

Mkandara
Let us assume JK hakutumia udini kwenye kuteua wale mabalozi. Now, tell me in your own words, unakubaliana na ule uteuzi au la. Kama unakubaliana nao tupe sababu.
Again, let us assume the stasts kuwa watu wenye majina ya kikristo ni wengi kwenye uongozi wa serikali. Kitendo cha JK kuchagua mabalozi 6 ni upendeleo kwa waislamu kama wanawake ili wawe na idadi sawa na watu wa dini nyingine au ni modern jihad. Kama siyo udini ni nini? Tueleze tusiojua mambo mapya kwenye dunia hii tufunge midomo yetu.
Also, let us assume viongozi waliopita wamechangia kuwa na idadi ndogo wa wailamu kwenye uongozi. Are we now applying Newton's third law of motion? "For every action, there is an equal and opposite reaction."
Kuhusu kwa nini viongozi wengi wa serikali ni wakristo, I do not want to say anyting watu watakuwa offended.
 
Mkandara,

Ninahitaji ku-clear my name samahani kwa wanabodi kwa kuwaingilia,

Kwanza hakuna aliyenijibu kwa hasira kule maoni my new permanent home, wala aliyenitukana if anything kuna mtu aliyeniomba radhi kama hakunijibu kistaarabu,

Kule maoni hakuna matusi kwa hiyo nipo permanent, na sikumjibu yoyote hata wewe kwa hasira, nimekujibu kama nilivyokujibu kwenye mada ya Salim, humu TEF kuwa ninakubali kutokubaliana, unless kama hiyo inaaashiria hasira then yes!

Sio lazima nisikilize hewa au NONESENSE!, HAPANA ninaingia kwenye forum kujifunza in the process kufundisha, sasa sitaki kuendelea kuwa mjinga kwa kusikiliza ujinga ili nionekane nimo kwenye crowd, msimamo wangu toka nimeingia siku ya kwanza kwenye forum BCS unaeleweka na kila mtu humu, moja ni moja kwangu haiwezi kuwa mbili,

Nimejifunza mambo mengi ambayo nilikuwa siyajui humu kwenye hizi forum, na kila siku ninaendelea kujifunza, na siku zote huwa sijiingizi kwenye nisiyoyajua, mambo ya personal attacks niliamua kuachana nayo baada ya BCS sasa sina nafasi nayo, wachangiaji wanapoandika mambo muhimu ninajifunza kila siku,

lakini sio rais wa nchi yangu anapochagua viongozi 12, wa dini yake ya Kiisilamu, eti nikiuliza basi sipendi kusikiliza kama wengine wanaonisikiliza NO! Halafu huyu rais atafanya nini next tukinyamaza? I am sorry bro,

huyu rais Kikwete must stop now huu ujinga, asifikiri tunampenda kiasi hicho kwamba akisema ruka basi tuwe tunauliza urefu gani, huyu mtu anaanza kutuchukulia wabongo for granted, sasa ni lazima tusimame tuhesabiwe, forget about history, some of us tulikuwa hatujazaliwa wakati Mwalimu anachagua wakristo, Rwanda walikuwa hawajauana!


Kwa hiyo hatumpi kiongozi yoyote free pass ya kutupandisha mkenge halafu tuje kuwaambia watoto na wajukuu wetu nini? kuwa tulimuona yule rais Kikwete akianza lakini hatukujua kuwa atatufikisha kwenye kuuwana, haitatokea on our watch ninasema hivi kwa sababu salaam zimeshafika Ikulu tayari, tena asifanye mchezo kwenye hili na mtu yoyote asifanye mchezo na hili, benki wauze sawa, viwanda wabinafsishe wagawane hela sawa,

lakini tuachie bongo yetu na umasikini wetu na amani yetu, hata kama ina unafiki mwingi lakini ni amani ambayo haipo Afrika nzima, kwenye hili hakuna kulala,

Wasalam na samahani kwa wanabodi wote!
 
Mzee Es,
Mimi sina beef na maoni yako na wala hayawezi kubadilisha kitu kwa mwenye macho. Na kumbuka kwamba hata wewe unaweza kusema swala likaonekana NONSENSE kwao sio iwe wewe tu mjuzi wa kufikiri. Nitarudia kusema kwamba unafanya hasira na hazina kificho kwa sababu hupendi mtu aseme unachosema wewe ni nonsense ila wanachosema wengine. Hili neno kama unapenda kulitumia basi nawe kuwa MUWAZI kukubali linapotumika kwako na hawa jamaa. Na nakuomba unielewe kwamba sisemi unayoandika ni nonsense isipokuwa huna points nzito za kuhalalisha udhanifu unaojenga fikra hizi za udini.

Sam,
Kwanza tafsiri yako imefunga mada hii. Na ikiwa mtu haelewi unachosema hapa basi hawezi kuona deep ndani ya swala hili.
Lets say, JK hakutumia dini kuwa kielelezo cha uchaguzi wake jibu lake rahisi sana. Hawa watu wanafaa kazi ile...
Mkapa alipoingia mwaka 1995 alibadilisha sekretarieti alitangaza mara moja kusitisha uhai wa sekretarieti ya CCM (Miwnyi) wakati huo chini ya Katibu Mkuu - Bw. Lawlence Ghama na kuweka yake mpya. Kwangu binafsi that was a political move kuweka watu waliokuwa upande wake bila kujali dini zao. Kisha Mkapa huyu huyu aliondoa sheria ya kuajiriwa maisha ndani ya chama na kuweka miaka mitano tu. Which was a good move kwa chama chao na ilitakiwa kila mwajiriwa lazima atume application kwa nafasi zake. Aliyofanya JK is the same na hakubadilisha sheria isipokuwa watu. Ikiwa waislaam ndio wanamuunga mkono zaidi ndani ya CCM (mtandao) basi huko CCM kumeisha ingia udini, mnachotakiwa kutueleza sisi ni huo udini ndani ya CCM. Nadhani tutakuwa wazi kukubaliana kwamba tabaka hizi za mitandao zinaongozwa na dini.
Kuhusu Uteuzi wa Mabalozi, JK kawaondoa mabalozi wengine ni waislaam tena wa mkeka na kuweka hao. Mtu kama Mapuri ambaye ambaye alikuwa ktk sekretarieti ya Mkapa kaondolewa huko na kupewa Ubalozi China kwa sababu Mapuri ndani ya Chama alikuwa mtu wa Mkapa.
Hakuna kificho kwamba kuna beef kati ya JK na Mkapa kama tulivyoelezwa na Mzee Es ingawa sioo wazi na ukiangalia swala la balozi wa Italy hili swala lilizungumziwa long time na Mkapa alijua kinachoendelea huko Rome. Soma blog hii ya mshikaji utapata picha kamili http://kurunzi.blogspot.com/

Na kama kweli JK anatumia udini basi angevuruga Viongozi wote wa ngazi za juu serikalini na mabalozi kwa sababu hawa ndio wawakilishi wa nchi nzima ktk taasisi zote.
Mwisho, umeniuliza kama sasa tuna apply Newton's third law of motion. No brother, labda hukusoma vizuri maelezo yangu. Mimi najaribu kufuata nyayo zenu kimawazo. Yaani kama anavyosema Mzee ES hataki kuona makosa yakitendeka leo, kesho iwe kazi kuwaeleza wajukuu. Je, ikiwa dhana yako ni potovu utawambia watoto wako pia makosa yako. Vigumu sana binadamu kula mavi yake mwenyewe na ndicho mnachofanya hapa. Ikiwa waislaam wengi JK ajihadhali lakini ukweli ni wakristu wengi afanye nini? hili ndilo swali langu kwenu. Binafsi nimesema niliyaona yote haya toka mwanzo na sikuyaona kama udini na kunahitajika marekebisho.
Haya sio mageni na ushahidi wenyewe mumeuweka wazi hali ilikuwa ikijulikana hivyo toka awali. Kwa nini msifanye kutafuta ukweli kabla hamjashutumu. Na pia kwa nini msichukulie kuwa uchaguzi ni political move ambayo JK mwenyewe lazima ashauriwe na watu wake (Mtandao) isipokuwa dini.
What does he gain?..ikiwa nchi yetu haina udini!.. Je, yeye mjinga kiasi ambacho anafahamu Pengo na wakristu wanatazama kila move zake. Udini tunao sisi mshikaji hilo kubali...na sisi ndio tutakao karibisha vita vya kidini. Kumbuka mchungaji wa Rwanda ambaye alitangaza redioni kuanzisha mauaji ya Watusi wote huyu hakuwa kiongozi wa serikali bali mchungaji tu na kachagua kabila lake.
 
Mkandara ,

Kwanza nitumie nafasi hii kukushukuru kwa maelezo yako , ila nina swali moja tuu hili deal la kununua hilo jengo huko Rome JK akuhusishwa ? Manake kama sikosei yeye ndio alikuwa waziri wakati huo ! Na kama alikuwa anajua nini kinaendelea kwa nini aku-act kipindi hicho ili kuliondolea taifa hasara ? Tena mimi naona wizara ya mambo ya nje ndio ya kulaumiwa sana kwani wao ndio walikuwa incharge wa hilo deal Rais anachofanya ni kusaini tuu mkataba.
 
Jamani kwani waislam ni asilimia ngapi na wakristu ni asilimia ngapi?

mnataka idadi sawa au uwiano? au yale yale ya Muungano wa Tanzania bara na Visiwani! 37 mili na 1 milioni?

Mimi maoni yangu ni kuwa Rais aangalie Uwezo wa mtu kwanza na suala la udini baadaye na hili linahitaji tu Busara kwa nchi kama yetu!


Rais akiweka mbele ushabiki wa kidini utamrudi yeye tena mapema tu!

Inagawaje bado ninaamini mtu mwenye akili timamu tena Rais wa nchi kama Tanzania hawezi kuchagua watu kwa kufuta dini zao. Ninaogopa hata kuchangia kwenye hii mada! Labda tumpe muda kwanza!

Kama nilivyosikia kuwa taarifa iko IKULU, it means message sent labda ndiyo maana ameteuwa wakuu wa mikoa wawili wote wakristu!

Pia Mwema amepangua safu yake!
 
Mkandara,

Sio lazima nisikilize point zako na sio lazima usikilize za kwangu, hapa sio mahali pa PR au kutaufta umaarufu, hapa ni mahali pa kujadili kero za wananchi, sasa kero zinazidiana umuhimu,

Ninasema hili la dini sijali ni nani anahusika, lakini hakuna free pass msimamo kwenye hili ni kwamba Kikwete must stop now, amepewa nchi ina amani, maelezo yako na ya wengi kuhusu hii issue ya yeye kuchagua vioingozi 12 Waisilamu hAYATOSHI na ninayo haki ya kuyaktaaa maoni yenu kama mlivyo na haki ya kukataa yangu,

kwenye hili Mkandara you can say all you want, ninasema sina mpango wa kuwa mkimbizi katika maisha yangu, nimefanya mengi behind hii issue kuhakikisha rais anapata ujumbe, na nina uhakika umefika kwani tayari nimeona response,

In the future cha muhimu ni kuweka tu maoni yako, na watu wataweka ya kwao lakini usiseme fulani ameandika kwa hasira na mwingine ameandika kwa furaha, uless wewe ni mtaalamu wa kuwasoma watu hata usipowaona, halafu sina mpango wa kusikiliza NONESENSE, na ninapoweka NONESENSE ninaomba watu wasisikilize,

ila ninawaomba watu wasikubali ujinga ili waonekane wamo, hata kama umesemwa na mimi, na wala sijawahi kusema mimi ndie mtaalamu ninayejua kila kitu, hapana, lakini siwezi kukaa pembeni kuona nchi yangu inataka kupelekwa kwenye ujinga, tusije tukaacha shughuli zetu muhimu kwenda kuandamana kupinga vikatuni vilivyochorwa na mjinga mmoja huko Ulaya! Rais aache huu mchezo tena sasa!
 
Mzee ES
Karibu hapa nyumbani kwangu. Nakutakia kila raheri na kile kijiwe upambane na akina Frank.
Mkandara
Siasa zako ni za vijiweni sana, Toka lini Mapuri akawa mtu wa Mkapa? Mapuri ameondolewa kwenye uongozi CCM kwa sababu ya ushauri aliyopewa JK. Hivi ulitegemea Mapuri aendelee kuwa Katibu mwenezi wa CCM wakati vyombo vyote vya habari vilikuwa haviandiki upuuzi wowote anaosema? Au hata hili hujui? Mapuri hakustahili kupewa ubalozi hana sifa hizo. Wale mabalozi wote sita hawana sifa hizo za ubalozi.
Na hilo beef la Mkapa na JK ni mambo ya mitaani tu. JK alikuwa na beef na watu ambao hawakum-support kwenye mipango yake ya kugombania urais lakini kwa sasa amejifunza hana beef na mtu yoyote ila ana mapungufu kwenye uongozi ambao bado anajifunza kama tukinyamaza basi tusitarajie mabadiliko yoyote, kama tukiendelea hivi hivi kwa "kukazana" kusema basi tutegeme kuwa JK atakuwa rais mzuri sana baada ya miaka michache kama anayafanyia kazi maoni ya watu. I am sorry sijalizika na majibu yako lakini hey it's all good. Just one more question for you, kama Mkapa alifanya makosa fulani ya uongozi, JK akifanya hivyo hivyo basi hayo siyo makosa? Principles of equilibrium.
Na yale mambo uliyoandika maoni yanahitaji maelezo. Hivi hao watu JK aliyowasafisha ni wakina nani? Kigoda pamoja na kwamba siyo waziri yeye ndiye aliyesaidia kuandaa bajeti. Achana na mambo ya magazeti, hauna kiongozi anayemuogopa JK. HAKUNA. Mkapa ndiyo alikuwa ana udikteta na alikuwa hana rafiki. Huyo Sumaye mwenyewe anashukuru Mungu muda umeisha, alikuwa anatukanwa kama mtoto mdogo. Watu wote walituingiza kwanye mkenge wa mikataba feki kuanzia Ngasongwa mpaka Chenge wote wanadunda na utajiri wao. Huyo Balozi wa Italy amefukuzwa kazi kwa sababu alikula hizo hela yeye tofauti na mabalozi wengine ambao walikubali dili. Hebu chunguza toka 2000 mpaka 2005 ni balozi ngapi zimefanyiwa marekebisho hewa? Please Mkandara let us keep standard ya kijiwe kwa kutoandika Mapuri ni mtu wa Mkapa.
 
Mzee Sam,

Nimekusikia mkuu, lengo lilikuwa kuwapa nafasi na wengine wapumue naona limefanikiwa, kwetu sisi sasa ni kuiona njia ya ku-exit hizi forum kwa ujumla maana kazi illiisha na BCS, yaliyobaki ni mazungumzo baada ya habari!

Nakutakia mafanikio na kijiwe chako bro!
 
Sam,

Hali yako, naona nawe umekuja juu nadhani takuwa bora ukizungumza hoja zako kulingana na mada hii sidhani kama mimi ndiye nimekuwa mada yenyewe. Nimewajibu kila swali lakini nyie mnakwepa na kutafuta sehemu za kuongeza maswali tu.
Kuhusu Mapuri nitauliza hivi? ikiwa JK kachagua sekretarieti yake mnasema ni hawa ni waislaam - watu wake. Inakuwaje Mkapa kumchagua Mapuri sio mtu wake hali mtu huyu anafahamu vema kwamba nafasi hiyo lazima awe mtu wako?.
Pili, Kazi yake ilikuwa katibu mwenezi na ikiwa kama vyombo vya habari havikuandika upuuzi wake hali viliandika upuuzi wakati wa Mkapa, Je huoni kama kuna hila hapa toka magazetini. Na imekuwaje wewe umefahamu huo upuuzi hali vyombo vya habari havikuandika...Ni upuuzi upi huo na data hizi umezipata wapi? au ndio kupitia vijiwe vyenu, yaleyale unaandika ya vijiweni lakini huoni kundu lako ila la Mkandara.

Ikiwa Mapuri hafai kuwa balozi naomba tena utupe sifa za balozi. Umekwepa swali hili toka mwanzo na bado unarudisha.
JK na Mkapa wamekuwa na beef ya utawala toka uchaguzi na mzee Es katueleza mengi sana ambayo sikuona hata sehemu moja wewe ukipinga. wapo watu waliopinga sana lakini sii wewe. Pili hata swala la balozi linajulikana na watu wote kwani JK alipoleta mbele ya Mkapa aliambiwa - Hii sii kazi yako. Hii ina maana ilijulikana mapema kwamba amekula zile fedha na hakushughulikiwa kwa sababu Mkapa mwenyewe alikuwemo ktk kila hatua ya deal hilo. Rudia tena kutazama na kusoma vizuri hiyo tovuti upate kuelewa mengi nadhani umenusanusa tu.
Sam,
Sijasema kwamba Mkapa alifanya makosa, hili ni lenu kwa mtazamo wenu. Binafsi nakubali na Uchaguzi wa Mkapa kwa sababu hao watu waliweza kutetea dira yake hata kama mimi sikukubaliana nayo. Ameuza malizetu sio kwa sababu ni mkristu ila kwa sababu hakuwa kiongozi bora. Kwa maana hii nasema hata Hitler aliwachagua watu ambao wanaweza kuendesha shughuli zake. Now, nikirudi kwa JK ikiwa kweli JK anataka kuleta Udini na hii ndiyo dalili yake basi kazaneni kuhakikisha anaondoka mapema kabla haijawa nchi ya kiislaam. Maneno matupu hayavunji mfupa na kuuliza hutapata jibu ng'oo.

Mzee Es, labda kwa kumaliza hoja nadhani huwezi kubadilisha kitu. ndio imetoka hiyo na bado watachaguliwa wengi. Wee jikate hakuna noma mshikaji sisi tunaendelea kudunda kama zamani! Na labda itakuwa bora sana mkijikata maanake inaonyesha hakuna mpya.
 
Mkandara
Mapuri ni mpuuzi, sijaona neno jingine lenye heshima kama hilo. Kabla sijaendelea naomba usiniusishe na uteuzi wa CCM, hayo ni mambo ya chama mimi sihusiki huko, wakimteua Mapuri kuwa mwenyekiti wa CCM mimi siko huko ni jukumu ya wanachama, mimi wanaouniusu ni viongozi wa serikali yetu tukufu. Narudia tena, Mapuri ni mpuuzi. Kitendo cha kufagilia wale wanamagereza kupiga raia na waandishi wa habari hakina maelezo ndiyo hasa sababu ya vyombo vya habari kuacha kuandika kitu chochote kilichokuwa kinatoka mdomoni mwake.
Toka uhuru tumekuwa tuna utaratibu wetu wa kuwapa watu ubalozi ambao hawastahili, sifa moja kubwa ya balozi ni kwamba awe na knowledge ya foreign affairs na relations between countries to countries. Watu wanasomea International Relations for years kwa nini wapewe wendawazimu? Nina mfano wa balazo wa kweli kama Dr. Mahiga anayetuwakilisha UN, he has PhD in International Relations na anaiweza kazi. Mapuri ana nini? mwalimu JKN tunaweza kumsamehe kwa sababu alikuwa hana watu wa kutosha, kuanzia Mwinyi hadi JK hana sababu ya kufanya hivyo. Nenda pale foreign ukaangalia watu wangapi wenye elimu zao wanasubiri safari. Give me a break Mkandara. Mapuri and co. NO.
Kuhusu beef ya JK na BWM kuna mambo mengi yalisemwa. Mimi siyo wewe ambaye ukiambiwa JK ni mdini kesho yake unaanza kumtetea wakati kuna uwezekano anao. Mzee ES alipokuwa anatoa data zake nilikuwa namsikiliza nisingeweza kubisha tu wakati sina ushahidi ,mambo aliyokuwa anasema yalikuwa hayaonyeshi kama kuna beef ila ilikuwa zinaonekana na kwamba kila mmoja alikuwa analinda personal interests. Angekuwa ana beef naye asingeweza kumpa ndege ya serikali aende nayo kokote anakotaka.
Rufuji
Hayo mambo ya Zenji yananitia kichefuchefu, hivi kumbe hela yetu ya kodi na ile 40% itatumika kulipia viongozi wa dini. Mungu tusaidie huu muungano ufe. Hawa wa bara tutapambana nao. Hapo ndipo utaona kuna kitu kinaendelea, pengine hata hawa wa bara wanalipwa na serikali. Wakituonyesha dalili kama hizi lazima tuseme udini ufe na serikali isiwe na dini.
Mzee ES
Hapa ndipo nimefika, nitakazana mpaka nihakikisehe TEF imefika kiwango cha BCS. Kuna watu wengi wana mawazo mazuri tu humu ila naona wengi wamekata tamaa kwa mambo yanavyoendeshwa nyumbani lakini halali mtu. You are party of the family tutakuenzi hivyo na hakuna atakayetuyumbisha.
 
