Wanene kuongezewa marupurupu

Wanene kuongezewa marupurupu

Zitto,

Kwanza nikupe pongezi ya kujibu tuhuma ulizopewa. Pili, natumaini hilo jibu ndio jibu lako la mwisho mpaka utakapofikia uamuzi wa kusemea swala hili ama utakapoacha kujikanyaga. Tatu, ukija kusema hapa, uje kusema ukweli, ama usiseme kabisa. Kimya ni bora kuliko kusema uongo.

CDF,
Hakuna udharura wa kujadili, nadhani muda utumike kufanya utafiti zaidi jinsi gani mfuko huo utaratibiwa. Tujifunze kwa kina toka kenya ambao wameanzisha mfuko huo mwaka 4 iliyopita. Ni vyema pia tukakukumbuka kwamba kenya haikuanza hii mifuko leo ilianza toka miaka ya 60 -majimbo system (1963), District Development Grant Program (1966), the Special Rural Development Program (1969/70), the Rural Development Fund, District Development Planning (1971), and the District Focus for Rural Development (1983'84).

Kwa maelezo mafupi, msome Dr. Ludeki Chweya, Senior Lecturer, Department of Political Science and Public Administration, University of Nairobi at

http://www.africanexecutive.com/modules/magazine/articles.php?article=720
 
Kichuguu kwako wewe hili linaishia kwenye kuiba mke wa mtu tu, sisi wahafidhina tunaangalia bigger picture, ikiwa ameweza kuiba mke wa mtu hutashindwa kuliibia taifa given a chance! we call it LOGIC!
Ndugu yangu Masatu,

Nadhani unakosea unaposema unatumia LOGIC, labda ungesema WISDOM. Logic haisupport kabisa arguments zako. Ingawa sielewi ulikuwa unaongelea LOGIC gani, lakini katika mazingira ya mada hii ni dhahiri kuwa unatumia Propositional Logic inayotumia Predicate Calculus kufanya reasoning, na hasa hasa nadhani unajenga hoja yako kwa Modus Ponens au Hypothetical Syllogism.

Modus Ponens unaweza kuwa umeitumia hivi: "Mtu akilala na mke wa watu then mtu huyo ni mwizi." Wakati Hypothetical Syllogism unaweza kuwa umeitumia hivi: "Mtu anayetembea na wake za watu siyo mwaminifu," na "mtu asiyekuwa mwaminifu ni mwizi."

Rules hizi zote ni false kwa vile unachukulia kuwa: (a) Mwanamme ni superior kwa mwanamke, kwa hiyo mwanamme ndiye aliyedictate terms za kulala na mwanamke yeyote. (b) Mwanamke anatumika kama kifaa tu, subject ya logic ni mwanmme, ndiyo maana Modus Ponens inamfanya mwanamke aonekana kama "ameibwa." (c) Ubaya wa Hypothetical Syllogism ni kuwa unachukulia kuwa wizi ni set kubwa sana ambayo ina watu wote wenye tabia mbaya. Kwamba mtu akiwa na tabia mbaya kama kulala na wake za watu basi huyo tayari ni mwizi. Maelezo mengi yanaweza kutolewa kuonyesha limitations za rules hizo. Ni kutokana logical limitations za argument kama hizi ndiyo maana kosa la kulala na mke wa mtu siyo criminal case.

Ingawa nakubalina nawe kabisa kuwa kitendo cha Mheshimiwa Mbunge kulala na Mbunge mwenzie ambaye ni mke wa mtu siyo kizuri kimaadili, lakini tusistretch sana swala lile. Tungepiga kelele sana kama tu Mheshimiwa Mbunge angekuwa amelala na secretary wake ambaye ni mke wa mtu kwa vile hapo kunakuwa na differential power kwamba Mbunge katumia madaraka yake kumlazimisha huyu mwanamke akubali kufanya kitendo kile, lakini hawa ni wabunge wawili wenye hadhi sawa, tena mwanamke anatoka chama tawala.
 
