SOCIOLOGISTTZ
JF-Expert Member
- Jun 16, 2013
- 2,615
- 929
Alikula bata ujanani huyo sasa uzeeni ndiyo hivyo
jamani ila wamama wameteseka eti ila sameheni blackwomaninakera sana sana best,hivi mtu unaachaje damu yako kabisaaa? yaani huitambui, tungekuwa hohehahe leo hii angetuomba tuonane?
jamani ila wamama wameteseka eti ila sameheni blackwoman
wewe samehe tu !huwa naumia sana nikikumbuka mama alivyokuwa anateseka, yaani aliteseka sana na sisi,kuna wakati unaona mama ameshindwa kufanya maarifa ya ada lakini yupo radhi akakope anapopajua, kurudisha sasa? mama anakuja kudaiwa mbele yetu hatuna la kufanya, wacha kabisa, inahitaji moyo kumsamehe yule mzee aisee, lakini tunashukuru ndio alitupa usongo huu wa maisha tulionao sasa hivi.
.......enough! Imetosha sasa kuwatolea mifano marehemu,
Angalau wao wanauhakika wa malazi ya milele huko walikozikwa.
Baina ya sisi kwa sisi humu ndani, nani ana jeuri ya kusimama ahesabiwe kwamba angalau ana kibanda chake cha vyumba viwili na ana angalau hati ya makazi?
Tupeane mbinu za kujikomboa badala kuwasimanga marehemu.
Tuanze kujiuliza kuna ugumu gani kujijengea nyumba?
Utasikia majibu ya ajabu ajabu humu...mfano;
1. Kiwanja kipo mbali
2. Nasubiria fungu kubwa la pesa
3. Sijapata mtu wa kunipa msukumo...
Yale yaleee...na haijalishi wewe ni mwanamke au mwanaume, wote mjenge bana!
Jamani, tunawasema wazee wetu lakini na sisi vijana wa sasa hebu tujiangalie upya life styles zetu jinsi zilivyo. Wangapi wanawekeza kwenye nyumba na ardhi?
Wengi sana utakuta akianza kazi na kuwa na kipato;
i) Anakopa benki ili anunue gari na fenicha.
ii) Nyumba ya kupanga ya mpaka shs laki 6 kwa mwezi
iii) Simu, mavazi, vipodozi, saa na accessories zingine ndio usiseme
iv) Kusiwe na uzinduzi sijui wa Diamond au Twanga lazima ahudhurie...Asipohudhuria anaoneka yeye si wa mjini
v) Parties na viwanja ndio usiseme......!!
Hayo yote ni symbol ya kwamba ''mambo yako yako safi hapa mjini''.....Lakizi yote hayo ni matumizi makubwa na yanayozidi kipato chako. We have start living within our own means!
Baada ya kusoma posts nyingi, nimegundua kumbe pamoja na kupiga kwangu ulabu kwa wingi, mimi ni bonge la baba wa kutiliwa mfano.
Shukran ziwaendee wanywaji wenzangu ambao michongo mingi ya maisha nimeipata kwao tukiwa kaunta ya juu.
Kwa vijana wa kiume, hebu fanyeni mchakato wa kuoneana wivu wa kimaendeleo.
Tuache kusema ya wazee wetu waliokosea, tuingie msituni tuwanyime watoto wetu cha kutusema hapo baadae.
Tutoe kwanza boriti kwenye macho yetu ili tuweze kuona kibanzi kwenye macho ya wazee wetu.
Hakuna kinachoshindikana tukidhamiria kwa dhati.
Kwa ushauri na michongo ya maisha, odm napatikana kaunta ya juu, fesibuku pub, Boko Basihaya. Dsm Tanzania.
Baada ya kusoma posts nyingi, nimegundua kumbe pamoja na kupiga kwangu ulabu kwa wingi, mimi ni bonge la baba wa kutiliwa mfano.
Shukran ziwaendee wanywaji wenzangu ambao michongo mingi ya maisha nimeipata kwao tukiwa kaunta ya juu.
Kwa vijana wa kiume, hebu fanyeni mchakato wa kuoneana wivu wa kimaendeleo.
Tuache kusema ya wazee wetu waliokosea, tuingie msituni tuwanyime watoto wetu cha kutusema hapo baadae.
Tutoe kwanza boriti kwenye macho yetu ili tuweze kuona kibanzi kwenye macho ya wazee wetu.
Hakuna kinachoshindikana tukidhamiria kwa dhati.
Kwa ushauri na michongo ya maisha, odm napatikana kaunta ya juu, fesibuku pub, Boko Basihaya. Dsm Tanzania.
Mkuu Masaki mtu anayefanya yote hayo bila kufikiria future yake na bila kuwa na kipato cha kutosha hana akili timamu kabisaaaaaa......
Ila kama mtu anaweza kuafford...why not? Ili mradi haji kesho kukukopa, haina tatizo...kuna watu wana mavipato ya kufa mtu..let them live their lives
Na mwisho, kila mtu ana his "own means" ...kwamba hiyo ni relative sana tu...kama alivyosemaga mzee wa vijisent, "kila mtu na viwango vyake"
hommie Asprin, tatizo wakikuona Basi haya fesibuku pale wanapata impression kwamba 'unakunywa hela ya matofali' lol
Nyamayao samehe tu mzee alikuwa hajui atendalo, ukipata msaidie ivo ivohuwa naumia sana nikikumbuka mama alivyokuwa anateseka, yaani aliteseka sana na sisi,kuna wakati unaona mama ameshindwa kufanya maarifa ya ada lakini yupo radhi akakope anapopajua, kurudisha sasa? mama anakuja kudaiwa mbele yetu hatuna la kufanya, wacha kabisa, inahitaji moyo kumsamehe yule mzee aisee, lakini tunashukuru ndio alitupa usongo huu wa maisha tulionao sasa hivi.
Hahahah kama wife ndo ananipigia hesabu kabisa. Bia moja ni tofali mbili haya baba niambie leo umekula tofali ngapi? lol
Anasahau wakati unakula tofali kazaa Masaki anakupa mchongo wa mashamba ya bei rahisi Kerege.
Asprin hapo kwenye bluu tuko pamoja sana!
Na huo mchongo usingeweza kuupata kama ungekaa na mkeo nyumbani mkisaidiana kupika si ndio? Nchi hii jamaa alishasema "kula uliwe" lol
Halafu usisahau na vile viburudisho vyetu kwa pembeni..hapa gines...hapa kiburudisho...hapa mchongo..maisha yanasonga...
Kaizer, hapa nazungumzia wale ambao wanaishi above their means. Kama starehe ziko ndani ya uwezo na kipato cha mtu, then fine. Ila angalizo langu lilikuwa ni kwamba hapa vijana tunawasema wazee hawana hata kibanda, walikataa viwanja Upanga, Mikocheni na Tangi Bovu kwa kusema kwamba ni porini. Leo hii kuna vijana ukiwaambia kuna viwanja Tuangoma vinauzwa anasema ''huko mbali'' au ''mimi mjanja hivi niwe na kiwanje Temeke?''! Yaani ni mvinyo wa zamani kwenye chupa mpya!
Tujifunze kutokana na makosa haya ya wazee wetu!
Na vile viburudisho vingine vilivyomo kwenye katiba yetu usisahau homy.
Mkuu watu wana underestimate nguvu ya bia kwenye kuleta maendeleo, hasa pale inaponywewa baa.
Michongo mingi ya maisha nimeipata mbele ya Guines na Grants, kongoro likiwa shahidi