Wanaume na 'kuchezea maisha'.....

Wanaume na 'kuchezea maisha'.....

The boss kaongea point leo..sijui wanaume wanasapoti kwa kumaanisha au basi tu.sababu ukiangalia,most men wako hivo.hasa hapa mjini dar,panachanganya sana watu.maisha ya kuigana na kuendekeza marafiki wasio na maendeleo..
Unakuta mtu analipwa mshahara wa kawaida tu ila mwanaume anaenda kukata kucha saluni na kusuguliwa miguu,kweli??ilimradi aonekane nae wamo kitaa.hana kiwanja wala maendeleo ya msingi,gari kakopa benki na kutwa wanawake.
Hivi mwanaume kuwa mhuni ni lazima eeh?its like imekuwa desturi mwanaume lazima apitie kipindi cha kuhangaika hovyo na women.wanaita 'phase ya ujana' wasijue hiyo ndo inadetermine uzee.ndomana maryoo wamezidi.janaume lipo lipo tu,akimuona kwenye gari utasema wa maana kumbe mkewe ndo anamuweka mjini.hana mipango,mshahara haileweki unapoishia.
mtu anaendekeza pombe,akitoka kazini lazima apitie bar.ukiwaona humu jf wanajitetea eti mbona mwanaume unakunywa bia na watoto wanaenda shule.we kila siku unaache elf 10 bar,kwa wiki ni elf 70.bado hujafanya tu kitu cha maana nayo?hapo familia yake haijatoka out karibu mwaka.ukidunduliza hizo elf 10 ukaenda vacation hata hapo ufukweni na familia,bado hujajenga kitu kweli??..
Men get serious...

umesema kweli tupu, na hapo nilikobold... LAITI kila mtu angejua maisha anayoishi leo yanatokana na yale aliyoyafanya hapo awali, na kesho yako inategemea leo umefanya nini.

Vile unavyotaka uwe ni 10 years, inategemea na unavyojiandaa sasa na kuhakikisha itakuwa hivyo. Hebu nikahangaike mie
 
yaani mkwe nishaanza tatizo son wako ananirudisha nyuma.mkwe ukitaka ufanikiwe kuwa na roho mbaya.

....kabisa!!!

Ukitaka kufanikiwa uwe na roho mbaya!

"To be successful you have to be selfish, or else you never achieve. And once you get to your highest level, then you have to be unselfish. Stay reachable. Stay in touch. Don't isolate." Michael Jordan.
 
The Boss, unaongelea topic ambayo naiogopa kuliko zote. Najiuliza kila siku, when is it the right time kufanya hizo investments basi? Manake kila hela ninayopata inapata matumizi yasiyo ya msingi. Kuna kujispoil (wants and not needs, lara 1 keshatuzodoa), holidays na michango ya harusi, ndugu wasiotaka kuwajibika na uwiii!
Hayo majumba najenga lini? Hizi hela nilizonazo ndo ntakuja kuzijutia wakati saa hizi hazinitoshi?
Mbu njoo rafiki

Aisee siyo siri yani hazitoshi kabisa na hao mafundi ujenzi wa siku hizi kila nyumba anayojenga mnagawana vifaa nusu kwa nusu
 
Last edited by a moderator:
....kabisa!!!

Ukitaka kufanikiwa uwe na roho mbaya!

"To be successful you have to be selfish, or else you never achieve. And once you get to your highest level, then you have to be unselfish. Stay reachable. Stay in touch. Don't isolate." Michael Jordan.

Mkuu moskwito nikuambie kitu? Gurumo angekuwa na mafanikio hapa mjadala kama ungekuwepo mkewe angetajwa kama sehemu ya mafanikio. Hali imekuwa tete hatusikii ikisemwa mkewe ni sehemu ya matatizo.

