Wanaume na 'kuchezea maisha'.....

Wanaume na 'kuchezea maisha'.....

Subiri nipate hela ya mafao
Babuuuuu.....Najaribu kukuona utakavyokuwa ukiponda raha na Heaven on earth hapa.
download.jpg
 
Last edited by a moderator:
kweli dear i promise from today nachange ! yaani nipe mwaka namiliki ka mjengo .. bora hata nioe kwenye kamjengo kangu akinipasua kichwa natimua! mambo ya kuumbuka hapa mjini hata konda hakupigii mluzi siwezi

aisee naomba ulitilie maanani kabisa kabisa, maisha gani hayo unaishi? hata kama hutokuja kuishi kwenye hiyo nyumba lakini unayo na utajua utafanyia nini, upangishe ufanyaje ni yako aise,au sisi tuliokuzwa kwa hasira za mzazi mmoja kututelekeza na mmoja kuhangaika na sisi mpaka unatamani ukatize masomo kwamba unamuumiza sana ndio tuna usongo sana na haya maisha? mie huo mkopo wangu wa kwanza nilienda kukarabati nyumba ya mama nyamayao, nyingine nikawekeza ninavyoweza, naweza kukwambia sikuunywea hata fanta, niliamini hizo fanta zipo tu na ntakuja kuzinywa nitakavyo, sasa hivi sizungumzii fanta nazungumzia ballantin, wewe wewe! au ndio za kimjini mjini "kujenga kitu gani" asikwambie mtu hakuna anaetamani maisha yake yote yaishie kwenye vinyumba vya kupanga, na ufanye sasa hivi mana ukishaingia kwenye kuanzisha familia mambo ni mengi sana, jipange kwa sasa kwa popote utakapofikia sawa tu ili mradi usichana haujapita kwa vipodozi na malecwig.
 
afadhali nyie angalau you have a place to call it home
DEMBA wazazi wetu wamefanya makosa mengi sana
Na wengi tu ambao hadi leo hatuna mahali pa kupaita nyumbani
Kuna wengine nyumbani ni kwa babu yao
Sasa unaweza kujiuliza iweje babu awe na kwake halafu baba ashindwe?

Kuna mabo mengi sana
Lakini baba na mama ni msingi mkubwa sana wa kuimarisha familia
Wakiparaganyika mazazi aliebaki na watoto ni kazi kubwa kuiimarisha hiyo familia
Wakati mwingine watoto wanakuja kuwa na maisha mabovu na ukiangalia kwa makini chanzo ni wazazi

Kuna rafiki yangu mmoja aliniambia mwaka 2001 kuwa wakati huo alinunua tv na alikuwa na umri wa miaka 24
Katika familia yao ya watoto 7,kwenye familia yao hawakuwahi kuwa na godoro la sponji,yeye ndio alikuwa wa kwanza kulinunua

Unaweza tu kuifikiria hiyo familia ilikuwa inaishi maisha gani wakati baba yao alikuwa ni mfanyakazi serikalini kwa muda mrefu sana!

Inauma sana!
 
Last edited by a moderator:
boss uko sahihi, huenda maisha ya siasa ya kijamaa ilichangia kuathiri fikira za wazee kama hawa mchukulie marehemu Mzee Timoth Apiyo. kisha linganisha na nafasi aliyokuwa nayo serikalini. aidha pia muziki wa kipindi kile ulikuwa wa burdani ya kutegemea kiingilio (gate collection). ama pia nashindwa kumuelewa huyu mzee GuRUMO kauli zake hazifanani na hadhi aliyonayo ktk anga za muziki nina wasiwasi na upeo wake pia.
Mara ya kwanza niliposikia Mzee Gurumo wa Msondo Ngoma anadai ameimba zaidi ya miaka 50 na maisha yake bado ya 'kimaskini mno' niliona kuna kitu hakiko sawa... sikuwa na ushahidi tu lakini nilikuwa na uhakika kwa vyovyote vile 'atakuwa alichezea maisha ujanani'

Sasa jana walioona akifanyiwa interview na Salama kipindi cha MKASI watakubaliana na mimi huyu Mzee na wengine wengi tunaosikia
wakihojiwa na vyombo vya habari ..wakilaumu serikali kwa kutowajali. Wengi wao walipata 'golden opportunities' za kuwa na maisha bora lakini 'walichezea pesa' na 'opportunities hizo' so many times...

Mfano: Mzee Gurumo jana alisema alilipwa 'elfu ishirini' mwaka 1978 ili kuhamia bendi ya Sikinde...kumbuka kuwa Mshahara wa Rias mwinyi mwaka 1992 ulikuwa 'elfu ishirini na saba tu' sasa pata picha huyu mzee alikuwa na pesa kiasi gani? Na mshahara wake ulikuwa 'shilingi elfu tatu' mwaka hu0 1978... wakati kima cha chini mpaka mwaka 1987 kilikuwa hakijafika 'shilingi elfu saba'

Kuna Mzee mwingine alitunga kitabu riwaya 'Simu ya Kifo' alilipwa 'elfu kumi na mbili ' miaka hiyo nyumba Kariakoo zinauzwa shilingi 'mia nne' na alikufa bila nyumba wala kibanda..

Orodha ni ndefu...na wapo wengine Baba zetu, Wajomba, babu na kadhalika ukiwaona uzeeni wanavyolalamika na kuomba wasaidiwe.... utasema hawakupata chochote ujanani kumbe anasa, starehe na kuhonga wanawake ndo sababu....

Ukweli ni kwamba watu 'huchezea maisha mno' halafu uzeeni hutafuta wa kumpa lawama mara watoto, mara serikali na kadhalika....

Huyu Mzee Gurumo alikuwa sio mtu wa kupewa gari na Diamond... angekuwa na magari na majumba tele ya kuwarithisha watoto na wajukuu...
 
NN asante
na hii dhana pia inaumiza wengi mno
mtu hawezi ku afford gari
anajilazimisha kununua hata kwa mkopo,mwisho
hela ya mshahara yoote inaishia kwenye mafuta
ndo mwisho anashindwa fanya ya maana,sababu gari linam cost mno..

yaani hiyo kitu ipo sana,nina marafiki/ndugu/colleagues nawaona, unakuta mtu slip inasoma elfu 80, ana mikopo ya kutosha ukiangalia/uliza kafanya nini hakuna gari wanapaki kwenye nyumba za kupanga/ccm, halafu ndio wasumbufu wakubwa wa kutugongea 10-10 huku maofisini, yaani mie sijui bwana watu wanaishi maisha gani, jamani ishini kwa uwezo wenu, mjikune pale mkono unapofikia usilazimishe ufikie magotini kumbe unaishilia kiunoni.
 
Huu mjadala unanikumbusha mjadala wa kuwa na nyumba au gari kianze kipi...baadhi hapa naona tumeshaanza au bado tunawaza kuwa na gari na huna nyumba tayari unaelekea kuwa kama Gurumo....Gurumo ana nyumba analia umaskini na anadhani kiwa anahitaji gari

It goes down kwa mtu mwenyewe na priorities zake...sikubaliani naye pia.anavyoilaumu serikali...kama alivosema The Boss ni kwamba alikuwa na fursa nyingi hakuzitumia..au labda ndo alijenga na ndio alikoishia hapo....ila kwa mwanamuziki wa calibre yake angeweza kwenda mbali zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Huu mjadala unanikumbusha mjadala wa kuwa na nyumba au gari kianze kipi...baadhi hapa naona tumeshaanza au bado tunawaza kuwa na gari na huna nyumba tayari unaelekea kuwa kama Gurumo....Gurumo ana nyumba analia umaskini na anadhani kiwa anahitaji gari

It goes down kwa mtu mwenyewe na priorities zake...sikubaliani naye pia.anavyoilaumu serikali...kama alivosema The Boss ni kwamba alikuwa na fursa nyingi hakuzitumia..au labda ndo alijenga na ndio alikoishia hapo....ila kwa mwanamuziki wa calibre yake angeweza kwenda mbali zaidi.

unadhani huyu mzee hata hiyo gari aliyopewa na diamond kwasasa ataifaidi/fanyia nini? ya kumpeleka kwenye matibabu ama?
 
Huwezi kufaidi kila kitu,
Mzee Gurumo wa Msondo Ngoma alifaidi totoz, maisha ya starehe na anasa;
Mwisho amekosa mali, sijui hata kama nyumba anayo na kama ipo ni kibanda tu.
........Wanasema ..........mwache aponde mali ...........
Dokta Remmy wakati wa uhai wake aliwahi kuhojiwa na Channel Ten, alisema "usione kiuno changu kimepooza, kimepooza na mengi. Enzi zetu tulikuwa tunakula papuchi bila uoga wa ugonjwa wa AIDS. Tulikuwa na STDS tu ambazo ukimeza rangi tatu kwisha".

Alisema akiwapanga mademu aliowatafuna wanaweza kujaza hata lori.
 
hii kwa kweli inaumiza kichwa sana wazee wetu wakiona vijana wanakimbizana kujipanga kimaisha, lakini hii sio kwa vijana wote wengeine wamekalia starehe mtindo mmoja.

Ila kuna wengine ambao wanajisahau kwa kukalia kusema maisha magumu mshahara sijui mdogo, hawataki kujinyima kutafuata walau kibanda!

Kwangu naamini pale unapoanza ajira ndio unapotakiwa kujipanga kwa maisha yako ya kustaafu baadae, na sio kusubiri kiinua mgongo sijui pension...
 
Kwanza hata hiyo miguu ya kukanyagia mafuta na breki anayo?


kuna mambo ya ajabu kweli, haya alikuwa na nyumba, gari kaipata sasa, kifuatacho? huyu mzee sasa hivi alitakiwa ametulia nyumbani kwake akijiuguza taratibu bila malalamishi kibao ya kulaumu hivi na vile, angekuwa na vijimradi vya kumuingizia senti angekuwa analalamikia wengine kwa sasa?
 
unadhani huyu mzee hata hiyo gari aliyopewa na diamond kwasasa ataifaidi/fanyia nini? ya kumpeleka kwenye matibabu ama?

Kwanza aajiri dereva, pili anunue wese + foleni za dar, tatu kuna service na maintanance costs nyinginezo kama ulinzi, hujaweka Insurance, Road license nk, nk, nk.....from there tuje kwenye faida sasa.
 
mada imenikumbusha mbali sana
mtu anafuja mali zake atakavyo kwenye uzee anataka afanyiwe kila kitu utafikiri wakati anazo alikutambua
kusomesha kwa taabu hata chakula na malazi ilikuwa taabu sio kwamba hana anaona wapo wa muhimu kuwahudumia anapostaafu anarudi kwa mwanzo na kuamrisha apewe hela za kwenda bar/anasa kutengeneza jina kama livyokuwa mwanzo...inabidi kusaidia kwa vile ni mzazi wako lakini inakera sana
na hii ipo kwa baadhi ya vijana wengi kuishi kwa kuiga kuendekeza starehe mfukoni hana kitu anaishi kwa kukopa mwisho wa siku kilio serikali inawasahau vijana
 
Kwanza aajiri dereva, pili anunue wese + foleni za dar, tatu kuna service na maintanance costs nyinginezo kama ulinzi, hujaweka Insurance, Road license nk, nk, nk.....from there tuje kwenye faida sasa.

kuwa na gari starehe lakini gharama.....sasa kama maisha yake ndio hivyo atawezaje kulihudumia na gari lenyewe haliingizi kipato chochote usishangae baada ya muda linageuka nyumba ya panya
 
unadhani huyu mzee hata hiyo gari aliyopewa na diamond kwasasa ataifaidi/fanyia nini? ya kumpeleka kwenye matibabu ama?

Ndio maana nimesema "anadhani kuwa anahitaji gari"....kwa hali ilivyo yuko desparate tayari......na sio vibaya kama itamsaidia kumpeleka kwenye matibabu in a more comfortable way kuliko angepanda boda boda au? Fun cargo should be comfortable...sijui anaweza kuendesha? lol
 
Back
Top Bottom