mmh nimeshagombana nae hadi kufikiaGombaneni nae sasa hivi
atawasumbua mno huyo baadae...
atawatolea laana msipompa pesa...hapo baadae
mngeanza kugombana nae sasa
ha haaa, ila tukiwaambiaga sisi ndo tuna-determine future yenu mnakataa, lol!
Umenikumbusha!
Leo tulikuwa na mjadala hapa maeneo ya kazi
Kuna jamaa walikuwa wanadai kuna watu "wamepangiwa" kukosa na wengine kupata,nikawauliza kuhusu walipotoa huo mtazamo wao hawakuwa na majibu ya kuridhisha kabisa wakabaki wananiambia tu eti Mungu ndie anaepanga nani apate nini na kwa kiasi gani
Nilichowaambia mimi ni kuwa watu kama hawa ndio wanafanya watu waendelee kuwa maskini hasa watoto wao wanaowalea,wanawafanya wabweteke bila kujibidiisha kikazi na kifikra
Pia wanataka kumfanya Mungu aonekane ni mwenye upendeleo wa kuwapa wengine nyingi na wengine kidogo jambo ambalo sio kweli
Nijuavyo mimi Mungu hapangi nani apate na nani asipate ila ameweka kanuni ambazo kila atakaezifuata na kuzitii na pia kufanya kazi kwa bidii kwa uangalifu na kutumia akili kwa kiwango chake atapata kwa kiwango hicho,haya mambo ya kukaa na kudanganyana eti Mungu hajanipangia kuwa tajiri ni maneno ya kivivu na ni maneno ya kukemewa kwa nguvu zote
Wazee kama hao uliosema hapo wamevuna kwa kiwango chao kama walichezea watakula kuchezea hoko,Mungu sio boi wako wa kufix mistake zako tena nyingi za kijinga unazozifanya kila uchao
Ukiwa mhongaji utavuna uhongaji!!!!!!!
well said. tujifunze kuwekeza ktk maisha y baadae tho ha2jui cku ye2 ya kufa
Hahaha...
Kuna fursa nyingi mno za kutukomboa kiuchumi huwa tunazipuuzia pengine kwa kutokuwa na uelewa au udumavu wa akili au kutothubutu.
Mathalani Tanzania imejaaliwa ardhi yenye rutuba na yenye kustawisha mazao chungu tele...huu ni mfano mdogo mno wa fursa ambayo sisi Wabongo tunaipuuzia...ni Watanzania wachache mno wenye uelewa au ufahamu wa kilimo chenye tija.
Wanasema eti Mungu hakuwapangia!!
Hata aibu hawaoni
Ifike mahali tuwajibike kwa makosa yetu!
Kwangu mimi hii itakuwa the best thread i have ever read,na si kwasababu inaongelea maisha ya wazee wetu bali kwa jinsi ilivyojaa umakini.
Back to the topic:
Ukiangalia kuna wazee wengi ambao mpaka leo nashindwa kuelewa kwamba nini kilitokea katka maisha yao mpaka mwisho wa siku wanaishia kuadhilika kwa kiasi kibaya,
Kuna wazee wengi ambao nisingependa kutaja majina yao wamekuwa wakiongelewa mara kwa mara kwamba wanahitaji misaada wakati ukiangalia ni watu ambao wamewahi kuwa na majina makubwa hapa nchini na kutambulika hata nje ya mipaka,lakini kwa kukosa umakini wanaishia kudhalilika
Hivi siku moja tukipata rais ambae ataroa tamko kuwa baada ya mwaka mmoja kijana yoyote asie na kazi anatakiwa either amepata cha kufanya au kama hana aondoke mjini na kwenda kwenye mashamba na kujikusanya vijana angalau wa 5 na serikali iatawapa eneo na penbejeo kwaajili ya kilimo na itawapa mahitaji yote muhimu kwaajili ya chakula na kilimo kwa muda wote watakaokuwa mashambani
Halafu ikaweka sheria kali ya kwenda mijini hovyo na ni marufuku kuonekana kijana anazurula hovyo bila kazi na baadhi wakakkamatwa na sheria ikachgukua mkondo wake unadhani kutakuwa na asie na kazi?
Unadhani kutakuwa na njaa?
Thubutuuuuuuuuuuuu!!!!!!!!!!!!
Wazee wa aina hii wapo wengi sana tena wengine walikua bahili hata kusomesha mtoto. Kumbuka kipindi hicho ada ya shule ilikua ndogo sana lkn mtoto ikitokea kafeli walikua hawajisumbui kutafuta njia mbadala ya kumuendeleza mtoto. Inashangaza sana mzee wa miaka 70 kutokua na nyumba , halafu wanalalamikia uongozi wa nyerere wanaudhi sana. Hawakufikiri kuhusu maisha yao ya baadae.hiyo ni kweli mkuu sijui wazee hawa wa zamani hawakuwa na ufahamu? mimi naona walikuwa wanapata vitu vingi bure na nafuu so wakajisahau. Nina mfano hai jana tu hapa ofisini kuna mzee mmoja mfanyakazi mwenzangu wao ndo watu wa kwanza kuajiriwa hapa ofisini hiyo ni miaka ya sabini tunakaa njia moja hivi sasa jana kaniona napita zangu kuja job yeye yupo kituoni mm sikumuona sasa akaja ofisini akasema mtani kama nilikuona wewe ukiwa kwenye gari Fulani hivi ila nikajiuliza mbona gari yako ninayoijua sio hiyo? nikamwambia nilikuwa mimi basi akaanza kulalama yani sisi tulichezea maisha mtu ulikuwa unapewa kila kitu bure mwisho wa siku unachukua mwanamke jioni unaenda pumzika nae!! yani kuanzia chakula, bia, usafiri wa kurudishwa home vyote ni bure! sasa anajuta na kusema tazama vijana wa siku hizi mambo yenu yalivyo mazuri sisi tumebaki kuwakodolea macho tu! sasa nashindwa kusema mfumo uliokuwepo ni tatizo au ni akili ya mtu binafsi!
Kweli my twin mke aweza kuwa tatizo pia. Umenikumbusha mengi mno nakumbuka mara kadhaa wanawake wamelaumiwa ktk familia nyingi. Hata sasa ukijaribu kuangalia baadhi ya familia kama mama ni weak basi familia hiyo huwa ina shida sina maana wababa wakati wote wanategemea wake zao la hasha kwani kuna wababa strong pia aweza kuwa na mwanamke mwenye matumizi makubwa lkn akambana na kuandaa future vema.But all in all......
maisha ya watu wengi sana yakiharibika huwa tunaonewa sana wamama......
kuna kipindi pia huwa naingiaga huu mkenge, kuwa sisi ndo tunapaswa kushika control ya maisha ya familia zetu.
familia nyingi ambazo mama ana vision ya maendeleo huwa inafika mbali sana..... hata kama huyo mama hana kipato kikubwa.
Kuna watu wengi sana wa karibu nami ambao walikuwa na kipato kikubwa sana lakini wameishia kuwa na maisha mabaya sana sababu wake zao walikuwa hawaangalii sana future ya familia, wao ni kuvaa, kula, kunywa........ ananunua vitu vingine havina hata maana, sababu tu mume ana hela......
lakini pia kuna familia ambazo unaona kabisa hawana uwezo kiviiileeee, lakini mama kila siku anafanya juu chini angalau tu future ya familia iwe nzuri.
Naelewa kabisa kuna wababa ambao hawashauriki, hasa na wake zao. lakini mke ana uwezo wa kujua kabisa kuwa mume anapenda sana kusikiliza ushauri wa nani, anaweza kumtumia huyo mtu.
Kuna familia ambayo tunaichukulia kama wazazi wetu. ni watu wazima saana, wastaafu. lakini huyo mume anatusikiliza sana, kila tunachomshauri. Mke wake akitaka kufanya kitu chochote ambacho anajua mumewe ana uwezo nacho huwa anatuomba sisi tumshauri, ni kweli tukiongea naye tu anatoa hela faster, hata kama mkewe alishambishia saaana.
Huwa najifunza mambo mengi sana kwa kuwa karibu sana na watu wazima, haya maisha siyo kama tunavyoyaona kwa nje, kuna mengi yaliyojificha ndani ya nyumba.
usikute mzee wa watu (huyu tunayemjadili) hakuwa na starehe kihiiivyooooo, je alikuwa na mke mshauri?
Kweli haingii akilini lkn ndio kawaida ya binadamu kupenda kuhamishia lawama kwa mtu mwingine bila kujitazama yeye amechangia kiasi gani hali kuwa hivi. Wazee wengi walikua walevi sana na wapenda starehe , yaani umenigusa sana mkuu na hii post huwa najiuliza hivi kizazi cha wazee wetu walikuaje mbona wengi wanafanana akili. Halafu wazee hawa walikua bahili sana hata kutoa support ktk familia . hebu fikiria Enzi hizo karibu huduma nyingi walikua hawalipii kama huduma za afya zilikua nzuri. Kupeleka mtoto shule pia ilikua free na elimu ilikua bomba, wengine walishindwa hata kununua uniform za watoto kisa ubinafsi. Si umeona mzazi wa mbunge flani anadai mwanae kamtelekeza eti anasema alikua sijui japan kikazi for 10 yrs hivyo hakuweza kumhudumia mwanae . Nilikasirika sana kusikia hivyo nikajiuliza mshahara wake alikua anaufanyia nini.Mtu kulipwa elfu tatu mwaka 1978 ni 'milionea sana tu'
leo analia 'hakupata chochote'
Wanaudhi watu wa aina hii. Halafu usipowasaidia walalamishi hawakumbuki kabisaa walikotoka kweli watu husema mla kunde husahau lkn mzoa maganda huwa hasahau.Tena hujisifia kwamba bila mimi usingezaliwa , basi mwenzio nashangaaga sana na kusema kwani usingezaa wewe mtoto huyo si angezaliwa kwingine tena ulimpotezea opportunities nyingi tu. Ifike mahala wazee wa kesho wasiige hii tabia ya wazee wetu .haya yanatokea kwa mtu ambayo yupo very close na mimi.....
babake alikuwa anajulikana mji mzima kwa hela, watoto wake walikuwa wanatembea kwenye magari tu, enzi hizo ambazo umiliki wa baiskeli ulikuwa shida. alibahatika kuwa na mtoto mmoja (nje ya ndoa), ambaye kwa sababu alikataliwa na baba na mama wa kambo basi alijisomesha ili angalau aweze kujikwamua kimaisha.
wale watoto wa ndani walikuwa na starehe tu kiasi kwamba hakuna aliyekumbuka shule.
huwezi amini kwa sasa huyo mtoto aliyekataliwa ndo anahudumia ukoo mzima, kuanzia baba/mama aliyemkataa, watoto wa watoto wao ambao walikataa kwenda shule, na watoto wa mzee ambao bado wanaenda shule......
na sasa mzee sababu anaona mwanaye alishasamehe na kuamua kuhudumia "familia" yake basi ameanza kudai haki yake kama mzazi, anatamka kabisa kuwa nahitaji kiasi hiki kwa mwezi..... bila aibu
Umeona pia na mataanuzi wanayofanya. Kweli serikali ina sehemu yake lkn hebu tuanze na wao je wana mkakati wowote wa kuutokomeza umasikini. Ukiwaangalia huoni kutwa kushindana kwa starehe na mavazi.Mkuu The Boss pamoja na hayo inawezekana mzee ngurumo kuna makosa alifanya ambayo yamemfimisha hapo.
Lakini lazima thkubali serikali yetu haijaamua kuwasaidia wasaanii na kazi zao zinaibiwa kila leo.nimesikia wanaweka sticker kwenye kazi zao kupitia tra lakini hii ni njia inayo inufahisha serikali moja kwa moja si msanii.
Bado kuna tatizo kabisa ambalo lina changia umaskini wa wasanii wetu, watu wana burn kazi zao mitaani na hakuna sheria za kuwadhibiti maharamia wa kazi zao.
Na hawa wasanii wetu nao ni tatizo kabisa kwanza hawana umoja kabisa,pili kila leo wanakula futari na rais lakini wanashindwa kushinikiza sheria za kuwabana wezi wa kazi zao. Wana shindwa kumuomba rais kuunda kikosi kazi cha kupambana na wezi wa kazi zao nchi nzima,kinyume na hapo wanaishia kupiga nae picha alaf wanakuja kwenye media kusema tunakufa masikini wakati hawajui kutumia nafasi wazipatazo.
Hakikisheni mnambana awe na vitega uchumi atakuja kuwasumbua na kuwatia aibu. Wazee wa aina hii huwa wepesi sana kulaumu watoto wao. Jitahidini na mshirikiane ktk kumshauri juu ya future yake ili asiwaaibishe.yaani The Boss umetugusa wengi, babangu anaelekea kustaafu lakini hata nyumba hana. halafu sioni kama hili linamuumiza yaani sie tumekuwa wa kuishi kotta wakati mzee ana uwezo wa kujenga lakini anaendekeza starehe hadi uzeeni. sas sijui atamlaumu nani.