Tunaonewa sana wanaume
 
Mara ya kwanza niliposikia Mzee Gurumo wa Msondo Ngoma
anadai ameimba zaidi ya miaka 50 na maisha yake bado
ya 'kimaskini mno' niliona kuna kitu hakiko sawa..
sikuwa na ushahidi tu lakini nilikuwa na uhakika kwa vyovyote vile
'atakuwa alichezea maisha ujanani'

Sasa jana walioona akifanyiwa interview na Salama kipindi cha MKASI
watakubaliana na mimi huyu Mzee na wengine wengi tunaosikia
wakihojiwa na vyombo vya habari ..wakilaumu serikali kwa kutowajali.
wengi wao walipata 'golden opportunities' za kuwa na maisha bora
lakini 'walichezea pesa' na 'opportunities hizo' so many times...

mfano Mzee Gurumo jana alisema alilipwa 'elfu ishirini'
mwaka 1978 ili kuhamia bendi ya Sikinde...kumbuka
kuwa Mshahara wa Rias mwinyi mwaka 1992 ulikuwa 'elfu ishirini na saba tu'
sasa pata picha huyu mzee alikuwa na pesa kiasi gani?
na mshahara wake ulikuwa 'shilingi elfu tatu' mwaka hu0 1978..
wakati kima cha chini mpaka mwaka 1987 kilikuwa hakijafika 'shilingi elfu saba'

Kuna Mzee mwingine alitunga kitabu riwaya 'Simu ya Kifo' alilipwa
'elfu kumi na mbili ' miaka hiyo nyumba Kariakoo zinauzwa shilingi 'mia nne'
na alikufa bila nyumba wala kibanda..

Orodha ni ndefu...na wapo wengine Baba zetu,Wajomba,babu na kadhalika
ukiwaona uzeeni wanavyolalamika na kuomba wasaidiwe....utasema hawakupata chochote ujanani
kumbe anasa,starehe na kuhonga wanawake ndo sababu....

ukweli ni kwamba watu 'huchezea maisha mno' halafu uzeeni hutafuta wa kumpa lawama
mara watoto,mara serikali na kadhalika....

huyu Mzee Gurumo alikuwa sio mtu wa kupewa gari na Diamond...
angekuwa na magari na majumba tele ya kuwarithisha watoto na wajukuu...
The Boss msimlaumu sana Mzee Gurumo. Kwani ulikuwa hujui kwamba fedha za wanamuziki wa zamani zilikuwa zinaishia kwa waganga wa maruhani...?

Inawezekana starehe zilichangia lakini kwa kiasi kikubwa wanaumuziki wa zamani walikuwa ni washirikina sana, kama huamini muulize mzee Kitime atakupa ukweli wa mambo
 
....kabisa!!!

Ukitaka kufanikiwa uwe na roho mbaya!

"To be successful you have to be selfish, or else you never achieve. And once you get to your highest level, then you have to be unselfish. Stay reachable. Stay in touch. Don't isolate." Michael Jordan.
si ajabu mzee wa watu hakuwa mbinafsi, ona sasa uzee umemfika huku hali mbaya. mi mwenyewe nataka nijifunze uselfish nisjie nikaji'gurumo' bureee.
 
ana watoto wangapi? na katembea na wanawake wangapi? labda aliwekeza huko na huo ni uwekezaji atiii!
The Boss msimlaumu sana Mzee Gurumo. Kwani ulikuwa hujui kwamba fedha za wanamuziki wa zamani zilikuwa zinaishia kwa waganga wa maruhani...?

Inawezekana starehe zilichangia lakini kwa kiasi kikubwa wanaumuziki wa zamani walikuwa ni washirikina sana, kama huamini muulize mzee Kitime atakupa ukweli wa mambo
 
yaani The Boss umetugusa wengi, babangu anaelekea kustaafu lakini hata nyumba hana. halafu sioni kama hili linamuumiza yaani sie tumekuwa wa kuishi kotta wakati mzee ana uwezo wa kujenga lakini anaendekeza starehe hadi uzeeni. sas sijui atamlaumu nani.
we are sealing on the same boat
 
huu uzi umenikuna sana, ngoja nitoe my personal story labda naweza inspire vijana wa mujini

Nilipomaliza university nilibahatika kupata deal moja ambayo ilikuwa inanipa pesa nzuri sana, it was way beyong my expectations. i was just 24 yrs old. Sasa bwana nilichanganyikiwaje? yaani nilikuwa nagawa pesa kama njugu, mara nimewanunulia wazazi gari, wadogo zangu ndio usiseme walizifaidi sana pesa zangu, macousin wakija home lazima waondoke na wekundu wa kutosha, nikitoka out na marafiki mi ndio wa kulipa bill na viingilio lol. yaani ili mradi roho yangu ilikuwa nzuri kupita maelezo.

basi kumbe baba yangu mda wote huo ananichora tu. siku moja akaniita akaniambia anashida na kama 5m anaomba nimpatie. mi nikamshangaa maana haikuwa kawaida yake kuomba lakini haikuwa tabu kwangu nikampatia. Mda wote huu pia nilikuwa na ndoto ya kununua nyumba Masaki lol! Basi dingi kila akiniambia kununua kiwanja mi namjibu kuwa nazichanga za kununua nyumba masaki.

ikapita kama miaka 2 ivi, akili ikaanza kunijia huenda sitoweza nunua masaki, maana ilikuwa kila nikiuliza natajiwa malaki ya dollars lol. Basi nikamuomba baba anisaidie kutafuta kiwanja, akasema sawa. siku chache baadae akaniambia haya twende nikakuonyeshe, tukafika mahali akaniambia unakumbuka ile 5m niliyokuomba? ndio...basi nilinunua viwanja 2 na chenji iliyobaki nikanunua trips za kokoto na mawe. yaani sikuamini jamani. yaani zile kokoto na mawe nilijenga na zikabaki, mpaka leo nikiziangalia natoka machozi, maana baba alifariki miezi michache baada ya kunionyesha viwanja. thamani ya viwanja ivyo sasa ivi kama nikiamua kuuza si chini ya 80m kwa kimoja, imagine ukilinganisha na bei nilionunulia. na iyo ni baada ya miaka less than 10

yale mawe nimeamua kuyaacha hapo kama ukumbusho, na pia watoto wangu wakikua ntawambia hii adithi ili nao wawe inspired. nimejifunza kuna baadhi ya investiments ukifanya you can never go wrong, no matter what.
 
duh aisee mshukuru sana baba yako! kila siku ubusu hata hilo kaburi lake!
aisee huu uzi hadi naona aibu hapa yaani namuomba tu mungu mwaka kesho niwe hata na room moja aisee! ukiona wanawake tunavochezea hela miaka hii? kila siku nguo mpya? kuoshwa miguu saluni ..kuogeshwa yaani kila wiki kuna mtu saluni na mashoping laki tano inaisha
bado michango ya kitchen party na sare zake na masendoff! hapo bado ndugu si unajua tulivo na huruma?
eeh MUNGU tusaidie!
 
Kumbe na wewe unaishi kota kwa wazazi wako kama DEMBA

Nlikuwa sijui ngoja nicheki na Kaizer
sisi hatujawahi ishi kota na mimi siishi kwa wazazi Asprin nitake radhi .ila baba yetu alilipwa mafao meengi baada yakustafu hatujui hela alihonga wapi na alianza kazi akiwa na 17 yrs serikalini hahahahaahahah
 
Last edited by a moderator:
duh aisee mshukuru sana baba yako! kila siku ubusu hata hilo kaburi lake!
aisee huu uzi hadi naona aibu hapa yaani namuomba tu mungu mwaka kesho niwe hata na room moja aisee! ukiona wanawake tunavochezea hela miaka hii? kila siku nguo mpya? kuoshwa miguu saluni ..kuogeshwa yaani kila wiki kuna mtu saluni na mashoping laki tano inaisha
bado michango ya kitchen party na sare zake na masendoff! hapo bado ndugu si unajua tulivo na huruma?
eeh MUNGU tusaidie!

we acha tu. na kwa mfano leo hii ukimwambia kijana twende tukanunue mashamba mkuranga anakuona we humtakii mazuri maana ataishije nje ya jiji..... lakini nakuhakikishia after 5 years ardhi uliyonunua kwa acre 400,000 utauza maradufu ya hapo yaani ardhi ni mtaji tosha. na ukiangalia 400,000 kwa mwanamke ni gharama ya salon kwa mwezi tu. Wamama acheni utumwa jamani
 
utumwa usio na maana ndugu yangu! hapo hujaweka simu ya millioni na pochi ya laki 3 na viatu vya dollar kadhaa eti designer! uuuwiiiiiiii! na hapo mtu kapangisha kaapartment ka laki nne kwa mwezi! baada ya miaka 10 umepauka hata miluzi hupigiwi tena hata na konda wa daladala hakusalimii ndo utajua mjini kuna wenyewe! wallah leo nabadilika
yasije nikuta ya gurumo mie
 
Back
Top Bottom