Wanawake tujikumbushie vituko vya leba

Wanawake tujikumbushie vituko vya leba

Nawaheshimu sana wanawake maana najua ni yepi mnapitia
Mna moyo na uvumilivu wa hali ya juu kiukweli wanaume tusingeweza.
Asikuambie mtu kitu uchungu ni maumivu yasiyo kipimo lkn kwa kuwa binadamu tunasahau lkn kuna baadhi ya wamama ni wakatili sana kwa watoto wao nadhani hawa hawakuupata ule uchungu wenyewe wa kilo 200 walijifungua watt wakiwa hawajakomaa ndy maana lkn kama mtt alimpa shida atampenda kaama jicho vile.
I salute you women's.
Giving birth is a sacrifice of women to her baby.
Kwann wanaume wasingeweza
 
Wanawake manjiji over-rate sana. Raiti na wewe ungejua maumivu ninayopitia kuapata hela ya kukuhonga ukanunue wigi na lipstick...ungepewa kiti hicho ungekikataaaa.
Naweza nikikatae kweli ninavyopenda kupewa hela hivi halafu mie ndo niwe natoa mimi uwiii
 
Poleni sana mama zetu , nawaheshimu sana, ndio maana huwa nikimkwaza mama au mama akinikosea mimi ndio huwa nawahi kumuomba msamaha.

(1)Nakumbuka mwaka 1996 kabini kwa wakimbizi nchi fulani hapa jirani, nikiwa mfanyakazi wa kada inayofanana na Afya dawa.. niko njiani nakwenda zangu field , ghafla namuona mama anahangaika sana ananiita kwa jian... H... ntabale , ndafuye!! means H.. nisaidie nakufa , niifika hapo na kuanza kumusaidia japo mimi sio mkunga , huku nikiita akina mama waliokua wanapita njiani , tulifanikiwa kumzalisha huyu mama na nilipokea mtoto kwa mara ya kwanza ...mama alinishukuru sana hakujali kabisa kama niliona visivyoonwa....

( 2) Kesi ya pili ni wakati tunafanya repatriation ya wakimbizi tena kesi mfano wa hii ulinitokea tena kipindi hiki huyu mama alikua mbioni akikimbia mamlaka lakini uchungu ulipomzidia hakujali tena na hakuogopa kupigwa na mamlaka alikaa chini nikawahi kumsalidia na akina mama waliokua nao wanapita mbiombio kunusuru maisha yao ... lakini walikubali kumsadia huyu mama ..mimi nikiwa mmoja wao kwa curtain ya vitenge vilivyozunguushwa tu tu kwa kushikana mikono. Allah awajaalie mama zetu
 
Unaweza usiamke kabisa ukawa wa kitandani. Mungu aliumba miili yetu kwajinsi ya ajabu kila kitu kina function accordingly. Sasa ukianza tena kwenda against nature lazima madhara yawepo


Hamna kitu ambacho Hakina effects duniani. Epidural kwa nchi zilizoendelea ni kama panadol tu, kwanini upitie mateso kama option ya kupunguza maumivu ipo? Labda kwa TZ ndio tuogope maana bado ni kitu kipya kwetu. Ni sindano hiyo hiyo inayochomwa wakati wa operation na mbona tunaona kawaida tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom