Wanaume na 'kuchezea maisha'.....

Wanaume na 'kuchezea maisha'.....

ni swala la kujua tu malengo yako. pamoja na kila kitu unachotaka kujifanyia/kufanyia watu, unatakiwa kujua mwisho wa siku wewe unataka nini.
huwa nawatimuaga ndugu zangu ambao wao na mimi wote wafanyakazi, wao inapofika muda wa kulipa ada ya shule ya mwanaye anakuja kwako kukuambia anaomba msaada hana hela ya ada, hali kadhalika inapofika kulipa kodi ya nyumba.
Huwa najiuliza hiki kitu hakijatokea ghafla, mtu unajua kabisa mwezi fulani nalipa ada/kodi kiasi fulani. Mshahara wako kwa miezi 2 hautoshi kulipa (usiniambie ulikuwa unategemea dili). kwa nini usianze ku-accumulate kidogo kidogo mpaka itakapokamilika? hilo deal likitokea utafanyia kitu kingine.....

Salutu! kuna watu uwaona wenzau kama wajinga vile,wewe msgahara wako wote umeukopea school fee ya watoto unaenda kupiga mizinga, mkopowote jmeenda kununulia viwanja.sikusaidii ng'oo!
 
Mfanyakazi nalikumbuka sana na coverage yake ya ile kesi mpiga picha/mwandishi wa habari (jina limenitoka kidogo) ndo iliyompaisha Masumbuko Lamwai kutoka kwenye obscurity na kuwa household name. Nilikuwa napenda sana kusoma 'Amini Usiamini'.

Je, kwa sasa umesikia huo mshahara ni mara 58 zaidi ya ule wa kima cha chini toka kwa nani/wapi?

Alikuwa kupiga picha Joseph Senga, alishambuliwa na Askari akiwa kazini. Mmoja wa witnesses alikuwa Askari mmoja Deusdedith Kajuna...and yes Lamwai was a lawyer for Senga na alikataa jina kutoka hapo...But say what? Kama topic hii ilivyo he to messed up his opportunity...Leo hii Lamwai si lolote si chochote...wamekuja vijana wengine katika sheria na wamemfunika both professionally and in business success...so the topic by The Boss I relevant na mtambuka (cross-cutting)...
 
Hiyo 'haujamtoa kwenye umaskini' inahitaji qualification nadhani. Maana kuwa na gari tu haimaanishi kwamba mtu ndo ushatoka kwenye umaskini na kutokuwa na gari haimaanishi mtu ni maskini.

At least as far as our community is concerned, owning a car is an outward manifestation of mambo safi...which holds true in many aspects...na ndiyo sababu hata yeye analalamika kuwa Hana gari!
 
Mara ya kwanza niliposikia Mzee Gurumo wa Msondo Ngoma
anadai ameimba zaidi ya miaka 50 na maisha yake bado
ya 'kimaskini mno' niliona kuna kitu hakiko sawa..
sikuwa na ushahidi tu lakini nilikuwa na uhakika kwa vyovyote vile
'atakuwa alichezea maisha ujanani'

Sasa jana walioona akifanyiwa interview na Salama kipindi cha MKASI
watakubaliana na mimi huyu Mzee na wengine wengi tunaosikia
wakihojiwa na vyombo vya habari ..wakilaumu serikali kwa kutowajali.
wengi wao walipata 'golden opportunities' za kuwa na maisha bora
lakini 'walichezea pesa' na 'opportunities hizo' so many times...

mfano Mzee Gurumo jana alisema alilipwa 'elfu ishirini'
mwaka 1978 ili kuhamia bendi ya Sikinde...kumbuka
kuwa Mshahara wa Rias mwinyi mwaka 1992 ulikuwa 'elfu ishirini na saba tu'
sasa pata picha huyu mzee alikuwa na pesa kiasi gani?
na mshahara wake ulikuwa 'shilingi elfu tatu' mwaka hu0 1978..
wakati kima cha chini mpaka mwaka 1987 kilikuwa hakijafika 'shilingi elfu saba'

Kuna Mzee mwingine alitunga kitabu riwaya 'Simu ya Kifo' alilipwa
'elfu kumi na mbili ' miaka hiyo nyumba Kariakoo zinauzwa shilingi 'mia nne'
na alikufa bila nyumba wala kibanda..

Orodha ni ndefu...na wapo wengine Baba zetu,Wajomba,babu na kadhalika
ukiwaona uzeeni wanavyolalamika na kuomba wasaidiwe....utasema hawakupata chochote ujanani
kumbe anasa,starehe na kuhonga wanawake ndo sababu....

ukweli ni kwamba watu 'huchezea maisha mno' halafu uzeeni hutafuta wa kumpa lawama
mara watoto,mara serikali na kadhalika....


huyu Mzee Gurumo alikuwa sio mtu wa kupewa gari na Diamond...
angekuwa na magari na majumba tele ya kuwarithisha watoto na wajukuu...

Wazee wa zamani hawakua na challenge ,walibweteka sana......kama ukipata mda ukaongea na wazee...na kuna wengine walioko kwenye 40-50...story zao zinauzi sana....limtu limepanga, halina hata kiwanja alafu linasema ohhh hapo kijitonyama /mikocheni tuliitiwa viwanja bure tuakakataa....eti sababu kulikua ni tindiga......napataga hasira sana.
 
Samahani Kibibi Jongo, Eiyer . Kuna watu hawalali katika maisha yao wao kucha kutwa wanahangaika kusaka maisha tena wakiwa na mipango mizuri ya kipesa lakini mwisho wa siku hawafanikiwi wanabakia hohehahe hili linasababishwa na nini? Pia huwa ?

Hakuna kitu kama hicho
Huwezi kufanya kazi kwa bidii halafu ukawa na mipango mizuri ya kifedha halafu usifanikiwe

Unaweza kufanya kazi sana,kufanya kazi sana kuna maana ya kuingiza sana pia
Lakini ukawa unatumia sana pia
Hapa kosa ni lako

Kanuni ya kufanikiwa inasema kuwa haijalishi unaingiza kiasi gani bali unatunza kiasi gani!
 
Pole sana kila mtu ana woga na 'future'
me included but kuwa na woga ni first step
as long as unaogopa itakusaidia...sanaa

pesa ndo hizi hizi tu
unapandisha nyumba kozi tatu zingine una spend
ukirudi unaongeza kozi nne na una spend kidogo

The Boss hiyo ndiyo reality...mwanzoni nilikuwa najiuliza sana watu wanawezaje kujenga? Thinking of my father, aliwezaje kujenga? Nikasema no starehe, no nothing unnecessary...kweli mambo yakabadilika...nikapata plot, nikanunua building materials...na sasa kibanda kinaiunuka...umri ukienda my kids will realize kwamba I did something for them! Mambo yanawezekana sema tu vijana wanataka Verossa na kuning'inia SamakiSamaki!
 
......kutoa lawama kwa serikali na kumtolea lawama mzazi wako yote sawa!

......be responsible for your own life!

Halafu utasikia wengine oohh, "baba ndio kichwa cha familia" ...jukumu lake hilo, akiweza mke anataka compliments, "behind every successful men....!"
C.r.a.p!
 
Jamani mnapoyasema yeye msimsahau na Mungu wote tungekuwa kama daimond nan angekuwa ngurumo?kumbukeni kwamba jitihada zako pekee hazishindi kudra za MUNGU.simtetei ngurumo wala simlaumu kila kitu kinasababu yake............

tukisema hivi hawa watu watazidi kujiendekeza tu, kama diamond sikumbuki nimesoma wapi kwamba ana nyumba nne hadi sasa, (kama hicho chanzo kilikuwa cha ukweli)imagine, na pesa anayoingiza anaipangilia na starehe anazifanya pia, sio kila kitu ni Mungu jamani nae katupa uwezo wakufikiria/tafakari/chuja jema na baya, kiujumla kama kijana ukifikisha 35 yrs (tena hapo umechelewa pia) na una uwezo wa kuingiza chochote kwa siku/mwezi na hujafanya lolote kwenye maisha i.e nyumba etc umebakia kubadilisha kila aina ya magari/simu, uanze kuamka sasa, tena uamke kwa speed zoteeee! tunawaona wengine kama mr blue, chidi benzi etc nao walikuwa kwenye mfumo wa sasa lakini wako wapi leo hii? mtu kama ray c alikuwa kwenye channel nzuri tu.
 
The Boss hiyo ndiyo reality...mwanzoni nilikuwa najiuliza sana watu wanawezaje kujenga? Thinking of my father, aliwezaje kujenga? Nikasema no starehe, no nothing unnecessary...kweli mambo yakabadilika...nikapata plot, nikanunua building materials...na sasa kibanda kinaiunuka...umri ukienda my kids will realize kwamba I did something for them! Mambo yanawezekana sema tu vijana wanataka Verossa na kuning'inia SamakiSamaki!

It's true........ hahahahaaa kama ulikuwepo samaki samaki! Halafu mwisho wa siku wakikuta vijana wenzao wamewekeza au wametoka, watakwambia ooo hiyo sembe.
Kuna wengine wameuza sembe watoto wa Ilala na Kariakoo miaka ya nyuma, hawana hata kijiko.
Mpaka leo wapo kwenye Nyumba za wazazi wao na kujukuu wamejukuu.
NOTE Simaanishi hakuna wauza sembe HAPANA! Ila tunaongelea umeuza sembe au umeajiriwa au umeuza nyanya, au whatever, UMEFANYA NINI?
 
Hakuna kitu kama hicho
Huwezi kufanya kazi kwa bidii halafu ukawa na mipango mizuri ya kifedha halafu usifanikiwe

Unaweza kufanya kazi sana,kufanya kazi sana kuna maana ya kuingiza sana pia
Lakini ukawa unatumia sana pia
Hapa kosa ni lako

Kanuni ya kufanikiwa inasema kuwa haijalishi unaingiza kiasi gani bali unatunza kiasi gani!

Ok hizo ni kanuni za kiuchumi nazielewa vizuri sana. Mimi msingi wa maswali yangu ni kwamba hata huyo aliepata ufahamu wakielimu akajua how much to consume kulingana na income yake nae kabarikiwa akili hiyo na Mungu. Kwakuwa wapo wenye ujuzi huohuo lakini hawautumii kujipatia hayo maisha safi. Mzee Ngurumo na watu wamfano wake waliobahatika kupata neema kipindi cha ujana wao wakazichezea wao walikosa neema ya ufahamu wa kuwekeza kwa ajili ya maisha ya baadae. Nikiwa na maana kwamba umaskini na utajiri pia ni sehemu ya mipango ya Mungu. Mungu anajua nani atakuwa mzembe ktk utajiri alionao na mwisho ataja kuwa maskini. Sema ni siri yake Mungu kwani hakuna aliezaliwa anajua kuwa yeye atakuwa tajiri au maskini. Huwezi ukakaa tu chini ukawa na fikra kuwa utapata tu kwakuwa Mungu ndie anaejua wewe utakuwa tajiri bali mtu unapaswa kuhangaika na kujitafutia ila ikitokea umekosa pamoja na juhudi zote ulizoonyesha katika kutafuta unapaswa kuamini kuwa Mungu ndie aliepanga hayo na hapo itakusaidia pia Kumshukuru kwakila jambo la furaha au la shida. Ndio maana as a human being we do our best and God do himself the rest. Unapokuwa unasema Mungu hajui nani atakuwa maskini au tajiri manake wewe unakuwa mpingaji wa kwamba Mungu hajui mambo ya siri. Wakati yeye ndio anaejua yaliokuwa, yanayotokea sasa na yatakayotokea kesho tusioijua wewe na mimi. Cc Kibibi Jongo.
 
Last edited by a moderator:
Tatizo la watu wengi ni kuweka vipaumbele....

ndiyo maana huwa na kumbuka sana kauli ya Mwalimu Nyerere..."Kupanga ni kuchagua"!!!

Babu DC!!

wakati naanza kabisa kazi fresh from chuo, kampuni niliyokuwa nafanyia ilikuwa inatujali sana wafanyakazi wake, mikopo nje nje, baada ya mwaka wenzangu wote nilioanza nao kazi wana magari mazuri mie bado naenda job na taxi but wanajua nimechukua mkopo mzuri tu, ilikuwa maulizo kila siku, nyamayao mkopo wako umepeleka wapi, hivi kwanini huna gari jamani, bla bla kibao, wengine mawazo yetu yalikuwa kushika viwanja kadhaa wao ilikuwa magari na masimu mazuri, kupanga ni kuchagua.
 
yaani The Boss umetugusa wengi, babangu anaelekea kustaafu lakini hata nyumba hana. halafu sioni kama hili linamuumiza yaani sie tumekuwa wa kuishi kotta wakati mzee ana uwezo wa kujenga lakini anaendekeza starehe hadi uzeeni. sas sijui atamlaumu nani.

umenikumbusha wakati mzee kastaafu akafanikiwa kujenga kibanda last minute, kwa mara ya kwanza nikapata kusikia sauti ya mvua kwenye nyumba ya bati ambayo haijawekwa ceiling it was hard, ukizingatia nimezaliwa na kukulia kwenye nyumba za sirikali za vigae.

Anyway kwa watoto wa baba yetu, we took it positive kiasi kwamba hakuna mtoto ambaye alifikisha 30yrs bila kuwa na nyumba, so tulijifunza kutokana na makosa ya mzazi; you can do the same.
 
Unavyopenda mambo ya hivyo, hata sijui unajisikiaje... Lol!

Ila ni kweli, mtu ukipata mke wa hovyo imekula kwako!

na ukipata mume wa hovyo je?

Mimi nafikiri ukipata mke wa hovyo na ukakubali kufuata uovyo wake nawe ni wa hovyo au akili zako ni za kushikiwa. Ofcourse kama couple mnahitaji kuwa na malengo mliyokubaliana na strategy mlizokubaliana.
 
Kwenye hili sina ubishi mkubwa mwenzangu....

Mwenzenu hadi sasa, karibia vitu vingi sifanyi bila ruhusa ya bibi....ila wakati mwingine anakaba sana hadi natamani kukimbia nyumba....

Mwanamke wa hovyo ni zaidi ya kiroba cha misumali.....

Ndiyo maana nawakubali na kuwaheshimu akina na mama wenye busara zao, wakiongozwa na Bibi DC, mama yangu mazazi na wengine kibao....!!

Babu DC!!

That's right Mkuu! Mwanamke wa hovyo ni sawa kiroba cha misumari!
Ndiyo maana Bible inatueleza Mwanamke -------- huibomoa Nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe!
Upumbavu ni pamoja na kutokuwa mshauri na msaidizi mzuri kwa mume wako katika kumanage mapato ya familia.
Saa nyingine utaona mwanaume amepambana amewekeza, lakini mke ni mtapanyaji! Kuna kabila wanawake wa ivyo wanaitwa mlango wa nane! Vijana ulizeni babu na Bibi zenu!
 
na ukipata mume wa hovyo je?

Mimi nafikiri ukipata mke wa hovyo na ukakubali kufuata uovyo wake nawe ni wa hovyo au akili zako ni za kushikiwa. Ofcourse kama couple mnahitaji kuwa na malengo mliyokubaliana na strategy mlizokubaliana.
rafiki, dont underestimate the power of a woman....never......
hawa ni wajanja tu wakiwa nje yetu..... wakiwa ndani ya 18 hawafurukuti, hata uwe smart namna gani
 
Mkwe wewe umeshajipanga? Ama bado upo upo? Mie sijielewi kama nishafikia pa kilujipanga ama bado!
kweli usipojipanga ujanani uzee wako lazma uwe wa tabu sana, ahsante kwa kutukumbusha hili The Boss.

Babu nakumbuka kukusifia hapa wewe na TIMING kwa kukiri wazi juu ya msaada wa mawazo na kubanwa na bibi. Sasa sie wanawake tuna taabu sana. Unamshauri mume hasikii, unakaba hakabiki ndo kwanza anakimbia na kulalamika humfai. Ndio maana mie na paw tumekubaliana kutofautiana baadhi ya mambo. Hata kama haamini kwenye ndoto yangu at least nataka baraka za kuota na sio kuanza kujenga nyumba kwa siri.

Kuna ndugu yangu alijenga nyumba kwa siri, mume akajua akaenda kuipiga nyundo. Wakati huo huyo mama anaishi nyumba line polisi, na mume ni mishen tauni! Mama alianza kujengewa na mwanae kwa uongo mwingi na lile limwanaume lilikufa baadae. Yaani leo tukikaa hapo kwenye nyumba yao tunasimuliwa na watoto wanarecall yale maisha! Mama asingekomaa sijui wangeishia wapi saa hizi!
Kwenye hili sina ubishi mkubwa mwenzangu....

Mwenzenu hadi sasa, karibia vitu vingi sifanyi bila ruhusa ya bibi....ila wakati mwingine anakaba sana hadi natamani kukimbia nyumba....

Mwanamke wa hovyo ni zaidi ya kiroba cha misumali.....

Ndiyo maana nawakubali na kuwaheshimu akina na mama wenye busara zao, wakiongozwa na Bibi DC, mama yangu mazazi na wengine kibao....!!

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
......kutoa lawama kwa serikali na kumtolea lawama mzazi wako yote sawa!

......be responsible for your own life!

Halafu utasikia wengine oohh, "baba ndio kichwa cha familia" ...jukumu lake hilo, akiweza mke anataka compliments, "behind every successful men....!"
C.r.a.p!
kuna rafiki huwa anamlalamikia baba yake kuwa hakuwajengea misingi mizuri, baba yake nae huwa anamwambia tatizo sio mimi mwanangu tatizo babu yako!! kweli kila mtu awajibike na asimame kutokea pale alipo na kusonga mbelena si kufikiria amefikaje pale.
 
rafiki, dont underestimate the power of a woman....never......
hawa ni wajanja tu wakiwa nje yetu..... wakiwa ndani ya 18 hawafurukuti, hata uwe smart namna gani

Kwanza, za kuadimika?
Kwa maneno mengine, mwanaume akiharibu au akitengeneza ni sababu ya mwanamke? Akicheat au akiwa mwaminifu ni sababu ya mwanamke? yeye hana will na uwezo wa kufanya maamuzi yake mwenyewe?
 
Back
Top Bottom