Mkandara,

Mwenye macho haambiwi aone, finally rangi yako imetokea tena very clear, kwamba umesimamia wapi kwenye masuala ya dini,

message imefika IKULU, na rais amefahamishwa jinsi mbunge wetu mmoja alivyoaibishwa majuzi pale JFK, kwa sababu ya kuwa na jina la Abdallah!

Alivuliwa mpaka chupi pamoja na kuwa na pass ya diplomatic, tulipowauliza wamarekani, wakasema nyinyi Watanzania si mliandamana kuhusu Taliban, this is what you get back!

Mungu Aibariki Bongo, na Amani Yetu tusije tukaacha kazi kwa sababu ya vikatuni!
 
sam said:
Mzee ES
Hapa ndipo nimefika, nitakazana mpaka nihakikisehe TEF imefika kiwango cha BCS. Kuna watu wengi wana mawazo mazuri tu humu ila naona wengi wamekata tamaa kwa mambo yanavyoendeshwa nyumbani lakini halali mtu. You are party of the family tutakuenzi hivyo na hakuna atakayetuyumbisha.

:) Na mimi nakusupport!
 
TuTsis against HUuts,luosagainst Gikuyus,Lan'gos againstA Cholis Wakristo against waislam ,light skin againstdark skin,Africans what is our real problem,...wither africa??????????what's going on guys?have we lost our focus?.This topic real annoyed me ,i'm sick of us looking to one another based on somebod's faith.
peace!!!!!!
Willo
 
Willo
The reasoning mind can not work under any form of favoritism.
 
Mzee Sam & Fillga,

Heshima mbele, ahadi tumeisikia sasa matendo na ninawaahidi kuwa you have my support at anytime, na hasa mzee Sam usije ukaruhusu watu wakawadanganya wengine, BCS ilijengwa kwa nguzo moja tu ya one way,

either unakubali au unakataa, lakini sio hadithi nyingi za kutaka kuwa politically correct mbele ya jamii, NO! Malumbano ni lazima yawe honest na ikibidi provocative, ili kuleta ukweli,

BCS ndiyo iliyokuwa chanzo cha mwisho wa Mahita, alijaribu kila njia kutuma watu waharibu mada lakini wapi, akakwama, ndio anayo mapesa ya wizi, lakini hakuna heshima! Ni kwa sababu ya makelele ya wananchi, ninasema hivyo ili asije mtu akasema kuwa mnapoteza muda bure kusema maovu hapa ya serikali na viongozi wake,

Malumbano lazima yalenge viongozi personally, maana ni uwezo wao mdogo kikazi na kuongoza ndio maana as a nation tumekwama, hotuba za Mwalimu ni clear na kama zingefuatwa kikamilifu tungekuwa mbali, tena sana kama China, Mzee Sam ukweli ni ukweli, moja ni moja haiwezi kuwa mbili, heshima na jamii inakuja kutokana na ukweli, regardless ya how much mawe utarushiwa, hakuna negotiations mbele ya ukweli, wala eti kukubalika na watu, hakuna! ukweli ni ukweli na uongo ni uongo!

Tumeona ya kutosha enzi ya Mwinyi, tumeona ya kutosha enzi ya Mkapa na sasa yanataka kuanza tena, sasa hivi tutaingia kwenye ile jumuiya aliyotaka kutuingiza Mwinyi na Diria, na tutaingia kama tutakubali kupigwa hadithi za alinacha, kuwa ati ni uwezo, ati wakristo ni wengi mno toka enzi ya Mwalimu, na blah! blah! blah!

watanzania ni lazima tuweke miguu chini tuhesabiwe, Mzee Sam ninakuamini, na I have your back anytime, Mzee Fillga heshima na Salute,

katika maisha yangu sina mpango wowote wa kuwa mkimbizi siku moja NO WAY! Tutabanana hapa hapa bongo, na Dodoma haendi mtu!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom