Wasabato, hii kitu ina maana gani?

Wasabato, hii kitu ina maana gani?

Maandiko matakatifu yapo wazi kwamba Tusisujudie wala kuabudu sanamu yoyote ile na amri hii si kwa wasabato tu bali ni kwa wote
Mind you kuweka vinyago vya watu au matoy nyumbani kwako sio shida as long as hauviabudu wala kuvisujufia
Kwamba unakubaliana kuwa sanamu na picha hazina shida kuwa nazo ili mradi tu huziabudu na kuzipa uhai kuchukua nafasi ya Mungu...?
 
Unazingua kuna Alama gani hapo....? Mi nafikiri huo ni ubao tu wakuandikia Details za Marehemu husika.
Kwani wasingeandika hapo kwenye tiles au marble...? Kwann wasitumie rectangular board ili hayo maandishi yaenee vizuri...
 
Tunaposema mapokeo najua tunamaanisha ni mafundisho ya wanadamu ni tamaduni za kibinadamu ,yaani ni kinyume cha mafundisho ya Mungu. Sasa ukisema biblia ni mapokeo sijakuelewa hapo mkuu, labda tusadiane
Yes! Biblia ni mapokeo....haijateremshwa....ni kazi za watu zilizopokelewa na kanisa katoliki, kisha kuchambuliwa vizuri na kuwa Compiled kisha wakaita hicho kitabu Biblia..
 
Eti ehhh....kwamba hicho ni kibao....kwamba unatufanya sisi ni matahira...??

Mimi sijasema huo ni Msalaba....kwanza huwezi kuwa msalaba huo......

Kwa haraka haraka inaweza kuwa ulikuwa Msalaba ila umekatwa kwa juu...

Ndio ninauliza hiyo alama ina maanisha nini...?
Sasa ndio nmekwambia hicho kibao kinaonesha DOB na DOD mkuu
 
Mkuu nataka nifahamishwe hiyo ni alama ya nini...??? Ina maahisha nini..?

Na kama ni alama inayo masnisha kitu fulani, mbona sasa Mtakuwa mnaenda kinyume na Mafundisho ya muanzilishi wa Usabato Ellen G White, ambaye alipiga marufuku alama yoyote kwenye Usabato...?
Bado napata ukakasi na sentensi zako "za ellen ,kazuia,mwasisi" weka vzr
Maandiko yamekataza hzo alama na sio kwamba Ellen kazuia
Ngoja niendeleee kukufuatilia reply zako
 
hayo maneno yaliyo andkwa hapo juu Kama kumbkumbu kwa wataofika pale. ...
Wewe unafikili Yale Maneno yangeandkwa vipi ? Wao wamelaza na mengne chini
Naomba jibu wangetumia namna gn kuyaandka ili kwamba yasomeke vzr???
 
Kwa uelewa wako ili andiko lina maana gani. .?

Kutoka 20:4
Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
 
hayo maneno yaliyo andkwa hapo juu Kama kumbkumbu kwa wataofika pale. ...
Wewe unafikili Yale Maneno yangeandkwa vipi ? Wao wamelaza na mengne chini
Naomba jibu wangetumia namna gn kuyaandka ili kwamba yasomeke vzr???
Kwanini wasingeyaandika kwa kutumia kibao cha Marble (rectangular) ili hayo maandishi yaenee vizuri....hilo kaburi linaoneka ni expensive sana....kwanini wasitumie ubao mkubwa...

Hapo inaonesha na kama mwanzoni ulikuwa ni msalaba, ila wakaukata hapo juu...kutengeneza alama ya T....

Ndio nauliza hiyo T inamaanisha nini..?
 
"Kwa wanaopotea msalaba ni upumbavu, bali kwetu sisi tunaookolewa msalaba ni nguvu ya Mungu" 1Wakolintho 1:18
Ahsante mkuu....

Kwa mantiki hiyo Wasabato ndio wale maadui wa Msalaba waliotajwa na Biblia...?
 
Ndugu yangu Otorong'ong'o elewa kuwa tunaoabudu siku ya JUMAMOSI ama siku ya SABATO tupo kwenye madhehebu mengi sana yanakadiria kufikia madhehebu tofauti kama 500 na zaidi. Mimi na dhehebu langu hatutumii kabisa aina yoyote ile ya "sanamu" au picha au msalaba. Isitoshe sisi katika kanisa la KWELI la MUNGU tunafahamu kuwa MESSIAH hakufa "msalabani", bali alikufa "mtini", yaani alitundikwa kwenye "nguzo" na siyo "msalaba".

Ukisoma Biblia yako vizuri(nafahamu wewe huijui wala huisomi Biblia), utaona kuwa YESU alitundikwa kwenye "NGUZO" na siyo kwenye MSALABA. Kuna tofauti kubwa sana ya NGUZO na MSALABA..... Ukiona kwenye Biblia pameandikwa neno "msalaba" fahamu kwamba ni makosa ya "utafsiri wa lugha" yaliyofanywa kwa makusudi na watafsiri wa mwanzo.

Tunafahamu kwamba vitabu vyote vya Agano Jipya viliandikwa kwa Lugha ya KOINE GREEK. Ni kitabu kimoja tu cha WAEBRANIA ndicho kilikuwa kimeandikwa kwa KIEBRANIA. Neno la Kigiriki linalomaanisha NGUZO ni "stauros", neno hili ndilo linalopatikana kwenye maandiko ya kale na maana yake ni nguzo na siyo "msalaba". Neno la Kigiriki linalomaanisha "msalaba" ni "diaschizo", neno hili diaschizo halikuwepo kabisa katika vitabu vyote vya kale vya Injili.

Msalaba mnaoutumia ninyi Wakatoliki asili yake ni UPAGANI ulioanzishwa na Tamuzi huko Babiloni ya kale. Herufi "T" ilitumika ili kumuenzi Tamuzi ambaye baada ya kufa aliabudiwa kama mungu. Kutokea hapo Upagani ukaenea dunia nzima na alama yao kuu ni "+" msalaba ambao asili yake ni neno Tamuzi.

Hivyo basi sisi tulioa katika CCOG kamwe hatutumii alama ya "msalaba" sababu tunaujua UKWELI, na ukweli ni huu; MUNGU hafungamani na Upagani hata siku moja. Huwezi kuchanganya mambo ya MUNGU na mambo ya Beliari, huwezi kuchanganya IBADA ya MUNGU na ibada ya mashetani kama wafanyavyo Wakatoliki na Maprotestant.


Hivyo basi kutokana na swali lako nafikiri hao SDA ndiyo wanatakiwa kukujibu na siyo mimi. Nafikiri umeelewa sasa kuwa mimi siyo Msabato wa SDA, mimi ni MSABATO wa CCOG, ili kujifunza zaidi ingia hapa; www.ccog.org
Duh, hawa wachungaju watatupasua vichwa kwa kutulisha sumu mpya na advanced daily!
 
Waislamu na Wakatoliki ni kitu kimoja ingawa wengi hawaijui "siri" hii iliyofichika kwa miaka mingi sana. Muasisi wa Ukatoliki ndiyo huyo huyo muasisi wa Uislamu. Siri hii imefichika lakini wenye hekima na busara yaani wale wanaozishika Amri za MUNGU na imani ya YESU KRISTO wanaijua siri hii maana imedhihirishwa kwao.

Lakini kwa faida ya wengi nitaigusia kidogo siri hiyo, nayo ni hii; mtoto wa kike wa Muhamad alikuwa anaitwa FATIMA na aliishi na kufia eneo moja kule Portugal na eneo hilo alipozikwa leo hii linajulikana kama FATIMA. Hapo hapo alipofia Fatima mtoto wa Muhamad ndipo alipotokea yule "mwanamke wa ajabu" na kujifanya yeye ni mama ya MESSIAH. Mwanamke huyo wa ajabu aliwatokea wale watoto 3 wanaojulikana kama watoto wa FATIMA!. Na moja ya mambo aliyowaambia ni kuwa eti, dini zote ni sahihi mbele za MUNGU!... Ukweli ni kwamba dini zote siyo "sahihi" mbele za MUNGU.

Leo hii Waislamu huwa wanaenda pale FATIMA kuabudu na Wakatoliki nao wanaenda pale pale FATIMA kuabudu. Hili ni fumbo na udanganyifu wa Shetani ili aendelee kuwapoteza wale wote wasioipenda KWELI ya MUNGU. Uislamu ni kazi ya Shetani na Ukatoliki pia ni kazi ya Shetani.

Mwenye masikio na asikie....
We jamaa ushakuwa polluted, cdhan ka utasalimika. Hivi FATIMA ndipo asili ya kanisa Katoliki? Je, FATIMA ndiye mwanzilishi wa uislamu? Muwe mnajiongeza mnapopofushwa na mafundisho mfu ya wachungaji wenu!!
 
Ni kweli hawaamini msalaba na hapo hakuna msalaba ila ni T kwaajili ya maandishi au anwani
 
Yaani huo si msalaba bali ni kifaa kilicho tumika kama utambulisho wa marehem alie pumzika pale chini
 
View attachment 919233

Wakuu mbali mbali habari za Wakati kama huu...

Nimeleta huu mahsusi ili Wasabato watuambie hii ina maanisha nini...

Tunafahamu ndugu Yetu Isaack Gamba(R.I.P) alikuwa ni Msabato.....Na kwa kadiri ya Mafundisho ya Wasabato ambayo yalihasisiwa na Nabii Ellen Gould White, Msalaba kwenye Kanisa la SDA ni haramu, upagani....Kwa Kifupi Ellen G White alikataza waumini wake kuwa na misalaba na alama zozote kwenye kanisa lake....

Sasa nilikuwa naomba ufafanuzi kutoka kwa Wasabato hicho ni kitu gani kwenye kaburi la ndugu yetu Isaack Gamba....maans siyo Msalaba...je! Ni alama ya nini...? Inawakilisha kitu gani...?

Je! Mbona EGW alipinga alama ndani ya Kanisa....

Nawakaribisha..

@sactus anacletus
mitale na midimu
Dumelang
blackstarline
@Idhiambo
Ntuzu
Kitaja
Wasabato wamepotea mno.

Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.

1 Wakorintho 1:18
 
Gamba alipoagwa Lugalo waliweka msalaba kamili. Wamefika Bunda wakauchinja juu ikawa T. Wanahangaika tu. Msalaba halisi ni umbo la kila mwanadamu anapobana miguu chini pamoja na kutawanya mikono kwa pembeni
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom