Wanawake tujikumbushie vituko vya leba

Wanawake tujikumbushie vituko vya leba

Kwani unapodungwa sindano ya ganzi ili kung'oa jino inakuwaje husikii uchungu?

Naelewa ni vitu viwili tofauti lakini vinalingana.

Uchungu wowote mwilini hutokea pale receptors zinapopeleka habari ya uchungu kwenye ubongo na ubongo kutoa jawabu kuwa hakika huu ni uchungu.

Uchungu wa uzazi unatokana na kutanuka kwa cervix ambayo inakuwa imefuka kabisa kuzuia hata tone la maji kutoka halafu hutanuka mpaka ukubwa wa sentimeta 10.

Ganzi inachofanya ni kuzuia receptors kupeleka habari ubongoni kwa hiyo uchungu hupati.
Uchungu wa uzazi unatokana na kutanuka kwa cervix?? Sawa
 
Tunahitaji mafundisho zaidi lakini siyo sehemu Za wazi Kama hizi ambako wanaume wanatusoma na watoto pia!
Kila ktk maisha kinahitajika mafundisho iki kiweze kufanyika Kwa usahihi !

Iwe siri kwa sababu gani wakati tukianzia O level shule mnachorewa hadi picha jinsi mwanamke anavyozaa??? Vitabu vimejaa mitaani na video za jinsi watu wanavyozaa Hiyo ni siri? Afterall wanaongelea maumivu ya labor na sio jinsi walivyozaa?Wanaozalisha wanaume, I mean, hamna wasichojua unless kuna watoto wa kindergarten hapa.
Don’t make life too serious utakufa mapema bure!
 
Vibaya hivyo! Wanaume wote tufe sasa dushe ungepata wapi!? Pole sana time ya kuongeza mwingine imewadia.

Mmmhh shikamooh mama mie nilivyoenda leba nasikia nilisema "uwiii wanaume wote wafe" manesi wakanijibu afe wa kwangu tu maana waume zao bado wanawapenda hahahhaha sitaki kusikia leba maana akili haikuwa yangu mweehh shkamooh mama
 
Ndiyo Madaktari hushauri kugegedwa mpaka last minute kama hakuna complications husaidia njia kufunguka kirahisi.

Hivi mjamzito asipofanya mapenzi kipindi chote cha ujauzito,anaweza akapata shida kujifungua?
 
Poleni sana na hongereni sana sasa hao watoto muwe na uchungu nao basi.
 
poleni sana mke wangu miezi minne mimba ilimtesa sana alikuwa anashindwa kuhema tukawa tunaweka godoro na net nje tunalala.Kufika miezi sita akaanza kuvuja maji.Akalazwa muhimbili kufika mimba miezi saba ilibidi ajifungue kwa OP kumuokoa mtoto yaani premature.Akakaa wodi ya Kangaroo karibu miezi miwili.Kwahiyo alikaa hosp zaid ya miezi mitatu kwakeli aliteseka sana nilijua nampoteza mke wangu mpendwa ila kabinti kana akili za ajabu yaan very bright
 
Mimi nilivyofika Leba ,nikapelekwa sehemu ya mapumziko walikuwepo wajawazito wengii,sasa uchungu ulikuwa haujanishika kivile nilikuwa natokwa na maji tu, daktari akanipima akasema bado,,sasa mle kwenye ukumbi kulikuwa na wamama wengi mwingine anaruka, mwingine anajivuta vuta chini, si nikaanza kuwacheka nikasema mbona mimi siumwii.

kKumbe bana uchungu unakuja taratibu, nikawa nashangaa kila muda unavyozidi kwenda maumivu yananizidia wale niliokuwa nawacheka wao wanajifungua wananiacha tu, kukakucha asubuhi niliona ni mwaka na nikasema sirudiii ,kama nilikuwa natembea uchungua ukaja ghafla naganda kama sanamu kama kuna mti ntaung'ang'ania kweli, ilifikia muda sitaki kuja kusalimiwa wala kuonwa na mtu yeyote maana watu wanavyozidi kuja kuniona ndivyo uchungu unazidi kuwa mkali nikawazuia.

Niliita majina yote ya Mungu nikawa namshika mama yangu namuambia aniombee haraka uchungu upoe kiuno changu kilikuwa cha moto nauchukua mkono wa mama nauweka kiunoni kwangu namwambia aniombee mama yangu mpaka alilia nilivyokuwa nahangaika nyie acheni jamani.

Usiku ulipofika saa 2 nikasikia kusukuma nikapelekwa chumbani nimefika kule kila nikisukuma hola,,wakaniwekea maji ya uchungu wapiii wakasema huyu anatakiwa kisu tu nikajitahidi kusukuma wakaja madaktari na manesi wamenizunguka mwingine kanishika kichwa ,mwingine tumbo anabinya,mwingine anaangalia njia ya mtoto (sitasahau)mtoto alitoka saa 8 nanusu kuamkia tarehe 8 na mwaka ....8 loo kazi niliipata

Sasa najiuliza wanaozaa watoto 7 au 8 wanawezaje?maana mim toka nizae sina hamu tena halaf sijawah pata maumivu kama yale toka nizaliwe sema na ukweli
Mama Aheshimiwe ,maana wanaume wangepewa huu uchungu hata dakika wangeukataa na wangetuheshimu sana
Ni kweli mnapitia magumu sana lakini je,unakua uchungu wa kupigwa teke la korodani!?
 
Hata nilikuwa naijua sasa
mada ya cku nying , hakuna dawa inaitwa hvo, kuna mahali panaitwa epidural space kwenye spinal cord huwa panachomekwa sindano ya kama mama anafanyiwa operation , lakin kama mama anatakiwa kuongezewa uchungu, dawa yake inaitwa oxtocin
 
Nimepitia comment nyingi, inaonesha kweli kuna uchungu ulio tofauti kabisa na tunavyodhani sisi wanaume. Hii sio hoja, hoja ni kwamba, mbona nguruwe, panya na viumbe wengine wanazaa watoto wengi tena pasi na msaada wala kujigalagaza? Hili nalo laweza kuwa ni uthibitisho wa uwepo wa Mungu na yote yaliyozungumzwa kumuhusu.

Ushauri, wanawake wachukue nafasi zao pasi kwenda kinyume na Asili kuu, kwakuwa tu ipo. Na mtaendelea tu kuzaa, kifungo chenu ni tamaa zenu ziwakazo juu yetu. Ova.
 
Iwe siri kwa sababu gani wakati tukianzia O level shule mnachorewa hadi picha jinsi mwanamke anavyozaa??? Vitabu vimejaa mitaani na video za jinsi watu wanavyozaa Hiyo ni siri? Afterall wanaongelea maumivu ya labor na sio jinsi walivyozaa?Wanaozalisha wanaume, I mean, hamna wasichojua unless kuna watoto wa kindergarten hapa.
Don’t make life too serious utakufa mapema bure!

Hapana siwezi kufa mapema Kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu!
Imeandikwa " Mwenye Haki wa Mungu ataishi Kwa Imani"
Haya tuje Kwenye hoja ya msingi;

Kama ni hivyo basi Hata chumbani kwa baba na mama watoto wakubwa wawe wanalala na wazazi wao kwa kuwa kinachofanyika kule wanakijua kuanzia four form wamefundishwa Kwenye somo la baiolojia? Au siyo?!
 
Hapana, unajua kila mtu ana namna yake ya kupunguza maumivu. Mwingine akipiga kelele anaona kupata nafuu na wengine tunapenda ukimya tu.
Mie siku zangu zilipofika, sikupiga kelele wala mayowe hata sikuinua mdomo wangu kusema neno ila nilikuwa nauma meno balaa. Na kwa kufanya vile nilikuwa naona napata nafuu

Hapo mwishoni sijakusoma vizuri , ulikuwa unauma meno watu ? Yani unawang'ta?
Au ile ya kuuma meno wewe mwenyewe ktk kujikaza huku ukiugulia uchungu kimoyomoyo ?
 
Hapana siwezi kufa mapema Kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu!
Imeandikwa " Mwenye Haki wa Mungu ataishi Kwa Imani"
Haya tuje Kwenye hoja ya msingi;

Kama ni hivyo basi Hata chumbani kwa baba na mama watoto wakubwa wawe wanalala na wazazi wao kwa kuwa kinachofanyika kule wanakijua kuanzia four form wamefundishwa Kwenye somo la baiolojia? Au siyo?!


Again wanaoelezwa hapa ni wanaume ambao ni waume za wahusika na madakatari wanaozalisha hao wanawake unaojifanya ni siri, kama ulilala nae akakupa mimba cha ajabu nini kwenye kutoa mtoto??? Come on ndo nakwambia don’t take life too seriously usije kufa kabla ya muda.
Hao watoto watafanya hayo kwa wake zao na waume zao watahusika. Ila kama huyo mtoto yuko hapa jf, si jambo sio ajabu kusoma hizi habari.
Mfano wako hauna kichwa wala miguu, huna point.
 
Hapo mwishoni sijakusoma vizuri , ulikuwa unauma meno watu ? Yani unawang'ta?
Au ile ya kuuma meno wewe mwenyewe ktk kujikaza huku ukiugulia uchungu kimoyomoyo ?
Unatafuna meno yako mwenyewe
 
ila hapana, ukitazama kwenye TV aisee inaelekea ni chungu sana,mie sijui kama nitaweza
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom