Ifahamu historia ya Wasabato

CarloJesus

JF-Expert Member
Nov 5, 2019
431
833
IFAHAMU HISTORIA YA WASABATO NA AIBU

Aibu inayofichwa ndiyo hii ifuatayo:

Ni hivi ndugu zanguni, kwa kuiweka bayana historia ya Wasabato, tuambatane katika kuwaelewa watu wanne ambao hutajwa kama watangulizi au waasisi wa dhehebu la Wasabato. Mwishoni nitayapembua waliyofundisha kibiblia na kisaikolojia.

Mtu wa kwanza ni William Miller, wa pili ni Hiram Edson, wa tatu ni Joseph Bates na wa nne na wa mwisho awe Bi Ellen G. White.

Tukianza na Bw. William Miller, yeye alizaliwa mwaka wa 1782 katika mji wa Pittsfield, Massachusetts, huko Marekani. Ingawa alizaliwa katika familia ya Kikristo, aliuacha Ukristo alipokuwa kijana mbichi. Kwa kweli hakuiamini Biblia kuwa neno la Mungu. Basi, akajiunga na jeshi. Baada ya kutumika kama mwanajeshi kwa muda mfupi, akaishi kama mkulima. Kumbe, mwaka wa 1816, akaongoka na kuurudia Ukristo wake kwa kasi mpya. Kwa kweli, tangu mwaka huo wa kuongoka kwake, Bw. William Miller alisoma unabii kwa kina na hasa unabii uliohusu kurudi kwa Yesu Kristo, Bwana wetu.

Kumbe, kutokana na kujifunza huko, Bw. William Miller akashawishiwa kwamba mwisho wa dunia ungetimia mwaka 1843. Kifupi, Bw. William Miller alishawishiwa kufundisha jinsi hiyo na unabii wa kitabu cha Danieli 9:24-27, unabii unaohusu majuma sabini yaliyowekwa kwa ajili ya watu wa Mungu, taifa la Israeli.

Zaidi ya hayo, katika Danieli 8:13-14, kuna unabii wa watakatifu wawili wanaoulizana lini patakatifu patatakaswa. Mintarafu unabii huo, Bw. William Miller alitafsiri kwamba patakatifu patakapotakaswa, ni dunia hii iliyochafuliwa na dhambi za kila sampuli. Kwa maoni yake, mwaka wa 1843 B.K., ndio mwaka ambao Yesu Kristo angerudi katika dunia iliyonajisiwa kupita kiasi na dhambi na hivyo kuitakasa kabisa kwa kuwapo kwake.

Msimamo huu ulimfanya awe maarufu sana katika sehemu nyingi za Marekani, na hatimaye akawa mhubiri mkubwa wa dhehebu la Kibaptisti. Kwa kuwa mwisho wa dunia ulikuwa unaambatana na kurudi kwa Yesu Kristo, ambako kwa Kiingereza huitwa “Christ’s Advent”, wafuasi wake walianza kujulikana kama “Adventists” au kwa Kiswahili “Waadventisti”, yaani “Watu watarajiao kurudi kwa Kristo”. Ijapokuwa mwanzoni hakutaja tarehe bayana ya kurudi kwa Yesu, punde si punde alisema kurudi kwa Yesu kungekuwa kati ya tarehe 21 Machi, 1843 na 21 Machi, 1844.

Baada ya mambo kufikia hapo, mfuasi mmoja wa Bw. William Miller aliyeitwa Samwel Snow, akawa jasiri zaidi na kutaja kwamba Kristo angerudi tarehe 22 Oktoba, 1844 saa 6.00 usiku; yaani ndipo parapanda litakapopulizwa, mbingu kukunjwa kama kurasa, na Yesu Kristo kufika kwa utukufu mwingi. Lakini mambo hayakutukia hivyo walivyohubiri. Basi, kwa vile Kristo hakurudi kama walivyotarajia, Bw. Miller akakiri kukosea kwake, lakini akawaonya wafuasi wake wasisahau kwamba Kristo atarudi upesi.

Kwa bahati mbaya, Bw. William Miller alifariki mnamo mwaka 1849 ndoto yake ya kumwona Yesu akirudi upesi ikiwa bado haijatimia. Hadi hapo, ieleweke kwamba Bw. William Miller, hakuwahi kuwa Msabato. Hivyo kama Mbaptisti, alikuwa anasali siku ya Bwana, yaani Jumapili au Dominika. Kutokana na kutokutumia kwa utabiri wa Bw. William Miller wafuasi wake wengi wakarejea nyuma.

Basi, tumwachie Bw. William Miller hapo, nasi tusonge mbele tukamwangalie mtu wa pili, yanii Bw. Hiram Edson. Kwa bahati, bwana huyu alikuwa kati ya Waadventisti wachache waliobaki baada ya kuvunjika moyo kwa wafuasi wengine wa William Miller kutokana na kutorudi kwa Kristo kama ilivyotazamiwa. Kwa upande wake kwa kusudi la kuwafariji wenzake kwenye huzuni yao, yeye alidai kwamba Mungu alikuwa ametoa jibu kwa aibu yao kwani alipata mafunuo juu ya kile kilichofanyika siku hiyo ya tarehe 22 Oktoba, 1844.

Kwa jinsi gani? Sikiliza. Alifundisha kwamba alioneshwa kulikuwa na hekalu mbinguni mfano wa hekalu la duniani. Akadai hekalu hilo lilikuwa na sehemu mbili: patakatifu na patakatifu pa patakatifu, yaani sawa na lilivyokuwa hekalu la Kiyahudi zamani zile. Kumbe, kilichofanyika siku hiyo ya tarehe 22 Oktoba, ni kwamba Kristo alitoka patakatifu na kuingia patakatifu pa patakatifu. Akasema kwisha Yesu kuingia patakatifu pa patakatifu atabaki humo mpaka siku atakapokuja duniani mara ya pili.

Mintarafu swali, Yesu anafanya nini siku zote hizo? Akasema Yesu anafanya ‘hukumu ya upelelezi’ kwa Kiingereza “investigative judgement”. Kwa maelezo hayo mapya akadai kwamba kitu alichokuwa amekosea Bw. William Miller kilikuwa tafsiri tu, kwa maana kwamba utakaso uliofanywa tangu siku ile ya tarehe 22 Oktoba haukuwa wa dunia hii, bali wa patakatifu pa patakatifu katika hekalu hilo la mbinguni.

Kwa namna hii, Bw. Hiram Edson akawa Mwadventista wa kwanza, hata kabla hajawa Msabato, kuleta duniani maelezo ya kuwafariji wenzake kwa kutorudi kwa Kristo siku ya tarehe 22 Oktoba 1844. Hivi basi, mchango wake mkubwa kwa teolojia ya Wakristo ambao baadaye walijiita Wasabato ni suala hilo la ‘hukumu ya upelelezi’. Kifupi, kwa maelezo hayo, Wasabato wanafundisha kwamba Yesu Kristo, tangu 22, Oktoba 1844 yuko huko mbinguni, katika patakatifu pa patakatifu akichunguza kwa kina maisha ya Wakristo wote ambao majina yao yapo katika kitabu cha uzima wa milele na kuamua nani anastahili kufutiwa dhambi zake zilizosamehewa wakati alipoamini. Hivyo, kila mtu anayeonekana kurudi nyuma, naye hakutubu dhambi zake zote, anafutwa jina lake kutoka katika kitabu cha uzima na hivyo huko, mwishoni mwa historia, atakosa nafasi katika ufufuo wa kwanza. Kinyume chake, kwa upande wao, wote ambao walitubu dhambi zao, majina yao yanabaki kitabuni pasipo kufutwa, nao watafufuliwa katika ufufuo wa kwanza.

Ndugu zangu, hadi hapa umeshagundua mafundisho ya uongo. Mbinguni hakuna hekalu. Huo ndio ukweli wa kibiblia maana mwandishi wa kitabu cha Ufunuo anatuandikia habari za maono yake matakatifu mintarafu Yerusalemu ya mbinguni akisema “Nami sikuona hekalu ndani yake, kwa maana Bwana Mungu Mwenyezi na Mwanakondoo, ndio hekalu lake” (Ufu 21:22). Sasa iweje Bw. Hiram Edson amzungumzie Yesu anayetoka patakatifu kuingia patakatifu pa patakatifu? Zaidi ya hayo, mafundisho ya hukumu ya upelelezi ni uzushi kwa sababu ni matokeo dhahiri ya tafsiri potofu ya neno la Mungu.

Haya tuachane naye, nasi twende tukamwangalie mtu wa tatu, ambaye ni Bw. Joseph Bates. Kikazi, Bw. Joseph Bates alikuwa baharia. Bada ya kustaafu kwake alihamia Fair Haven, katika jimboni Massachusetts, huko huko Marekani. Kwa kweli, Bw. Joseph Bates ni mmoja wa viongozi maarufu wa Waadventisti. Yeye aliposoma maandishi ya Thomas Prebble kuhusu Sabato, alishawishiwa kuamini kwamba Sabato ya Wayahudi ilikuwa siku halali kwa watu wote wa Mungu kuabudu. Basi, akaandika kijitabu chake kilichoitwa, “The Seventh Day Sabbath, a Perpetual Sign””.

Baada ya kitabu hicho Bw. Joseph Bates aliendelea kuandika vijitabu kuhusu Sabato. Hivi bwana huyu anakumbukwa sana na Wasabato kwa mchango mkubwa katika kuirudisha Sabato ya Agano la Kale. Kwa kweli, ni yeye aliyekuwa wa kwanza kutafsiri siku ya Jumapili kama siku ya alama ya mnyama; na kwamba siku ya Sabato ndiyo muhuri wa Mungu kwa watu wake walio waaminifu, yaani Waadventisti Wasabato 144,000 (rej. Ufu 7:4).

Kutokana na ushawishi wake huu, kuabudu siku ya Jumamosi, kukaanza kupata nguvu nyingi, zilizoambatana na vitisho vya hukumu kali kwa wanadamu wote wasioishika Sabato ya Agano la Kale. Kifupi, miongoni mwa Waadventisti waliomfuata Bw. Joseph Bates kwa karibu, walikuwa ni James na mkewe Ellen White. Kumbe, Bi Ellen White ndiye aliyeuendeleza usabato, kwa motomoto zaidi kuliko watu wengine wote naye anaheshimiwa na Wasabato kama nabii wao. Kwa hali hii ya mambo, yafaa tumalizie historia hii fupi kwa kumwangalia mwanamama huyo hata kama ikiwa kwa kifupi sana.

Ndugu zanguni, Bi Ellen G. White, anafahamika pia kwa jina la Bi Ellen Gould Harmon. Ni kwamba kabla hajaolewa alikuwa anaitwa Ellen Gould Harmon na baada ya kuolewa kwake na mpenziwe James White, aliyekuwa mhubiri wa kibaptisti aliyekuwa muadventisti hapo tarehe 30 Agosti, 1846 akajulikana kama Bi Ellen Gould White.

Kwa kufupisha mambo, Bi Ellen Gould Harmon alizaliwa mwaka 1827 huko Goharm, jimboni Maine, maili kumi hivi toka Portland. Akiwa mtoto mdogo bado, wazazi wake walihamia Portland kwenyewe. Hapo mwanzoni, yeye pamoja na familia yake walikuwa wafuasi wa dhehebu la Methodisti. Kumbe, familia ya akina Ellen ilijiunga na uadventisti baada ya Bw. William Miller kuhubiri mjini Portland katika mwaka wa 1840 na 1842. Lakini kwa kuwa familia hiyo ilisadiki maneno ya Bw. William Miller, kanisa lao la Methodisti liliitenga familia hiyo. Familia nzima ilitengwa kwa sababu ya kuyapokea mafundisho ya Kiadventisti. Kwa ujumla, mchango wa Bi Ellen White ulianza kama alivyodai mwenyewe kwamba alipokea maono mengi nyakati mbalimbali, maono ambayo baadaye yalimfanya ajulikane kama nabii wa Waadventisti. Inasemekana maono yake ya kwanza yalimjia mwezi Desemba, 1844, yaani si muda mrefu sana baada ya watu kukatishwa tamaa na kutokurudi kwa Yesu Kristo.

Bi Ellen White aliingia ulingoni akidai kuliona kundi la Waadventisti wakisafiri katika njia yenye mwanga wa utukufu, huku wakiongozwa ya Yesu hadi walipoufikia mji wa Mungu. Bi Ellen akadai kwamba baada ya kuonywa katika maono ya pili asikae kimya juu ya yale aliyooneshwa, alilazimika kutangaza na kuyahubiri maono yake wazi mahali pengi. Kuanzia hapo, Waadventisti wa Portland na Maine wakaanza kumtambua Bi Ellen White kama nabii wao na kusisitiza kwamba Roho Mtakatifu alikuwa juu yake na kwamba ilikuwa ni lazima unabii wake ufuatwe na Waadventisti wote popote pale walipokuwa.

Kama jambo hilo halitoshi, mwezi Februari 1845, Bi Ellen White alidai kupata maono yaliyothibitisha maono ya Bw. Hiram Edson mintarafu kitu kilichotokea hapo tarehe 22 Oktoba 1844, yaani kwamba Yesu alikuwa ameingia patakatifu pa patakatifu katika hekalu la mbinguni. Zaidi ya hapo alidai kwamba miaka miwili baadaye, alipata maono mengine ambapo alidai kwamba alichukuliwa na kupelekwa katika hekalu la mbinguni. Alisema kwisha kufikishwa mbinguni, kwanza kabisa aliingizwa patakatifu na baadaye patakatifu pa patakatifu ambapo aliona amri kumi zikiwa ndani ya sanduku la agano.

Tukiwa tayari kusonga mbele, tunaweza kujiuliza swali dogo la kuchangamsha bongo zetu. Hebu tujiulize, hivi, humo patakatifu pa patakatifu Bi Ellen White alikumta Yesu akifanya hukumu ya kipelelezi? Tukikijibu wenyewe, ndugu yangu, jibu ni kwamba suala hilo haligusiwi ilivyotarajiwa. Basi, acha tuzidi kumfuatilia katika madai ya maono yake. Bi Ellen White anasema alipong’aza macho yake kwenye sanduku la agano la humo hekaluni, aliona amri ya sabato ikiwa imezungukwa na utukufu na hapo eti akang’amua kwamba amri ya kushika Sabato ilikuwa kubwa zaidi.

Ndugu yangu, hadi hapo, tukimpima Bi Ellen White kibiblia, anaongeza uongo mwingine mbaya. Uongo wa kwanza ni ule wa kuliona hekalu mbinguni wakati mbinguni, Maandiko Matakatifu yanasema hakuna hekalu (rejea tena Ufu 21:22). Uongo wa pili ni huu wa kuhesabu amri ya kushika Sabato kama amri kuu kwani amri ya kwanza na kubwa kupita zote, kadiri ya Yesu Kristo mwenyewe, ni ile ya kumpenda Mungu huku ikifuatiwa na ya pili yake, yaani ile ya kumpenda jirani kama tunavyojipenda sisi wenyewe (rej. Mt 22:34-40).

Lakini basi, ndugu zanguni, maono aliyopata Bi Ellen White yakawa, kwake na hatimaye kwa Wasabato wote, kurunzi la kutafsiria Maandiko Matakatifu yote. Ndipo, kwa njia ya vitabu vingi alivyoandika, mafundisho ya Kiadventisti yakasambazwa. Hivyo, tangu wakati huo, Waadventisti Wasabato, huitafrisi Biblia kwa vipimo vya maono ya White, na siyo kuyatafsiri maono ya Bi White kwa vipimo vya Biblia. Je, si ajabu ya mwaka hiyo? Basi, ndugu yangu, fumbuka macho ya roho yako, uyaone na kuyapima mambo haya sawa sawa pasipo kiwi cha macho! Usitoe hoja ya uongo!
Basi, kwa kukata maneno, Bi Ellen White ndiye aliyewapandikiza chuki Wasabato dhidi ya Kanisa Katoliki. Amelifanya hilo kwa kupitia vitabu vyake vingi vyenye chuki ambavyo vinasomwa na kutumiwa na Wasabato karibu kama misahafu. Kwa taarifa yako, baadhi ya vitabu hivyo ni, kama vile, Vita Kuu, Afya na Raha na Siri ya Ushindaji. Ndani ya vitabu hivi Kanisa Katoliki linatukanwa na kushtakiwa kuhusika na maovu mengi. Kwa mfano, wanashtakiwa kuondoa amri ya kuabudu Sabato. Wanashtakiwa kuabudu sanamu. Wanashtakiwa kumwabudu Bikira Maria. Wanashtakiwa kumwabudu Baba Mtakatifu (Papa) ambaye eti ndiye mnyama anayetajwa katika kitabu cha Ufu 13:1-18. Wanashtakiwa kufundisha mambo ya kidunia badala ya ufalme wa Mungu. Wanashtakiwa kuongeza vitabu kwenye Biblia na mengine mengi ya namna hiyo yanayosikika mitaani na katika mahubiri yao. Mungu utuhurumie!

Ndugu zanguni, kwa ujumla, kanisa la Wasabato likawa muungano wa vikundi vitatu vya Waadventisti: mosi, kikundi cha Bw. Hiram Edson, kilichosisitiza zaidi mafundisho ya huduma ya Yesu patakatifu pa patakatifu mbinguni; pili, kikundi cha Bw. Joseph Bates, kilichosisitiza zaidi kufuata Sabato ya Agano la Kale; na tatu kikundi cha Bi Ellen G. White, kilichomwona Bi Ellen kama nabii ambaye unabii wake ni lazima ufuatwe na Waadventisti wote duniani.

Vikundi hivi vilipoungana Waadventisti Wasabato wakapata kujichipusha duniani. Mwaka 1860, jina la Seventh Day Adventist lilichaguliwa nalo likawa jina rasmi la Waadventisti hao. Kishapo, mwezi Mei, 1863, katika mkutano mkuu wa kwanza, uliokuwa na wawakilishi kutoka majimbo yote Marekani, isipokuwa jimbo la Vermont, kanisa la Wasabato likazaliwa rasmi duniani.

Basi, tukipiga muhtasari wa historia ya Wasabato, tuseme tu kwamba mwasisi wa Waadventisti Bw. William Miller alikuwa ni Mbaptisti lakini mwanzilishi wa Wasabato yaani Bi Ellen G. White alikuwa ni Mmethodisti. Hata hivyo, kwa kuhitimisha sehemu hii, yafaa sote tukumbuke kwamba makanisa hayo mawili, yaani Wabaptisti na Wamethodisti si chochote isipokuwa matawi ya kanisa la Anglikana, kanisa lililoanzishwa na Mfalme Henry VIII wa Uingereza hapo mwaka 1534 baada ya kukasirika kukataliwa na Kanisa Katoliki kumwacha mkewe aliyeshindwa kumzalia mtoto wa kiume.

WASABATO MITUME WA MATUSI DHIDI YA KANISA LA KWELI

Msomaji wangu bila shaka umeiona historia ya aibu na ya zigzaga ya Wasabato. Wasabato wenyewe huificha sana historia hiyo, hasa kwa wafuasi wao wanaoingia katika kanisa lao putaputa. Hufichwa ukweli kama paka wanaosafirishwa katika gunia. Kwa nini? Wanafichwa ili wasiujue ukweli walikotokea wasije wakajua kwamba wamekosea njia kiimani.

Kifupi, madai yao kwamba Baba Mtakatifu, Kanisa Katoliki au Mfalme Constantino ndio waliobadili Sabato kwenda Jumapili ni mojawapo ya matusi ya Wasabato. Wenyewe wanahubiri hayo kwa jasho jingi kabisa wakati ni kusepetuka kwa uelewa na fichio la aibu yao katika kushindwa kwao katika utabiri wa tarehe ya mwisho wa dunia, tarehe ambayo Yesu Kristo, Bwana wetu na Maandiko yanatuambia kwamba haitabiri kabisa. Kwa maneno mengine, ndiyo matawi ya chuki iliyokosewa mwelekeo na uongo wa binadamu dhidi ya wanadamu wenzake.

Tusisahau, kutokana kushindwa hoja na aibu kubwa waliyoipata mbele ya ukweli unaoshikiliwa na kufundishwa na Baba Mtakatifu na Kanisa Katoliki, Wasabato na makanisa mengine wameamua kutumia mbinu ya kujikosha kwa matusi makali. Wameamua kujitwika utume wa matusi wakati mwingine hata matusi ya nguoni. Kwa vyovyote, Wakatoliki hawana namna rahisi ya kukabiliana na madai hayo ya kimatusi. Usistaajabu haya kufanyika hivi. Kwa mtindo wa vijijini, ukishindwa hoja kwa mtu fulani unaanza kumtukania wazazi wake, nyumba yao na kadhalika.

KUITUNZA SABATO NI KUSHEREKEA MKESHA WA SIKU YA UHURU

Kuitunza Sabato mbele ya Dominika ingelingana na kusherekea mkesha wa siku ya uhuru badala ya siku ya uhuru yenyewe. Taifa litakalofanya hivyo litachekesha na labda litakuwa la watu punguani. Aidha mtu kupita huko na huko kuwahimiza watu washerehekee mkesha wa uhuru badala ya siku ya uhuru wenyewe ingelikuwa sawa na kucheza Ze Comedy.

Nani amegeuka mkondo wa mambo hata kugeukia tena Sabato wakati Wakristo wa kwanza kwa kumwelewa vyema Yesu Kristo walishaitupilia mbali? Jibu ni wazi. Ni mmoja wa waanzilishi wa dhehebu la Wasabato, yule mama anayejulikana kama nabii. Kwa taarifa yako waanzilishi wa dhehebu la Wasabato ni akina Hiram Edson, Joseph Bates, E.G. Harmon na Hellen White. Katika hawa aliyekuja na moto wa kurudisha Sabato ni huyo mama ambaye alikuwa mke wa E.G. Harmon. Mwanamke huyo anaheshimiwa na Wasabato kama nabii na vitabu vyake , kama vile Vita Kuu, Afya na Raha na Ushindaji, vinasomwa na Wasabato karibu kama misahafu.

WASABATO WASIMNYANYASE YEYOTE

Maono ya uwongo ya Bi Hellen yasiwe sababu ya kuwanyanyasia Wakristo wasio Wasabato. Wala si siri, makanisa yanayofuata mabadiliko yaliyoletwa na Mungu mwenyewe kutoka Sabato kwenda Dominika yananyanyaswa kweli kweli na kauli za Wasabato wanaomfuasa Bi Hellen White. Lakini, hivi unabii wa mama huyo ni wa kweli hata tutishike nao? Hapana, wala si wa kweli. Unabii wa mama huyu lazima tuukatae. Kwa nini tuukatae?

TUHIMIZANE TUMKATAE BI HELLEN NA MAONO YAKE

Ni kwa sababu kuna sababu tatu zinazotuhalalisha tumkatae Bi Hellen White kama nabii. Mosi, kitabu cha Ufunuo kinaonesha kufungwa kwa unabii, yaani kwamba baada ya mambo yaliyoandikwa humo kusingekuwa na ufunuo wowote wa pekee. Ukamilifu wa ufunuo ulitokea katika ujio wa Yesu Kristo. Alichosema yeye ndicho kitu cha kilele. Sasa Bi Hellen anakujaje na mapya kumpikua Yesu Kristo? Tunasoma, “Mungu ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi, amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu. Yeye kwa kuwa ni mng’ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akavichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu, amefanyika bora kupita malaika kwa kadiri jina alilorithi liliyo tukufu kuliko lao” (Ebr 4:1-4).

Si hivyo tu hata mintarafu ufunuo wa zamani mihuri yake imevunjwa na Yesu Kristo mwenyewe, sasa unabii wa Hellen White unaanzia wapi? Tunasoma, “Kisha nikaona katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma, kimetiwa muhuri saba. Nikaona malaika mwenye nguvu akihubiri kwa sauti kuu, Ni nani astahiliye kukifungua kitabu na kuzivunja muhuri zake. Wala hapakuwa na mtu mbinguni, wala juu ya nchi, wala chini ya nchi, aliyeweza kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama. Nami nikalia sana kwa kuwa hapakuonekana mtu astahiliye kikifungua hicho kitabu, wala kukitazama. Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba.

Nikaona katikati ya kile kiti cha enzi wale wenye uhai wanne, na katikati ya wale wazee, Mwanakondoo amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote. Akaja , akakitwaa kile kitabu katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi. Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele ya Mwanakondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya wakatakatifu, nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaaa hicho kitabu na kizifungua muhuri zake, kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa, ukawafanya kuwa ufalme wa makuhani, kwa Mungu wetu, nao wanamiliki juu ya nchi” (Ufu 5:1-10).

Mintarafu kusasambua ovyo ufunuo wa Mungu, mwandishi wa kitabu cha Ufunuo alishakatazwa, sasa Bi Hellen White anapata wapi nguvu ya kuja na ufunuo mpya? Kuhusu marufuku hiyo tunasoma, “Hata ngurumo saba zilipotoa sauti zao, nalikuwa tayari kuandika. Nami nalisikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Yatie muhuri maneno hayo yaliyonenwa na hizo ngurumo saba, usiyaandike” (Ufu 10:4). Hatimaye, maneno ya ufunuo yaliachwa wazi bila muhuri kwa vile yalivyokuwa njiani kutimia. Juu ya jambo hili, tunasoma hivi: “Akaniambia, Usiyatie muhuri maneno ya unabii wa kitabu hiki kwa maana wakati huo umekaribia” (Ufu 22:10). Sasa Bi Hellen White anaongezaje maneno ya ufunuo mpya?

Pili, tuukatae unabii wake kwa vile zile anazoziita njozi, kama elfu mbili hivi, ni batili kwani zinaonesha jinsi alivyojaa chuki kwa Baba Mtakatifu na Kanisa Katoliki nasi tunajua kwamba si kazi ya Mungu Roho Mtakatifu kumjaza mtu chuki kali hivyo dhidi ya mwanadamu mwingine. Kazi hiyo hufanywa na Shetani nayo huonesha kwamba moyo wa mtu umejaa uovu kwani kilichomjaa mtu moyoni ndicho kimtokacho. Tunasoma, “Kwa maana hakuna mti mzuri uzaao matunda mabaya, wala mti mbaya uzaao matunda mazuri; kwa kuwa kila mti hutambulikana kwa matunda yake; maana katika miiba hawachumi tini, wala katika michongoma hawachumi zabibu. Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake” (rej. Lk 6:43-45). Hakika chuki dhidi ya Baba Mtakatifu na Kanisa Katoliki inatoka katika moyo uliofurika uovu. Na kwa jinsi hii maono yake hayawezi kutoka kwa Roho Mtakatifu.

Tatu, tuukatae unabii wake kwa sababu mafundisho yake yanaonesha kwamba haijui Biblia. Hoja hii ya tatu nimeshaishuhudia tayari. Nimesema ameota ndoto akaona huko mbinguni kuna hekalu wakati Maandiko yanatakaa jambo kama hilo (rej. tena Ufu 22:22-24). Kisha nimeshashuhudia kwamba kule kusisitiza kwamba Sabato ndiyo amri kuu kunapingana na kile alichotuambia Bwana wetu Yesu Kristo aliyesisitiza kwamba amri kuu ni upendo (rej. tena Mt 22: 34-40). Naomba itoshe nilivyokuambia nawe uyapuuze maono ya Mrs. Harmon tunayemchambua hapa.

MAJIBU KWA MASHTAKA YA ZIADA

Nikiendelea kidogo, naomba ruksa nijibu mashtaka mawili sambamba wanayotoa Wasabato dhidi ya Wakatoliki: mosi kwamba ndio mnyama yule Shetani aliyejipa jukumu la kubadili majira na pili kwamba Kanisa lenyewe linakiri kufanya hivyo katika Katekisimu zake na katika vitabu vya waandishi fulani fulani wa Kanisa Katoliki.

Mintarafu hoja ya kwanza ni hivi mnyama ni Bi Hellen White aliyethubutu kumpinga Mungu. Mungu aliibadili siku ya Sabato yeye akijipa jukumu la kuirudisha kwa maelezo ya maono yake batili kabisa. Tumeshaonesha jinsi yalivyo batili kwa kadiri ya mizani na darubini ya Maandiko Matakatifu.

Halafu mintarafu hoja ya pili ni hivi Kanisa linajihusisha na mabadiliko hayo si kama ‘mtendaji’ kwani hakuna mkutano mkuu (mtaguso) wowote wa Kanisa Katoliki uliojadili hoja ya Sabato na kuamua kuibadili kwenda Dominika ila kwamba Mungu aliibadilisha Sabato pale alipoanzisha enzi ya Israeli mpya yaani Kanisa. Natumaini wasomaji wangu hoja hii si ya kitaalamu mno kiasi cha kutonielewa ninachosema. Ninasema hivi Kanisa linajisikia kuhusika na ubadilishaji wa Sabato kwenda Dominika kwa vile Mungu aliufanya kuanzia pale lilipoanza kuwako nalo kwa mamlaka uliyopata kutoka kwa Mungu ikayasimamia na kuyaendeleza mabadiliko hayo.

MALUMBANO SASA YAKOME

Naomba hadi hapa shtaka la kwamba Kanisa Katoliki limebadili majira, yaani kutoka Sabato kwenda Dominika (Jumapili), lififie kabisa. Si unajua kwamba hoja yenyewe hukokotolewa kutoka Dan 7:25 mahali palipoandikwa, “Naye atanena maneno kinyume chake Aliye Juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye Juu, naye ataazimu kubadili majira na sheria”.

Kama unavyoisoma sasa, hoja hii haitaji Kanisa Katoliki bali kwa kinyume chake inawataja Wasabato wenyewe. Ndugu zangu Wasabato haliwafahamu jambo hili kwa sababu ndivyo ilivyo, “Jambo usilolifahamu ni sawa na usiku wa giza.” Kwa vipi? Ni hivi, kama Yesu kwa maneno na matendo yake alisema Sabato si lolote na wala si chochote “maana mtu hakuuumbwa kwa ajili ya Sabato”, mtu anayesema Sabato ndiyo yote katika yote ndiye anayeazimu kubadili majira na sheria. Na moja kwa moja mtu huyo anakuwa ndiye mpinga Kristo kwa sababu anapingana na kauli ya Kristo mwenyewe. Hilo ndilo alilofanya nabii Hellen na kuwasadikisha maelfu ya watu kauli yake kengeufu.

Aidha, kama Yesu alisema kwamba amri kuu ni upendo (rej. Mt 22:37) na akataka iwatambulishe wafuasi wake popote watakapokuwa (rej. Yn 13:35), anapokuja nabii Hellen na kusema eti amri kuu ni Sabato ni upinga Kristo wa wazi wazi na kumfuasa mpinga Kristo kama huyo ni kuwa wapinga Kristo wadogo wadogo nyuma ya huyo mkubwa. Ona ushuhuda wa Maandiko Matakatifu. Bila shaka, hata wewe unakumbuka Yesu aliulizwa swali juu ya amri ya kwanza na kuu naye akatoa jibu mwafaka hata wasomi na walimu wa enzi zake wakamvulia kofia.

Tunasoma, “Na Mafarisayo waliposikia ya kwamba amewafumba kinywa wale Masadukayo, walifanya shauri pamoja. Mmoja wao, mwanasheria, akamwuliza, akimjaribu: Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu? Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii” na wakati akiwaaga wanafunzi wake jioni iliyotangulia kifo chake alisema na kuagiza, “Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi” (Yn 13:35). Sasa Nabii Hellen anathubutuje kusema kinyume cha maneno hayo ya Kristo ambaye tumepewa tumsikilize? Kama huo si upinga Kristo wenyewe ni nini tena? Hukumu mwenyewe; wewe ni mtu mzima. Hivi wewe na mimi na sisi sote hatukumbuki maneno ya Maandiko Matakatifu, “Huyu ni mwanangu, mpendwa wangu, msikieni yeye” (Mk 9:7)? Na kwa upande wetu, kwa nini, tunamsikiliza binadamu tena? “Tumechanganyikiwa” au “tumerogwa”?

UCHAMBUZI WA KISAIKOLOJIA WA WALIOHUSIKA NA HISTORIA HII YA AIBU

Jina Ugonjwa Tunaoweza Kumtuhumu Upinga Kristo Wake Ulipo William Miller Megalomania – kujidai kujua kuliko Yesu Kristo kwa kujaribu kuitaja tarehe ya mwisho wa dunia Kukokotoa tarehe ya mwisho wa dunia kinyume na Mk 13:32.

Samwel Snow Megalomania – kujidai kujua kuliko Yesu Kristo kwa kujaribu kuitaja tarehe ya mwisho wa dunia Kukokotoa tarehe ya mwisho wa dunia kinyume na Mk 13:32.

Hiram Edson Schizophrenia – kuona hekalu ambalo halipo mbinguni na kudai mwisho wa ulimwengu umeshatokea. Kuota ndoto ya kuliona hekalu mbinguni ni kinyume cha Ufu 21:22-23.

Joseph Bates Megalomania – kujidai kujua kuliko Yesu Kristo kwa kuunga mkono uongo kwamba mwisho wa ulimwengu umeshatokea. Kuidharau Jumapili, siku aliyoitumia Bwana kufanya mambo yote makubwa.
Hellen White Schizophrenia – kuona hekalu ambalo halipo Kuota ndoto ya kuliona hekalu mbinguni ni kinyume cha Ufu 21:22-23 na kudai Sabato ndiyo amri kuu kinyume na Mt 22:34-40.

MASWALI NA MASHTAKA 12 MAARUFU YA WASABATO KWA WAKATOLIKI

i. Sabato ndiyo siku ya kuabudu iliyoamriwa. Wakatoliki ndio walioifuta Sabato na kuweka Jumapili.
ii. Wakatoliki wanafuata mapokeo ya binadamu, hawajui na wala hawafuati Maandiko Matakatifu.
iii. Baba Mtakatifu ndiye mnyama yule anayewakilishwa na namba 666. Namba hiyo imeandikwa kwenye kofia na mavazi yake.
iv. Wakatoliki wameifuta amri ya pili ya Mungu. Wamefanya hivyo ili waabudu sanamu.
v. Wakatoliki wanaabudu sanamu. Tazama sanamu makanisani mwao!
vi. Kwa nini Wakatoliki wanakunywa pombe wakati imekatazwa kwenye Biblia?
vii. Wakatoliki wanamwabudu Bikira Maria. Kwa nini wanamfanyia heshima kubwa isivyostahili?
viii. Je, Bikira Maria alikuwa na watoto wengine zaidi ya Yesu Kristo?
ix. Kanisa Katoliki linafanya makosa kuwatangaza wanadamu kuwa watakatifu. Mwanadamu ana uwezo gani wa kumtangaza mtu mwingine kuwa mtakatifu?
x. Wakatoliki wana sakramenti saba. Wana makosa kwa sababu hazijaandikwa kwenye Biblia.
xi. Kuungama ni kwa Mungu moja kwa moja. Kuna uhalali gani kwenda kuungama kwa mapadri wakati wenyewe wana dhambi?
xii. Wakatoliki wana hatia kubwa kwa sababu hawataki kuokoka. Kwa nini Wakatoliki ni wabishi hivyo?

