Wanaume na 'kuchezea maisha'.....

Wanaume na 'kuchezea maisha'.....

DEMBA wazazi wetu wamefanya makosa mengi sana
Na wengi tu ambao hadi leo hatuna mahali pa kupaita nyumbani
Kuna wengine nyumbani ni kwa babu yao
Sasa unaweza kujiuliza iweje babu awe na kwake halafu baba ashindwe?

Kuna mabo mengi sana
Lakini baba na mama ni msingi mkubwa sana wa kuimarisha familia
Wakiparaganyika mazazi aliebaki na watoto ni kazi kubwa kuiimarisha hiyo familia
Wakati mwingine watoto wanakuja kuwa na maisha mabovu na ukiangalia kwa makini chanzo ni wazazi

Kuna rafiki yangu mmoja aliniambia mwaka 2001 kuwa wakati huo alinunua tv na alikuwa na umri wa miaka 24
Katika familia yao ya watoto 7,kwenye familia yao hawakuwahi kuwa na godoro la sponji,yeye ndio alikuwa wa kwanza kulinunua

Unaweza tu kuifikiria hiyo familia ilikuwa inaishi maisha gani wakati baba yao alikuwa ni mfanyakazi serikalini kwa muda mrefu sana!

Inauma sana!
well said mkuu, sisi tunapaswa kujifunza kupitia kwako na tusije kurudia makosa yao
 
Na usikute sasa hivi yuko kwenye maandamano ya wazee wa EAST Africa
kudai 'hela ingine' lol

Hahahahahaaaaa!!!! Inaonyesha The Boss baba yangu unamfahamu, maana ulilosema ni kweli kabisa, kila siku anapiga hesabu eti atalipwa tena milioni 500, anaidai serikali, basi huwa tunamtizama tu hatumjibu, serikali gani hiyo ya kumlipa hizo pesa? kama milioni 200, zilikwisha bila kufanya lolote, hizo 500 akipewa ndiy atafanya kitu? mimi na ndugu zangu huwa tunamwangalia hatumjibishi.
 
Mara ya kwanza niliposikia Mzee Gurumo wa Msondo Ngoma anadai ameimba zaidi ya miaka 50 na maisha yake bado ya 'kimaskini mno' niliona kuna kitu hakiko sawa... sikuwa na ushahidi tu lakini nilikuwa na uhakika kwa vyovyote vile 'atakuwa alichezea maisha ujanani'

Sasa jana walioona akifanyiwa interview na Salama kipindi cha MKASI watakubaliana na mimi huyu Mzee na wengine wengi tunaosikia
wakihojiwa na vyombo vya habari ..wakilaumu serikali kwa kutowajali. Wengi wao walipata 'golden opportunities' za kuwa na maisha bora lakini 'walichezea pesa' na 'opportunities hizo' so many times...

Mfano: Mzee Gurumo jana alisema alilipwa 'elfu ishirini' mwaka 1978 ili kuhamia bendi ya Sikinde...kumbuka kuwa Mshahara wa Rias mwinyi mwaka 1992 ulikuwa 'elfu ishirini na saba tu' sasa pata picha huyu mzee alikuwa na pesa kiasi gani? Na mshahara wake ulikuwa 'shilingi elfu tatu' mwaka hu0 1978... wakati kima cha chini mpaka mwaka 1987 kilikuwa hakijafika 'shilingi elfu saba'

Kuna Mzee mwingine alitunga kitabu riwaya 'Simu ya Kifo' alilipwa 'elfu kumi na mbili ' miaka hiyo nyumba Kariakoo zinauzwa shilingi 'mia nne' na alikufa bila nyumba wala kibanda..

Orodha ni ndefu...na wapo wengine Baba zetu, Wajomba, babu na kadhalika ukiwaona uzeeni wanavyolalamika na kuomba wasaidiwe.... utasema hawakupata chochote ujanani kumbe anasa, starehe na kuhonga wanawake ndo sababu....

Ukweli ni kwamba watu 'huchezea maisha mno' halafu uzeeni hutafuta wa kumpa lawama mara watoto, mara serikali na kadhalika....

Huyu Mzee Gurumo alikuwa sio mtu wa kupewa gari na Diamond... angekuwa na magari na majumba tele ya kuwarithisha watoto na wajukuu...

waliendekeza sifa ya moyo mbona wenzao walijenga...
 

Stori: Brighton Masalu
SIKU chache baada ya kustaafu muziki, mwanamuziki mkongwe nchini, Maalim Mohamed Gurumo ‘Mzee Gurumo' amekiri kupitia maisha mabaya ujanani ikiwemo kufumaniwa na mke wa mtu pamoja na uvutaji wa ‘sigara kubwa' Ijumaa linaanika.
Akizungumza katika mahojiano na Kipindi cha Mkasi kinachorushwa na Runinga ya East Africa chini ya Mtangazaji, Salama Jabiri mwanzoni mwa wiki hii, Gurumo alisema miongoni mwa mambo mabaya ambayo hawezi kuyasahau maishani mwake ni pamoja na hayo.
KUFUMANIWA:
Katika sakata hilo, Gurumo alisema kuwa ilikuwa ni mwaka 1961 ambapo alikuwa na uhusiano na mke wa mtu ambaye aligoma kumtaja, ndipo siku moja wakiwa nyumbani kwa mwanamke huyo ‘wakiponda kirauli' ghafla walisikia hodi na ndipo mwanamke huyo alipomwambia kuwa anayegonga mlango ni mumewe.
"Niliogopa sana, ikabidi nijibanze nyuma ya mlango, alipoingia tu nikatimua mbio kali sana, lakini hakujua kama ni mimi," alisema Gurumo.
Kuhusu uvutaji wa bangi, Gurumo alikiri kuwahi kuonja kilevi hicho ujanani mwake ambapo alibainisha kuwa alishawishiwa na mwimbaji mwenzake maarufu sana kwa wakati huo.
Alisema siku ambayo alivuta sigara kubwa, alipofika nyumbani baada ya kutengewa chakula, alimega ugali na kuchovya kwenye maji ya kunawa akidhani ni mchuzi.
"Siku hiyo ilikuwa mbaya sana kwangu, nilivuta kutokana na ushawishi, baada ya kufika nyumbani, wakati wa chakula nilimega ugali na kuchovya kwenye maji ya kunawa, nikasema mbona mchuzi hauna ladha nzuri, lakini baadaye nilijutia sana," alisema Gurumo na kuongeza:
"Nimepitia maisha ambayo si mazuri sana ujanani, lakini yote hayo ni mapito na imebaki kama historia tu kwangu, namuomba Mungu anisamehe kwa hayo," alisema Gurumo.

cc. The Boss
 
Last edited by a moderator:
Aliyekudanganya Gurumo hajajenga ni nani? Anaishi kwenye nyumba yake na nyingine kapangisha.

Ye kilio chake ni gari

sasa analia nini kuwa anamaisha magumu ka ananyumba ya kupangisha..

then nimesema waliendekeza sifa za moyo si aliendekeza sifa ya moyo naona umekua mkali ka mtoto wa kijicho vile..
 
Nyumba sijui but uisishangae akiwa hana
mbona marehemu Mzee Kipara alikuwa hana nyumba
na alikuwa kazaliwa mjini hapa hapa Dar?
na aliajiriwa RTD...miaka hiyo
pengine na makabila ya watu nayo huchangia. Mbona kina binti baraka kidude haja acha ata mtoto duh mengine is party of life.
 
Tulikua tunaishi nyumba za shirika ingawa tulikua na nyumba ambayo mzee alijenga enzi zake sinza..basi dingi akasema karibu nastaafu..nikistaafu woote kijijini...nataka nikapumzike na kero za dar...mama akakomaa akamwambia utaenda mwenyewe kjijini mimi na watoto wangu tutabaki mjini..nenda mwenyewe...mmmh basi dingi kupata pesa ya mafao fastaa tafuta kiwanja na kujenga nyumba ya ukweli japo kwa haraka...akafungua ofisi na gari akanunua...uzuri ni kwamba shirika lilikua halikufukuzi ndani ya nyumba mpk baada ya miezi kadhaa...ila tunamshukuru mama kwa ukali na msimamo...bila hivyo tungeenda kijijin au kurudI kwenye nyumba ya enzi zake sinza...mama akiwa legelege..mpenda anasa na kustarehe km mumewe familia huyumba...my dad had money na alikua banker wa maana..angeamua angemiliki majumba kibao mjini ukizingatia amesomea na kukulia dar..so he had every opportunity. .but ndo hivyo anasa...

Nilichojifunza hapa Watz tuna matatizo mengi yanayofanana aisee maana hawa wazazi wetu kiukweli kuna mambo mengi sana walitakiwa kufanya, lakini mistake walizozifanya ndio zimetufanya tuwe hivi leo kwa kujitahidi kuweka vipaumbele, na ndio maana ukiona mtu kafanikiwa usidhani ni hivi hivi tu kumbe kuna machungu mengi ali-experience udogoni sasa hataki kuwa kama mzazi wake na ndio maana siku hizi vijana wengi siku hizi hata hajafika 35 tu ama ana kiwanja au amekwisha jenga na watoto wakikua hawa-experience machungu ya kupanga sio kama sie tunahama mtaa huu kwenda ule na mpaka kumwagilia tofali tumemwagilia na nyumba bado haishi mpaka unaanza maisha, huwa nina kamsemo kangu kwamba unapoanza maisha unatakiwa uwe na mfumo tofauti na maisha kwa mzazi wako yaani kama alikuwa na radio mkulima wewe unachukua latest, kama alikuwa na nyumba yake basi wewe ukijenga unajenga ya viwango tofauti na vyake.
 
aisee naomba ulitilie maanani kabisa kabisa, maisha gani hayo unaishi? hata kama hutokuja kuishi kwenye hiyo nyumba lakini unayo na utajua utafanyia nini, upangishe ufanyaje ni yako aise,au sisi tuliokuzwa kwa hasira za mzazi mmoja kututelekeza na mmoja kuhangaika na sisi mpaka unatamani ukatize masomo kwamba unamuumiza sana ndio tuna usongo sana na haya maisha? mie huo mkopo wangu wa kwanza nilienda kukarabati nyumba ya mama nyamayao, nyingine nikawekeza ninavyoweza, naweza kukwambia sikuunywea hata fanta, niliamini hizo fanta zipo tu na ntakuja kuzinywa nitakavyo, sasa hivi sizungumzii fanta nazungumzia ballantin, wewe wewe! au ndio za kimjini mjini "kujenga kitu gani" asikwambie mtu hakuna anaetamani maisha yake yote yaishie kwenye vinyumba vya kupanga, na ufanye sasa hivi mana ukishaingia kwenye kuanzisha familia mambo ni mengi sana, jipange kwa sasa kwa popote utakapofikia sawa tu ili mradi usichana haujapita kwa vipodozi na malecwig.

Ulifanya la maana sana maana hizo fanta unazopenda zipo tu na nadhani una enjoy tu sasa hivi, kujenga ni kukubali adhabu kwa muda mfupi kama vile tulivyokuwa tunasaka elimu unahairisha usingizi kwa muda lakini leo una maamuzi yako mwenyewe juu ya usingizi wako kikubwa usijitese sana lakini pia uwe na nidhamu kwa matumizi yasiyo ya lazima. Nyumba inatakiwa uijenge mapema kama mwenyezi mungu amekujalia fursa ya kuwa na vijisenti sio unajenga umebakiza miaka 5 ustaafu
 
Naona vijana tunamjadili na kumhukumu huyu mzee, tutazame kumbuka leo kima cha mshahara cha watumishi walio wengi wa serikali ambao ni walimu , askari polisi, magereza, watumishi wa halmashauri zetu hakizidi Tsh 300000. Mfanyakazi wa serikali waliowengi graduate wanaanza na Tsh 590,000. Any way wacha tufanye analipwa Mill 1. Akikatwa huyu mtu PAYE 150,000 anabaki na tsh 850,000/= Toa NSSF 10%=100,000 au PPF 5%= 50,000 anabaki na 750,000 au 800,000/=
Kodi ya chumba 50,000 +10000 umeme na maji, usafiri 2000*26 Days=52,000 Lunch 3000 *30=90,000 Jumla 202,000 bado Mengineyo kama vocha, misaada kwenu 100,000,. Msosi wa jioni 90000/= Breakfast 1000*30= 30000. Unabaki na Tsh 328,000. Hapo nimepigia kwa kijana anayeanza kazi hana mke wala hajaanzisha familia. Angalia leo bei ya kiwanja hapo mjini ni sh ngapi? Inabidi uweke mishahara mingapi ili uweze kununua uwanja?. Shukuru sasa hhivi mikopo imekuwa nje nje bila hiyo wewe hata hicho ki Verosa ungenunua? Tuache kuwabeza wazee wetu mishahara haijawahi kuwa inatosha tangu mwanzo wa dahali. NB, Hapo huyo kijana hanywi hata kabia wala maji ya chupa yaani ni bahiiri hatari.
 
