Wanyamwezi na wasukuma

Wanyamwezi na wasukuma

JokaKuu

Nashukru kwa kunielewa katika baadhi ya vipengele kwenye postings zangu.

Kusema kuwa Urais haumaanishi maendeleo si kweli. Kama Rais atakaa pale Ikulu kwa miaka 5 au kumi halafu tusione maendeleo basi huyo hatufai.

Ni kweli Nyerere ametawala taifa hili kwa miaka 24 hakuleta maendeleo si Butiama wala Tanzania yote. Wewe unategemea kweli kwa sera za siasa ya Ujamaa na Kujitegemea zingeweza kuleta maendeleo yeyote kwao Butiama au Taifa hili??Joka Kuu huwezi kunishawishi kuwa Rais hahusiani na Maendeleo ya nchi husika iwe Tanzania au nchi yeyote duniani.

Tunamshukru Nyerere kutuletea Uhuru na mambo mengine kama umoja na mshikamano. Lakini hili la Maendeleo Baba wa Taifa mimi ninampa below average. Kila Mtanzania anajua Tanzania imeanza kubadilika economically and Politically baada ya Mzee Alhaji Ali Hassan Mwinyi(rtd president) al-maarufu Mzee Ruksa.

Amekuja Mkapa akazama kwenye Utandawizi ikawa kila kitu ni kubinafisisha au kwa lugha nyingine kugenisha kila kitu. Kwa hiyo Mkapa alizama kwenye kujinufaisha mwenyewe na wawekezaji.Hata Mkapa huko kwao Nanyumbu nasikia hajajenga hata nyumba. Nasikia alikuwa akienda likizo anafikia nyumba ya ma-padre! What a shame. Lakini the same president nasikia ana nyumba sijui kama kajenga au kanunua a very executive house huko Lushoto kwa Wasambaa. Pengine na huko kwa wakwe zake Kilimanjaro.

Kwa hiyo mimi nasema Rais ni chachu ya maendeleo,anaweza aidha akajenga au akaharibu kabisa uchumi wa nchi. Hivo bado narudi kwenye point yangu kuwa hulka ya mtu inaweza ika-contribute a lot economically and politically.

Hapo mwanzo nilisema kuwa Wasukuma na Wanyamwezi ni watu waadilifu,waaminifu na Wachapa kazi. Kwa hiyo siku wakipewa nafasi ya kuingia pale Ikulu wanaweza kubadilisha mambo. Tuna watu wachapa kazi wazuri kama kina John Pombe Magufuli Waziri wa Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo. Unategemea mtu kama huyu akipewa Ikulu kutakuwa na ubabaishaji? Magufuli ame-prove kwamba anaweza ku-fit any Ministry kwa maana hiyo anaweza kukaa hata Ikulu.

Tuna kina Dk. William Shija,ambaye sasa yuko Uingereza kama Katibu Mkuu wa Mabunge ya Jumuia ya Madola. All these are prominent figures from the Sukuma and Nyamwezi tribes!!!!

Mheshimiwa Sitta ni kweli amekuwepo kwenye madaraka katika karibu awamu zote tangu enzi za Mwalimu. Sitta hana ufisadi wa aina yoyote labda kama unataka kumzushia au kumpakazia. He is clean na ni mchapa kazi mzuri tu na ndiyo maana sasa hivi anaendesha Bunge letu kisomi kwa slogan ya "Standard and Speed)si ubabaishaji kama wa kina Pius Msekwa(mkara!). Spika ambaye alikuwa very biase kwa CCM against Upinzani. That is not democracy at all.

We need people who can bring changes to our country. Hatutaki blaa blaa,ubabaishaji na usanii mwingi. We want changes now not tomorrow,we have the people who can bring those changes. These people are Sukumas and Nyamwezis.

Habari ya kwamba Wabunge wa mikoa ya Shy,Mza na Tbr hawajaleta maendeleo siyo kweli mheshimiwa Joka Kuu. Hawa wabunge wana-fight sana bungeni kwa ajili ya Mandeleo katika mikoa yao lakini serikali inawatilia kauzibe. Utakumbuka kwenye kikao cha Bunge la Bajeti mwaka huu. Kulitolewa hoja nzito sana na Mheshimiwa Selelii kuhusu Barabara ya Segera-Chalinze. Kuwa barabara hiyo iko kwenye kiwango cha lami lakini ilikuwa imeanza kupanuliwa tena iwe 2 ways. Selelii akahoji inakuwaje barabara ya lami iendelezwe kupanuliwa ilhali kuna barabara zilishapigiwa kelele Bungeni tangu enzi za Mwalimu ziwekwe lami lakini mpaka leo hakuna lami. Kila Bajeti hakuna fedha. Na hii ni kwa mikoa hiyo tu ya Wasukuma na WANYAMWEZI. Mikoa mingine ya kina Shukru Kawambwa na kina Pesambili Mramba(fisadi) fedha ya kujenga na kupanua mabarabara kwenye maeneo yao ipo...!!!!Why???Kwanini???
 
Hongera Edward Kidaha Makwaia on your big day,saturday!
Watu wa BOT ,mnamjua vizuri Mr Makwaia kwenye kitengo cha kompyuta.
His father Chief Makwaia and Brother were decent guys,but the system put them down.Mpaka leo Wasukuma wamekosa mwelekeo!!!!!!!
October 26, 2009

Mh. Edward Kidaha Makwaia

Huyu pichani ni Mh. Edward KIDAHA Makwaia ambaye tarehe 31 octber 09 atatawazwa kuwa chifu wa Busia. Edward ni mtoto wa Chief David Kidaha Makwaia.

Sherehe hizo zitafanyika Busia katika mkoa wa
shinyanga siku ya jumamosi kuanzia saa nne asubuhi.

nawasilisha
mdau kassimOctober 26, 2009

mdau kassim
16511139-6722687538094619157

16511139-6722687538094619157
 
..historia ya Chifu Kidaha Makwaia.

..Chifu mpya atakuwa Paramount Chief wa Wasukuma wote, au atakuwa Chifu wa Busia-Shinyanga?

Chief David Kidaha Makwaia of Tanzania, who has died aged 84, was one of the last great bridges between colonial and postcolonial Africa. Paramount chief of the Sukuma Federation and an ally of Tanganyika's governor from 1949 to 1958, Lord Twining, Makwaia liaised between British rulers and various constituencies of their Tanzanian subjects, witnessing East Africa's transition from imperialism through independence to postcolonial repression.Makwaia's life offers a window to the overlapping identities and cosmopolitan experiences that defined the colonised elites of 20th-century Africa. He was born a Muslim son of the Sukuma chief, Makwaia Mwandu of Usiha, in the Shinyanga region of Tanganyika. He trained in agriculture at Uganda's Makerere University College in the early 1940s before entering Lincoln College, Oxford, where he read principles and praxis of local government, philosophy and politics.
Makwaia's political life unfolded along multiple channels bestriding the worlds of Tanzania's colonial rulers and its local chiefdoms. He succeeded his father as Usiha chief in 1945 and later became "paramount chief" of the Sukuma Federation, an autonomous institution of more than 50 chiefdoms, with its own offices and flag. This won him British recognition as an authoritative native voice - a privilege cemented by his appointment in the same year as the first of two Africans to Tanganyika's Legislative Council (Legico).
Other offices followed. In the course of the 1950s, he served as the only African member of the East African royal commission on land and population, was an unofficial member of the governor's executive council, and a consultant to the colonial government as an administrator in the African aspirations section of the social welfare department.
He was a guest at Queen Elizabeth's coronation in 1953; two years later he was awarded an OBE. He was viewed by the British as a likely president of Tanzania. Along the way, Makwaia underwent a conversion, embracing Roman Catholicism. This reawakening shaped his subsequent sense of mission. Although one of the most influential chiefs in East Africa, he was not driven by the need for power, but had always considered himself a servant of the people.
As the winds of independence gathered steam, he facilitated the political rise of his long-time college friend Julius Nyerere by winning him British support as well as by securing the allegiance of Sukuma chiefs to Nyerere's party, Tanu (Tanganyika African National Union). As prime minister, later president of independent Tanganyika, Nyerere repaid Chief Kidaha, as he was known, by abolishing the role of chiefs, and banishing him for some months to the remote Tunduru district of the Southern Province for undisclosed reasons. This experience alienated him from politics forever, prompting him to turn his energies to private business and religious pursuits.
In the 1960s and 1970s, he served as managing director of Market Research (T) Ltd, and was appointed public relations officer of the Nairobi-based East African Railways and Harbours administration. Upon his retirement in 1975, he moved to the northern Tanzanian town of Moshi, where he operated a private insurance agency. Active in local religious affairs, he founded the Moshi chapter of the Order of Franciscans.
At the time of his death, Chief Kidaha had resumed the leadership of the Sukuma community from his late brother Hussein, and was active in preserving Sukuma cultural legacies. He was buried at Ibadakuli in Shinyanga, the site of his state house during the heyday of his chiefdom. Most people who met the chief commented on his charismatic yet welcoming presence. He was proud of having fulfilled his promise to his father to ensure all his 43 siblings were properly educated.
He is survived by his wife, Grace, his former wife, Mary, four children, Misuka, Edward, Jonathan and Simona, eight grandchildren, and two great grandchildren.
· David Paul Kidaha Makwaia, politician and businessman, born May 7 1922; died March 31 2007
 
Makoye2009,

..bora ungeanza kuwashika mashati Wasukuma na Wanyamwezi wenzako kuliko kuporomosha lawama to the rest of us kwa matatizo yanayolikabili taifa zima.

..Tanzania nzima ina matatizo kama hayo uliyoyazungumzia kwamba mnayo huko Usukumani na Unyamwezini.

..Chunya na Mererani wameachiwa mashimo wakati madini yao yametoweka. Tanga wameachiwa mapori pale yalipokuwa mashamba ya mkonge, maeneo ya Kusini zao la korosho liliporomoka kutokana na operesheni vijiji. Kilimanjaro wanalia vyama vya ushirika vilivunjwa na kuwatia umasikini, Mbeya,Rukwa,Songea,Morogoro "big 4 regions" wanadai wao ndiyo wanaolisha lakini hawaoni maendeleo etc etc.

..utaona kwamba kila eneo la Tanzania, infact kila kabila, likiamua linaweza kutoa madai kama yako. sasa siyo vizuri kunyooshea kidole maeneo/makabila mengine, wakati sote tunataabika na utawala mbaya wa CCM.

..mwenzako alikuja hapa akalalamika kwamba Wasukuma na Wanyamwezi mmenyimwa nafasi za kutumikia ktk uongozi. akaongeza kwamba hata nafasi za ufisadi mmepunjwa, kana kwamba ufisadi ni jambo la kujivunia.

..tumemuonyesha hapa kwamba Watanzania toka Usukumani na Unyamwezini ambao walishika madaraka makubwa ktk taasisi nyeti hapa Tanzania.

..wakati mwenzako analalamika kwamba Wasukuma na Wanyamwezi mmenyimwa nafasi za uongozi, wewe unaibuka unadai mlipewa nafasi hizo lakini hiyo ilikuwa ni hujuma kwenu.

..pia nimesikitishwa sana na kitendo chako cha kutoa maneno ya dharau kwa Mzee Rashidi Mfaume Kawawa "Simba wa Vita." binafsi nadhani inabidi ujipange upya na urudi ukiwa umetulia kidogo. hii lugha na madai uliyoyatoa would make some ppl uncomfortable and not willing to associate with you.

NB:

..kwa taarifa yako Paul Bomani aliwahi kushika nafasi nyeti ya Waziri wa Fedha, kabla hajateuliwa Balozi Marekani.

..pia Paul Bomani hakuwahi kushindwa uchaguzi na hivyo kulazimika kuondoka wizara ya Fedha? wenye kumbukumbu naomba mnisaidie.

..jaribu kuwabana wabunge wa Usukumani na Unyamwezini ili wakusanye nguvu za wananchi kuleta maendeleo huko.

..pia Wabunge wengine huko ni matajiri[Diallo,Masha,Salum Khamis Salum,..] wakubwa, haitakuwa vibaya kama watajitolea kusaidia na kuchangia maendeleo.

..Wabunge kama Selelii nao wajitahidi kuandika project proposals na kutafuta wafadhili kwa miradi mbalimbali, siyo kusubiri kupiga kelele kwenye vikao vya bunge. huyu anapaswa kuiga mfano wa mpiganaji mwenzake Anna Kilango ambaye juzi amechangisha milioni 300 kwa chama cha wakulima wa tangawizi jimboni kwake.

Jokakuu:

Jokakuu:

Ujamaa sucks. Kitu kilichorudisha nyuma maendeleo ya Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Tabora na mingineyo ni siasa za Ujamaa. Nimeishi Mwanza.

Wasukuma ni watu wanaotafuta pesa kwa kazi ze juhudi na vilevile wanaojua kutumia. Vitu hivi viwili ni muhimu katika maendeleo ya uchumi wa jamii yoyote.

Mtu yoyote aliyekuwepo Mwanza na kushuhudia juhudi za ujenzi wa kiwanja cha Kirumba, angeweza kusema kuwa watu wa Mwanza wangeweza kujenga mabarabara kwa kujitolea bila kuomba misaada kutoka serikalini.

Lakini juhudu zao zinakwamishwa na mipango mibovu ya kiserikali.
 
Zakumi,

..nakubaliana na wewe kwamba Wasukuma ni wachapakazi wazuri tu.

..pia napenda kuongeza kwamba mikoa ya Mza,Shy,Tbr, imebarikiwa rasilimali nyingi.

..nakubaliana na wewe pia kuwa Tanzania tumerudishwa nyuma kutokana na siasa na uongozi uliokosa ubunifu.

..nisichokubaliana nacho ni baadhi ya madai kama yalivyowasilishwa na makoye2009 na Mwanamasala.

..sikubaliani na madai kwamba Wasukuma na Wanyamwezi wamekuwa wakinyimwa nafasi za uongozi na kisiasa na makabila madogo. makabila madogo yapi hayo?

..Paul Bomani, Saidi Maswanya, Samuel Pundugu,Mark Bomani,Samuel Sitta,Francis Nyalali,Balozi Nhigula,Balozi Dr.Chagula,Bob Makani, Charles Kabeho,Yasebasi Pius Ngwandu,Ernest Nyanda,Abubakar Mgumia,Dr.George Mlingwa, Prof.Costa Mahalu, Prof.Mgongo-Fimbo, Prof.Ibrahim Lipumba, Judge William Sekule,Andrew Chenge,Dr.Andrew Shija,John Rubambe,Ali Karavina, Dr.Msekela, Prof.Mgombelo, Rostam Aziz,Paulo Dialo, Dr.Festus Limbu,John Momose Cheyo,Laurian Kego Masha,etc etc sasa hapa utaniambia hawa wenzetu wamenyimwa nafasi za uongozi?

..pia sikubaliani na madai kwamba akipatikana Raisi Msukuma au Mnyamwezi basi makabila hayo au mikoa hiyo itakuwa na uhakika wa kupiga hatua ya maendeleo.

..binafsi nadhani njia ya uhakika zaidi ambayo imekuwa tested and proven that it works ni wenyeji na wadau wa mikoa hiyo kuwa na umoja na mshikamano ktk kuhamasisha juhudi za kujiletea maendeleo. vilevile wachague viongozi, haswa wabunge, makini zaidi wenye uwezo wa kuhamisisha maendeleo kwa kutumia rasilimali zilizoko ktk mikoa hiyo.

..kama wenyeji wa Mwanza waliweza kuchangishana na kufanya kazi kwa kujitolea wakajenga uwanja wa Kirumba basi sidhani kama wanashindwa kuchangishana kujenga hospitali, shule, vyuo, vyenye hadhi Tanzania nzima kama ulivyo uwanja wa Kirumba.

..kwa mtizamo wangu mikoa ya Mza,Shy,na Tbr, ni eneo ambalo wamekosekana viongozi wa kuwaonyesha na kuwahamasisha kwamba wanao uwezo wa kujiletea maendeleo bila kuwa wategemezi kwa serikali kuu.
 
Sasa maana ya serikali kuu itatoka wapi iwapo watu watatakiwa kuendelea bila kutegemea serikali kuu ???

Uanzishaji wa serikali kuu ulienda sambasamba na kuvunjwa taasisi za kimajimbo au kikabila.

Kila kitu kina price tag yake. Kuvunjwa kwa taasisi za kikabila hili kujenga taifa kulikuwa na faida zake. Lakini price tag yake ni kuwa kuna baadhi ya makabila wamelipa zaidi ya kile wanachotakiwa.
 
''.......As the winds of independence gathered steam, he facilitated the political rise of his long-time college friend Julius Nyerere by winning him British support as well as by securing the allegiance of Sukuma chiefs to Nyerere's party, Tanu (Tanganyika African National Union). As prime minister, later president of independent Tanganyika, Nyerere repaid Chief Kidaha, as he was known, by abolishing the role of chiefs, and banishing him for some months to the remote Tunduru district of the Southern Province for undisclosed reasons. This experience alienated him from politics forever, prompting him to turn his energies to private business and religious pursuits.
In the 1960s and 1970s, he served as managing director of Market Research (T) Ltd, and was appointed public relations officer of the Nairobi-based East African Railways and Harbours administration. Upon his retirement in 1975, he moved to the northern Tanzanian town of Moshi, where he operated a private insurance agency. Active in local religious affairs, he founded the Moshi chapter of the Order of Franciscans.
At the time of his death, Chief Kidaha had resumed the leadership of the Sukuma community from his late brother Hussein, and was active in preserving Sukuma cultural legacies. He was buried at Ibadakuli in Shinyanga, the site of his state house during the heyday of his chiefdom. Most people who met the chief commented on his charismatic yet welcoming presence. He was proud of having fulfilled his promise to his father to ensure all his 43 siblings were properly educated.
He is survived by his wife, Grace, his former wife, Mary, four children, Misuka, Edward, Jonathan and Simona, eight grandchildren, and two great grandchildren.
· David Paul Kidaha Makwaia, politician and businessman, born May 7 1922; died March 31 2007....''END OF QUOTE.

Mwanamasala,

Wabeja sana kwa haka ka historia ka Mh. Chief Makwaia bila shaka katafungua macho wengi akiwemo Joka Kuu.

Sasa yale nilikuwa nasema kuhusu Nyerere kuwagandamiza wasukuma yanaanza kujidhihirisha. Soma hiyo quote hapo juu hasa sentensi zilizokolezwa kwa wino mwekundu,labda niirudie tena''..his long-time college friend Julius Nyerere by winning him British support as well as by securing the allegiance of Sukuma chiefs to Nyerere's party, Tanu (Tanganyika African National Union). As prime minister, later president of independent Tanganyika, Nyerere repaid Chief Kidaha, as he was known, by abolishing the role of chiefs, and banishing him for some months to the remote Tunduru district of the Southern Province for undisclosed reasons .Hasa haya maneno mawili ya mwisho, UNDISCLOSED REASONS!!!!!!!!!

Fikiria msukuma msomi,chief wa kabila maarufu aliyetambuliwa na wakoloni kuwa angeweza kuwa Rais wa Tanganyika by then, lakini Nyerere kwa kuhofia kuwa atatwaa madaraka akaamua kumnyamazisha kwa ujanja uleule nilitangulia kuusema huko nyuma!

Huo ndio ulikuwa mfumo wa utawala wa Nyerere. Kuwanyamazisha wale wote walikokuwa wanaonekana ni threat kwa nafasi yake au utawala wake particularly Wasukuma na Wanyamwezi.

Joka Kuu nilishasema na nasema tena Wabunge wetu wa Shy,Mza,Tbr wanafanyakazi nzuri tu. Ni wasomi,waelewa,wachapa kazi na wanajua uchumi. Ndiyo maana nilikurejesha kwenye ule mjadala mkali wa Bunge la Bajeti 2009,ambapo Selelii na Diallo walihoji uhalali wa serikali kuanza kuendeleza/kupanua barabara ambazo tayari zina lami badala ya kupeleka pesa hizo kwenye barabara zisizo na lami hasa huko mikoa hiyo iliyosahaulika tangu enzi za mkoloni.

Nitaendelea.
 
Tangu uhuru makabila haya yamepigwa chini na makabila madogo madogo!Maendeleo ya mikoa yao yako chini sana,ingawa natural resources nyingi zinatoka huko.Kisiasa tangu akina James Mapalala,Kasanga Tumbo,
Chief Fundikira na Chief Makwaia wapigwe chini na Nyerere ,mikoa hiyo haina uwakilishi kabisa katika maamuzi ya serikali.

Ukiangalia mafisadi wengi wanatoka makabila madogo madogo!Wapinzani wa serikali pia ni kutoka makabila madogo.Mpaka haya makabila yaibuke ,yaseme enough is enough,ufisadi na stupidity ya nchi yetu utaendelea milele.Tujadili!!!!!!!!!!!!!!!!

Hivi RA nae si tunaambiwa ni mnyamwezi🙄?
 
Sitta alishashukiwa kuwa alikomba hela za CDA ila Mungu bariki ilikuwa miaka ile ya Nyerere (Baba yetu uliyeko Msasani ..... utusamehe makosa yetu kama ulivyomsamehe Barongo....). Anyway, Sitta sijui kaisadia vipi Tabora. Ningelipenda kulifahamu hilo. Pia akina Kapuya na wengine wamesaidiaje watu katika kuboresha maisha yao?
Nilibahatika kuongea na mzee mmoja tukiwa safarini. Alikuwa akilalamika jinsi Tumbaku inavyomaliza miti na kuharibu afya za wakulima. Akawa akisema wako busy kutafuta zao jingine ili kuachana na Tumbaku kwa wananchi wa Sikonge. Hawa watu wangelikuwa wakihusisha wasomi na watu aarufu wa maeneo tunayotoka.

I wish tungelifanya kikao kikubwa sana pale DODOMA kwa Wanyamwezi na Wasukuma wote kufika bila bila kujali ni Wapinzani wa kisiasa. Huu hata watu kama Chenge na Hosea inabidi wawepo. Na wakifika hapo mnaanza kuwapa LIVE ukweli wao kuwa kama MIPAPA ya nchi, wanasaidia vipi Wanyamwezi wao? Hivi hawaoni Wachaga jinsi wanavyofanya kwao mara wakishika madaraka? Pia tungeliomba waanze kampeni ya MADARAKA mikoani. Haya mambo ya kuletewa RC na DC na Rais ni matatizo matupu.

By the way, kwa Sikonge kuna wasomi wawili zaidi yaani Jaji Mstaafu Mfwalila na aliyekuwa mwandishi wa Rais kwa miaka mingi (kama sikosei) na sasa ni balozi wa Tanzania Russia, balozi Patrick Chokalla. Kwa watu maarufu wengine kwa Tabora unaweza kuongeza Mzee Rupia (sijui Tabora hata kama huwa anafika), Said El Maamr, (Sallim A. Sallim???) na kijana wa NBA Hasheem Thabeet (nimesikia!!). Kwa kweli tuna watu wengi sana na inatakiwa tusiwe masikini namna hiyo na hasa Tabora. Mwanza na Shinyanga wenzetu walau mnapumua.
 
Vagosya/Vakima (naomba niende offtopic),
Jana nilikuwa napitapita nikakumbana na nyimbo za dini. Nikakumbuka nyimbo fulani za zamani. Labda mwingine na yeye ni mpenzi wa hizi basi na yeye afaidi na hapo hapo nina OMBI:
Kama kuna mtu ana nyimbo za Mwanza Town Choir hasa hizi kwenye hii site hapa chini basi naomba tusaidiane. Ukifungua hii site, ziko chini kabisa ila inabidi uwe na real player. http://www.amefufuka.com.

Hiyo album zinapotoka hizo nyimbo kwa kweli ninazimiss saaana.

Hapa naweka video ya kwaya ya Makongoro. Huu wimbo nafikiri unafahamika sana na hii kama sikosei ni moja kwaya ya zamani sana East Africa.

[ame]http://www.youtube.com/watch?v=viGEKKOHNLs[/ame]
 
Sikonge we are together.Hii ni flashback saafi kabisa.

You make me remember those good old days when I was a primary school boy and attending sunday schools and church sermons on sunday at a nearby AIC Church in my home village.

Hapa wa kwetu umenikumbusha mbaali sana. Natamani hizo siku zingelirudia. Hizi nyimbo ukizisikiliza kulikuwa na kitu kama utakatifu na ucha Mungu wa kweli ndani ya mioyo ya watu uki-compare na sasa. Enzi hizo usingelisikia habari ya mauaji ya albino wala wachawi. Watu walikuwa karibu na Mungu!

Ubarikiwe sana kwa kawimbo haka.

Wabeja namhala.
 
Zakumi said:
Jokakuu:

Sasa maana ya serikali kuu itatoka wapi iwapo watu watatakiwa kuendelea bila kutegemea serikali kuu ???

Uanzishaji wa serikali kuu ulienda sambasamba na kuvunjwa taasisi za kimajimbo au kikabila.

Kila kitu kina price tag yake. Kuvunjwa kwa taasisi za kikabila hili kujenga taifa kulikuwa na faida zake. Lakini price tag yake ni kuwa kuna baadhi ya makabila wamelipa zaidi ya kile wanachotakiwa.

ZAKUMI,

..labda ni kushindwa kwangu kujieleza vizuri lakini sikuwa na maana hawa wenzetu wasipate huduma yoyote toka serikali kuu.

..nilichokuwa najaribu kusema ni kwamba ndugu zetu hawa wanaweza kuendeleza utamaduni kama ule uliowawezesha kujenga uwanja wa Kirumba kufanya mambo makubwa, ya maana, na ya manufaa kwao.

.kama kuvunjwa kwa Uchifu na Vyama vya Ushirika kuliudumaza mkoa kama Kilimanjaro, basi sitashangaa kwamba uamuzi huo wa Baba wa Taifa ulikuwa na negative impact ktk mikoa ya Mza,Shy,na Tbr.

MAKOYE2009,

..sidhani kama Selelii na Dialo are up to the development challenges facing their constituencies.

..mbunge kama Selelii yeye kazi yake ni ku-take cheap shots kwa Mawaziri kwa kutumia hoja za kikabila-kabila.

