Wanene kuongezewa marupurupu

Wanene kuongezewa marupurupu

Poa mkuu..nitaifanyia kazi. Cha ajabu kilichostua wengi hapa..mpaka tukaamua kufanya research ni kwamba mwalimu alikuwa categoriacal kwamba waziri muhusika atapeleka sheria bungeni baadaye, meanwhile kodi ianze kulipwa mara moja! The moral of the story ni kwamba mwalimu alijua kabisa kwamba hakuna kodi inayolipwa bila baraka za bunge kwa hiyo alichokuwa anakifanya ilikuwa kinyume cha sheria. ..lakini aliamua kuignore. ....

Kichuguu hata kama ni local tax lazima iwe sanctioned/iwe na baraka za sheria mama. Kwa mfano hizi kodi za halmashauri na nyinginezo ni kanuni (au sheria ndogo ndogo zinazobarikiwa na mheshimiwa Mizengo Pinda) sio sheria as ACT....... Tukiwa objective swala linabakia kwamba katika hizi nchi zetu ni rahisi kwa viongozi kuignore sheria zilizopo na kutuswaga tuu....as we have seen and continue seeing........


waziri wa fedha alipeleka muswada bungeni ie income tax act, wabunge wakakataa. mwalimu akasema kodi ilipwe bila sheria (au kwa sheria iliyokataliwa). akaliita bunge, akawaambia msipopitisha sheria hii ninavunja bunge tunaenda katika uchaguzi. alitoa kitisho hiki miaka michache baada ya halmashauri kuu ya TANU kuwafukuza uanachama na kisha ubunge wabunge 7,akina mwakitwange na choga. wabunge wakajua uchaguzi ukiitishwa chama hakitawapitisha kuwa wagombea. Hivyo wakalegalize muswada wa mwalimu. Sheria hii ilitumika toka 1973 mpaka 2004.
 
waziri wa fedha alipeleka muswada bungeni ie income tax act, wabunge wakakataa. mwalimu akasema kodi ilipwe bila sheria (au kwa sheria iliyokataliwa). akaliita bunge, akawaambia msipopitisha sheria hii ninavunja bunge tunaenda katika uchaguzi. alitoa kitisho hiki miaka michache baada ya halmashauri kuu ya TANU kuwafukuza uanachama na kisha ubunge wabunge 7,akina mwakitwange na choga. wabunge wakajua uchaguzi ukiitishwa chama hakitawapitisha kuwa wagombea. Hivyo wakalegalize muswada wa mwalimu. Sheria hii ilitumika toka 1973 mpaka 2004.

Ohoo Ustaadhi Zitto!!

Hali yako mwinyi! Glad to see ur back. Khabari za "Tora bora" Mheshimiwa...
 
Mzee Zitto,

Mheshimiwa karibu mkuuu, kuna maswali mengi sana mkuu hapa kwako tena hata mimi this time ninayo kibao, je upo?

Sema ndugu yangu tumkome nyani giladi, upoooooooooooooo!
 
Mheshimiwa Zitto,

Hata mimi nina maswali lakini nataka kujua kama upooooooo! Isije ikawa huyo ni Zitto mwingine!
 
Mheshimiwa Zitto,

Afadhali umerudi na kutupatia ufafanuzi wa mambo ambayo wengine wetu hatukuwa na uhakika nayo, nashukuru sana katika ufafanuzi wako wa malipo ya wabunge na hii historical fact ya kodi ya maendeleo. Kumbe mwalimu alikuwa mtishiaji vile; sikuwa nimeipata hii. Nakumbuka tu kuwa alitishia wabunge kuhusu kuhamishia makao makuu Dodoma mwaka 1973 au 74 hivi.

Inawezekana utaulizwa maswali mengi sana hapo baadaye kwa vile ulikuwa ukisubiliwa sana. Hata hivyo, kabla mambo hayajaanza naomba unifahamiashe mambo machache kuhus wabunge kama ifuatavyo:

(a) Je hizi posho za mafuta ya kutembelea majimbo wanalipwa wabunge wote ikiwa ni pamoja na wale wa kuteuliwa au ni kwa wabunge wa kuchaguliwa tu?

(b) Kuna logic gani kutumia flat rate za posho za mafuta kwa wabunge wa nchi nzima ikiwa kuna wabunge kama wale wa Zanzibar na Dar es Salaama ambao wanawakilisha maeneo madogo tu tofauti na wabunge kadhaa wa bara amabao wanawakiliasha maeneo makubwa sana.

(c) Kwa nini bunge lisiwaajili staff wa wabunge badala ya kumwachia mbunge kufanya hivyo. Inakuwa ni kazi ya ziada kwa mbunge kutunza mahesabu ya payroll wakati kazi yake ni kuwakiliasha wananchi wa jimbo lake. Mngeweka utaratibu ambao bunge linaweka viwango vya wasaidizi wa wabunge na kumwachia mbunge kuamuwa ni nani watakuw awasiadizi wake. Akishachaguw awasaidiza wake wanakuwa ni waajiliwa wa bunge na hivyo ofisi ya bunge kuwa responsible na mambo yote ya mahesabu

(d) Personally huwa nakereka sana na hii posho ya wabunge kuhudhuria vikao vya bunge wakati ndiyo kazi yao. Nikijaribu kufikiria kazi dereva aliyeomba na kuajiliwa kazi ya kuendesha gari kwa mashahara unaojulikana halafu baadaye adai posho ya kuweka ufunguo kwenye gari, sioni mantiki yoyote. Je kazi ya hii posho ya kuhudhuria vikao vya bunge ina maana gani hasa? Nini mantili yale.
 
uamuzi huu wa kamati ya bunge unaonesha kuwa hata Tanzania tunaouwezo wa kupunguza gharama na kupeleka pesa katika vipaumbele muhimu. Mfanowa Mauritania ni mzuri sana. Lakini Tanzania Waziri analipwa dola 1100 tu, theluthi tu ya malipo ya waziri wa mauritania, nchi masikini kuliko tanzania

Take home income ya waziri ni kiasi gani? Maana kuna marupurupu mengi (fedha na in-kind) ambayo sio sehemu ya mshahara na hayakatwi kodi.
 
hanMheshimiwa Zitto,


Hivi kweli Mauritania ni maskini kuliko Tanzania? Data zangu zinaonyesha kuwa nchi maskini kuliko zote duniani ni Malawi, wakati Tanzania ni ya nane kutoka chini (imejikwamua kidogo). Mauritania haimo katika kumi poorest. Hebu ona:

Poorest Countries in the World

1 Malawi $ 600
2 Somalia $ 600
3 Comoros $ 600
4 Solomon Islands $ 600
5 Congo, Democratic Republic of the $ 700
6 Burundi $ 700
7 East Timor $ 800
8 Tanzania $ 800
9 Afghanistan $ 800
10 Yemen $ 900


Hata Afghanistan inatuzidi
 
Mh.Zitto,

Karibu sanaa na shukrani umekuja kutupa ukweli nje ya taarifa tulizokuwa nazo. Pamoja na yote hayo nimeshindwa kuelewa swala la mafuta hadi sasa. Lita 1000 za mafuta kwa nini zinapigwa hesabu ya umbali wa mbunge toka alipo hadi Dodoma? hivi kweli nyote mnatumia magari yenu kusafiri hadi Dodoma?.. na ikiwa hivyo kwa nini msitumie usafiri wa taifa kama vile ndege kisha Bunge likawa na usafiri wake pale Dodoma kwa Wabunge?..Naomba elimishwa ktk hili.
Pili, kwa nini Wabunge wote wasipatiwe makazi na bunge hapo kwa muda wote waataokaa hapo kama vile kambi ya wanamichezo wetu ama semina za kazi.
Tatu, nashindwa kuelewa kwa nini mbunge anabeba mwenyewe jukumu la kuhudhulia Bunge hali pale ni sehemu ya kazi yake aliyochaguliwa na kukabidhiwa na wananchi.
Na nne, Je, ni kweli milipokea tayari marupurupu kabla ya muswada kuwakilishwa bungeni?.... yaani haya ni marudio tu!.

Binafsi sijawahi kuwa mbunge wala mbunge alokuwa karibu nani kupata kuuliza swali hili, lakini napata taabu sana kuelewa kwa nini wabunge wetu mnakuwa mnaachiwa uhuru mkubwa wa maamuzi ktk kazi mlokabidhiwa na wananchi hali tumeona washiriki wengi wa michezo, semina na mikutano, pia wawakilishi wetu nje huwekwa ktk kambi kwa masharti ya kuhudhulia na kushiriki kuwezesha ufanisi wa shughuli yenyewe.
Ndugu Zitto, wabunge mnatumia kodi zetu, swala la fedha sii hoja yangu kubwa ikiwa kazi inafanyika na bunge sio sehemu ya mchezo ambapo kila mbunge ana uamuzi wake kuhusu vikao fulani. Na kama ulivyosema kuwa kila mbunge hujilipia malazi ina maana wabunge wetu wengi wanaweza kuwa wanakwenda Dodoma kuendesha ufuska zaidi ya kazi waliyotumwa na wananchi. Kisha hakuna mtu wa kumuuliza wala ulazima wa yeye kuhudhulia, sana sana anapoteza posho ya siku ambayo ni Tsh.70,000 baada ya malipo yote. Mtu yeyote anaweza kusamehe baadhi ya siku akiwa na Kimwali cha Kinyiramba ubavuni. Hizo sabini nitazipata kesho ama kesho kutwa kwani matumizi ya siku hayazidi 40,000.
Naomba kuwakilisha!

Kichuguu,
hata mimi kanishtua sana aliposema Mauritania maanake navyojua mimi hawa jamaa wanakimbilia South na Botswana ktk maendeleo ya kijamii!
 
Mtanzania,
Sina Wilaya!...

UK - mjomba kamati zake za ufundi usifanye mchezo!.. utaondoka, muulize Kamando alimeza chura siku ya uchaguzi!..
Mwibara (Kibara) nilikokulia wamesha nisahau!
 
Wana JF
http://ippmedia.com/ipp/nipashe/2007/06/09/92178.html hii inaeleeza tunachojadili humu.

So pesa anayopata mbunge ni net? ule mkopo si wa kwao? kwanini Zitto azitoe, kwani mbunge angetaa shanging akawapa anapewa pesa yake net ingalikuwaje? Kumbuka zitto, wabunge mmeomba pesa zenu zisikatwe Kodi au hili utakataa? wabunge wetu kama wengine wengine wote wa Tanzania wameweka maslahi yao mbele. Hii inauma sana, hapa hujahesabu posho za kuhudhuria kikao maalum, kama wewe unavyosema ni mjumbe wa kamati xyz na pale unapohudhuria ktk vikao general vya bunge...
Angalieni Wazir Mkuu wa Palestina Mh. Ismail Haniya, ni yeye peke yake dunia nzima anaepata mshahara wa $1500.0
 
kwa mapeni hayo lazma kila mtu atagombea ubunge watu wote tutakuwa wanasiasa
 
Mtanzania,
Sina Wilaya!...

UK - mjomba kamati zake za ufundi usifanye mchezo!.. utaondoka, muulize Kamando alimeza chura siku ya uchaguzi!..
Mwibara (Kibara) nilikokulia wamesha nisahau!


Kaka ingawa hali inaendelea kuwa mbaya, tamaduni za kisiasa Tanzania bado zinaruhusu kugombea nje ya eneo la jamii yako ni suala la kujiandaa na kuwa makini na mazingira unayoishi.

Kamando alizidi masifa kaka (the guy he is too pompous and insensitive kukubalika vijijini) na vilevile aliharibiwa na Mfadhili wake "Mzee Msekwa" alipojaribu kumuadhiri Mama Beijing na kuishia kumjengea sympathy na kama unavyojua wapiga kura nchini ni kina mama.

Anyaway ukirudi mapema nyumbani yote yawezekana. Tatizo ni kuwa utaingia na timu gani....timu ya ushindi ama timu ya mabadiliko ama yawe ya kweli ama ya kisanii...

Tanzanianjema
 
Hivi Zitto ana shangingi naye?

Nijuavyo mie mkopo wa shangingi ni wa lazima hata kama unataka kununua Corola ni lazima uchukuwe mkopo wa milioni Arobaini. Hivi kuna ukweli wowote kuhusu hili Kaka Mheshimiwa Sana Zitto mwana wa Kabwe

tanzanianjema
 
Mafao na mishahara ya wabunge isipangwe na wabunge!!! mbona madaktari hawajipangii mishahara yao na mafao yao? walimu hawajipangii... wahandisi hawajipangii... why wabunge? Iundwe tume maalum isiyotokana na wabunge (majaji, utendaji, na tume ya utumishi wa umma) wawapangie mishahara yao na mafao yao..!!
 
Zitto: Ngoja kwanza; kwanza sahihisho kidogo, hivi Mauritania sio ndiyo kwa kiingereza ni Mauritius au? Kama hivi ndivyo, basi sahihisho ni kwamba hii nchi ni ya pili kwa utajiri baada ya Seychelles. HDI ya Mauritius ni 0.800 na Seychelles ni 0.800. I hope ulimaanisha nchi tajiri kuliko Tanzania!

Nirudi kwenye mjadala: Nisaidie mambo matatu: Mosi, ukitaka kupima mishahara sio vizuri kulinganisha na nchi zingine. Kuna msemo kwenye economics kuwa an inappropriate example leads to wrong formulation of questions and answers. Sasa katika hili, ukitaka kujua kama wabunge wetu wanalipwa vizuri au vibaya, inabidi ulinganishe mishahara yao na wafanyakazi wengine nchini Tanzania. Lakini tutapima mishahara kulinganisha ni nchi zingine tutapata majibu yasiyo. Kwa hiyo tukitaka kuwa fair tuangalie tunavyogwana hiyo keki ndogo miongoni mwa wabunge na wanasiasa wengine, walimu, madaktari, wahadhiri, n.k. Tupatie hizi statistics ndio tujue mambo yakoje.

Pili, wakati wabunge wanazidi kujiongezea posho kando na mshahara, wabunge haohao wameidhinisha sera ya kufuta utaratibu wa marupurupu katika sekta zingine. kwa mfano walimu walikuwa wanalipwa posho ya mazingira magumu ya kazi, ikafutwa. Wahadhiri walikuwa wanalipwa posho ya mafuta na ufundishaji, zote hizi zilifutwa. Sasa kwa nini kunakuwa na double standard?

Pili, katika nchi zilizoendelea mishahara ya wanasiasa huwa ndio ipo chini ukilinganisha na wafanyakazi wengine wa kada ya kati. Kwetu, hali ikoje?
 
Kaka Mauritania na Mauritius ni nchi mbili tofauti. Mauritania ipo karibu na Morocco na Algeria wakati Mauritius ni kisiwa ama visiwa katika bahari ya Hindi. Watanzania tunahistoria ya kuenda kuweka mambo sawa kule Mauritius wakati wa enzi za Mwalimu. Mauritania ni wale waliofanya mapinduzi makini hivi karibuni na sasa nchi yao ina mfumo mpya na wanasiasa wapya wakijenga nchi yao...

Tanzanianjema
 
Mkandara,

Tutabanana humo humo, inabidi kuanza kupambana nao kwa karibu badala
ya kupiga kelele za mbali.

Najua siwezi kuzuia wabunge wasiidhinishe milioni 100 ya kununulia shangingi, ila ili kuwaumbua unachukua hiyo pesa na kuwapa mkopo vijana na wakulima kwenye jimbo ili waendeleze kilimo/biashara zao. Sitahitaji hata senti tano kwenye pesa za mkopo wa gari. Nafikiri nina uwezo wa kununua gari la milioni 10 mpaka 15 kwa mshahara wangu na hilo ndilo litakuwa gari la mbunge.

Kule vijijini mikopo interest ni asilimia mpaka 50, ukiwasaidia vijana wakapata pesa zao hizo kwa interest ya asilimio 0, si utakuwa umesaidia?

Sasa vijana kama 20 tukiamua hivyo si tayari tumewaumbua wazee? Sasa wangapi muko tayari kutangaza rasmi hamtakubali shangingi? Itabidi kabla ya
kwenda kugombea tuwasomee vitabu kabisa ili msije mkatusaliti.
 
heshima zenu wakuu,

kweli inabidi wabunge wetu wanapozungumzia mishahara na posho zao wasilinganishe na nchi nyingine bali na hali halisi ya tanzania. sasa kama wao milioni moja haitoshi je hao wananchi wanaopata elfu 60 ndo inakuwaje? ni majuzi tuu tumesikia wafanyakazi wa sunflag arusha wamedondosha mkong'oto kwa waanjiri wao baada ya mishahara yao ya 40 elfu kukatwa na kupewa 27 elfu!!

sina maana kusema wabunge nao wapokee 60 elfu la hasha bali inabidi wajue watanzania wanateseka sana kwa mishahara midogo hivyo ni vyema wabunge wetu wakapanga mikakati ya kusaidia kuelekeza pesa kwenye mambo ya msingi ambayo kwa njia moja au nyingine yanaweza rahisisha maisha ya mtanzania badala ya wao kuweka maslahi yao mbele.
 
Back
Top Bottom