The boss kaongea point leo..sijui wanaume wanasapoti kwa kumaanisha au basi tu.sababu ukiangalia,most men wako hivo.hasa hapa mjini dar,panachanganya sana watu.maisha ya kuigana na kuendekeza marafiki wasio na maendeleo..
Unakuta mtu analipwa mshahara wa kawaida tu ila mwanaume anaenda kukata kucha saluni na kusuguliwa miguu,kweli??ilimradi aonekane nae wamo kitaa.hana kiwanja wala maendeleo ya msingi,gari kakopa benki na kutwa wanawake.
Hivi mwanaume kuwa mhuni ni lazima eeh?its like imekuwa desturi mwanaume lazima apitie kipindi cha kuhangaika hovyo na women.wanaita 'phase ya ujana' wasijue hiyo ndo inadetermine uzee.ndomana maryoo wamezidi.janaume lipo lipo tu,akimuona kwenye gari utasema wa maana kumbe mkewe ndo anamuweka mjini.hana mipango,mshahara haileweki unapoishia.
mtu anaendekeza pombe,akitoka kazini lazima apitie bar.ukiwaona humu jf wanajitetea eti mbona mwanaume unakunywa bia na watoto wanaenda shule.we kila siku unaache elf 10 bar,kwa wiki ni elf 70.bado hujafanya tu kitu cha maana nayo?hapo familia yake haijatoka out karibu mwaka.ukidunduliza hizo elf 10 ukaenda vacation hata hapo ufukweni na familia,bado hujajenga kitu kweli??..
Men get serious...