Nakubaliana nawe Rwabugiri lakini bado nasisitiza kwamba haifai kujenga hoja juu ya msingi mbovu. Hilo sahihisho la uongo alilolitoa ndilo alilotumia kujengea hoja yake. Bora angesubiri kwanza jibu akishapata uhakika ndipo aendelee na hoja yake.
mbali na kuzikata hizo oc huku h/w wala hata hizo zilizopitishwa haziji na watu wamekaa wanasubiri rais achaguliwe labda ndo zitaanza kuflowjuzi alhamis kamati ya fedha ya bunge,ambayo mimi ni mjumbe, ilimwagiza waziri wa fedha kuondoa asilimia 15 kutoka katika bajeti ya matumizi mengineyo na kupeleka pesa yote kujenga barabara.
Hii ilifuatia taarifa tuliyopata kutoka kamati ya miundombinu kuwa hakuna barabara mpya zitakazojengwa maana pesa zilizotengwa ni kidogo. Uamuzi huu wa kamati ya bunge utaongeza bajeti ya miuondombinu kwa zaidi shs 393 bilions.
Uamuzi huu wa kamati ya bunge unaonesha kuwa hata tanzania tunaouwezo wa kupunguza gharama na kupeleka pesa katika vipaumbele muhimu. Mfanowa mauritania ni mzuri sana. Lakini tanzania waziri analipwa dola 1100 tu, theluthi tu ya malipo ya waziri wa mauritania, nchi masikini kuliko tanzania