Wanene kuongezewa marupurupu

Zitto, Mbunge hawezi kuwa mtendaji, na hapaswi kuwa mtendaji. Jukumu lake lake kubwa ni kutunga sheria na kuisimamia serikali. Tatizo tulilonalo ni kuwa wabunge wanafanya kazi ya kutunga sheria sawasawa, tatizo kubwa ni kwenye kuisimamia serikali. Kwa maana ya kwamba wao wakiwa ni wawakilishi wa watu wana uwezo wa kuhoji na kutaka maelezo ya kina kuhusu jambo fulani. Endapo jambo fulani katika utendaji haliendi wanavyotaka wanauwezo wa kulitungia sheria na kulibadilisha au wakati wa bajeti kulikatia pesa (the so called power of the purse). Ina maana gani, kama Wabunge wangeona kuwa Rada haitustahili wangegomea kuitengea pesa? Kama wabunge wanaona vijana Ukraine wanastahili ile ahadi ya serikali na mikopo yao waliyonyang'anywa basi wabunge wangeweza kuwatengea fedha.

Nakubaliana na wewe kuwa haiwezekani fedha zinazotakiwa kutumika kwenye majimbo yao zipitishwe kwa wabunge. Wao si watendaji na hawastahili kuwa watendaji. Pesa zozote wanazoomba kwa ajili ya majimbo yao ni lazima zipitishwe kwa watendaji, halmashauri, kata, n.k but never kupitia ofisi zao.

By the way, kwanini kati ya watumishi wote wa jamhuri yetu wabunge peke yao ndio wawe wanajipangia mishahara, posho na marupurupu mengine? Hata Rais hajipangii mshahara!!
 
Mzee mwanakijiji,

Ndugu yangu nitasema kitu kimoja na naomba maelezo yenu!..Wabunge ni akina nani?...kisha nambie kati yao wangapi ni Mawaziri na Manaibu waziri, Mameya na kadhalika.. kama sii watu hawa hawa ambao mnawatazama ktk swala la majimbo yao!
Nani aliyezuia fedha za hawa wanafunzi huko Ukraine?...Mbunge na waziri!
Nani aliyepitisha Richmond...Mbunge na waziri.. yaani tunacheza pale pale na double role za wacheza sinema isipokuwa tunacho tofautisha sisi ni staring na co star! hali ukweli unabaki kuwa ni mtu yuleyule!
Chukulia Msolla huyu ni Mbunge na waziri pia. Je, Utendaji kazi wa wizara yake unakuja vipi ikiwa huyu ni Mbunge na wizara yake imepewa fedha hizo hizo mnazotaka kuzipiga vita kwenda kwa wabunge! I mean what is the different?
Kisha tusijaribu sana kuiga vitu mahala ambapo kwetu haiwezi kabisa kufanya kazi. Navyofikiria mimi mbunge ni mtu ambaye ana nafasi mbaya sana ktk uchaguzi..Na believe me wabunge ndio hupata taabu sana kwa wananchi kila kukicha kusikia madai, malalamiko na hata shida za watu kuliko kiongozi yeyote yule. Mbunge anajua matatizo ya wananchi wake lakini he has no say!.. Halmashauri za wilaya na miji ni wafujaji wa fedha sana tu lakini kama mbunge atakuwa katikati yao, hii itaondoa matumizi yasiyokuwa priority ya wananchi. Kama tumeshindwa na hao ma DC kisha unawapa Halmashauri za wilaya na miji uwezo wote ndugu zangu tumekwishaaa! Ni lazima kuiweke ngao ya wananchi kabla hamjafanya makosa ya kutoa penalty dakika ya tisini!
Hatuwezi kuajiri tena mtu mwingine kushika nafasi ya DC ni Upumbavu kusema tuongeze Gavana wa kuchaguliwa.. Hii tunaongeza hesabu ya matumizi yetu hali serikali inatakiwa kubana matumizi.
Nakubali kabisa kuwa Pesa zilizokuwa allocated kwa ajili ya majimbo yao ni lazima zipitishwe kwa watendaji hao halmashauri, kata, kama serikali yetu ingefikiria kuwa hadi sasa Wabunge ndio Mawaziri wetu na bado fedha inapitia ofisi zao! Waziri kachaguliwa na nani? RAIS! wadhifa huu unatangulia mwajiri wake wa kwanza ambaye ni mwananchi!
 
