Wasabato, hii kitu ina maana gani?

Wasabato, hii kitu ina maana gani?

Mkuu hii siyo sumu mpya, haya ni mambo ambayo yalikuwepo tokea enzi na enzi, huu ni ukweli ambao ninyi "vipofu" mmefichwa ili msiujue. Mmefichwa sababu hamuipendi KWELI bali mnaupenda uongo na kuutenda ndiyo maana mmeletewa uongo ili muufurahie zaidi. Kwenye maandiko matakatifu hakukuwa na neno msalaba, bali lilikuwepo neno nguzo au mti. Hili neno "msalaba" limeingizwa ili kuwapotosha watu na kuwafanya watu washikamane na UPAGANI. Msalaba asili yake ni UPAGANI na BWANA MUNGU kamwe hafungamani na Upagani, wala vitu vya kipagani haviko kwake.

Mkuu fahamu kwamba ukimtafuta MUNGU kwa dhati hakika utamuona na Yeye atakufunulia mambo usiyoyajua wewe wala babu zako. Tatizo lenu ninyi Wakatoliki mnabweteka sana na hamtaki kujishughulisha katika kuitafuta KWELI ya MUNGU.
Kwanza jina tu la kanisa lenu linatia mashaka, CCOG????

Elimu pia mnazopewa mf hii ya msalaba naona pia mnapofushwa kwa hadithi za Esopo. Mtu anajitungia then anawalisha kondoo ujinga!

Je, nyie na hicho kijidhehebu chenu ndio wenye Biblia halisi kuliko wengine? Je, source ya hiyo Biblia yenu yenye maandishi yanayokinzana na wakristo wengine ni ipi?

Kikubwa Tenda wema, mpende Mungu na jirani baaasss! Zilizobaki ni mbwembwe za wajasiliamali wasaka sadaka!
 
Sasa kama wanaupinga msalaba unategemea wawekwe kundi gani?
Wapinga Kristo mkuu, hii haina ubishi ,hizi ndzo roho za mashetani zidanganyazo, mtume paulo kwa wagaratia sura ya 6:14 anasema laikini mm hasha nisione fahari juu ya kitu chochote ila msaraba wa Bwana wetu Yesu kristo,ambao kwa huo ulimwengu umesurubishwa kwangu na mm kwa ulimwengu, sasa mtu au kikundi cha watu wanaoupuuza msaraba ambao ndiyo asiri ya mema hao nahukumu kusema ni wapinga Kristo
 
Hakuna kitu unajua wewe, yaani uko gizani mbaya sana.
Tunachotofautiana ni waalimu tu, hata wewe unachojua ni sumu tu isiyo na faida then unakuja kuiita "kweli" mtoto akizaliwa akaambiwa 1+1=9 ataamini hivyo tu.

Kwa taarifa yako I was once msabato kindakindaki, baada ya kuona tunaoshwa kwa upupu nikajiondoa kwa kasi ya boing!!
 
Tunaposema mapokeo najua tunamaanisha ni mafundisho ya wanadamu ni tamaduni za kibinadamu ,yaani ni kinyume cha mafundisho ya Mungu. Sasa ukisema biblia ni mapokeo sijakuelewa hapo mkuu, labda tusadiane

Kaangalie maana ya "mapokeo" katika Kamusi. Biblia hasa Agano Jipya hapo awali halikuwa katika maandiko Bali ni vitu ambavyo Mitume waliwahaadithia wafuasi na wafuasi wakawaadithia waliowafuata mpaka hapo walipoamua kuyaweka katika maandishi. Kumbe yaliyomo katika Biblia ni masimulizi yaliyotokana na njia ya Mdomo na hivi hayo kwa namna yoyote ni mapokeo.
 
Waislamu na Wakatoliki ni kitu kimoja ingawa wengi hawaijui "siri" hii iliyofichika kwa miaka mingi sana. Muasisi wa Ukatoliki ndiyo huyo huyo muasisi wa Uislamu. Siri hii imefichika lakini wenye hekima na busara yaani wale wanaozishika Amri za MUNGU na imani ya YESU KRISTO wanaijua siri hii maana imedhihirishwa kwao.

Lakini kwa faida ya wengi nitaigusia kidogo siri hiyo, nayo ni hii; mtoto wa kike wa Muhamad alikuwa anaitwa FATIMA na aliishi na kufia eneo moja kule Portugal na eneo hilo alipozikwa leo hii linajulikana kama FATIMA. Hapo hapo alipofia Fatima mtoto wa Muhamad ndipo alipotokea yule "mwanamke wa ajabu" na kujifanya yeye ni mama ya MESSIAH. Mwanamke huyo wa ajabu aliwatokea wale watoto 3 wanaojulikana kama watoto wa FATIMA!. Na moja ya mambo aliyowaambia ni kuwa eti, dini zote ni sahihi mbele za MUNGU!... Ukweli ni kwamba dini zote siyo "sahihi" mbele za MUNGU.

Leo hii Waislamu huwa wanaenda pale FATIMA kuabudu na Wakatoliki nao wanaenda pale pale FATIMA kuabudu. Hili ni fumbo na udanganyifu wa Shetani ili aendelee kuwapoteza wale wote wasioipenda KWELI ya MUNGU. Uislamu ni kazi ya Shetani na Ukatoliki pia ni kazi ya Shetani.

Mwenye masikio na asikie....
asante kwa porojo.
 
nimempa maoni yangu kuwa, ni platform ya kuandikia majina na taarifa ya marehemu, maana wasingeandika kwenye tiles.
Ila kama kanisa hakuna makubaliano au doctrine kuhusu unapoandika jina au taarifa za marehemu basi mahali unapopatumia pakaeje ingawa kwa asilimia kubwa Juu ya kaburi wanaweka kama jiwe maalum au kamnara kadogo ka kuandikia taarifa za muhusika hasa ulaya kulingana na style mbalimbali za graveyard. Inaonekana majibu hayo kwake ni mepesi yeye anataka majibu magumu kwa maswali ambayo anadai ni mepesi inagawa pia anadai majibu hajui. I

habari za siku mingi mkuu.
Habari ni njema kabisa.
Mi nimeona jitihada zako kujaribu kuliondoa swali kwenye msingi wake.

Kwa lugha nyepesi ni kwamba ndani ya kanisa kila mmoja anaamua utaratibu na mtindo wake. Akiamua kuandika kwenye ubao wenye umbo la msalaba siyo kosa na hata akitengeneza sanamu ya ndama na kuitumia kuandika maelezo yake kisha kuweka kwenye kaburi siyo shida.

Mkuu hebu naomba tusaidiane hapa.
 
Unafahamu msimamo wa Ellen G White juu alama na nembo...? Unafahamu kuwa kanisa la SDA linasema alama zote ni za shetani na ni upagani...? Je! Lini mmneanza kubadili mafundisho ya muanzilishi wa Usabato Ellen G White...?
Wew ndo unafahamu hivo na wew si msabato
Mimi ni muadventista msabato wa muda mrefu.
 
Hicho chaweza kuwa kibao cha kusimika baadae mbele ya kaburi kwenye mchanga ili kumtambulisha aliyelala kwa ndugu watakaochelewa mazishi
 
Wew ndo unafahamu hivo na wew si msabato
Mimi ni muadventista msabato wa muda mrefu.
Unaweza kuwa Msabato fuata upepo tuu.... Kwataarifa yako GC kwasasa inafanya marekebisho mengi ya mafundisho ya EGW....na nyaraka zingine zenye mafundisho tata ya EGW yanateketezwa kama si kufichwa..

Kwani hujui Fundisho la Utatu Mtakatifu liliwekwa juzi juzi tuu....Hujui kuwa GC ilificha nyaraka za EGW zinazopinga Utatu Mtakatifu...


Endelea kuwa maamuma....na ni bora uendelee kuwa maamuma...ukifukua zaidi juu ya SDA utakufa
 
Inamaana mafundisho ya Wasabato siyo consinstance.....???
Sawa wameng'oa!
Maswala yanakuja...

1. Kwanini wang'oe
2. Baada ya kung'oa hiyo alama T inamaanisha nini. ??
Hivyo unataka kutuambia mafundisho na miiko ya kisabato haipo uniform kwa kanisa zima...? Kwamba kanisa sio moja...?

Kwamba pengine kulingana na mazingira mahalia na kutoka na sababu za kimazingira kusali Jumamosi hakupo ila Jumapili...??

Kwamba kutokana na mazingira kuna Wasabato wanakula nguruwe kwakuwa eneo husika hakuna nyama mbadala...???

Ndio maana nikakuuliza unafahamu msimamo waSDA...? Au wewe sio SDA..? Ama hujui unachokitetea.. ? Au ndio kujitoa ufahamu huko..?
Kanuni kuu ya Kanisa ni Bibilia 66 Books.
Kutokq katika Bibiliq Kuna Misingi 28 ambayo ni Universal.
Lakini katika operation kuna miongozo ya Division ambayo kulingana na mahala husika bila kuvunja kanuni za kibibilia wanaoperate kwa utofauti.
Mfano Ukienda Division ya Middle East huwezi kukuta kuna mkutano wa Hadhara lkn kuna underground movement za kupenyeza imani na watu wengi wanabatizwa kimyakimya. Ukija Tanzania Au ECD Tunafanya mambo hadharani.
Kwa Kukusaidia hata kanisa la Mitume lilikuwa Moja, lenye umoja, lkn kulikuwa na tofauti kati ya kanisa la Yerusalem na Maeneo mengine bila Kuvunja misingi mikuu ya Injiri, Mfano Tohara.

Kuhusu kung'oa mbao hizo ni hisia zako na JF huwa hatujadili hisia na mihemko ya mtu vinginevyo ukili na wewe ndiye fundi uliyeunda hilo jeneza.
Pia Sioni Huo Uoga wa kung'oa sehemu ya platform ya kuandikia taarifa ya marehemu kisa wanaogopa msalaba wakati wako wasabato wengi hata hapa tanzania wanazikwa na taarifa zao zinaandikwa kwenye mbao zenye umbo sanjari na msalaba. Na haijaanza leo tangu kitambo. Nashangaa wapenzinwa kuabudu mbao za kutunzia taarifa mnaweweseka nini. Hata wiki mbili zimepita mchungaji kaendesha huduma ya mazishi ya mtoto na mbao za taarifa zilikuwa na umbo la kujumlisha.
 
Kuhusu kung'oa mbao hizo ni hisia zako na JF huwa hatujadili hisia na mihemko ya mtu vinginevyo ukili na wewe ndiye fundi uliyeunda hilo jeneza.

Taarifa nilizozipata ni kuwa Huo msalaba uliokatwa katikati, wakati wa kuagwa pale Lugalo Msalaba huo ulikuwa kamili kabisa....

Wadau wanashangaa kwann umekatwa
 
Pia Sioni Huo Uoga wa kung'oa sehemu ya platform ya kuandikia taarifa ya marehemu kisa wanaogopa msalaba wakati wako wasabato wengi hata hapa tanzania wanazikwa na taarifa zao zinaandikwa kwenye mbao zenye umbo sanjari na msalaba.
Usitufanye wote matahira huku ndani sawa! Hakuna msabato anayezikwa na juu ya kaburi kukawekwa msalaba....

Huko ni kwenda kimyume na mafundisho ya muasisi wa SDA Bi Ellen g White
 
Habari ni njema kabisa.
Mi nimeona jitihada zako kujaribu kuliondoa swali kwenye msingi wake.

Kwa lugha nyepesi ni kwamba ndani ya kanisa kila mmoja anaamua utaratibu na mtindo wake. Akiamua kuandika kwenye ubao wenye umbo la msalaba siyo kosa na hata akitengeneza sanamu ya ndama na kuitumia kuandika maelezo yake kisha kuweka kwenye kaburi siyo shida.

Mkuu hebu naomba tusaidiane hapa.
hahaha jitihada gani mkuu.
Ukienda kanisa la wasabato chenai wanavua Viatu, ukija kwetu tunavaa.
Hata taratibu za Uendeshwaji wa Ibada zinaweza kutofautina bila kuvunja kanuni za msingi za kibibilia. Ndio maana hata kanuni ya kanisa inatoa option zaidi ya mbili na kutoa room of improvement ili watu wabarikiwe zaidi kulingana na mahala. Sio dhambi.
Kuna Vitu vingi ambavyo havivunji kanuni za kibibilia ambayo kuna utofauti kati ya division na division ili injili ipenye kwa wahusika bila compromise Biblical Principles na Fundamental Believes.
Kama huwa unasoma bibilia utanishangaza kushangaa utofauti wa baadhi ya vitu bila kuvuja kanuni za kimaandiko ambazo zilikuwepo hata kanisa la awali. Ukisoma ule mkutano wa Baraza la kanisa uliofanyika Yerusalem utagundua Kanisa lililokuwa Yerusalem lilikuwa na utofauti na kanisa lililokuwa antiokia au hata efeso.

Kuhusu Kaburi na sehemu ya Kutunzia Kumbukumbu za Marehemu NDAMA HaPANA (taarifa za marehemu utaziweka puani au kwenye masikio?), Ila kibao sawa maana lengo ni kuwasilisha taarifa ila sio umsalaba ule. Kimsingi kanisa linahimiza simplicity katika kila jambo na kuepuka kila mwelekeo wa kiibada au ambao utaleta mashaka kwa wasioamini.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom