BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,832
- 287,782
Wabunge Tanzania waongezewa marupurupu
*Ni mapendekezo ya bajeti ya 2007/2008
*Waongezewa posho, mafuta katika magari
*Mikopo ya elimu ya juu pia yaongezwa
Na Mwandishi Wetu
WAKATI sekta ya maendeleo ikitengewa fedha kidogo kwenye bajeti ya mwaka 2007/08, neema imewashukia wabunge baada ya serikali kusikiliza kilio chao cha muda mrefu.
Kilio cha wabunge kimekuwa ni kuongezewa maslahi na katika bajeti inayotarajiwa kuwasilishwa bungeni wiki ijayo na Waziri wa Fedha, Zakia Meghji na sasa kimezaa matunda kwa kuwa mapendekezo ya bajeti yanaonyesha kuwa wameongezwa Sh9.3 bilioni kwenye posho.
Wabunge wamekuwa wakilalamikia posho wanazolipwa kuwa hazikidhi mahitaji kulingana na hali ya uchumi ilivyo sasa.
Baada ya kuchaguliwa kushika nafasi ya Spika, Samwel Sitta aliahidi kuhakikisha maslahi ya wabunge yanaboreshwa kwa kuzingatia hali halisi ya uchumi.
Hivi sasa wabunge wanalipwa lita 500 za mafuta, Sh1.2 milioni kama mshahara na Sh1.2 milioni za kuhudumia jimbo kwa mwezi na katika nyongeza mpya, sasa wataongezewa mafuta kutoka lita 500 hadi 1,000 kwa mwezi.
Katika kila kikao, mbunge hulipwa Sh140,000 kwa siku, ikiwamo Sh55,000 posho ya kujikimu na Sh85,000 kwa ajili ya posho ya kuhudhuria kikao.
Katika bajeti ya mwaka jana, Bunge lilitengewa Sh34.5, lakini mwaka huu fedha hizo zimeongezwa na iwapo mapendekezo yatapitishwa, Bunge litatengewa Sh42.5 bilioni, ikimaanisha kuwa taasisi hiyo imepangiwa kuongezwa Sh8 bilioni.
Katika maboresho ya masilahi ya wafanyakazi kwa mwaka wa fedha 2007/08, pia serikali imetenga Sh91.5 bilioni kwa ajili ya nyongeza za mishahara na inatarajia kuanza utekelezaji wa awamu ya kwanza ya kuboresha maslahi ya watumishi wa umma kulingana na mapendekezo ya Tume ya Rais.
Akiwasilisha taarifa ya makadirio ya bajeti kwa mwaka 2007/08 kwenye Kamati ya Fedha na Uchumi jana, Waziri wa Fedha, Zakia Meghji, alisema kiasi hicho ni hatua ya kwanza ya mapendekezo ya tume hiyo.
Katika Wizara ya Elimu ya Juu, serikali imetenga nyongeza ya Sh54 bilioni kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi. Mwaka jana, mahitaji ya mikopo kwa wanafunzi yalikuwa Sh140 bilioni, lakini serikali ikatoa Sh63.5 bilioni. Baada ya kuonekana fedha zilizotolewa zilikuwa ndogo sana, serikali ikakopa Sh47 bilioni kutoka benki za ndani na hivyo jumla ya fedha za mikopo kwa wanafunzi kuwa Sh111.3 bilioni.
Meghji alisema, Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limeongezewa Sh7 bilioni kwa ajili ya posho ya chakula kwa askari. Wakati bajeti nzima ya Ngome mwaka jana ilikuwa ni Sh189.5 bilioni, mwaka huu fedha hizo zimeongezwa hadi kufikia Sh199.8 bilioni.
Kulingana na taarifa ya Wizara ya Fedha, Sh5 bilioni zimetengwa kwa ajili ya wafanyakazi watakaopunguzwa Mamlaka ya Majitaka na Majisafi Dar es Salaam (Dawasco) na Sh4 bilioni zimetengwa kushughulikia kesi zinazohusu mamlaka hiyo.
Bonde la Ihefu limetengewa Sh1.5 bilioni kuhifadhi mazingira, huku bajeti ya mishahara ya Wizara ya Maji ikipungua kutokana na kuhamisha wahandisi 83 wa maji kwenda halmashauri.
Kuhusu ruzuku iliyotolewa kwa Tanesco kutokana na ukame na mafuta kupanda, inaonyesha Sh20 bilioni zilitumika kulipia nishati hiyo kutoka Songas na IPTL na Sh101.4 bilioni zilinunua mitambo ya kuzalisha na kusambaza umeme.
Taarifa hiyo inaonyesha Sh103.6 bilioni zilitumika kukodi mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura na Sh125 bilioni ni dhamana ya mikopo kwa ajili ya kulipa umeme kutoka Songas na IPTL.
Hata hivyo, wabunge walihoji hatua ya kuendelea kutoa ruzuku kwa Tanesco, wakati hakuna ukame na uzalishaji wa umeme unaendelea kama kawaida.