Ndg yangu KINYENGELI unayosema yanaweza kuwa na ukweli flan lkn kumbuka kipindi hicho Pesa ilikuwa na thamani tofauti na miaka hii Mtu alikuwa analipwa Ths 10 kwa mwezi na ameweza kujipanga! leo tsh 10 hata ukimpa mtt haitaki mi nadhani zamani maisha yalikuwa rahis sana na Baadhi ya wazee we2 hawakufikiri kwamba Maisha yangekujakubadilika Ghafla namna hii!
 
Wallahi naapa, machozi yamenitoka..

Nikikumbuka enzi ya mzee, stori zake na sasa anavyonihenyesha, acha tu!

On the other side na mi nikifikiria nnavozitumbuaga, mmh!

Thanx The Boss.
 
Naona majadala wetu mtamu na wenye mafunzo umepoa, ngoja niuchangamshe kidogo.

Hiki kibao cha Msondo/OTTU/JUWATA/NUTA kikiwa na "Kamanda" Maalim G kinaujumbe murua sana lakini chakushangaza maisha ya muimbaji hayakusadifu kabisa maudhui adhimu aliyoyatoa.

Kilinge kiendelee The Boss, Dark City, Asprin, DEMBA, Kaunga, @ Nyamayao, Fixed Point, The Prof, Jodoki Kalimilo nk...........
 

Attachments

Last edited by a moderator:
Nilichojifunza hapa Watz tuna matatizo mengi yanayofanana aisee maana hawa wazazi wetu kiukweli kuna mambo mengi sana walitakiwa kufanya, lakini mistake walizozifanya ndio zimetufanya tuwe hivi leo kwa kujitahidi kuweka vipaumbele, na ndio maana ukiona mtu kafanikiwa usidhani ni hivi hivi tu kumbe kuna machungu mengi ali-experience udogoni sasa hataki kuwa kama mzazi wake na ndio maana siku hizi vijana wengi siku hizi hata hajafika 35 tu ama ana kiwanja au amekwisha jenga na watoto wakikua hawa-experience machungu ya kupanga sio kama sie tunahama mtaa huu kwenda ule na mpaka kumwagilia tofali tumemwagilia na nyumba bado haishi mpaka unaanza maisha, huwa nina kamsemo kangu kwamba unapoanza maisha unatakiwa uwe na mfumo tofauti na maisha kwa mzazi wako yaani kama alikuwa na radio mkulima wewe unachukua latest, kama alikuwa na nyumba yake basi wewe ukijenga unajenga ya viwango tofauti na vyake.

Well said!!
 
kweli kaka wazee wengi wa zamani inaonekana waliendekeza sana starehe, dingi yangu mkuwa wakati huo anafanya kilimanjaro Hotel sigara yake ilikuwa REX akifika kijijini tu hizo mbwembwe kijiji kizima kinamuamkia lakini mpaka anastaafu aliishia kurudi kijijini na kukaa kwenye nyumba ya udongo. katika wasanii wakongwe afadhali naona majuto kidogo amewekeza hapo Tanga. wengine wote naona ilikuwa ponda raha kufa kwaja
1744177969949.png
 
T.I.D,Blue,Chid Beenz,Ray C baada ya miaka 30 watakuja na ngonjera hizo

vijana maofisini wanaokopa Verossa na kila mwezi kuhonga nusu mshahara nao pia
hata haijafika 30, ndo kwanza 12. Na tunawaona hapo ulipotabiri
 
Back
Top Bottom