Samahani, nilipoandika post hiyo hapo juu kulikuwa na jibu la Masatu tu, unfortunately sikuipost immediately kwa hiyo wakati nakuja kuipost nikakuta kuna posts nyingine kibao!. Hebu tuendelee na mjadala wa maslahi ya wabunge, hili la Zitto nadhani halitufikishi popote, wanaolitaka walipeleke kule kwenye vibweka vya wakubwa.
 
Kichuguu.. watu wakielewa hizi nadharia za mathematical logic wataona kuwa zinakubaliana kabisa na philosophical logic. Na wakishaelewa hili watakuwa wapesi kunusa contradictions na fallacies in their argument. Kati ya vitu vya msingi katika mantiki (logic) ni jinsi gani mtu unafikia hitimisho (conclusion) baada ya kufuata hatua fulani. Ukiruka hatua fulani basi unaweza kufikia hitimisho ambalo si la kweli au lenye makosa ya kimantiki. Nashukuru kwa kutoa somo hilo hapo juu.
 
Mh Zitto,

Shukran kwa ufafanuzi wako.

Kimsingi suala halikuwa "kukulazimisha" useme lahasha! Baadhi yetu tulichokuwa tunasisitiza uwepo wa fair play baina wanasiasa na watu mbalimbali wanaojadiliwa humu.

Inashangaza na kushtusha kuwa kuna watu wamejipachika u-press secretary, wako na kuwa mafundi wa kukujibia hoja ilhali wewe mwenyewe upo na una uwezo tosheleza wa kujibu au kama ulivyoamua kutojibu.

Wengine wameenda mbali kidogo na kudai haya mambo ni binafsi na hayana umuhimu kujadiliwa humu JF. Kwa wadau kama mimi hii ilikuwa U-turn ya mwaka. Kimsingi tulitaka ufafanuzi iweje wengine ( EL, JK, JM, nk ) mambo yao ya binafsi yanajadiliwa kwa undani (bila kujali kama ni kweli au uzushi) lakini cha kushangaza hawa madali hawakuthubutu kusema hayo ni mambo binafsi na wengine ndio wakawa wanashabikia kabisa.

Kwa bahati mbaya Mh na wewe yamekukuta ( whether ni kweli au si kweli) hawa self-proclaimed press secretaries wamekuwa wakali as anaejadiliwa ni nabii fulani.

Kama nilivyotangulia kusema hakuna anaekushurutisha kusema, wewe enjoy exclusive privilege uliyopewa na "wakubwa" mpaka muda muafaka na kama ulivyosema at ur owns terms.

Lakini kukumbusha tu wenzio ktk siasa na wakubwa kufikia kuitwa Waziri Mkuu hawaruhusiwi hata kusema naenda kula ni kosa kubwa wanatakiwa wajibu hapo hapo. At least tumejua kuwa hizi ndio "standards" za hapa JF. Bahati mbaya wengine wageni tulikuwa hatujui kama ni "haramu" kuhoji mambo au viongozi wa Chadema.
 
Zitto check your PM....

Masatu pole sana kama unafikiri unaonewa. Let me put you at ease... yote yanazungumzika... Lowassa angekubali nimpigie simu baadaye wale ya kwenda kula msingesikia! Msolla angekubali kuzungumza na mimi badala ya kukata simu nisingeweka hiyo hadharani. Kama angeniambia nipe siku kadhaa nifanyie uchunguzi nisingelalamika. Zitto, kaja kawaambia nitazungumza watu hawataki, wanataka sasa! so, umetosheka na jibu la Zitto au bado unataka details zaidi?
 
Zitto check your PM....

Masatu pole sana kama unafikiri unaonewa. Let me put you at ease... yote yanazungumzika... Lowassa angekubali nimpigie simu baadaye wale ya kwenda kula msingesikia! Msolla angekubali kuzungumza na mimi badala ya kukata simu nisingeweka hiyo hadharani. Kama angeniambia nipe siku kadhaa nifanyie uchunguzi nisingelalamika. Zitto, kaja kawaambia nitazungumza watu hawataki, wanataka sasa! so, umetosheka na jibu la Zitto au bado unataka details zaidi?

Mwakjj

Hapana sioni kama naonewa, tatizo ni ugeni tu nilikuwa sijui "standards" za JF kiasi naanza kuzijua nitajitahidi niji-adjust kufit kujua the "untouchable ones" keep it up... Jiunge na Chadema kwa maendeleo.. hakuna kulala mpaka kieleweke!
 
Mheshimiwa Zitto,

Mengi yanaandikwa magazetini na sio kila linaloandikwa gazetini ni sahihi kwa mhusika

Nimefurahi kusikia kwa maandishi yako mwenyewe unathibitisha kwamba yale
yaliyoandikwa gazetini ni maneno yako sahihi. Kwa maana hiyo unakanusha kuhusika na hiyo kashfa.

Mimi nakubali kukanusha kwako na kwa hilo tuendelee mbele. Ila tu kuanza kuongelea agenda nyingine kwa wale waliotumia haki yao ambayo kila mwana JF anayo ni sawa na ku question basic principle ya JF ambayo ni haki ya kutoa hoja na kujibiwa kwa hoja bila kuanza kupachikwa majina mengine unless kuna ushahidi wa kutosha.

Nina uhakika unapokuwa Bungeni unategemea ukitoa hoja yako itajibiwa kwa hoja na sio mhusika kuanza kuongelea ajenda zingine.

Kuhusu mijadala kubadilika kadri inavyoenda mbele nafikiri hiyo ndio JF yenyewe na wewe una uzoefu wa kutosha juu ya hilo na hakuna haja ya kulia
foul play sasa wakati kubadilika huko kunatokea kila siku na kwenye mijadala mbalimbali, mfano mzuri ni mjadala wa Tido Mhando ambao sasa umeenda kwa Mwakyembe.

Mafanikio mema katika kazi zako.
 
Habari za masiku tele ndugu zangu.

Nimeona ni muhimu niingie katika mjadala huu ili niweze kuweka wazi baadhi ya facts zisaidie mjadala wetu.

Mshahara wa Mbunge kwa mwezi Tshs. 1,200,000. Kodi inakatwa asilimia 30 ambayo ni sawa na Tshs. 360,000. Kwa wale ambao wamechukua mkopo wa magari kila mwezi analipa Tshs. 500,000. hivyo pato la mbuge baada ya makato ni Tshs 340,000.

Posho ya ubunge

Hii tunapewa shs 1,000,000 kila mwezi. pesa hii ni kwa ajili ya huduma za ubunge kama mawasiliano, kulipa wasaidizi, kuganya utafiti kwa ajili ya miswada na pia mafuta. Mafuta tunalipwa kwa sasa lita 500 kwa mwezi kwa wastani wa shs 1000 kwa lita.

Posho ya kujikimu na vikao
katika hili tunalipwa shs 55,000 tunapokuwa dodoma kwa ajili ya malazi na chakula. kuna habari kuwa tunapewa nyumba dodoma, sio kweli bali kila mbunge anatafuta makazi yake.
mbunge akihudhuria kikao cha bunge analipwa shs 70,000 kwa kikao. hivyo kwa wale wanaohudhuria kwa siku ni 125,000.

maombi ya wabunge:
wabunge walitaka kulipwa zaidi pesa ya mafuta ili iendane na bei ya mafuta na pia kulingana na ukweli kuwa baadhi ya wabunge majimbo ni makubwa sana na hivyo lita 500 kwa mwezi ni kidogo. mfano, mimi kutoka dodoma mpaka kigoma kwenda na kurudi ni km 1100 hivi.

pili, wabunge walitaka kuongezewa uwezo wa kuajiri wasaidizi wenye elimu kubwa zaidi. mfano mimi msadizi wangu ambae ana shahada ya sheria ninamlipa shs 500,000 kwa mwezi. kwa malipo ya sasa ninatakiwa kulipa shs 70,000 kwa mwezi.

mimi sijajua kwa malipo ya sasa yaliongozeka ni kiasi gani kitakwenda kwa mishahara na maeneo mengine. hivyo siwezi kucomment na kusema nini.

ukweli ni kwamba mjadala wa malipo kwa wabunge vs matunda ya kazi zao ni mjadala muhimu sana. lengo liwe ni kuzuia malipo makubwa bila tija na pia kuepuka kuwa na wabunge wasioweza kufanya kazi sawasawa ya kuisimamia serikali

Jamani huyu Mzinzi amerudi kinyemela? nina maswali ya kumwaga juu yake au atajibu wakili wake mwanakijiji.
 
Mswahili,
Tafadhali ndugu yangu tupe pumzi na sisi...
Umesha sikiwa vya kutosha maana kila hoja ya Zitto Mada zote humu ndani, warudisha habari ya maswala. Imekuwa basi kila aendako?.. Hakuna kiongozi msafi Tanzania hilo jua na liweke mbele kabisa. Nadhani bora ifunguliwe mada inayohusu nyumba ndogo za viongozi!..Aibu tupu aibu.
 
Mkandara.

Sikuelewi? huyu bwana alifukuzwa Zanzibar University kwa ugoni akiwa mwaka wa kwanza tu alikuwa mwanafunzi wa B.B.A.

tulijua kwa vile amekuwa mbunge atajistahi. Mkandara unajua future ya Amina ameharibu huyu mpuuzi? wewe kama Amina angekuwa dada yako ungejisikiaje? Mpanjia ameanza upya kisa huyu mpuuzi wewe unasema tumwache.
angekuwa nchi za watu akingefukuzwa uanachama na ubunge.

anaweza vipi kujadili marupurupu wakati yeye anatumia muda huo kutembea na dada zetu au wake zetu. hatujui Mpanjia kama kamuachia Mwenyezi Mungu au atamshughulikia huyu mzinzi.

Namshauri Mpakanjia kuwatafuta vijana pale Uwanja wa fisi au Tandika siku akija Dar ni kumfuturu huyo jamaa hiyo ni dawa nzuri sana.

Mtu huyu huyu kamuharibu Dada yetu Muhonga kwa na kumdanganya atamuoa.

Mkandara.
Fikiria unyonge anaoupata mtoto wa Medi na Chifupa? inabidi week day akae kwa baba yake na weekend aende kwa babu yake kwani amina sasa hivi hayuko katika hali nzuri.

sisi tuliolelewa kwenye malezi ya wazazi wawili tunajua faida ya mtu kukua ukiwa na baba na mama.

Zitto amelelewa na mama yake tu hadi jina lake la surname ni la upande wa mama yake'. baba yake alikataa mimba ya mama yake.labda kutokana na background hiyo hajui nini kinampata mtoto wa Amina au ndio ile roho mbaya "mbona na mimi nililelewa na single parent"

Mkandara nimekuwa nikiheshimu na kuona ni mtu mwenye upeo mkubwa humu kwenye JF unafanana na Mwanasiasa lakini kuja kutetea uovu namna hii umeniangusha ndugu yangu.
 
Zitto amelelewa na mama yake tu hadi jina lake la surname ni la upande wa mama yake'. baba yake alikataa mimba ya mama yake.labda kutokana na background hiyo hajui nini kinampata mtoto wa Amina au ndio ile roho mbaya "mbona na mimi nililelewa na single parent"


Damnnn,

Kumbe it is this personal? Halafu huyu ndio anayetaka kujua "ukweli"? Now I can understand the logic behind comments zako katika mijadala ya udini na uchaga!!!!

Tanzanianjema
 
Tanzania Njema.

Zitto na Amina ni dini moja hapo hakuna suala la udini usipindishe mada. wakupinga kama habari hii ya uongo ni Zitto mwenyewe sio wewe. tunamjua Zitto nje ndani. kalelewa na upande wa mama yake( kikeni) na tuna hadi file ya mama yake kukimbia Dar kama unataka niende personal sema?. huko sintakwenda kwani itakuwa kumuumbua Mheshimiwa Mzee wa chini.

ila wakati mwingine mtu anapofanya jambo la kinyama au aibu unakwenda kwenye background yake. hujawahi kusikia ukoo huu una akili za nature. au mtoto huyu kachukuwa tabia au busara kwa babu yake? Zitto hakutoka familia yenye malezi mazuri au kwa kiswahili rahisi yenye heshima. sijawahi kutoa kauli mbaya kwa Mkumbo hujiulizi Tanzania njema? Tabia ya mtu inaweza kuwatukanisha wazazi wako au kuwa praise.
 
But unachofanya ni cha kinyama zaidi kuliko huo unaouita unyama na jaribu kujua ukweli wa issue ya Zitto na Amina kwa undani halafu umuhukumu kwa ushahidi uliokuwepo (kama upo) lakini sio kumhukumu kutokana na ......nashindwa hata kusema zaidi ...aleykum salam...

Tanzanianjema
 
Tanzania N.
Mie sijawahi kuzini na mke wa mtu. wewe unafurahi kumuona Amina kaharibikiwa? wewe unaona raha Medi anaanza upya maisha yake? wewe unaona raha mtoto wao anahangaika alizoea kuwaona baba na mama wakiwa pamoja katokea mshenzi mmoja ambaye wewe unaona tunamuonea?

Masuala ya historia ya Zitto sijazua hata moja. amekulia kwenye shida sana hilo halina hata chembe ya ubishi na family yake si yenye maadili.mama yake Mzazi hakanyagi Dar kwa takribani miaka kumi. ukitaka sababu nitaziweka wazi kwenye PM yako.

Yako mengi tulikuwa tunanyamaza tukijua jamaa mstarabu kumbe anatuona wajinga sasa tutafungua rasmi Nani Zitto.

TN.
Michael Tyson hawasumbuwi wamarekani kwa tabia zake za mikasa mingi. ni kutokana na kuijua background yake. hakuwa na baba na wala hamfahamu na amekuwa kwa shida sana.
samahani mkuu kwa kukuudhi.lakini ukweli lazima tuuweke wazi. Mpakanjia hakuwa na haja ya kwenda bungeni angeniona tu.
 
Mswahili,

Kumbe unafahamiana na Mbunge Zitto personally kisasi hicho; inaelekea una data zake nyingi sana. Hata hivyo kwenye hili la Mbunge Amina, hakuna data zilizotolewa kumtia Mbunge Zitto hatiani, ndiyo maana tunashauri jambo hilo liachwe kusudi tuendelee kujadiliana mambo mengine yaliyo mbele yetu. Kukumbusha mlolongo wa mambo katika sakata hili kama yalivyoripotiwa, kama kumbukumbu yangu iko sahihi naweza kuorodhesha matukio saba vile yanayo-summarize sakata lote kama ifuatavyo:

(a) Inasemekana Mbunge Amina alionekana na Mbunge Zitto kwenye bar moja pale Dodoma huku akiwa amevaa koti la Mbunge Zitto. Mtu mmojawapo aliyewaona wabunge hawa katika position hiyo akawapiga video au picha kwa kutumia cameraphone.

(b) Naibu Waziri Mmoja aliipata hiyo video ya (a) hapo juu. Akamwita Medi, mme wa Mbunge Amina, aje waonane ofisini kwake hapo Dodoma. Medi akaitikia wito wa Waziri na kuja Dodoma. Yaliyojadiliwa huko ofisini hayajulikani, ila inasemekena kuwa video ile ilitumika kumshawishi Medi ampe talaka mke wake, ambapo Naibu Waziri yule alimsaidia Medi kumwandikia Spika barua kutoa taarifa kuwa amemtaliki mke wake Mbunge Amina kutokana na kubainika kuhusika kimapenzi na Mbunge Zitto. Vile vile akamtaka Spika amwonye Mbunge Zitto kwa kitendo kile.

(c) Mbunge Amina akakanusha kuwepo kwa uhusiano wa kimapenzi kati yake na Zitto na kudai huo ni uzushi uliofanywa na Naibu Waziri fulani ili kumvurugia ndoa yake na hivyo kumchafulia jina kusudi asitimize azma yake ya kuwania uenyekiti wa UVCCM kama alivyokuwa ameshatangaza kutaka kugombea. Zaidi ya hapo akaahidi kuwa ataongea na waandishi wa habari ili kuweka mambo hayo wazi zaidi.

(d) Baba wa Mbunge Amina akamzuia binti yake asiongee na waandishi wa habari yale aliyotaka kuzungumza kuhusiana na sakata hilo kwa madaia kuwa yalikuwa ni mambo ya kifamilia zaidi na kisiasa. Kwa hiyo yale ya kifamilia watayongea wao kama kifamilia na yale ya kisiasa yataongelewa kichama.

(e) Mbunge Zitto akakaripotiwa akikanusha kuwapo kwa uhusiano wa kimapenzi kati yake na Mbunge Amina. Na akatishia kumpeleka mahakamani mtu yeyote atakayekuwa anamchimba katika mambo yake binafsi.

(f) Kukatokea habari nyingi za kutatanisha kuhusu hali ya Mbunge Amina: Kwanza zilianza kuwa Mbunge Amina ametoweka na wala haijulikani aliko, mara ikaripotiwa kuwa Mbunge Amina ameharibikiwa akili, wengine wakahisi kuwa ameshikilliwa na kundi fulani ili asitoe taarifa alizokuwa akitaka kutoa.

(g) Medi, mme wa Mbunge Amina, akatangaza kuwa bado anampenda mke wake wala hana matatizo na familia ya mke wake. Akaonekana akiwa kituo cha basi kumpokea mmoja wa wazazi wa Mbunge Amina aliyekuwa akitokea bara. Akasema hataki kuongelea mambo yanayohusu ndoa yake hiyo tena, na akawataka watu waache kumwandama mke wake ili kumpa nafasi ya kufanya kazi zake sawasawa.


Baada ya taarifa hizo saba, hatuna taarifa nyingine za zinazoonyesha dhahiri kuwa Mbunge Zitto na Mbunge Amina kweli walifanya yale wanayoshukiwa kufanya au walisingizwa tu kwa sababu za kisiasa. Leo hii Mbunge Zitto amerudia tena kutamka kuwa hakuhusika na jambo lile. Sasa kama wewe una taarifa zaidi kuhusiana na hilo basi ziweka hapa. Na kama hujaridhika na majibu yao, na unataka kutafuta habari hizi kikamilifu positively, nadhani unaona kabisa kuwa Wabunge Zitto na Amina siyo mashahidi wa kuuliza kwa vile wameshazikanusha kwa nguvu sana. Hata ukipiga kelele vipi hutapata lolote jipya labda kama unatafuta jambo lingine kwa Zitto ikiwa na kutaka kutumia huu mwanya kutoa background chafu kuhusu malezi yake ambalo nadhani siyo jambo la kistaarabu. Kwa mtazamo wangu nadhani kama kweli unataka taarifa hizi kwa kina, watu wa kuuliza vizuri ni Medi na yule Naibu Waziri. Lakini kwe vile Medi naye ameshasema kuwa hataki kuziongelea tena na alishaonya watu wasimfuatefuate mke wake kuhusiana na jambo hilo unabadki na source moja tu. Nadhani umfuate yule Naibu Waziri ambaye ndiye aliyetoa taarifa hizo kwa Medi. Kwanza inawezekana kweli taarifa zile hazikuwa za ukweli, na ndiyo maana huenda baada ya Medi kutulia na kuzitafakari akaona hakuna haja ya kuziongelea tena, na hivyo kutangaza kuendelea kumpenda mke wake.

Kuhusu kuvuruga ndoa ya Amina na Medi, mtu wa kumpa lawama zaidi nadhani ni yule Naibu Waziri aliyemwita Medi na kumshawishi amwache mke wake. Tumekua tukifundishwa kuwa ugomvi wa mme na mke usiuingilie, lakini bwana huyu aliingilia mambo ya unyumba wa wengine. Kama angekuwa na nia njema, angemwonya Amina kabla ya kufikisha taarifa hizo kwa mumewe.

Mimi binafsi simfahamu Mbunge Zitto na wala sina ushabiki na chama chochote cha siasa: Siyo CCM, CUF, CHADEMA, NCCR,TLP, UDP, DP, na utiriri mwingineo, kwa hiyo usiseme kuwa namtetea au ni msemaji wa Zitto kwa vile yeye ni CHADEMA, la hasha. Nimeondoka Tanzania wakati vyama hivyo ndiyo vinaanza tu, wakati huo Zitto alikuwa bado yuko sekondari na mimi nilikuwa nafundisha Chuo Kikuu. Kwa hiyo niamini kabisa kuwa siko biased katika swala hili. Nadhani tunataka kwenda mbali sana, hakuna lolote jipya litakalopatikana kwa kuandika posts nyingi ulizoweka sehemu tofauti tofauti kuhusiana na jambo hilili. Kwanza, kama kungekuwa na ushahidi kuwa kweli walifanya mambo yale na wakakiri, tungelaumu wote wawili siyo mmoja tu.

SAMAHANI KWA KUANDIKA POST NDEFU VILE, SIKUJUA KUWA ITAKUWA NDEFU.
 
Kaka Mswahili....

Katika maisha nimejifunza kitu kimoja kikubwa...wazungu wanasema "what goes around, comes around"....unachokifanya hapa leo utakikumbuka....inshaalah utaweza kusoma makosa kama nilivyosoma na sio kwa machungu makubwa kama niliyopitia mimi........na najua wewe ni mtu wa imani.......critisism na vijembe ni part of the game but not katika level uliyofikia hapa....

Tanzanianjema
 
Mswahili,

Kama uko serious, nakushauri kuwa wakati ungali hai duniani hapa usinyooshye mkono wako kusema yule ni masikini, au yule kakulia kwenye taabu. Walisema unapopanda mlima, usisahahu kuwasalimia unaowakuta njiani kwa vile unaweza kukutana nao tena wakati unatelemka mlima ukiwa umechoka. Kuna mifano ya watu wengi sana waliokua kwa taabu lakini wakawa watu wa muhimu sana katika jamii na vile vile kuna watu wengi waliokua kwa raha wakaishia maisha ya taabu; hakuna sheria katika maisha. Wanasema aliyekupa wewe ndiye aliyemnyima mwingine, and when god closes one door, he opens the other. Sitaki kusema kuwa unalofanya ni kufuru, lakini sijui kama unajua unachofanya.
 
Mswahili,

Nakuomba punguza jazba na usiende personal kwasababu mheshimiwa Zitto hajafanya lolote la kumdharau mtu hapa zaidi ya kujaribu kuficha au kutokusema nini kilitokea. Aidha ameshasema hahusiki na hiyo kashfa, wacha tumwamini kwasasa ila tunaweka kwenye kumbukumbu hilo maana kaandika
kwa maandishi yake mwenyewe wala sio kukaririwa na gazeti. Kama kuna siku ukweli zaidi utajulikana ndio tutaweza kujadiliana zaidi.

Kichuguu, naona umechambua mtiririko wa matukio, jamaa alitishia kwenda mahakamani, mbona hajaenda? Hayo ndio mambo ambayo tumeyasikia na kuyaona sana huku Majuu. Ukiona mtu anatishia kwenda mahakamani halafu haendi jua kuna mambo hayako sawa. Magazeti yaliyoandika hizo habari wala hayajaomba msamaha, Nchimbi hajaomba msamaha, kwa mazingira hayo nilitegemea jamaa afanye kweli. Tena ana personal lawyer ofisini kwake kwahiyo mambo kwake ni rahisi mno.
 
Back
Top Bottom