Mkandara, kuna jambo moja ambalo limefichika katika hekima ya maneno yako, nalo ni uelewa wa nani anafanya kazi gani, na nani anatakiwa kufanya kazi gani. Wananchi wanapolalamikia kuhusu matatizo yao kwa wabunge wao wanafikiri mbunge ana uwezo wa kufanya jambo fulani la kiutendaji kama kuamuru kitu fulani kifanyike au kisifanyike. Na upande mwingine wabunge wengine licha ya semina 101 bado hawajaelewa nguvu kubwa na uwezo mkubwa walionao kuisimamia serikali na kuiwajibisha ikibidi.

Baadhi ya wabunge bila ya shaka wanafikiri wanaweza kufanya jambo lolote lile kwa vile wao ni wabunge. Ukweli ni kuwa Mbunge hawezi kumfukuza kazi mtumishi wa serikali au vinginevyo. Hivyo haja ya kuelewa kazi na wajibu wa wabunge ni ya muhimu sana, kwani baadhi ya matatizo yasingetokea.

Tatizo jingine ni kuwa licha wabunge wengi kuelewa uwezo na wajibu wao kutokana na uwingi wa wabunge wa CCM inakuwa vigumu kwa wabunge hao kuiwajibisha serikali ya chama chao, na wale upinzani kutokana na uchache wao inakuwa vigumu kuwajibisha serikali yenye wabunge wengi Bungeni. Ndio maana kwa maoni yangu mimi sililii Katiba mpya kwanza, nalilia wapinzani kuondoa wingi wa wabunge wa CCM bungeni hapo ndipo Bunge tutaliona uwezo wake. SAsa hivi kina Zitto hata wapige kelele vipi Bungeni hawawezi kubadilisha mwelekeo wa utendaji wa Bunge isipokuwa kwa huruma ya CCM!
 
Dr. Salim alisema uongo ukirudiwa rudiwa bila kuijbiwa hugeuka ukweli.
Let me do this on my own terms.

Hawa ndio viongozi wa chama M-badala! kuongoza jimbo tu mnamaliza wake za watu je mkifika huko Ikulu si mtafungua madunguro? heri ya hao wanaofanya biashara Ikulu...

Zitto, hili suala la binafsi kama utalizungumzia utalizungumzia on your own personal terms siyo kwa kufurahisha JF au watu wachache wanaotaka kuridhisha udadisi wao tu. NI kweli jambo hili lilivuta hisia za watu wengi na mambo ya kitaifa n.k. Kama tulivyosema awali kama CCM na wahusika upande huo hawataki kuzungumzia kwanini tukulazimishe wewe ulizungumzie ilimradi tu tujue "nini kilitokea". Ukisema ndiyo ilikuwa kweli, utaulizwa "mlilala hoteli gani" ukisema hizo ni njama za kisiasa utaambiwa "tukuamini vipi wewe wakati ilishasemwa...". In any case hakuna atakayeridhika kwani majibu yatazua maswali zaidi ambayo yatahitaji majibu zaidi yakakayo zua maswali zaidi, na gurudumu la maswali yasiyoisha na majibu yasiyotosheleza litazidi kubingirishwa.

Kwa hiyo tusubiri CCM waanze kusema kwanza... In a way the whole thing sasa imekuwa CCM wanampaka matope Zitto! Yaani uroda ale yeye kwa raha zake halafu CCM wanafanywa kuwa scapegoat! This is only in JF where a spade is not a spade rather a big Spoon!
 
Masatu,

Nakubaliana na wewe, JF wako very soft kwenye mambo yanayohusu upinzani na hasa CHADEMA. Hiyo ni weakness kubwa sana, consistency ndio njia pekee itakayoifanya JF iwe credible. Kama tunabadilika kulingana na jambo linamhusu nani, hapo hatutakuwa tofauti na Sitta (Spika wa bunge).
 
Nimeipenda hii strategy ya "kutokea" ya Zitto. Ile ya kwanza ya kumsingizia Rais ilikuwa amateurish prepared lakini hii ya hapa JF ya kufafanua posho za wabunge sound to work, though so far so good. Mwkjj and his coy are doing more than enough. Keep it up bro......
 
Nitoke Vpi!!!?
 
Hivi kuna lolote atakalosema Zitto litakalowaridhisha? Kama mmeshaamua "uroda ale yeye kwa raha zake" sasa kinachotakiwa kujulikana ni nini? Mimi ni mhalisia, siyo mwota njozi. Mnachotaka kujua ni je tunda lilikuwa tamu au la! na ilikuwa kuwaje... Kwa vile Zitto ni mwanachama hapa basi tumefikia mahali pa kuamini kuwa tuna haki na tunastahili habari za maisha yake binafsi. Kwa vile tunahisi tunamjua Zitto basi atuambie sisi washkaji zake mambo yalivyokuwa. Akisema ndiyo amekula, tutaridhika? Akisema hakula tutaridhika? akisema nizungumze kwa wakati wangu muafaka, tutaridhika?

Mtanzania, hili jambo linahusu vipi upinzani au Chadema? Mimi siko soft kwenye suala la upinzania au chama chochote cha siasa, sipendi mtu, sipendelei mtu wala siogopi mtu to me all are fair game! Ila kwa hili nilishalizungumzia na kuliweka kwenye maudhui yake. Zitto ni mtu mzima na kasema atalizungumzia kwa wakati muafaka, kwanini tusikubali hilo tumekuwa kama watoto waliodekezwa "I want it, I want it now!". Sisi ni watu wazima na mtu mzima kasema kwa wakati huu hayuko tayari kulizungumzia kwanini sisi tumlazimishe ilimradi tu tutosheleze udadisi wetu?

Halafu kusema "Hawa ndio viongozi wa chama M-badala! kuongoza jimbo tu mnamaliza wake za watu je mkifika huko Ikulu si mtafungua madunguro? heri ya hao wanaofanya biashara Ikulu..."... ni maneno yasiyo na umakini yakipinduliwa upande wa pili. Hivi kuna wana CCM wangapi ambao wamekula wake za watu? Je hujawahi kusikia jamaa ambaye mke wake alichukuliwa na Waziri na yeye mwenyewe akapewa Ukuu wa Wilaya? Hujasikia habari za Kiongozi mmoja ambaye kila akija US wakati huo akiwa waziri alivyokuwa akijifungia ndani na mtu asiye mke wake hadi kukosa vikao muhimu vilivyomleta? Kama tungetaka kuwapigia kelele, mbona tungepiga kelele sana! Siyo kwamba hatujui, tunajua kuna mambo mengine ni ya binafsi na tukianza kuyazungumzia yanataka kutupoteza kwenye mambo muhimu!

Zitto akiamua kuzungumzia sasa hivi sina tatizo ni uamuzi wake, akitaka kuzungumzia mwezi ujao sawa sina tatizo, akigoma kulizungumzia kabisa sina tatizo...ni uamuzi wake! kati ya vitu vilivyoko mawazoni mwangu suala la Amina na Zitto liko mbali kweli!
 
Jamani, watu wote mnaotaka Mheshimiwa Zitto awataarifu kuwa alikula yule mtoto, mnataka atumie lugha gani hadi mfahamu. Kuwa ndiyo nilimtafuna? Ameshatoa jibu ambalo liko wazi kabisa. Kumbukeni kuwa Mheshimiwa Zitto ni msema ukweli na katika sakata hili ana majibu mawili tu:

(a) Kama shutuma zile ni za uwongo, Mhesimiwa hawezi kushindwa kusema ukweli kuwa "Jambo lile kweli halikutokea kabisa ila kuna mchezo mchafu nilifanyiwa; kwa sasa hivi details sitaki kuzitoa."

(b) Kama shutuma zile ni za kweli, Mheshimiwa hawezi kuesema kweli zilitokea kutokana na fedheha yake. Vile vile atashindwa kusema uwongo kuwa hazikutokea wakati zilitokea; hivyo atanyamaza tu; this is exactly what he has done.

Ingawa ni jambo la kukatisha tamaa kabisa hasa kwa vile kuna watu walikuwa wanamtegemea Mheshimiwa Zitto kuwa na standard kubwa sana na hivyo kutoa mfano wa aina ya uongozi tunaotegemea, ndiyo hivyo tena, maji yaliyomwagika hayawezi kuzolewa tena. Wakati sakata hili bado lina nguvu, niliwahi kuongea na ndugu yangu mmoja pale Dar aliyehappen kuwa anamfahamu sana huyu dada kwa vile walifanya kazi pamoja pale redioni; jamaa huyu anasema mtoto yule ni moto sana, anapenda sana yale majambo ya sirini, na anaweza kumfuatilia mwanamme yeye mwenyewe akimtaka. Jamaa huyu hakushangaa kabisa alivyosikia tuhuma zile kwa vile alitegemea kuwa kuna wabunge kadhaa wanatinga tu na hasa vijana. Kwa vile Zitto naye ni kijana it becomes obvious.

Ushauri wangu, JF tumwache Mheshimiwa Zitto ajisahaulishe na mambo yale kusudi aweze kuconcetrate kwenye kazi za umma. Pamoja na purukushani ile, bado ana nguvu na uwezo wa kuleta mabadiliko katika mfumo wa bunge letu kama tutamsaidia kuyasahau yale mambo. Yeye siyo wa kwanza kukumbwa na mikasa ya aina hii. Hapa Tanzania wabunge na wanasiasa wengi wanafanya hivyo hivyo, tatizo tu hawajashikwa. President Clinton na President Kennedy walifanya mambo hayo hayo lakini yalikwisha na leo hii legacy yao ni kubwa tu katika historia ya marekani.
 
Mtu kanyosha kidole kukuonyesha mwezi...Hebu acheni kungangania kuzungumzia kidole badala ya kujadili mwezi...

Hebu tukate issues.
 
Hivi kuna lolote atakalosema Zitto litakalowaridhisha? Kama mmeshaamua "uroda ale yeye kwa raha zake" sasa kinachotakiwa kujulikana ni nini? Mimi ni mhalisia, siyo mwota njozi. Mnachotaka kujua ni je tunda lilikuwa tamu au la! na ilikuwa kuwaje... Kwa vile Zitto ni mwanachama hapa basi tumefikia mahali pa kuamini kuwa tuna haki na tunastahili habari za maisha yake binafsi. Kwa vile tunahisi tunamjua Zitto basi atuambie sisi washkaji zake mambo yalivyokuwa. Akisema ndiyo amekula, tutaridhika? Akisema hakula tutaridhika? akisema nizungumze kwa wakati wangu muafaka, tutaridhika?

Mtanzania, hili jambo linahusu vipi upinzani au Chadema? Mimi siko soft kwenye suala la upinzania au chama chochote cha siasa, sipendi mtu, sipendelei mtu wala siogopi mtu to me all are fair game! Ila kwa hili nilishalizungumzia na kuliweka kwenye maudhui yake. Zitto ni mtu mzima na kasema atalizungumzia kwa wakati muafaka, kwanini tusikubali hilo tumekuwa kama watoto waliodekezwa "I want it, I want it now!". Sisi ni watu wazima na mtu mzima kasema kwa wakati huu hayuko tayari kulizungumzia kwanini sisi tumlazimishe ilimradi tu tutosheleze udadisi wetu?

Halafu kusema "Hawa ndio viongozi wa chama M-badala! kuongoza jimbo tu mnamaliza wake za watu je mkifika huko Ikulu si mtafungua madunguro? heri ya hao wanaofanya biashara Ikulu..."... ni maneno yasiyo na umakini yakipinduliwa upande wa pili. Hivi kuna wana CCM wangapi ambao wamekula wake za watu? Je hujawahi kusikia jamaa ambaye mke wake alichukuliwa na Waziri na yeye mwenyewe akapewa Ukuu wa Wilaya? Hujasikia habari za Kiongozi mmoja ambaye kila akija US wakati huo akiwa waziri alivyokuwa akijifungia ndani na mtu asiye mke wake hadi kukosa vikao muhimu vilivyomleta? Kama tungetaka kuwapigia kelele, mbona tungepiga kelele sana! Siyo kwamba hatujui, tunajua kuna mambo mengine ni ya binafsi na tukianza kuyazungumzia yanataka kutupoteza kwenye mambo muhimu!

Zitto akiamua kuzungumzia sasa hivi sina tatizo ni uamuzi wake, akitaka kuzungumzia mwezi ujao sawa sina tatizo, akigoma kulizungumzia kabisa sina tatizo...ni uamuzi wake! kati ya vitu vilivyoko mawazoni mwangu suala la Amina na Zitto liko mbali kweli!
 
Mwanakijiji,

Sitashangaa tena hata Mkapa akisema atawajibu mwaka 2020. Zitto ni mwana JF na anatakiwa kufafanua hii kashfa kwanza na kama hawezi sasa
aseme wazi kwasababu case iko mahakamani au kwasababu nyingine na wengine tutaelewa.

Wakati wote Zitto amekuwa akitumia banner ya kusema kweli, huwezi kuwa msema kweli wakati unachagua ukweli wa kuusema.

Mnaojaribu kumnasua mnatengeneza a very bad precedence here at JF.

JF lazima ibaki consistence muda wote, ninachokiona hapa na sisi tunaanza kuwa na sheria moja kwa CCM na nyingine kwa wale tunaoweza kuwaita friends of JF kama alivyo mheshimiwa Zitto.
 
Jana niliandika hapa kuhusu jambo hili. Ukiangalia, ni kuwa ongezeko kubwa liko kwenye posho, ambapo kabla ya kuongezewa, walikuwa wakilipwa TShs145,000 kwa siku wakati wakiwa Dodoma bungeni. Kati ya hizo, TSh.85,000 zilikuwa ni posho ya wao kuhudhuria kikao cha bunge! Ni kama vile kuhudhuria kwao bunge wanatufanyia favor wakati ndiyo kazi waliyoomba! It does not make sense!!!!!

Sijui siku Madaktari nao wakisema ili kuingia Thieta nao wawe na posho ya thieta tutasemaje. Serikali na wabunge wanatufanya sisi mbumbumbu sana. Na kwa mtaji huu, Wataalamu wote wazalendo wataishia ng`ambo tuu.
 
Mwanakijiji,

With all due respect, mimi nimemwuliza Zitto, nashangaa toka lini umekuwa msemaji wa Zitto?

JF haina swali dogo au kubwa, kila hoja hujibiwa kwa hoja kama banner yako hapo juu inavyosema.

Let him answer the questions, akikaa kimya pia tutaelewa na tutajua maana yake.
 
Mtanzania, miye simjibii najaribu kuelezea kile alichosema ambacho inaonekana ni vigumu ndugu zangu kuelewa. Kasema atalizungumzia jambo hilo in his own terms, kwanini hatutaki kusubiri azungumzie? Kwanini tumlazimishe kuzungumzia jambo ambalo ameahidi kulizungumzia wakati muafaka? Hicho ndicho kinachonifanya kushindwa kuelewa.
 
Mwanakijiji,

Basi hilo ndilo tatizo kwa wengine, kama kwako sio tatizo basi heshimu fikra, akili , na mawazo ya hao wanaotaka kujua.
 
Back
Top Bottom