..Selelii amekaa bungeni muda mrefu, lakini anashindwa kujua taratibu zinazotumika ktk ku-allocate funds kwa ajili ya ujenzi wa barabara. Mbunge makini na effective ni yule anayefuatilia mgao wa fedha wizarani, na wakati bajeti inajadiliwa ktk kamati za kisekta.

..umemtaja Waziri Magufuli kama mtu makini na anatokea maeneo yenu. sasa unazidi kuonyesha kwamba kumbe hamjanyimwa nafasi za kutumikia au hata kufanya ufisadi.

..sasa naomba kuuliza kwanini amekaa pale ujenzi kama naibu waziri na baadaye waziri na ameondoka bila kumjengea Selelii barabara?

..hata barabara ya Rombo-Tarakea ambayo Selelii aliilalamikia sana bungeni, ujenzi wake ulianza wakati Magufuli ni waziri wa Ujenzi.
 
..hivi Hilal Hemed Hilal,Rostam Aziz,Imalaseko,Kishimba,Paul Dialo, Paul Rupia, Andy Chande[anadai amezaliwa Bukene], Khamis Salum Khamis, hawawezi kuchangishana wakajenga walau shule 10 zenye hadhi inayoeleweka maeneo ya Mwanza,Shinyanga,na Tabora?

..hebu angalieni El-Hillal Minerals ati wamevuna almasi ya thamani ya USD 2,871,226 halafu wamelipa royalty USD 143,500. hawa ni ndugu zetu Watanzania, sasa wana-invest kiasi gani ktk social service mkoani Shinyanga?

El Hillal to increase diamond Output

"The Tanzanian diamond mining firm El Hillal Minerals Ltd is set to increase its production to 84,000 carats by December this year.
The increase will earn the Shinyaga based company $18.9 million annually. This will become possible after a new processing plant is installed by mid year, bringing the company's installed capacity to four plants.
El Hillal is a $20 million investment, licensed in 2003 to mine a 38 sq-km diamond field in Mwadui, Shinyanga. It was admitted to membership of the World Diamond Market last November, according to its chairman Hillal Hamad Hillal.

Between February and December last year, El Hillal had mined 12,875.15 carats of diamond worth $2,871,226.62. A five per cent royalty fee was paid to to the Tanzanian government, which amounted to $143,500.

With the expected acquisition of the new plant, output will increase to 49,500 carats worth $10.9 million.
The three processing plants currently in operation have a processing capacity of 230 tonnes per hour 20 hours a day, with a four hour shift change.
As a result of the expansion, El Hillal expects that between July and August this year, it will sell its minerals from Tanzania – meaning that diamond buyers would follow the market to Tanzania where diamond cutting will be undertaken. This may result in the additional recruitment of 120 employees. The mine currently employs 180 people.
Mr Hillal said that, apart from two expatriates, the rest of the staff are Tanzanians.
The company expects to spend a total of Tsh133 million ($126,666) this month as compensation to owners of land who are resident in mining areas. Besides undertaking compensation, the company covers holes caused by mining activities and preserves nearby forests to address environment concerns.
El Hillal will become the second company with mineral processing capabilities in Tanzania. In November last year, another company, Mwananchi Gold Company Ltd, was inaugurated by former president Benjamin Mkapa, with its focus being the processing of gold."
 
Umefulia fuli. Karne ya ishirini na moja unazungumza habari makabila? Kabila langu mimi ni Mtanzania soon ntakuwa MueastAfrika na Baadaye Muafrika adios
 
njooni Kilimanjaro mjifunze nini maana ya maendeleo..............tumeni wajumbe tutawafundisha
nasikia huko kilimanjaro wanawapenda saana , maana jama nasikia wanakuja na maredio yao makubwa, ni muziki na pombe kwenda kwa mbele na upole, mzee wa kiraracha yeye anaongeza majengo tu.
 
Nilikimbia hii mada ila ngoja nichangie kidogo.

Jamani Wanyamwezi, wasomi wetu na watu maarufu wametuangusha au niseme tumejiangusha wenyewe. Niliposema Wanyamwezi hatufai, wengine walinishangaa. Ila hebu muone Sitta na hao wanaomwita kaka. Hivi wanafanya nini kwa Mkoa wa Tabora? Hata lami imefanya kupita kuelekea Shinyanga na Mwanza na vinginevyo tusingelipata kitu kama Kigoma tu. Ndiyo maana kipande cha barabara kutoka Nzega kuja Tbr mjini, kimechoka ni hakuna.

