Wasabato, hii kitu ina maana gani?

Wasabato, hii kitu ina maana gani?

hahaha mkuu naona unakomaa sio mchezo.
Kaiulize familia yake, maana kama umesema sio msalaba unataka sisi tupige ramli.

kwa harakaharaka naona kama ni kibao cha kuandikia maandishi yaliyoandikwa hapo.
Kuhusu Msalaba wasabato wamejikita kwenye maana ya Msalaba na Yesu alichokifanya pale msalabani sio Ile Miti au sanamu ya misalaba. Hata ukikuta imewekwa na msabato mahali usipaniki, maana Kilicho nyuma ya msalaba ndio kinamaana kwa msalaba sio ule mti, Ukimkuta anaubusu, au kuuonyeshea tendo lolote la kiibada kanakwamba unasehemu katika ibada au wokovu wake muulize vizuri labda yuko darasa la ubatizo.

Pia ukisema Hellen White kasema kitu, vizuri kukionyesha, usijekujikuta unatembelea kwenye uzushi ulionyweshwa bila kutafakari.
Umejibu vyema.
Binafsi nimejifunza kitu katika majibu yako.

Lakini pia nina maswali.
1/Je, Kwenye makanisa ya wasabato huwa hawaweki msalaba(iwe nje, juu, au ndani)?

2/Je, Makaburi nayo vitu, huwa hayana misalaba?

3/Je, alama ya msalaba kwa wasabato ni jambo haramu, dhambi au linaloepukwa?
 
unatumia kigezo gani kuchambua majibu ni sahihi au sio sahihi huku wewe hujui majibu sahihi.
unaweza kutoa mbinu.
hahaha
Ungejikita kwenye kueleza hii mkuu

tapatalk_1541183969278.jpeg
 
Ila mbona vitu vingine rahisi kuelewa, kama hakuna kuweka misalaba kwenye kaburi basi wameweka hicho kibao, hakina maana yoyote, lengo ni kupata tu sehemu ya kuandika jina la marehemu hapo kama ukumbusbo, kwamba mtu akiambiwa hili ndio kaburi ya Gamba anaelewa.

Swala la umbo la 'T' si hoja, hata lingekuwa umbo ya 'O' poa tu ilimradi kuna nafasi ya kuandika jina
 
Kwanini isiwe just a simple rectangular box halafu yaandikwe hayo ya kuandikwa..??

Kwanini iwe ni msalaba uliokatwa kwa juu...??? Nini Wasabato mnataka kutuficha...?? Kuna siri gani hapo...??
we jamaa ulikuwepo huo msalaba unavyokatwa?
maana doh! shekhe umekazia kweli kweli.
anyway, mm mwenyewe nipo hapa kujifunza dini zenu nyie Wakristu.
tuendelee.....
 
Nje ya mada:Nini kilichosababisha gamba kutokuwa na mke hadi anafikisha umri wa miaka 48?
Hili swali ulipaswa au lilipaswa kuulizwa wakati Isac Gamba akiwa hai.
Yote kwa yote, huenda hili linaweza kuwa mojawapo ya jibu.
-Hakutaka kuoa katika maisha yake(Kuoa ni utashi tu wa mtu, sio kanuni ya lazima kimaisha).

-Huenda wakati wake wa kuoa ulikuwa bado (Kila jambo huwa lina majira yake)

-Alikuwa bado anatafuta au kusubiri kumpata binti wa kumfaa kumuoa (Duniani kila mtu na wake)
 
Umejibu vyema.
Binafsi nimejifunza kitu katika majibu yako.

Lakini pia nina swali.
Kwenye makanisa ya wasabato huwa hawaweki msalaba(iwe nje, juu, au ndani)?

Makaburi nayo vitu, huwa hayana misalaba?
Wasabato SDA maana kuna wasabato zaidi ya madhehebu 500, hata humu JFvtu kuna watu wanaiamini Sabato na kuitetea na sio SDA, wapo reformers, Baptists, Judaism etc sasa hata mleta mada lazima awe specific.
Kuhusu MSALABA - Wasabato wanaamini zaidi kile kilichofanywa pale msalabani na sio huo msalaba kama OBJECT.
Hivyo kwa uzoefu wangu maana wasabato wametapakaa nchi zaidi ya 215 duniani kuna mahala wanaweka kwenye makanisa kulingana na mazingira ya huko na kuna mahala hawaweki. Hata Misalaba makaburini kuna pengine wanaweka na pengine hawaweki. Ila Fundisho la Kanisa ni Kiini cha Ibada ya Wasabato ni tukio lililotokea pale Msalabani sio Huo Msalaba. Hata Bibilia inaposema tujivunie msalaba sio ile miti bali Tukio lilifanyika pale msalabani (Ukombozi). Hicho kifaa hakina tija yoyote katika imaninya kisabato. Hata ukikuta kimewekwa hakina element yoyote ya Ibada zaidi ya uwakilisho ndio maana kwa asilimia kubwa hukikuti.

Ila mimi ni msabato, Bibilia yangu Inamsalaba, wala siwezi kuitupa kisa inamsalaba maana hauna kitu chochote kwangu. Tofauti na imani ya mleta mada kiasi cha kulazimisha, wao wanachonga misalaba, wanaiabudu, wanaitumikia, wanaipa heshima ambayo ilipaswa kwenda kwa Mungu, na kuna ushahidi usiopingika hata na wahusika sasa kutafuta unafuu wa kukosolewa huko wanatafuta huruma kwa kulazimisha na wengine kuwaweka katika viwango vyao vya ibada za sanamu.

hicho ndicho naweza kukisema, hata juzi kuna dada alikuwa msabato kafariki, nimeona wao wameweka msalaba wenye taarifa yake, na mchungaji alikuwepo wengine hawaweki, wengine wanaweka kitu kama jiwe lenye taarifa zake.
 
mwisho wa siku mkuu utakuja uwe msabato naona unawakubali sana.
Karibu kanisani sabato hii asubuhi mkuu Otorong'ong'o
sio dhambi kusali na wanadamu wenzako wasabato mkuu.
Mkuu mitale na midimu salaam!
Nilikuwa ninafuatilia ili nione jibu, lakini nachelea kusea kwamba, umesema, wasabato hamukuweka hiyo alama bali familia ya kisabato ndo imeweka kwa hiyo otorong'ong'o akaiulize hiyo familia ya kisabato inamaanisha nini badala ya kuwauliza wasabato?.
 
ukiweka na fundisho, utaonekana unaongea mambo ya maana.
fundisho kuhusu T maana mimi silijui. nadhani hata hao wachungaji hawalijui,
Lakini pia wasabato msibani huwa hawaongei na nawaconcentrate na maiti bali ninyi mlio hai, maana wafu hawajui lolote.

Hata mkitelekeza maiti wachungaji watakuja kuongea na walio hai na kukumbusha maagizo ya Mungu bila kujali amewekewa T, X, Y au Z achilia mbali msalaba.
Kwa hiyo alama siyo shida mkuu?
 
Kwa hiyo alama siyo shida mkuu? Na ni sahihi kutumia yoyote kwani kanisa halina shida na alama yoyote!
 
Mkuu mitale na midimu salaam!
Nilikuwa ninafuatilia ili nione jibu, lakini nachelea kusea kwamba, umesema, wasabato hamukuweka hiyo alama bali familia ya kisabato ndo imeweka kwa hiyo otorong'ong'o akaiulize hiyo familia ya kisabato inamaanisha nini badala ya kuwauliza wasabato?.
nimempa maoni yangu kuwa, ni platform ya kuandikia majina na taarifa ya marehemu, maana wasingeandika kwenye tiles.
Ila kama kanisa hakuna makubaliano au doctrine kuhusu unapoandika jina au taarifa za marehemu basi mahali unapopatumia pakaeje ingawa kwa asilimia kubwa Juu ya kaburi wanaweka kama jiwe maalum au kamnara kadogo ka kuandikia taarifa za muhusika hasa ulaya kulingana na style mbalimbali za graveyard. Inaonekana majibu hayo kwake ni mepesi yeye anataka majibu magumu kwa maswali ambayo anadai ni mepesi inagawa pia anadai majibu hajui. I

habari za siku mingi mkuu.
 
sijaona popote fundisho la kutoweka sehemu ya Kuandikia Jina, bila kujali umbo lake.
Ila Hiyo comment ni kwa case ya mtu asiyemsabato aliyekifa na kususwa na kanisa lake.
Mfano jamaa mmoja kanisa lilimsusa kisa mlevi wa kupindukia huko mtwara, alikuwa angrican, Wainjirist wa sabato walikuja wakachukua jukumu na kupata fursa ya kuwafundisha wanakijiji '' wafu hawajuinlolote''. Na kusimamia shughuli yote ya kuuhifadhi mwili wa maiiti ile iliyotengwa.
Hata mimi nikikuta mtu katelekezwa kisa alikuwa hasali, na watu wanahitaji huduma ya neno nitawafundisha japo sio mchungaji wala mtumishi ni muumini wa kawaida tu. Na sitajali alama, anachomwa moto, au anazikwa kimitindo gani, Ila nitawakumbusha mahusia ya Mungu bila wasiwasi.
Huwezi kutenga udongo.

Kwa hiyo lengo katika Msiba huwa kutoa mahubiri tu kwa walio hai?
 
Kwa mjibu Wa mafundisho yenu Imeandikwa: " usijifanyie sanamu ya kuchonga...". Sote tunafahamu YESU alisulubiwa msalabani wenye alama +. Je kutengeneza kitu chenye ufanano na msalaba au unatoa au unaobeba alama ya msalaba inakuwa sio dhambi? Sio Sanamu hiyo?
 
Siyo msalaba, msalaba una alama ya kujumlisha +, hiyo ni T angalia vizuri. Labda we kipofu
 
Kwa hiyo alama siyo shida mkuu? Na ni sahihi kutumia yoyote kwani kanisa halina shida na alama yoyote!

Kuna maelezo pale #108 Kama hayajakuelea tunaweza kuteta kadili nafasi itakavyopatikana.

Kwa mjibu Wa mafundisho yenu Imeandikwa: " usijifanyie sanamu ya kuchonga...". Sote tunafahamu YESU alisulubiwa msalabani wenye alama +. Je kutengeneza kitu chenye ufanano na msalaba au unatoa au unaobeba alama ya msalaba inakuwa sio dhambi? Sio Sanamu hiyo?
sio mafundisho Yetu, bali Bibilia.
Sio sanamu, ni kifaa cha kutunzia kumbukumbu, hakina tofauti na jiwe ambalo lilifunga kaburi la Yesu. Lilichongwa na halikuwa sanamu wala element yoyote ya kiibada.
Ila zipo dini zinachonga, kutumikia, kuabudu na kuonyesha heshima za kiibada kwa miti hiyo.
hiyo ni machukizo kwa Mungu, na ni kumdhalilisha Yesu, kama na wewe huwa unashiriki acha mkuu.
 
Kwa hiyo lengo katika Msiba huwa kutoa mahubiri tu kwa walio hai?
Ndio.
Mahubiri ni Kwa ajili ya walio hali, na kuwapa faraja ya Bibilia wafiwa.
Maiti Imerudi mavumbini. Ni machukizo kwa Bwana kuongea na mfu.
Labda kama Huduma Hiyo mchungaji anataka kumfufua maiti kama Yesu, Elisha, Petro au Paulo atamuita na atafufuka papo hapo.
Vinginevyo maiti inapaswa kuyarudia mavumbi, na walio hai kukumbushwa wajibu wao kwa Mungu kabla hawajashuka kwenda katika kimya.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom