huu uzi umenikuna sana, ngoja nitoe my personal story labda naweza inspire vijana wa mujini
Nilipomaliza university nilibahatika kupata deal moja ambayo ilikuwa inanipa pesa nzuri sana, it was way beyong my expectations. i was just 24 yrs old. Sasa bwana nilichanganyikiwaje? yaani nilikuwa nagawa pesa kama njugu, mara nimewanunulia wazazi gari, wadogo zangu ndio usiseme walizifaidi sana pesa zangu, macousin wakija home lazima waondoke na wekundu wa kutosha, nikitoka out na marafiki mi ndio wa kulipa bill na viingilio lol. yaani ili mradi roho yangu ilikuwa nzuri kupita maelezo.
basi kumbe baba yangu mda wote huo ananichora tu. siku moja akaniita akaniambia anashida na kama 5m anaomba nimpatie. mi nikamshangaa maana haikuwa kawaida yake kuomba lakini haikuwa tabu kwangu nikampatia. Mda wote huu pia nilikuwa na ndoto ya kununua nyumba Masaki lol! Basi dingi kila akiniambia kununua kiwanja mi namjibu kuwa nazichanga za kununua nyumba masaki.
ikapita kama miaka 2 ivi, akili ikaanza kunijia huenda sitoweza nunua masaki, maana ilikuwa kila nikiuliza natajiwa malaki ya dollars lol. Basi nikamuomba baba anisaidie kutafuta kiwanja, akasema sawa. siku chache baadae akaniambia haya twende nikakuonyeshe, tukafika mahali akaniambia unakumbuka ile 5m niliyokuomba? ndio...basi nilinunua viwanja 2 na chenji iliyobaki nikanunua trips za kokoto na mawe. yaani sikuamini jamani. yaani zile kokoto na mawe nilijenga na zikabaki, mpaka leo nikiziangalia natoka machozi, maana baba alifariki miezi michache baada ya kunionyesha viwanja. thamani ya viwanja ivyo sasa ivi kama nikiamua kuuza si chini ya 80m kwa kimoja, imagine ukilinganisha na bei nilionunulia. na iyo ni baada ya miaka less than 10
yale mawe nimeamua kuyaacha hapo kama ukumbusho, na pia watoto wangu wakikua ntawambia hii adithi ili nao wawe inspired. nimejifunza kuna baadhi ya investiments ukifanya you can never go wrong, no matter what.