Zitto,
Kabla sijauliza maswali yangu ningependa kutoa maelezo yafuatayo;
Tunafahamu na kuheshimu uamuzi wako (kuzungumza/kutozungumzia) kuhusu jambo hili.
Hata hivyo ukiwa kama mdau muhimu sana ktk forum hii na kwa kweli tunajivunia kuwa na mtu wa calibre yako hapa na hususan kwa michango yako makini, yenye kina na ujasiri wako wa kupambana na uozo ktk nchi yetu ukiwa ndani na nje ya bunge.
Na kwa kuwa wewe ni miongoni mwa wanasiasa vijana na wenye mvuto ktk contemporary politics za Tanzania. Maswali yangu kwako ni haya;
1. Je Mh Zitto utakubali kuchukua pongezi zangu za dhati kwa niaba ya wana JF wote?
2. Je Mh kwa kukataa kutupa hii habari nyeti ( Breaking newz) sisi wana JF hapa huoni kuwa unainyima forum nafasi muhimu ya kujitangaza na kupata wasomaji wengi? na nafasi ya kujivunia kama miongoni mwa vyanzo muhimu vya habari ndani na nje ya nchi?
3. Kama namba 2 ni kweli. Je Mh utakuwa tayari kubadili uamuzi wako na kutupatia habari hii ambayo itakuwa ni hot sana (scoop)
4. Kama utaamua kubaki na msimamo wako wa kusubiri wakati "muafaka" kuelezea ukweli wote. Je huoni kuwa wakati unasubiri huo wakati hadhi na hishma yako kwa jamii itakuwa imeporomoka zaidi beyond repair?
Masatu,
Thats Ok labda tu niongezee maswali mengine...
5. Je Zitto wapiga kura wako wa kiume wa Kigoma Kaskazini utawa hakikishia vp usalama wa wake zao wanapokuja kukuona ktk surgery yako? Vilevile na wakazi wa Dodoma ambako utapiga "kambi" wa miezi miwili kuanzia mwezi ujao nao utawahakikishia vp usalama huo?
6. Je Zitto ktk mperampera ule na Amina ulitumia kinga?
Mheshimiwa naomba kutoa hoja......