Kuna mtu kama Rupia. Huyu bwana ni moja ya watu wachache sana waliofumbuka macho Tanzania. Ila sidhani kama ana hata kibanda huko Tabora alikotoka. Huyu mwingine kawa waziri ila kuwekeza kwake ni Madisco na kufungua bendi za mziki. Hakuna mradi mkubwa wa maana utakaotoa ajira kwa Wanyamwezi wake. Jamani nyie Tabora imechoka si kawaida. Nafikiri Shinyaga ina nafuu sana kulinganisha na Tabora. Tabora ni mkoa ambao kama unawekeza basi ili usaidie zaidi kuliko kusema utengeneze faida.
Sitta na wengine walikuwa wanaweza sana kutafuta hata investors nje na waje wawekeze nyumbani. Cha muhimu ni kuwa watu wapate ajira.....

Ila hakuna kukata tamaa. Uzuri ni kuwa, zamani watu hata hawakusema hili. Ila kwa sasa walau watu wanakaa na kuanza kufikiria sana jinsi ya kusaidia kwao. Lazima nikiri kuwa kuna mikoa/wilaya wako mbali sana kwa sasa. Anyway, mie ni mtu ambaye hufurahia maendeleo ya jirani zangu na hapo kujifunza kutoka kwao. Kama wao wameweza basi kwa nini sisi tushindwe? Nishaanza kujadili jinsi ya kuweka maji safi walau hospital ya Sikonge. Hii nimejiwekea kama Task yangu na nina imani kwa kuweka juhudi kubwa, mie na kikundi changu ninachounda, tutafanikiwa.........

Kule kwetu kuna kimsemo kinasema "Mmulika nyoka usiku, huanzia miguuni kwake...". Tusikae na kulialia kama Kanumba ila tuanze kumulika na sisi. Kama mtu ukifanya mpango wa msaada wowote na hasa ile itakayowafungua watu macho, basi itakuwa mwanzo mzuri sana.
sehemu hizo mtu hawezi ku-invest wakati miundo mbinu iko hoi, bararaba na umeme kwa kuanzia, then elimu.
 
Sitta alishashukiwa kuwa alikomba hela za CDA ila Mungu bariki ilikuwa miaka ile ya Nyerere (Baba yetu uliyeko Msasani ..... utusamehe makosa yetu kama ulivyomsamehe Barongo....). Anyway, Sitta sijui kaisadia vipi Tabora. Ningelipenda kulifahamu hilo. Pia akina Kapuya na wengine wamesaidiaje watu katika kuboresha maisha yao?
Nilibahatika kuongea na mzee mmoja tukiwa safarini. Alikuwa akilalamika jinsi Tumbaku inavyomaliza miti na kuharibu afya za wakulima. Akawa akisema wako busy kutafuta zao jingine ili kuachana na Tumbaku kwa wananchi wa Sikonge. Hawa watu wangelikuwa wakihusisha wasomi na watu aarufu wa maeneo tunayotoka.

I wish tungelifanya kikao kikubwa sana pale DODOMA kwa Wanyamwezi na Wasukuma wote kufika bila bila kujali ni Wapinzani wa kisiasa. Huu hata watu kama Chenge na Hosea inabidi wawepo. Na wakifika hapo mnaanza kuwapa LIVE ukweli wao kuwa kama MIPAPA ya nchi, wanasaidia vipi Wanyamwezi wao? Hivi hawaoni Wachaga jinsi wanavyofanya kwao mara wakishika madaraka? Pia tungeliomba waanze kampeni ya MADARAKA mikoani. Haya mambo ya kuletewa RC na DC na Rais ni matatizo matupu.

By the way, kwa Sikonge kuna wasomi wawili zaidi yaani Jaji Mstaafu Mfwalila na aliyekuwa mwandishi wa Rais kwa miaka mingi (kama sikosei) na sasa ni balozi wa Tanzania Russia, balozi Patrick Chokalla. Kwa watu maarufu wengine kwa Tabora unaweza kuongeza Mzee Rupia (sijui Tabora hata kama huwa anafika), Said El Maamr, (Sallim A. Sallim???) na kijana wa NBA Hasheem Thabeet (nimesikia!!). Kwa kweli tuna watu wengi sana na inatakiwa tusiwe masikini namna hiyo na hasa Tabora. Mwanza na Shinyanga wenzetu walau mnapumua.
hivi akina kapya sio wasomi? haewatoki sikonge? etc etc
 
Back
Top Bottom