Ndugu yangu Mkatoliki jaribu kuwa na majibu ya maswali haya, hutahangaishwa na Wasabato wowote katika imani yako na maisha yako yote. Kumbe, usipokuwa nayo siku zote utayumbishwa kama wimbi la baharini wakati ulipaswa kutulia tuli kama maji kwenye mtungi.

HATIMA: TUSIHANGAISHANE TENA JUU YA SABATO KWANI ILIKUWA KIVULI TU

Kwa sasa Wakatoliki wote tuhitimisha fikra zetu kwa nukuu hii: “Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au SABATO; mambo hayo ni KIVULI cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo” (Kol 2:16-17).

Ndugu zanguni, kama inavyosomeka katika aya hizi, Sabato ilikuwa kivuli na kivuli hakishonewi suti. Sisi ni watu wazima tuachane na Sabato. Nina hakika tutaadhibiwa na Mungu kwa hatia ya kukipa hadhi kitu kisicho na uzito wa kimani.
Imeandikwa na
Pd. Titus Amigu (2016)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CarloJesus,

Hayo yote ni marudio tulisha yatolea ufafanuzi! Ila kama unaamini Biblia na unaisoma naomba unioneshe Kitabu na mafungu yanayosema 1.Bikira Maria alipaishwa Mbinguni na anawasikiliza Wakatoliki Mnapokuwa mnamuomba kwa Shida zenu! 2.Muweke sanamu ndani ya Makanisa yenu 3.Mapadri na Maaskofu wasioe wawe wanafila Waumini.
 
Hayo yote ni marudio tulisha yatolea ufafanuzi! Ila kama unaamini Biblia na unaisoma naomba unioneshe Kitabu na mafungu yanayosema 1.Bikira Maria alipaishwa Mbinguni na anawasikiliza Wakatoliki Mnapokuwa mnamuomba kwa Shida zenu! 2.Muweke sanamu ndani ya Makanisa yenu 3.Mapadri na Maaskofu wasioe wawe wanafila Waumini.
Kiongozi umepaniki....mimi sifahamu lolote kuhusu hayo uliyodokeza

Labda na wewe uyaletee uzi hapa ...litakua Jambo jema


Lakini kuna Wana jf wapya wangependa kujua na kupata ufafanuzi wako pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aiseeeee wewe ni mtunzi sana wa hadithi, unakipaji sana kutunga story za kishenzi na kipagani kuwafurahisha washenzi na wapagani wenzio, kanisa la Waadventista wa Sabato mwanzishi wake ni Mungu mwenyewe na msingi wake ni Yesu Kristo, kanisa la Waadventista wa Sabato halijawahi kuweka imani yake kwa mtu au kikundi cha watu, kanisa la Waadventista wa Sabato linaongozwa na Biblia, Roho ya unabii na kanuni, hivyo naomba nikufahamishe kwamba vitabu vya roho ya kiunabii havipo juu ya Biblia na wala waumini wa kanisa la Waadventista hawategemei roho ya unabii kuielewa Biblia, acha kukurupuka kudanganya watu, kanisa hili ni watu wa Maandiko na wachambuzi wa Maandiko, waumini wake wanasifika kwa kusoma, kutafakari na kuchambua, halina waumini mazezeta, kwa Waadventista hata ukienda kwa katoto kadarasa la 2 katakufundisha Biblia na kukuchambiliwa ukweli wa Bibilia kuliko papa Francis.

Uache udanganyifu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nioneshe sehemu biblia inaonesha hakupalizwa mbinguni
Hayo yote ni marudio tulisha yatolea ufafanuzi! Ila kama unaamini Biblia na unaisoma naomba unioneshe Kitabu na mafungu yanayosema 1.Bikira Maria alipaishwa Mbinguni na anawasikiliza Wakatoliki Mnapokuwa mnamuomba kwa Shida zenu! 2.Muweke sanamu ndani ya Makanisa yenu 3.Mapadri na Maaskofu wasioe wawe wanafila Waumini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aiseeeee wewe ni mtunzi sana wa hadithi, unakipaji sana kutunga story za kishenzi na kipagani kuwafurahisha washenzi na wapagani wenzio, kanisa la Waadventista wa Sabato mwanzishi wake ni Mungu mwenyewe na msingi wake ni Yesu Kristo, kanisa la Waadventista wa Sabato halijawahi kuweka imani yake kwa mtu au kikundi cha watu, kanisa la Waadventista wa Sabato linaongozwa na Biblia, Roho ya unabii na kanuni, hivyo naomba nikufahamishe kwamba vitabu vya roho ya kiunabii havipo juu ya Biblia na wala waumini wa kanisa la Waadventista hawategemei roho ya unabii kuielewa Biblia, acha kukurupuka kudanganya watu, kanisa hili ni watu wa Maandiko na wachambuzi wa Maandiko, waumini wake wanasifika kwa kusoma, kutafakari na kuchambua, halina waumini mazezeta, kwa Waadventista hata ukienda kwa katoto kadarasa la 2 katakufundisha Biblia na kukuchambiliwa ukweli wa Bibilia kuliko papa Francis. Uache udanganyifu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu ungepinga kihoja hili bandiko

Sasa katoto kadogo kuchambua biblia kuliko papa Francis kanaingiaje humu....kimantiki umekosa hoja

Lakini kiroho...umekosa unyenyekevu....wewe Ni mjivuni,na wajivuni baba yao tunamjua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aiseeeee wewe ni mtunzi sana wa hadithi, unakipaji sana kutunga story za kishenzi na kipagani kuwafurahisha washenzi na wapagani wenzio, kanisa la Waadventista wa Sabato mwanzishi wake ni Mungu mwenyewe na msingi wake ni Yesu Kristo, kanisa la Waadventista wa Sabato halijawahi kuweka imani yake kwa mtu au kikundi cha watu, kanisa la Waadventista wa Sabato linaongozwa na Biblia, Roho ya unabii na kanuni, hivyo naomba nikufahamishe kwamba vitabu vya roho ya kiunabii havipo juu ya Biblia na wala waumini wa kanisa la Waadventista hawategemei roho ya unabii kuielewa Biblia, acha kukurupuka kudanganya watu, kanisa hili ni watu wa Maandiko na wachambuzi wa Maandiko, waumini wake wanasifika kwa kusoma, kutafakari na kuchambua, halina waumini mazezeta, kwa Waadventista hata ukienda kwa katoto kadarasa la 2 katakufundisha Biblia na kukuchambiliwa ukweli wa Bibilia kuliko papa Francis. Uache udanganyifu

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii sindano ni Kali Sana. Lazima uweweseke. Kuna vitabu vimeandikwa havitawaacha salama. Vinasambazwa kila mahali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
H = 0
E = 0
L = 50
L = 50
N = 0
Total A =100

G = 0
O = 0
U = 5 ( kama ninyi mfanyavyo)
L = 50
D = 500
Total B = 555

W = 10
H = 0
I = 1
T = 0
E = 0

Total C =11

Total A + B + C
100 + 555 + 11 = 666

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahio umeona wasabato tu??mbona u Uzi wako umegusia kua Anglican ilianzishwa na Huyo mfalme wa uingereza baada ya wakatoliki kumkatalia kumuacha mkewe ambae hajampa mtoto wa kiume???kumbe madhebu ndo yalianza hiv??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
H = 0
E = 0
L = 50
L = 50
N = 0
Total A =100

G = 0
O = 0
U = 5 ( kama ninyi mfanyavyo)
L = 50
D = 500
Total B = 555

W = 10
H = 0
I = 1
T = 0
E = 0

Total C =11

Total A + B + C
100 + 555 + 11 = 666

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ni kichaa!Halafu unaandika ujinga mtupu ndani ya Kanisa la SDA hawamtambui huyo Hellen labda huyo ni wa Kanisa lenu! kama ni Ellen ni sawa! Unajaribu kupost hesabu za kizushi na bado umechemka!Kama ni Ellen alisha fariki miaka mingi iliyopita na hakuna Mrithi wa jina lake ndani Kanisa, mpaka uhusishe jina hilo na mambo ya ajabu!
 
Hayo yote ni marudio tulisha yatolea ufafanuzi! Ila kama unaamini Biblia na unaisoma naomba unioneshe Kitabu na mafungu yanayosema 1.Bikira Maria alipaishwa Mbinguni na anawasikiliza Wakatoliki Mnapokuwa mnamuomba kwa Shida zenu! 2.Muweke sanamu ndani ya Makanisa yenu 3.Mapadri na Maaskofu wasioe wawe wanafila Waumini.

Eti wanafila waumini


Happy dude
 
H = 0
E = 0
L = 50
L = 50
N = 0
Total A =100

G = 0
O = 0
U = 5 ( kama ninyi mfanyavyo)
L = 50
D = 500
Total B = 555

W = 10
H = 0
I = 1
T = 0
E = 0

Total C =11

Total A + B + C
100 + 555 + 11 = 666

Sent using Jamii Forums mobile app

Duuuh .... Makubwa . Watu mnafukunyuaga vitu, jf ni zaidi ya chuo. Nimejifunza kitu kipya tena leo hii


Happy dude
 
Wewe ni kichaa!Halafu unaandika ujinga mtupu ndani ya Kanisa la SDA hawamtambui huyo Hellen labda huyo ni wa Kanisa lenu! kama ni Ellen ni sawa! Unajaribu kupost hesabu za kizushi na bado umechemka!Kama ni Ellen alisha fariki miaka mingi iliyopita na hakuna Mrithi wa jina lake ndani Kanisa, mpaka uhusishe jina hilo na mambo ya ajabu!

H = 0
E = 0
L = 50
L = 50
N = 0
Total A =100

G = 0
O = 0
U = 5 ( kama ninyi mfanyavyo)
L = 50
D = 500
Total B = 555

W = 10
H = 0
I = 1
T = 0
E = 0

Total C =11

Total A + B + C
100 + 555 + 11 = 666

Sent using Jamii Forums mobile app

Mambo ni moto kweli kweli


Happy dude
 
Luka 16:14-18
[14]Basi Mafarisayo, ambao wenyewe ni wapenda fedha, waliyasikia hayo yote, wakamdhihaki.
[15]Akawaambia, Ninyi ndinyi mnaojidai haki mbele ya wanadamu, lakini Mungu awajua mioyo yenu; kwa kuwa lililotukuka kwa wanadamu huwa chukizo mbele za Mungu.
[16]Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu.
[17]Lakini ni vyepesi zaidi mbingu na nchi vitoweke, kuliko itanguke nukta moja ya torati.
[18]Kila amwachaye mkewe na kumwoa mke mwingine azini; naye amwoaye yeye aliyeachwa na mumewe azini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo story yako umeiandika kiushabiki sana na kukandia uongo ili tuu upotoshe watu .

Mtu akisoma story yako anaona tuu mihemko tupu,Kwa watu makini hawezi kukubaliana na andiko lako.
Hizo hoja 12 za wasabato hujaweza kuzijibu kwa majibu najua huna majibu ya hizo hoja kwa sababu ni hoja za kweli



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom