chu! bhebhe ngalu, uliyomba ubustaarabu yaya guyomba ja mukaya? lekagi bhagosha.....chu! nalema gete.....neyo nahaya gukolwa!
Aise,hii thread imenifurahisha kweli kweli. Nene nali nsukuma kamo,ontuzu ku ba Chenge namhala o vijisenti na Cheyo namhala o kujaza watu mapesa!!!
Nimem-quote Ameoba maana amenifurahisha sana alivyonyambulisha kikwetu pale. Yaani ngalu Ameoba nimesoma nikaona kama niko Ntuzu kabisa.
Ok ngoja na mimi nichangia thread hii kama ilivyoanza. Kwamba huko Usukumani na Unyamwezini maendeleo hakuna tangu uhuru au kiswahili cha kisukuma/kinyamwezi MAENDELEO KUDUHU!
Huu ni ukweli ambao mtu yeyote mwenye busara,hekima na akili hawezi kuupinga. Hivi ni nani asiyejua kuwa DHAHABU NA ALMASI ya nji hii inatoka kanda ya Ziwa kwenye mikoa inayokaliwa na Wasukuma na Wanyamwezi kwa maana ya Mwanza,Shinyanga na Tabora? Tunajua Mara nako Dhahabu ipo lakini huko ni kwa Wakurya bwana. Bado mikoa hii ina utajiri wa mazao ya kilimo kama PAMBA, kuna MINOFU ya samaki wa Ziwa Victoria, kuna Ng'ombe wamejaa kwenye mazizi lakini maendeleo KUDUHU(hamna)!
Sasa ninachotaka kusema ni kwamba utajiri huu wa madini hauinufaishi mikoa hii ya WASUKUMA NA WAMYAMWEZI. Mikoa hii ndiyo yenye barabara mbovu kuliko mikoa yote ya Tanzania,ukija kwenye shule za sekondari(IV na VI) hakuna kitu pale. Labda hizi za KATA za mheshimiwa JK na waalimu wake wanaoitwa Vodafasta.
Barabara nzuri za lami na shule nyingi za sekondari pamoja na High school baada ya uhuru zilijengwa mikoa ya Kaskazini kwa maana ya Kilimanjaro, Arusha na Tanga. Yaani serikali ilikuwa inahamisha raslimali za Wasukuma na Wanyamwezi kwenda kuendeleza Mikoa ya watu wengine.
Ndiyo maana sera ya CHADEMA ya MAJIMBO mimi niliipenda maana ina sema kila mkoa au eneo husika linatajitegemea kiuchumi kwa maana ya kutumia raslimali zilizoko kufanya maendeleo muhimu. Kwa sera kama hii basi mikoa ya WASUKUMA na WANYAMWEZI ingelikuwa ni ULAYA!!!
Ndiyo maana nchi kama USA zimeendelea kwa kutumia sera kama hii. Lakini hapa TZ sera kama hii inaonekana ni ya kubagua maeneo kitu ambacho si kweli kwa maana bado raslimali hii iliyoko kwenye eneo husika itagawiwa kwa maeneo ambayo hayana kabisa.
Kwa wale wanaosema kuwa Wasukuma ni mafsadi sikubaliana nao. Sina haja ya kupiga kelele sana lakini wanaweza kujifunza toka kwa Spika wa VIWANGO NA MWENDO Mheshimiwa Sam Sitta mbunge wa URAMBO kwa Wanyamwezi!!!
Nitaendelea.
f