Wanawake tujikumbushie vituko vya leba

Wanawake tujikumbushie vituko vya leba

wanawake wa siku hizi shida tupu...... hii nini sasa.

nani asiyejua kuwa mnazaa kwa uchungu, hata kwenye biblia imeandikwa, sasa kuja kusimuliana humu ni kujikosea heshima wenyewe, wala haina maana, mnawadhalilisha wanawake wenzenu
 
Habari JF,

Tukiwa tunamalizia malizia week la wanawake duniani hebu wanawake wa JF tiririkeni kituko ulichofanya Leba ulipokuwa na uchungu.

Mimi niliongea maneno yote kichwani, mwisho nikasema namchukia ndugu yangu fulani ambaye kiuhalisia nampendaga sana.

Aisee ile kitu achana nayo uchungu ulipozidi sana niliona bora nife kuliko kuendelea kuumwa namna ile, yani inafika wakati unaona kifo ndo kitu rahisi.

Tiririka sasa
Baada ya kujifungua. Unakitega tena kipokee. Ukija tahamaki watoto 3. Hongera kuwa mama.
Ile hali ya kutuchukia mkiwa wajawazito huwa mnajifanyisha au ni nature?
 
Mama Sabrina Chances are utakuwa mvivu wa mazoezi na kufanya kazi za kutumia nguvu, na unapenda chips.

Nimesimuliwa na kina mama wazoefu na nimechunguza mwenyewe.

Nilipokuwa boarding sekondari moja Mwl moja alikuwa wakati wa kujifungua akienda hosp hayapiti masaa mawili. Lkn alikuwa anapiga kazi balaa na safari moja nakumbuka alishikwa uchungu akiwa shambani anapiga jembe, alirudi ndani ya masaa 2 kabeba mtoto.

Kina mama wengi wa vijijini wanaofanya sana kazi za mikono wanapata matatizo kidogo wkt wa kujifungua ukilinganisha na "mababy" wetu wa mjini.
 
Kwa heshma na taadhima naomba niwape hongera na salute kubwa kabisa kwenu wanawake mnaojielewa.

Leba kunafurahisha na kuudhunisha pia sometimes.
Asanteni sana.

IMG-20171113-WA0000-1.jpg
 
Mim nilivyofika Leba ,nikapelekwa sehemu ya mapumziko walikuwepo wajawazito wengii,sasa uchungu ulikuwa haujanishika kivile nilikuwa natokwa na maji tu ,,daktari akanipima akasema bado,,sasa mle kwenye ukumbi kulikuwa na wamama wengi mwingine anaruka,mwingine anajivuta vuta chini ,si nikaanza kuwacheka nikasema mbona mimi siumwii,,kumbe bana uchungu unakuja taratibu ,nikawa nashangaa kila muda unavyozidi kwenda maumivu yananizidia wale niliokuwa nawacheka wao wanajifungua wananiacha tu,,kukakucha asubuhi niliona ni mwaka na nikasema sirudiii ,kama nilikuwa natembea uchungua ukaja ghafla naganda kama sanamu kama kuna mti ntaung'ang'ania kweli ,ilifikia muda sitaki kuja kusalimiwa wala kuonwa na mtu yeyote maana watu wanavyozidi kuja kuniona ndivyo uchungu unazidi kuwa mkali nikawazuia,,,niliita majina yote ya Mungu nikawa namshika mama yangu namuambia aniombee haraka uchungu upoe kiuno changu kilikuwa cha moto nauchukua mkono wa mama nauweka kiunoni kwangu namwambia aniombee mama yangu mpaka alilia nilivyokuwa nahangaika nyie acheni jamani,,
Usiku ulipofika saa 2 nikasikia kusukuma nikapelekwa chumbani nimefika kule kila nikisukuma hola,,wakaniwekea maji ya uchungu wapiii wakasema huyu anatakiwa kisu tu nikajitahidi kusukuma wakaja madaktari na manesi wamenizunguka mwingine kanishika kichwa ,mwingine tumbo anabinya,mwingine anaangalia njia ya mtoto (sitasahau)mtoto alitoka saa 8 nanusu kuamkia tarehe 8 na mwaka ....8 loo kazi niliipata

Sasa najiuliza wanaozaa watoto 7 au 8 wanawezaje?maana mim toka nizae sina hamu tena halaf sijawah pata maumivu kama yale toka nizaliwe sema na ukweli
Mama Aheshimiwe ,maana wanaume wangepewa huu uchungu hata dakika wangeukataa na wangetuheshimu sana
 
Sidhani kama kuna kitu kigeni chochote duniani, uchungu na leba ni mambo ya kawaida kabisa uliza wanaosomea udaktari, kwa dunia ya leo iliyoendelea watu watakushangaa kusema jambo kama hilo, ukiingia YouTube kunazo hadi video ya kuzaa.... Sasa sielewi unazungumzia siri katika muktaza gani
wazaramo utawaweza mkuu wao kila kitu mpaka kipite unyagoni hata mm sijaona cha kuficha japo sijazaa ila natamani
 
Chances are utakuwa mvivu wa mazoezi na kufanya kazi za kutumia nguvu, na unapenda chips.
Nimesimuliwa na kina mama wazoefu na nimechunguza mwenyewe.
Nilipokuwa boarding sekondari moja Mwl moja alikuwa wakati wa kujifungua akienda hosp hayapiti masaa mawili. Lkn alikuwa anapiga kazi balaa na safari moja nakumbuka alishikwa uchungu akiwa shambani anapiga jembe, alirudi ndani ya masaa 2 kabeba mtoto.
Kina mama wengi wa vijijini wanaofanya sana kazi za mikono wanapata matatizo kidogo wkt wa kujifungua ukilinganisha na "mababy" wetu wa mjini.
Nilijifunza ujauzito wa pili wala haikuchukua two hours nilikua nimeshajifungua nilipiga zoezi mwanzo mwisho na uchungu unakua wa haraka. Ila kuna complications zingine ziko nje ya uwezo wa mama
 
Mi niliwekewa kidonge cha uchungu siku moja kabla ya due date. Nikawaaga rafiki zangu wale wa karibu kuwa naenda labor. Basi kila mara namuuliza nurse saa ngapi dawa itareact maana nilikua nishachoka nataka tu nimuone mtoto.
Niliwekewa saa saba mchana. Nikala mchana kama kawaida yangu nikawa busy nachat mwenyewe kwenye groups. Mama angu alikuwepo akakaa mpaka saa moja na nusu akasema ngoja arudi nyumbani akaniandalie chakula cha kesho asubuhi kama itakua sijajifungua.
Mama alivyotoka tu kule wodini nikaanza kusikia kama tumbo la period. Nakumbuka nilikua nimevaa wig nimepaka na lipstick mwenyewe. Mara nikawa sielewi elewi. Akaja nurse nikamwambia naumwa tumbo halafu kama najisikia kwenda kujisaidia haja kubwa. Akaniambia vua nguo zako jifunge tenge. Ile kujifunga tenge ndo kama nilimzindua huyu mkurya tumboni. Kutoka ward kwenda labor ni kama hatua kumi tu. Kufika nikakuta mama mtu mzima nae anasubiri kujifungua. Sasa nikaanza kutapika. Nikaanza kulia. Nikatupa wig kule maana niliona linanibana. Nilisali baba yetu mara kumi kumi. Nilikua nashikilia kitanda siachii. Nilijuta majuto yote. Nilijuta kwanini sikutoa mimba tu kuliko shida ninazopata. Nilijuta kuumwa mwanamke. Nilifikia hatua naomba Mungu anichukue tu kuliko maumivu ninayopitia.
Manurse walikoma na mimi mpaka wananiuliza mzigua gani muoga hivyo. Nilikua kiuno kikikaza sana nawaita wakija wanasema njia bado. Yule mama niliemkuta leba nikamuuliza mtoto wake wa ngapi yule anasema eti wa nne. Nikawa namuuliza unawezaje kuzaa watoto wote hao na maumivu yote haya. Ikafikia point wakanihamishia kitanda cha kujifungulia sasa. Kitendo cha kutoka kitanda nilicholala mwanzo mpaka kitanda cha kujifungulia niliona ni kama natoka Dar Moro kwa miguu japo ilikua ni kitanda cha tatu toka nilipokua. Nikaishiwa nguvu. Nikawekewa dripu. Sasa mkono niliokua nautumia kujisugua kiuno ukawa umewekwa dripu. Nikaambiwa nikae pozi moja tu. Pale ndo nikazidisha sala za Mungu kunichukua duniani.
Hapo nishajaribu kupush kama mara nne hamna kitu. Nurses wakatoka nje wakaniambia nikijisikia haja nijisaidie tu. Sijui nilijuaje muda umefika ila niliita kwa sauti manesi kuja wakasema sasa tayari anza kupush. Hapo nimeshakata tamaa ya kuishi mmoja akawa amekaa anasubiri mtoto atoke mwingine akawa anamsukuma tumboni anamleta chini.
Mungu wa ajabu sana the moment mtoto ametoka maumivu yote yalikata. Hata wakati wa kushonwa nyuzi wala sikuogopa sana na uoga wangu wote. Huyu mtoto mzuri nilie nae hapa nikimuangalia naona yale maumivu ya leba ni sawa tu kama nilipitia kumpata malaika mzuri hivi. Wanaume wangejua tunachokipitia leba wangetuheshimu sana.
 
Wamama nawaheshimu sana. Nakumbuka mke wangu alitaabika siku nzima akaja kujifungua siku ya pili yake tena kipindi hicho mimi nipo masomoni. Kipindi anahangaika mimi nikawa napiga simu kujua anaendeleaje yaani alikuwa mkali sijawahi kuona nilikuwa nachimbwa biti si la nchi hii.
hahaha pole chief
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom